Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Mkuu kwa upande wangu kilichoiangusha USSR ilikuwa ni matatizo ya ndani sana sana mfano Kushindwa kwa sera za Gorbachev : Mwaka 1987 utawala wa raisi Gorbachev ulianzisha sera mbili ili kuinua uchumi wa kisovieti uliokua unasuasua sera hizo ni Perestroika (Hii sera ililenga kuinua uchumi wa kisovieti kwa kukumbatia baadhi ya nadharia za soko huria kama kuruhusu baadhi ya raia wenye uwezo kuendesha biashara bila udhibiti wa dola yaani kuruhusu biashara huria hii haikukidhi mahitaji na haikua endelevu hivyo ilishindwa baadae).Sera nyingine ni glasnost hii sera ilihusisha uwazi hii ni baada ya kuona raia wengi wa muungano hawapendezwi na usiri pamoja na udhibiti mkubwa wa uendeshaji wa muungano hivyo baada ya mambo yaliwekwa wazi ambapo raia walifahamu ukweli wa matatizo yalioukabili muungano kama mdororo wa kiuchumi, huduma mbovu za afya, rushwa na mengineyo hivyo kuzusha upinzani dhidi ya muungano, pia kuna sababu kama Mkwamo wa kiuchumi Kumbuka USSR ilikuwa kubwa kuliko hata baadhi ya mabara kama Ulaya, Amerika kaskazini na Amerika kusini hivyo ilikuwa ngumu kupanga maendeleo kulingana na vipaumbele hivyo yako maeneo yaliyo faidika sana huku mengine yakiachwa nyuma. Kukosekana kwa ugatuzi Madaraka yote yalikuwa huko Moscow na mataifa madogo ya muungano yaliminywa japo nayo pia yalichangia kodi ila hayakuwa na sauti). Ubaguzi wa kieneo (Baadhi ya nchi ndani ya muungano zilijiona bora na zenye hadhi ya kupendelewa kuliko nyingine hivyo mbegu ya chuki ilimea na kusababisha baadhi ya maeneo kutaka kujitawala ) na kwa upande wa Marekani huwezi kusema waliiangusha USSR ila tunasema walichangia anguko la USSR kupitia sera za rais Reagan kama Kuunga mkono Mujahidina waliokuwa wakipigana na majeshi ya soviet huko Afghanistan kisilaha, fedha huku Pakistan akitoa mafunzo kwa wapiganaji wa Mujahidina, Kidiplomasia (Utawala wa Reagan uliendesha kampeni kali kuitenga USSR kimataifa na hata kusababisha nchi nyingi kususia olympic iliyofanyika Moscow mwaka 1982 Kumbuka hata marehemu bondia Mohamed Ali alifika Tanzania na kenya kama sehemu ya kampeni hiyo na pia kuna sababu kama Mashindano ya uzalishaji silaha za nyuklia yaliyogharimu uchumi na pato la serikali ya Kisovieti hivyo kifupi tunasema "USA was a major contributor but not a reason for the collapse of USSR".
Maelezo uliyo andika hapa yanaonesha shida kubwa ilikua ni ndani ya Soviet wenyewe na maelezo madogo sana yakimuhusisha USA(Soviet-Afghan war), lakini mwishoni unasema '' USA was a major contributor but not a reason for the collapse of USSR'', kwanini usiseme "USA was a minor contributor but not a reason for the collapse of USSR"...?? maelezo tafadhali mkuu
 
