KERO Supervisors wa Wanafunzi wa Masters - UDSM ni kero, wanatukwamisha wengi, Uongozi wa Chuo uchukue hatua

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kabla haujapata changamoto ya kuanza kuelewa unachojifunza unaanza kwanza kupata "changamoto" kutoka kwa mkufunzi. Ushauri wa kuutoa hapa sina ila kwa yule aliyeongelea suala la kufungua keshi na mimi ninaona ni jambo jema, kama wanafunzi mna ushahidi wa kufanyiwa michezo 'michafu' ili mshindwe kufaulu mitihani nendeni mahakamani.
 
Mimi na wenzangu kadhaa tunaosomea Shahada ya Uzamili (Master of Public Health - MPH) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tuna changamoto moja kubwa ambayo imekuwa kero kwa muda mrefu na kuendelea kuifumbia macho itakuwa ni sawa na kuendelea kufuga mtatatizo.

Tatizo letu kubwa ni kuhusu utendaji unaofanywa na Wasimamizi wa Kazi za Utafiti za Wanafunzi (Supervisors wa Research), hawa watu wa muda mrefu wamekuwa ni tatizo na kama hali hii haitekemewa au kuchukuliwa hatua watakuwa ni kati ya sababu zitakazokimbiza Wanachuo kusoma UDSM.

Kabla ya kuanza kusoma Masters hapo UDSM baadhi yetu tuliambiwa na waliosoma kuwa bora tutafute chuo cha binafsi kuliko kusoma hapo, tulipouliza tukaambiwa ni jambo gumu sana kuhitimu Masters na ukifanikiwa mara nyingi lazima uwe nje ya muda hata kama unasoma vipi na kujituma.

Utaratibu uliokuwepo siku za nyuma ilikuwa unapofika muda wa kukamilisha kazi yao na ukazidisha ilitakiwa mhusika alipe Tsh. 50,000 kwa kila mwezi, lakini sasa hivi utaratibu ulivyo ukichelewa kukamilisha Reasearch yako unatakiwa kulipa hela ya Semister nzima ambayo ni Tsh. Milioni 2.5

Uongozi wa UDSM unafanya hivyo kwa kuwa hauambiwi ukweli kuwa asilimia kubwa wanaosababisha Wanafunzi wanashindwa kukamilisha tafiti zao ndani ya muda ni Supervisors.

Supervisors wanajiona kama Miungu watu, kwanza unapopewa akusimamie picha linaanza kuja kumpata ni unatakiwa kuacha kazi upate kazi ya kumtafuta yeye.

Ukifanikiwa kumpata anaweza kukupa maelekezo ya kazi au ukamkabidhi kazi yako ili aipitie lakini akachukua zaidi ya miezi miwili kuipitia au kuja kumuona tena.

Tuna wenzetu ambao tulianza nao Masters pamoja, wao wapo katika vyuo vya binafsi kama ilivyo Chuo cha SAUT, sasa hivi wanaelekea kuhitimu, sisi ndio kwanza tunaendelea kuimba mapambio ya kuwatafuta Supervisors.

Mfano darasa letu tulikuwa Wanafunzi kati ya 25 hadi 30 lakini hivi tunavyoandika hapa wanaotarajia kuhitimu ni wawili tena ambao nao wamechelewa.

Supervisors ni shida, hawapatikani kirahisi na baadhi yao ukiwapata hawakupi majibu mazuri.

Ukisema uende ukashtaki au kuwasilisha malalamiko yako juu ya Supervisors, huwezi kupata msaada kwa kuwa unaenda kushtaki kwa wenzao.

Pili, suala la kutakiwa kulipa ada ya Semister nzima kwa uzembe unaofanywa na Mtumishi wa Chuo ni maumivu makubwa kwetu tunaosoma.

Kozi ya Miezi 18 unajikuta umeisoma Miaka mitatu, hapo unalipa ada ya Tsh. Milioni 7+ kisha uambiwe tena ulipe Tsh. Milioni 2.5 ni mateso yasiyo na maelezo hasa kwa kuw wengi wetu tunaosoma chuo hicho ni Wafanyakazi na wengine tuna familia.

Tunakuwa hatueleweki, kutumia muda mwingi kusoma, hela ya familia pia tunaipeleka

Uongozi unapewa taarifa tofauti
Tumefuatilia na kugundua kuwa Uongozi haufikishiwi taarifa sahihi, wanajulishwa Wanafunzi ndio wenye shida lakini uhalisia ni tofauti.

