Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Maelezo uliyo andika hapa yanaonesha shida kubwa ilikua ni ndani ya Soviet wenyewe na maelezo madogo sana yakimuhusisha USA(Soviet-Afghan war), lakini mwishoni unasema '' USA was a major contributor but not a reason for the collapse of USSR'', kwanini usiseme "USA was a minor contributor but not a reason for the collapse of USSR"...?? maelezo tafadhali mkuu
 
Huu uzi mzuri sana, umefanya watu tufikiri sana.
Hongera sana kwa kuchimba mkuu
 
Usisahau kuniita ukipata jibu, nimebwana kidogo hili wiki.
Baadae ntakuja kuchangia!
 
Mkuu hapo kumbuka Marekani ndio iliyokuwa kiongozi wa kambi ya magharibi (NATO) na hasimu mkuu wa USSR aliyeongoza mashariki (WARSAW) hivyo hakuwa mshindani mdogo na kuna mchango mwingi tu wa Marekani ambao wanahistoria wengi wameandika ambayo sijaiweka (Inahitaji ufatiliaji kidogo) mfano Maendeleo makubwa ya uchumi ya Marekani na washirika wake: Maendeleo haya ya kiuchumi yaliyoenda sambamba na maisha bora kwa raia wa nchi za magharibi yaliinadi na kuupa nguvu ubepari kama itikadi pekee yenye kuleta matokeo chanya kwa kila mtu na sio ushoshalisti. Kudhibiti kujipanua USSR ulimwengu wa tatu: hapa Marekani alihakikisha hii itikadi haisambai mfano hapa Africa huko Ángola akishirikiana na makaburu alimsaidia Savimbi kupambana na serikali ya kimarxi ya Angola iliyokuwa ikisaidiwa na majeshi ya Cuba na alifanya hivyo hata huko Amerika kusini. Kuongezeka utegemezi wa mafuta Marekani :kutokana na maendeleo makubwa ya kiuchumi Marekani pia nishati ya mafuta ilihitajika hivyo uzalishaji wa mafuta uliongezeka huko mashariki ya kati (Uarabuni) hivyo nchi hizo nyingi zilitajirika haraka kwa kuuza kwenye soko kubwa la Marekani na ili kulinda soko lao nyingi ziliamua kuikumbatia Marekani na kuitosa USSR na hata kusaidiana na Marekani kuipiga vita USSR. Zipo nyingi tu mkuu zinazoelezea mchango wa Marekani kuiangusha USSR.
 
Baazigar, wewe unajua kila kitu kuhusu kuanguka kwa mfumo wa kisoviet ila sema unataka kumchalenji Mkuu Proved,sasa mimi napendekeza wewe ongeza nyama kwenye komenti yake pale alipoungukiwa,ili watu tujifunze.natambua sana michango yako Mkuu Baazigar.
 

Hakika una ufahamu mkubwa sana wa issues za NATO na genge la wahuni la Putin
 
Ivi mtu akisema bila Putin tutegemee kuona Urusi dhaifu atakuwa yuko sahihi? Au Urusi ilivyo ni matokeo ya sera za Putin na kwa sasa hajaonekana wa kumrithi ndani ya Urusi ni sawa? Au Putin =Urusi?
Nile is Egypt and Egypt is Nile. Kama utakumbuka walimchukia baadae wakamhitaji. Putin ni mbabe mbele ya Marekani na hivyo wanaamini atawapigania Warusi wasinyanyasike na Marekani.
 
Ni kwa nini matajiri wengi wa Russia na China wanainvest wealth yao kule US na EU na sio kwao?
Ni kwa nini hupeleka watoto wao kupata elimu US na EU?
Kwanza ujue ni mbinu mojawapo ya upelelezi. Pili kupata taaluma inayoendana na mshindani wako. Tatu, vizazi vya warusi na wachina vinapoongezeka ndani ya USA na EU, vitasaidia sana kupooza uhasama baina yao. Itafikia wakati wataheshimiana. Yapo yaliyojficha lakini kwa nje haya yana maana.
 
Ni kwa nini matajiri wengi wa Russia na China wanainvest wealth yao kule US na EU na sio kwao?
Ni kwa nini hupeleka watoto wao kupata elimu US na EU?
Jibu ni rahisi sana:
1: Kwasababu fedha ya Marekani ndiyo inatumika dunia nzima kama utajiri wa akiba (Reserve Currency). Hivyo hata matajiri wa Uingereza na Ujerumani huwekeza kwa fedha ya Marekani na kwenye mabenki ya Marekani kwasababu yenyewe ndiyo yanasambaza fedha za Marekani.

2. Hili la watoto wengi wa Urusi kusoma Marekani halina usahihi mkubwa sana. Watoto wa Urusi wanasoma sana Ulaya hasahasa Uingereza. Wanaenda kusoma masomo ya Sanaa (Arts) kwasababu Sanaa ya Ulaya ndiyo ina ushawishi mkubwa duniani. Masomo ya Sayansi vyuo vya Urusi vina nguvu sana na vimetoa wanasayansi wengi waliowahi kupata tuzo za Nobel za Sayansi.
 