Mkuu kwa upande wangu kilichoiangusha USSR ilikuwa ni matatizo ya ndani sana sana mfano Kushindwa kwa sera za Gorbachev : Mwaka 1987 utawala wa raisi Gorbachev ulianzisha sera mbili ili kuinua uchumi wa kisovieti uliokua unasuasua sera hizo ni Perestroika (Hii sera ililenga kuinua uchumi wa kisovieti kwa kukumbatia baadhi ya nadharia za soko huria kama kuruhusu baadhi ya raia wenye uwezo kuendesha biashara bila udhibiti wa dola yaani kuruhusu biashara huria hii haikukidhi mahitaji na haikua endelevu hivyo ilishindwa baadae).Sera nyingine ni glasnost hii sera ilihusisha uwazi hii ni baada ya kuona raia wengi wa muungano hawapendezwi na usiri pamoja na udhibiti mkubwa wa uendeshaji wa muungano hivyo baadhi ya mambo yaliwekwa wazi ambapo raia walifahamu ukweli wa matatizo yalioukabili muungano kama mdororo wa kiuchumi, huduma mbovu za afya, rushwa na mengineyo hivyo kuzusha upinzani dhidi ya muungano, pia kuna sababu kama Mkwamo wa kiuchumi Kumbuka USSR ilikuwa kubwa kuliko hata baadhi ya mabara kama Ulaya, Amerika kaskazini na Amerika kusini hivyo ilikuwa ngumu kupanga maendeleo kulingana na vipaumbele hivyo yako maeneo yaliyo faidika sana huku mengine yakiachwa nyuma. Kukosekana kwa ugatuzi Madaraka yote yalikuwa huko Moscow na mataifa madogo ya muungano yaliminywa japo nayo pia yalichangia kodi ila hayakuwa na sauti). Ubaguzi wa kieneo (Baadhi ya nchi ndani ya muungano zilijiona bora na zenye hadhi ya kupendelewa kuliko nyingine hivyo mbegu ya chuki ilimea na kusababisha baadhi ya maeneo kutaka kujitawala ) na kwa upande wa Marekani huwezi kusema waliiangusha USSR ila tunasema walichangia anguko la USSR kupitia sera za rais Reagan kama Kuunga mkono Mujahidina waliokuwa wakipigana na majeshi ya soviet huko Afghanistan kisilaha, fedha huku Pakistan akitoa mafunzo kwa wapiganaji wa Mujahidina, Kidiplomasia (Utawala wa Reagan uliendesha kampeni kali kuitenga USSR kimataifa na hata kusababisha nchi nyingi kususia olympic iliyofanyika Moscow mwaka 1982 Kumbuka hata marehemu bondia Mohamed Ali alifika Tanzania na kenya kama sehemu ya kampeni hiyo na pia kuna sababu kama Mashindano ya uzalishaji silaha za nyuklia yaliyogharimu uchumi na pato la serikali ya Kisovieti hivyo kifupi tunasema "USA was a major contributor but not a reason for the collapse of USSR".
Huu uzi mzuri sana, umefanya watu tufikiri sana.
Hongera sana kwa kuchimba mkuu
 
Maelezo uliyo andika hapa yanaonesha shida kubwa ilikua ni ndani ya Soviet wenyewe na maelezo madogo sana yakimuhusisha USA(Soviet-Afghan war), lakini mwishoni unasema '' USA was a major contributor but not a reason for the collapse of USSR'', kwanini usiseme "USA was a minor contributor but not a reason for the collapse of USSR"...?? maelezo tafadhali mkuu
Usisahau kuniita ukipata jibu, nimebwana kidogo hili wiki.
Baadae ntakuja kuchangia!
 
