Supu ya pweza inanimalizia hela nashindwa kuiacha

Ungekuwa unakunywa pombe ungesemaje?
 
Hizo lumbulumbu ni ugonjwa kwa kweli, kimasihara tu unajikuta elfu 5 imekatika,
Mie siachi, sina fikra hizo.
 
Pweza wanauzwa kwa kilo. Huyo pweza wa 10K unampata wapi mwenzetu?
Najua pweza wanauzwa kwa kilo, ni mpaka afike ndani sokoni au eneo la mnada ndio anapimwa. Ukimfata nahodha au baharia kwenye chombo anakuuzia kulingana na ukubwa
 
Maisha hayapimwi kwa bajeti dhaifu za namna hiyo!

Unatupa au unakula mwenyewe?

Ungelikuwa unatupa ama kuhonga tungelikushauri vinginevyo.

Lakini mtu unakula kwa afya, halafu tena unaanza kujushitukia!

Unaweza kuchepusha matumizi ya supu, 'seva' ikajaa lakini ukaishia kuhonga,Tv usinunue na wala hapa usitokeze kutuomba ushauri, ikawa ni siri yako.

Wewe bwana kula, Tv ina bajeti yake na mwili una bajeti yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…