Hii ikiendelea UDSM itaendelea kukimbiwa kwa kuwa hakuna anayeweza kuvumilia usumbufu huo na kupoteza hela bila sababu za msingi.
Usitegemee jema kutoka kwa watu wanaoishi kwa Trauma, walio traumatized na circumstances za maisha,
Kama, wewe ni mkazi, wa, Dar, na unatumia daladala, umeishawahi, kuona jinsi watu wanavyolipuka ukimkanyaga, au kumgonga kwa begi! Reaction Yao, inakuwa kubwa balaa! Watu wanaoishi na, maumivu ya, kiuchumi, msongo, hutafuta nafasi ya kutolea hasira zao, sasa hao wasimamizi wenu,Hari ya kiuchumi mbaya,kama wao maisha Yao magumu, wanapigika, unategemea, watakutendea wema!penyeza rupia! Chukua gamba lako ukatsfute ugari wa watoto na shemeji yetu! Mambo ya kuelewa mbele ya safari
 
Wewe ni msomi na haki zako unaogopa kuzidau waziwazi, vipi ambai hawajaenda shule? wewe na wenzako mnashindwa kuwafe viongozi?

Watanzania nani alituroga? make huu uzezeta sio kabisa haijalishi mtu ana shule kiasi gani kichwani
 
Watanzania tuna la "umungu mtu", mtu akiwa kwenye kitengo ofisi, ukifika pale aringe we, alete nyodo, ni wachache saana walionyooka.
Kuna muda u ajikuta unatamani tu uwe mchawi.
Inasababshwa na aina ya wataliwa, Sasa wasomi wanapo kuwa kondoo na kugopa kuface viongozi unategemea nini?

Kenya huwezi kuta huu ujinga kwa sababu wakenya hii ikitokea wanaweza hata choma chuo moto. Shida ni ukondooo wa Wabongo
 
Usitegemee jema kutoka kwa watu wanaoishi kwa Trauma, walio traumatized na circumstances za maisha,
Kama, wewe ni mkazi, wa, Dar, na unatumia daladala, umeishawahi, kuona jinsi watu wanavyolipuka ukimkanyaga, au kumgonga kwa begi! Reaction Yao, inakuwa kubwa balaa! Watu wanaoishi na, maumivu ya, kiuchumi, msongo, hutafuta nafasi ya kutolea hasira zao, sasa hao wasimamizi wenu,Hari ya kiuchumi mbaya,kama wao maisha Yao magumu, wanapigika, unategemea, watakutendea wema!penyeza rupia! Chukua gamba lako ukatsfute ugari wa watoto na shemeji yetu! Mambo ya kuelewa mbele ya safari
shida sio hao shida ni ukondooo na uzezeta wa Watanzania ndio unao zaaa haya yote.
 
Kweli ndiyo maana CCM inatuona wajinga. Mnasoma na kufika level hii halafu mnashindwa kutatua matatizo yenu kwa kuambiana ukweli? Nyie elimu haijawakomboa hata kidogo. Moja ya malengo ya kusoma ni mtu kujua haki zake na kuzitatua bila kulalamika kwa siri. Ndiyo maana mkija mtaani watu wanashangaa wasomi wa hii nchi wako wapi? Aibu.
Mkuu hebu fikiria huyu ni masters anaogopa kiwango hiki, vipi raia ambaye hajaenda shule? anaweza fight kwa ajili ya haki zake? ndio maana nasema na nutasema shida kuuu ni ukondooo ulio changanyikana na uzezeta.
 
Ninavyojua Masters na PHD za UD ni kimeo sana. Upate bahati ya msimamizi mwenye moyo wa kazi.

Kama unataka Masters ya kujifunza, tafuta chuo nje ya nchi, kama ya kuweka kwenye CV nenda Open University 😂😂😂
shida ni ukondoo ulio changanyikana na uzezeta, Watanzania kudai haki zao ni ishu, huyu ni msomi anaogopa kama Panya kaona paka. Vipi mtu ambaye hajaenda shule kabisa? Haya mambo wala ahida sio hao superviser shida ni hao wanafunzi, hii ni triend ya ukondoo wa Wabongo
 
Ujinga wa waTanzania wengi ni kwamba unapofanikiwa jambo kwa taabu sana wanahisi ndio sahihi.

Huu utaratibu unaanzia kwa wanafunzi mkikutana mitaani utasikia Masters au Degree ya chuo flani ni noma lazima usote, yaani hatuangalii content ila tunaangalia kusota in general.... kuna kipindi chuo cha SUA kimesifika sana kwa ujinga huo.

Mwisho wa siku wanafunzi hawatoki na content ila wanatoka na ushujaa wa kushinda malumbano na vurugu nyingi za kufikia malengo ya kuhitimu.

Huyu mwanafunzi na yeye akipata kazi kuwa Lecturer anaenda kufanya yale yale. Wataanzania hatujuagi tunataka nini acha tuteseke huo ndio msuli wa UDSM kama mnavoitaga.
 