Maelezo uliyo andika hapa yanaonesha shida kubwa ilikua ni ndani ya Soviet wenyewe na maelezo madogo sana yakimuhusisha USA(Soviet-Afghan war), lakini mwishoni unasema '' USA was a major contributor but not a reason for the collapse of USSR'', kwanini usiseme "USA was a minor contributor but not a reason for the collapse of USSR"...?? maelezo tafadhali mkuu
Mkuu hapo kumbuka Marekani ndio iliyokuwa kiongozi wa kambi ya magharibi (NATO) na hasimu mkuu wa USSR aliyeongoza mashariki (WARSAW) hivyo hakuwa mshindani mdogo na kuna mchango mwingi tu wa Marekani ambao wanahistoria wengi wameandika ambayo sijaiweka (Inahitaji ufatiliaji kidogo) mfano Maendeleo makubwa ya uchumi ya Marekani na washirika wake: Maendeleo haya ya kiuchumi yaliyoenda sambamba na maisha bora kwa raia wa nchi za magharibi yaliinadi na kuupa nguvu ubepari kama itikadi pekee yenye kuleta matokeo chanya kwa kila mtu na sio ushoshalisti. Kudhibiti kujipanua USSR ulimwengu wa tatu: hapa Marekani alihakikisha hii itikadi haisambai mfano hapa Africa huko Ángola akishirikiana na makaburu alimsaidia Savimbi kupambana na serikali ya kimarxi ya Angola iliyokuwa ikisaidiwa na majeshi ya Cuba na alifanya hivyo hata huko Amerika kusini. Kuongezeka utegemezi wa mafuta Marekani :kutokana na maendeleo makubwa ya kiuchumi Marekani pia nishati ya mafuta ilihitajika hivyo uzalishaji wa mafuta uliongezeka huko mashariki ya kati (Uarabuni) hivyo nchi hizo nyingi zilitajirika haraka kwa kuuza kwenye soko kubwa la Marekani na ili kulinda soko lao nyingi ziliamua kuikumbatia Marekani na kuitosa USSR na hata kusaidiana na Marekani kuipiga vita USSR. Zipo nyingi tu mkuu zinazoelezea mchango wa Marekani kuiangusha USSR.
 
Maelezo uliyo andika hapa yanaonesha shida kubwa ilikua ni ndani ya Soviet wenyewe na maelezo madogo sana yakimuhusisha USA(Soviet-Afghan war), lakini mwishoni unasema '' USA was a major contributor but not a reason for the collapse of USSR'', kwanini usiseme "USA was a minor contributor but not a reason for the collapse of USSR"...?? maelezo tafadhali mkuu
Baazigar, wewe unajua kila kitu kuhusu kuanguka kwa mfumo wa kisoviet ila sema unataka kumchalenji Mkuu Proved,sasa mimi napendekeza wewe ongeza nyama kwenye komenti yake pale alipoungukiwa,ili watu tujifunze.natambua sana michango yako Mkuu Baazigar.
 
Usumbufu unaoletwa na Urusi ni sawa na ule wa kunguni au chawa tu kwa binadamu. Sababu za usumbufu huo ni tatu:

1. Urusi tofauti na USSR imegeuka kuwa "rogue state" isiyo na lengo kuu la kimfumo (strategic objective) zaidi ya kuwepo tu (mere survival/existence). USSR ilikuwa na lengo la kuigeuza dunia nzima kuwa ya kikomunisti kwa misingi la Marx/Lenin. Hiyo ilishindikana, USSR ikasambaratika na kupoteza ushawishi huo duniani kote. Leo hii Urusi inaongozwa na kikundi maslahi kilichokumbatia madaraka na kugawana fursa za kibepari kwa kubebana (cronyism & patronage). Ukomunisti ulishatupiliwa mbali; sasa ni ma-oligarchs tu yanayojuana na Kremlin. Kikundi hiki kinajua kabisa kuwa maslahi yake yanategemea Marekani na Ulaya. Huko ndiko kwenye uhakika wa uchumi wake. Leo hii nenda Central London utakuta wamiliki wakubwa wa ardhi na mali ni kutoka Urusi/Ukraine. Wamewekeza kweli huko Marekani na Ulaya. Hivyo kila wakati wanahangaika kuhakikisha watu rafiki (sympathetic) (Trump & co.) wanakuwa madarakani.

2. Muhimu sana hawa wahuni (akina Putin) wamerithi rasilimali nzito za kiteknologia ikiwa ni pamoja na za nyuklia, ardhi, maliasili na mifumo ya elimu ya hali ya juu toka USSR. Na hapo wanajitahidi sana kutoa upendeleo kwa watu wao wenye kuweza kuziendeleza rasilimali hizo ili wazitumia kupambana na Marekani na Ulaya. Kule kuwepo kwa miundombinu ya uhakika ya nyuklia na sayansi za anga ni kinga/tishio (deterrence) tosha kwa yeyote atakayefikiria kupambana na Urusi. Tena wakiwa "rogue state" hawajali hata kutoa mhanga idadi kubwa ya watu wao kwa maslahi ya kikundi tawala kilichopo Kremlin. Tofauti na Marekani na Ulaya ambao watu wao wana thamani kubwa sana, wanaojali maisha bora kwa kila mtu na kuna mifumo thabiti ya kusimamia haki za binadamu. Marekani wakijua wanapambana na "wehu" si rahisi kuwavamia Warusi huko Crimea, Syria na kwingineko bila kujihakikishia kutozuka vita ya nyuklia!