Nimehusisha both China na Russia.
Kumbuka China ndio inaongoza kwa wingi wa international students kule US.
Even Saudi and Japanese royal families send their kids to get college education in the US and EU. The same for the wealth and elite Russian, Indian and Chinese families
Ni kwa nini?
Tumeambiwa kuwa China na Russia zina mpango wa kuireplace US$$ as a global reserve currency na badala yake ziwe Russian Ruble na Chinese Yuan/Renminbi. (Something which only a drunkard sailor would agree) Kulikoni?
 
Russia has been a global power for a long while walijaribu mongols kuingusha wakafeli,akaja akafeli napoleon bonaparte na hitler naye akaangukia pua.
Real or “Trumped up?” Russian Legislator Boasts ‘S-700’ Air Defense Could ‘Shut Down’ the Planet
By
VT Senior Editors
-
October 25, 2018
1
1217


Ha ha haa! hii kitu naona Warussia watazalisha san hadi zifike S5500,HA HA HAA,na ninadhani hizi S300,400,500 Ni silaha hatari sana kwa kuzuia na kushambulia,wanajivunia sana Warussia.Hakuna ndegevita itakayoweza kuruka mbele ya S700,dah.
Vladimir Zhirinovsky, a Russian MP who has lead the nationalist Liberal Democratic Party (LDPR) since the 1990s, has let slip that Russia allegedly had “S-600” and “S-700” air defense systems


Utani mwingine bana lol!

“The Americans are scared in general, they are scared that the world’s best air defense system is Russia’s S-300. And we [also] have S-400, S-500, S-600, and S-700. We can shut down the whole planet, and no plane will [be able to] take off,” the MP joked.

Mzee anatamba huyu,hawajui wamarekani huyu,hebu msome na masihara yake

His statement prompted an explosion of laughter from another guest on the show and applause from the audience. The host played along with Zhirinovsky, cautioning him that he shouldn’t give away all secrets so as not to bring up the “dreaded S-1500 system.”

© Photo: YouTube/Sputnik
Special Delivery: WATCH New Video of Russian S-300 Deployment in Syria
The MP batted back the warning, claiming that the imaginary S-700 will “block everyone at the launch points for good, and this will be the last blow of the Russian counter-air defense system.”
The Russian military rolled out the S-400 Triumph defense system in 2007. The S-400 was created on the basis of the Russian S-300 air defense systems, but has significantly better performance capabilities in terms of effectiveness, coverage area, as well as variety of targets. Initially, the S-400 was named the S-300PM3 and it was intentionally designed to look like the S-300, so that the enemy could not recognize which system it was dealing with.
 

Marekani ni moja ya nchi bora kabisa kwenye suala za zima la Elimu hapa duniani. Vyuo vyake vina wasomi wakubwa wenye ushahiwishi duniani kwenye medani za taaluma. Wasomi wa dunia nzima wako Marekani. Asilimia 50% ya PhD za Marekani ni Foreign Born. The Green Card ni moja ya silaha za Marekani.

Lakini hoja yako ya pili ni mufilisi sana kwasababu imekaa kishabiki kuliko kitaalamu. Mtu yoyote makini hawezi kusema kwamba Russian Rubble inaweza kushindana na dola hata siku moja. Ila Chinese Renminbi inaweza kuiangusha kabisa fedha ya Marekani vizuri tu kama ambavyo fedha ya Uingereza iliangushwa na fedha ya Marekani. Kabla ya kukimbilia ushabiki ni vizuri ukasoma na kuelewa mlolongo wote wa kihistoria ambao ulifanya fedha ya Marekani kutawala duniani.

NB: Hembu labda uniambie ni kwanini unahisi fedha ya Marekani haiwezi kuangishwa ???
 
Putin na genge lake wanatumia rasilimali za umma kujiimarisha madarakani na kuwatisha mahasimu (Nato and Post Soviet states)
 

Naona tayari umeshafanya assumptions na kuniwekea maneno kinywani ambayo sijayaongea.
Nimeuliza maswali ili nijifunze na huo ushabiki unaousema sielewi umeutoa wapi!
Kuhusu mimi kuwa na hoja mufilisi - you are entitled to your own opinion so you can say whatever pleases you!
Anyways, thanks for clarifying kuwa Russian Ruble haiwezi kushindana na US$$ hata siku moja? Naomba ufafanue ni kwa nini?
Hoja yako ya kuwa Chinese Yuan huenda ikaireplace US$$ as a global reserve currency, naomba utujuze ni kwa nini Ruble ishindwe na Yuan iweze?
I’m not a monetary/economics expert ndio maana nimeuliza unielimishe kwa faida ya wote especially mtu kama mimi niliekimbia umande
Thanks
 
Putin na genge lake wanatumia rasilimali za umma kujiimarisha madarakani na kuwatisha mahasimu (Nato and Post Soviet states)
Vipi kama Putin na genge lake wangekua legelege,huoni kama Russia ingeshakua kama Afghanistan sa hizi,Maana yake Anko Sam angeshaweka serikali yake Moscow,
Hata huku kwetu Africa saa hizi vijana wa kiume wangekua wanachumbiwa tu kirahisi.Naamini ni heri Putin na genge lake wawepo duniani ili kuifanya dunia iwe sehemu salama kwa kuishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…