Hiko chuo siku hizi kimejaa vilaza sana wa hata kujielewa
Na haitakaa itokee ile migomo na fujo za kujitetea kama miaka ya zamani sababu kumejaa mafisi na mambulua mpaka wanachuo wenyewe

1733246057210.png

1733246079236.png
 
Hii tabia ni sugu sana kwa vyuo vingi nakumbuka miaka ya nyuma wakati nasoma shahada ya uzamili kama wewe wanafunzi wengi tulikutana na changamoto kama ya kwako/kwenu.

Supervisor kumpata ni shida ukimpata ukimpa kazi kusoma hasomi kwa wakati inafika wakati kazi inachukua mwezi kakaa nayo tarehe za defense zinasogea.

Mfano unakuta supervisor mmoja ana wanafunzi 5 na wote hawa graduate mwaka husika kisa research sasa unashindwa kuelewa wanafunzi wote watano ni wazembe au supervisor ni mzembe sana.

Kwakeli majority ya hao Dr’s na ma prof wanapenda kusujudiwa sana na niwasumbufu sana hawapendi vitu viende kwa njia nyepesi.

Baadhi ya classmate wali graduate baada ya miaka 3 (yani course ya miezi 18 unasoma miaka minne hadi mitano) wengine waliamua kuacha chuo kabisa baada ya kuona usumbufu umezidi.
 
Unadhani huyo Mwanafunzi wa Uzamiri anayesoma kwa mazingira hayo mpaka anamaliza atakuwa kweli ni Professional? Atamaliza ameshakuwa na roho kama hiyo hiyo ya uvivu.
Hakika. Kufeli kwa mwanafunzi ni kufeli kwa mwalimu, kama wako incompetent kwenye kazi zao basi wasipeleke hio incompetence kwa wanafunzi
 
Hii tabia ni sugu sana kwa vyuo vingi nakumbuka miaka ya nyuma wakati nasoma shahada ya uzamili kama wewe wanafunzi wengi tulikutana na changamoto kama ya kwako/kwenu.

Supervisor kumpata ni shida ukimpata ukimpa kazi kusoma hasomi kwa wakati inafika wakati kazi inachukua mwezi kakaa nayo tarehe za defense zinasogea.

Mfano unakuta supervisor mmoja ana wanafunzi 5 na wote hawa graduate mwaka husika kisa research sasa unashindwa kuelewa wanafunzi wote watano ni wazembe au supervisor ni mzembe sana.

Kwakeli majority ya hao Dr’s na ma prof wanapenda kusujudiwa sana na niwasumbufu sana hawapendi vitu viende kwa njia nyepesi.

Baadhi ya classmate wali graduate baada ya miaka 3 (yani course ya miezi 18 unasoma miaka minne hadi mitano) wengine waliamua kuacha chuo kabisa baada ya kuona usumbufu umezidi.
Kweli mkuu hii ni Common sana hasa kwa vyuo vikuu vya serikali
 
Hiko chuo siku hizi kimejaa vilaza sana wa hata kujielewa
Na haitakaa itokee ile migomo na fujo za kujitetea kama miaka ya zamani sababu kumejaa mafisi na mambulua mpaka wanachuo wenyewe

View attachment 3168256
View attachment 3168257
Chuo kimejaa machawa tupu.

Hatuwezi tena kupata wanafunzi mama akina Dr Mpoki Ulisumbisya na Kigwangala wa enzi hizo.

Product za kina Mnyika, Halima, Filkunjombe, kina Zito au kina Mwigulu hakuna tena.
 
Hii tabia ni sugu sana kwa vyuo vingi nakumbuka miaka ya nyuma wakati nasoma shahada ya uzamili kama wewe wanafunzi wengi tulikutana na changamoto kama ya kwako/kwenu.

Supervisor kumpata ni shida ukimpata ukimpa kazi kusoma hasomi kwa wakati inafika wakati kazi inachukua mwezi kakaa nayo tarehe za defense zinasogea.

Mfano unakuta supervisor mmoja ana wanafunzi 5 na wote hawa graduate mwaka husika kisa research sasa unashindwa kuelewa wanafunzi wote watano ni wazembe au supervisor ni mzembe sana.

Kwakeli majority ya hao Dr’s na ma prof wanapenda kusujudiwa sana na niwasumbufu sana hawapendi vitu viende kwa njia nyepesi.

Baadhi ya classmate wali graduate baada ya miaka 3 (yani course ya miezi 18 unasoma miaka minne hadi mitano) wengine waliamua kuacha chuo kabisa baada ya kuona usumbufu umezidi.
Walimu hawana Motisha sasa hivi mvua zimeanza wako Rufiji Kulima.Matikiti
 
Chuo kimejaa machawa tupu.

Hatuwezi tena kupata wanafunzi mama akina Dr Mpoki Ulisumbisya na Kigwangala wa enzi hizo.