3. Marekani na Ulaya ni jamii zilizo wazi (open societies). Mambo yao ni hadharani. Marais wao wakifanya faulo wanapashwa hadharani. Wanachunguzwa hadharani (Robert Mueller on Russian collusion). Wateule wa Rais wanapigwa interview hadharani. n.k. Kwa urusi, hiyo ni sawa na kuanika nguo zao za ndani hadharani. Rais wao (Putin) ni sawa na mungu! Athari zake ni kuwa watu hatari wanapata mianya kibao ya kuendesha uhalifu Marekani na Ulaya. Warusi wanatumia fursa hiyo kujaribu kuhujumu nchi za jumuia ya NATO. Marekani na Ulaya wanalijua hilo lakini hawako tayari kujifungia ndani kama Urusi. badala yake wanajiimarisha kitaaluma kukabiliana na chokochoko za Urusi na wahuni wengine. Na kwa kweli wamefanikiwa. Karibu harakati zote za Warusi wanazijua. Kuna wakati wanajifanya hawana uhakika ili kuwaingiza kwenye mitego.

Akina Putin wanajua vizuri sana kwamba hawaiwezi Marekani na washirika wake wa Ulaya. Kwanza, huko ndiko wanakohifadhia utajiri wao wa kifisadi. Ndiko wanakosomeshea watoto wao na ndiko ambapo kila Mrusi aliyefanikiwa anaotea kuwa na makazi na kumiliki mali kama ilivyo kwa watu wengine wa dunia ya tatu. Kitu nachoamini ni kuwa Urusi wangekuwa na viongozi wenye maono ya hali ya juu, kwa uwezo na rasilimali walizo nazo, wangekuwa tishio sana kwa washirika wa NATO. Bahati mbaya, wanaongozwa na watu wenye tamaa ya mali, madaraka na sifa (ujiko) bila falsafa kuu ya taifa. Watu ambao wanategemea kubebwa na miundombinu iliyowekwa na USSR ambayo sujui kama wataweza kuiimarisha ishindane na ya magharibi huko mbeleni.

Hakika una ufahamu mkubwa sana wa issues za NATO na genge la wahuni la Putin
 
Ivi mtu akisema bila Putin tutegemee kuona Urusi dhaifu atakuwa yuko sahihi? Au Urusi ilivyo ni matokeo ya sera za Putin na kwa sasa hajaonekana wa kumrithi ndani ya Urusi ni sawa? Au Putin =Urusi?
Nile is Egypt and Egypt is Nile. Kama utakumbuka walimchukia baadae wakamhitaji. Putin ni mbabe mbele ya Marekani na hivyo wanaamini atawapigania Warusi wasinyanyasike na Marekani.
 
Ni kwa nini matajiri wengi wa Russia na China wanainvest wealth yao kule US na EU na sio kwao?
Ni kwa nini hupeleka watoto wao kupata elimu US na EU?
Kwanza ujue ni mbinu mojawapo ya upelelezi. Pili kupata taaluma inayoendana na mshindani wako. Tatu, vizazi vya warusi na wachina vinapoongezeka ndani ya USA na EU, vitasaidia sana kupooza uhasama baina yao. Itafikia wakati wataheshimiana. Yapo yaliyojficha lakini kwa nje haya yana maana.
 
Ni kwa nini matajiri wengi wa Russia na China wanainvest wealth yao kule US na EU na sio kwao?
Ni kwa nini hupeleka watoto wao kupata elimu US na EU?
Jibu ni rahisi sana:
1: Kwasababu fedha ya Marekani ndiyo inatumika dunia nzima kama utajiri wa akiba (Reserve Currency). Hivyo hata matajiri wa Uingereza na Ujerumani huwekeza kwa fedha ya Marekani na kwenye mabenki ya Marekani kwasababu yenyewe ndiyo yanasambaza fedha za Marekani.

2. Hili la watoto wengi wa Urusi kusoma Marekani halina usahihi mkubwa sana. Watoto wa Urusi wanasoma sana Ulaya hasahasa Uingereza. Wanaenda kusoma masomo ya Sanaa (Arts) kwasababu Sanaa ya Ulaya ndiyo ina ushawishi mkubwa duniani. Masomo ya Sayansi vyuo vya Urusi vina nguvu sana na vimetoa wanasayansi wengi waliowahi kupata tuzo za Nobel za Sayansi.
 
Nimehusisha both China na Russia.
Kumbuka China ndio inaongoza kwa wingi wa international students kule US.
Even Saudi and Japanese royal families send their kids to get college education in the US and EU. The same for the wealth and elite Russian, Indian and Chinese families
Ni kwa nini?
Tumeambiwa kuwa China na Russia zina mpango wa kuireplace US$$ as a global reserve currency na badala yake ziwe Russian Ruble na Chinese Yuan/Renminbi. (Something which only a drunkard sailor would agree) Kulikoni?
 
Russia has been a global power for a long while walijaribu mongols kuingusha wakafeli,akaja akafeli napoleon bonaparte na hitler naye akaangukia pua.
Real or “Trumped up?” Russian Legislator Boasts ‘S-700’ Air Defense Could ‘Shut Down’ the Planet
By
VT Senior Editors
-
October 25, 2018
1
1217
hqdefault.jpg

Ha ha haa! hii kitu naona Warussia watazalisha san hadi zifike S5500,HA HA HAA,na ninadhani hizi S300,400,500 Ni silaha hatari sana kwa kuzuia na kushambulia,wanajivunia sana Warussia.Hakuna ndegevita itakayoweza kuruka mbele ya S700,dah.
Vladimir Zhirinovsky, a Russian MP who has lead the nationalist Liberal Democratic Party (LDPR) since the 1990s, has let slip that Russia allegedly had “S-600” and “S-700” air defense systems

Utani mwingine bana lol!

“The Americans are scared in general, they are scared that the world’s best air defense system is Russia’s S-300. And we [also] have S-400, S-500, S-600, and S-700. We can shut down the whole planet, and no plane will [be able to] take off,” the MP joked.

Mzee anatamba huyu,hawajui wamarekani huyu,hebu msome na masihara yake

His statement prompted an explosion of laughter from another guest on the show and applause from the audience. The host played along with Zhirinovsky, cautioning him that he shouldn’t give away all secrets so as not to bring up the “dreaded S-1500 system.”
1068622625.jpg

© Photo: YouTube/Sputnik
Special Delivery: WATCH New Video of Russian S-300 Deployment in Syria
The MP batted back the warning, claiming that the imaginary S-700 will “block everyone at the launch points for good, and this will be the last blow of the Russian counter-air defense system.”
The Russian military rolled out the S-400 Triumph defense system in 2007. The S-400 was created on the basis of the Russian S-300 air defense systems, but has significantly better performance capabilities in terms of effectiveness, coverage area, as well as variety of targets. Initially, the S-400 was named the S-300PM3 and it was intentionally designed to look like the S-300, so that the enemy could not recognize which system it was dealing with.
 
Nimehusisha both China na Russia.
Kumbuka China ndio inaongoza kwa wingi wa international students kule US.
Ni kwa nini?
Tumeambiwa kuwa China na Russia zina mpango wa kuireplace US$$ as a global reserve currency na badala yake ziwe Russian Ruble na Chinese Yuan/Renminbi. (Something which only a drunkard sailor would agree) Kulikoni?

Marekani ni moja ya nchi bora kabisa kwenye suala za zima la Elimu hapa duniani. Vyuo vyake vina wasomi wakubwa wenye ushahiwishi duniani kwenye medani za taaluma. Wasomi wa dunia nzima wako Marekani. Asilimia 50% ya PhD za Marekani ni Foreign Born. The Green Card ni moja ya silaha za Marekani.