Product za kina Mnyika, Halima, Filkunjombe, kina Zito au kina Mwigulu hakuna tena.
Wakina James Mbatia hadi kucha zilitolewa na kufukuzwa chuo kabisa

Watu kama akina Samuel Sitta, Jaji Warioba na wengine walioweza

kum challange Mwalimu Nyerere. Kwa sasa ni uchawa tu, Extended
high school.
 
Mimi na wenzangu kadhaa tunaosomea Shahada ya Uzamili (Master of Public Health - MPH) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tuna changamoto moja kubwa ambayo imekuwa kero kwa muda mrefu na kuendelea kuifumbia macho itakuwa ni sawa na kuendelea kufuga mtatatizo.

Tatizo letu kubwa ni kuhusu utendaji unaofanywa na Wasimamizi wa Kazi za Utafiti za Wanafunzi (Supervisors wa Research), hawa watu wa muda mrefu wamekuwa ni tatizo na kama hali hii haitekemewa au kuchukuliwa hatua watakuwa ni kati ya sababu zitakazokimbiza Wanachuo kusoma UDSM.

Kabla ya kuanza kusoma Masters hapo UDSM baadhi yetu tuliambiwa na waliosoma kuwa bora tutafute chuo cha binafsi kuliko kusoma hapo, tulipouliza tukaambiwa ni jambo gumu sana kuhitimu Masters na ukifanikiwa mara nyingi lazima uwe nje ya muda hata kama unasoma vipi na kujituma.

Utaratibu uliokuwepo siku za nyuma ilikuwa unapofika muda wa kukamilisha kazi yao na ukazidisha ilitakiwa mhusika alipe Tsh. 50,000 kwa kila mwezi, lakini sasa hivi utaratibu ulivyo ukichelewa kukamilisha Reasearch yako unatakiwa kulipa hela ya Semister nzima ambayo ni Tsh. Milioni 2.5

Uongozi wa UDSM unafanya hivyo kwa kuwa hauambiwi ukweli kuwa asilimia kubwa wanaosababisha Wanafunzi wanashindwa kukamilisha tafiti zao ndani ya muda ni Supervisors.

Supervisors wanajiona kama Miungu watu, kwanza unapopewa akusimamie picha linaanza kuja kumpata ni unatakiwa kuacha kazi upate kazi ya kumtafuta yeye.

Ukifanikiwa kumpata anaweza kukupa maelekezo ya kazi au ukamkabidhi kazi yako ili aipitie lakini akachukua zaidi ya miezi miwili kuipitia au kuja kumuona tena.

Tuna wenzetu ambao tulianza nao Masters pamoja, wao wapo katika vyuo vya binafsi kama ilivyo Chuo cha SAUT, sasa hivi wanaelekea kuhitimu, sisi ndio kwanza tunaendelea kuimba mapambio ya kuwatafuta Supervisors.

Mfano darasa letu tulikuwa Wanafunzi kati ya 25 hadi 30 lakini hivi tunavyoandika hapa wanaotarajia kuhitimu ni wawili tena ambao nao wamechelewa.

Supervisors ni shida, hawapatikani kirahisi na baadhi yao ukiwapata hawakupi majibu mazuri.

Ukisema uende ukashtaki au kuwasilisha malalamiko yako juu ya Supervisors, huwezi kupata msaada kwa kuwa unaenda kushtaki kwa wenzao.

Pili, suala la kutakiwa kulipa ada ya Semister nzima kwa uzembe unaofanywa na Mtumishi wa Chuo ni maumivu makubwa kwetu tunaosoma.

Kozi ya Miezi 18 unajikuta umeisoma Miaka mitatu, hapo unalipa ada ya Tsh. Milioni 7+ kisha uambiwe tena ulipe Tsh. Milioni 2.5 ni mateso yasiyo na maelezo hasa kwa kuw wengi wetu tunaosoma chuo hicho ni Wafanyakazi na wengine tuna familia.

Tunakuwa hatueleweki, kutumia muda mwingi kusoma, hela ya familia pia tunaipeleka

Uongozi unapewa taarifa tofauti
Tumefuatilia na kugundua kuwa Uongozi haufikishiwi taarifa sahihi, wanajulishwa Wanafunzi ndio wenye shida lakini uhalisia ni tofauti.

Hii ikiendelea UDSM itaendelea kukimbiwa kwa kuwa hakuna anayeweza kuvumilia usumbufu huo na kupoteza hela bila sababu za msingi.
Ahaaa, hivi bado mnarudi kusoma masters UDSM. Kuna vyuo vingi siku hizi hapa TZ vinatoa Masters. Acheni unyanyapaa! Piga chini Jalalani.
 
Back
Top Bottom