Lakini hoja yako ya pili ni mufilisi sana kwasababu imekaa kishabiki kuliko kitaalamu. Mtu yoyote makini hawezi kusema kwamba Russian Rubble inaweza kushindana na dola hata siku moja. Ila Chinese Renminbi inaweza kuiangusha kabisa fedha ya Marekani vizuri tu kama ambavyo fedha ya Uingereza iliangushwa na fedha ya Marekani. Kabla ya kukimbilia ushabiki ni vizuri ukasoma na kuelewa mlolongo wote wa kihistoria ambao ulifanya fedha ya Marekani kutawala duniani.

NB: Hembu labda uniambie ni kwanini unahisi fedha ya Marekani haiwezi kuangishwa ???
 
Real or “Trumped up?” Russian Legislator Boasts ‘S-700’ Air Defense Could ‘Shut Down’ the Planet
By
VT Senior Editors
-
October 25, 2018
1
1217
hqdefault.jpg

Ha ha haa! hii kitu naona Warussia watazalisha san hadi zifike S5500,HA HA HAA,na ninadhani hizi S300,400,500 Ni silaha hatari sana kwa kuzuia na kushambulia,wanajivunia sana Warussia.Hakuna ndegevita itakayoweza kuruka mbele ya S700,dah.
Vladimir Zhirinovsky, a Russian MP who has lead the nationalist Liberal Democratic Party (LDPR) since the 1990s, has let slip that Russia allegedly had “S-600” and “S-700” air defense systems
Putin na genge lake wanatumia rasilimali za umma kujiimarisha madarakani na kuwatisha mahasimu (Nato and Post Soviet states)
 
Marekani ni moja ya nchi bora kabisa kwenye suala za zima la Elimu hapa duniani. Vyuo vyake vina wasomi wakubwa wenye ushahiwishi duniani kwenye medani za taaluma. Wasomi wa dunia nzima wako Marekani. Asilimia 50% ya PhD za Marekani ni Foreign Born. The Green Card ni moja ya silaha za Marekani.

Lakini hoja yako ya pili ni mufilisi sana kwasababu imekaa kishabiki kuliko kitaalamu. Mtu yoyote makini hawezi kusema kwamba Russian Rubble inaweza kushindana na dola hata siku moja. Ila Chinese Renminbi inaweza kuiangusha kabisa fedha ya Marekani kama ambavyo fedha ya Uingereza iliangushwa na fedha ya Marekani. Labda uniambie ni kwanini unahisi fedha ya Marekani haiwezi kuangishwa (Naomba jibu la kitaalamu)

Naona tayari umeshafanya assumptions na kuniwekea maneno kinywani ambayo sijayaongea.
Nimeuliza maswali ili nijifunze na huo ushabiki unaousema sielewi umeutoa wapi!
Kuhusu mimi kuwa na hoja mufilisi - you are entitled to your own opinion so you can say whatever pleases you!
Anyways, thanks for clarifying kuwa Russian Ruble haiwezi kushindana na US$$ hata siku moja? Naomba ufafanue ni kwa nini?
Hoja yako ya kuwa Chinese Yuan huenda ikaireplace US$$ as a global reserve currency, naomba utujuze ni kwa nini Ruble ishindwe na Yuan iweze?
I’m not a monetary/economics expert ndio maana nimeuliza unielimishe kwa faida ya wote especially mtu kama mimi niliekimbia umande
Thanks
 
Putin na genge lake wanatumia rasilimali za umma kujiimarisha madarakani na kuwatisha mahasimu (Nato and Post Soviet states)
Vipi kama Putin na genge lake wangekua legelege,huoni kama Russia ingeshakua kama Afghanistan sa hizi,Maana yake Anko Sam angeshaweka serikali yake Moscow,
Hata huku kwetu Africa saa hizi vijana wa kiume wangekua wanachumbiwa tu kirahisi.Naamini ni heri Putin na genge lake wawepo duniani ili kuifanya dunia iwe sehemu salama kwa kuishi.
 
Back
Top Bottom