ROBERT MICHAEL
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 5,054
- 2,858
Mkuu asante sana kwa hiyi reply yako na huwa napenda sana kujadiliana na watu ambao kichwani wapo sawa,na wewe upo sawa haswa.Ukwe;i ni kwamba nchi za magharibi zinachagua nani wa kumuwekea vikwazo na nani wa kumuachia huru kulingana na matakwa yao wenyewe.Kwa mfano China hakuna demokrasia na ukiinua kichwa wanakutwanga(Tianmanen square masacre 1989,sijui wewe ulikuwa wapi). Na hawakuwekewa vikwazo ambavyo ni nail biting. Western countries ndo sababu kubwa sana ya china kuendelea. Ingawa China ipo number 2 lakini living standard average chinese ipo way below Japanese. Kwa kiasi fulani nakubaliana na wewe kuwa demokrasia(kama inavyokuwa defined na western countries) sio kichocheo cha maendeleo.Kuna mifano mingi ya nchi ambazo hazina demokrasia( As defined by western countries) lakini zimeendelea,kwa mfano China,Saudi Arabia,Qatar etc etc.Lakini ukichukua data na kuangalia nchi tajiri na wananchi wana maisha mazuri zaidi unaona nchi gani zinakuwa nyingi ? Zenye Democrasia au zisizo na Demokrasia ?NawasilishaNi kweli Korea kaskazini na Korea kusini ni nchi ambazo zipo eneo moja kijiografia lakini huwezi kuzifananisha kimaendeleo kwa muktadha wako,
Korea kaskazini na Korea kusini
ni kama mabondia wawili wanaopigna lakini mmoja kafungwa mikono ambaye ni Korea kaskazini na mwingine hajafungwa ambaye ni Korea kusini hawawezi kuwa na usawa katika kupigana
Ni kwamba huwezi kufananisha nchi iliyowekewa vikwazo na nchi yenye biashara huru
Halafu demokrasia ni mfumo tu sio nguzo au kisababishi cha kuleta maendeleo, japo demokrasia ni muhimu haswa kwa nchi kama yetu
Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa kabisa mkuu na ahsante kwa hoja yako nzuri iliyokaa sana kisomi.
Hebu sasa tupitie huo mfano wako wa usumbufu wa kunguni au chawa kwa binadamu katika hoja zako tatu.
Urusi kuwa Rogue State na kutokuwa na lengo kuu kimfumo hebu tuliangalie kiundani zaidi. Urusi anaitwa Rogue State kwasababu anavunja sheria kimataifa (International Law) pamoja na tamaduni zake ambazo ziliwekwa na mataifa yaliyoshinda vita ya pili ya dunia kule San Fransisco mwaka 1945. Amevamia Ukraine na kumega Crimea kosa ambalo ni kinyume kabisa na sheria za dunia yetu. Lakini sasa kama Urusi anaitwa Rogue State kwa kuvamia Ukraine mwaka 2014, Marekani aliyevamia Yugoslavia mwaka 1999, Afghanistan mwaka 2001 na Iraq mwaka 2003 bila ruhusa ya Baraza la Ulinzi la Umoja wa mataifa tumwiteje sasa ??? Rogue State au Benign Hegemony ??? (Nijuavyo sheria inakata kote kote)
Sijaitoa Marekani kwa vitendo vya kuwa rogue state. Lakini Marekani ina mfumo unaowezesha wananchi wake kujadili na "kuhukumu" watawala wao kwa maamuzi ya kihuni. Kwa mfano, rejea upinzani mkubwa wa ndani uliojitokeza kwenye vita za Vietnam na Iraq. Urusi iwe enzi za USSR au Russia Federation, hakuna mtu mwenye ubavu wa kuiuliza serikali kitu. It's always been a totalitarian state.
Pia nifahamuvyo mimi, kuachana na falsafa ya fulani hakukufanyi kuwa umekosa lengo kuu kimfumo. Maana ukiangalia kwa mapana hata Uchina aliachana na International Communist Enterprise na akajikitika katika masoko ya kujenga uchumi wake (Economic Pragmatism). Mwaka 2015 Urusi alitoa chapisho lake la mwelekeo na melengo makuu ya nchi (The National Security Strategy) ambapo aliainisha kila kitu wanachotarajia kukifanya kwa muongo ujao. Hapa utasemaje anatafuta kuwepo tu bila mkakati maalum ??? Au unaamini kwamba tokea mwaka 1999 baada ya Yeltsin kuachia madaraka Urusi imefika hapa kwa bahati nasibu au miujiza tu ??? (Kama umesoma Planning and Development naamini utakuwa umenielewa vizuri)
China wana mkakati kamili wa kuwa world economi and strategic power na wamejijengea nidhamu ya kimfumo kuelekea huko japo binafsi sipatani kabisa na totalitarian states. Urusi kiasi kikubwa inafanana na mafia state.
Umezungumzia kwamba Urusi ni Rogue State na iko radhi kuuwa watu wake kwa ajili ya kikindi cha watu wachache. Hebu nikuulize swali la kihostoria ambalo naamini ni rahisi sana tu: Hivi kati ya Urusi ya Kisovieti (USSR) na Urusi hii ya Putin ipi imeua watu wake sana na kukanyaga haki za binadamu ??? Ipi ni sehemu bora zaidi ya kuishi ??
Totalitarian states zote ziwe za kikomunisti au kibepari hazijali kabisa uhai na haki za binadamu. Zote zinaongozwa na vikundi iwe ni "party vanguards", juntas, oligarchs na "ruling cliques" za aina zote, vyenye tabia ya kutumia binadamu wenzao kama poni (pawns) katika kutimiza maslahi yao. Inapokuja suala la uhai na haki za binadamu huwa sipimi kwa idadi ya waliouwawa. It's all tragic! Kwa hapo, USSR na Russian Federation kwangu mimi ni walewale.
Katika hili nalo nakubaliana na wewe kidogo, lakini bado napata swali jingine gumu la kukuuliza. India ni jamii wazi na ndiyo nchi kubwa ya kidemokrasia hapa duniani (World Largest Democracy) lakini mbona bado kuna kiwango kikubwa sana cha rushwa na uhalifu ni mwingi kuliko hata Uchina ambako kumefungwa (Closed Society) ??? Kubwa zaidi Uchina imepiga hatua kwenye kila kitu kuliko India. Hapa tatizo liko wapi ??? Je, tukiruhusu demokrasia ndiyo tutakuwa tumeruhusu maendeleo ??? (Tafadhali angalia hii mifano vizuri kabla ya kujibu)
MALCOM LUMUMBANATO kwa pamoja wana idadi ya watu milioni 603.73.
URUSI peka yake ana idadi ya watu milioni 144.3.
NB: NATO ina watu mara sita zaidi ya Urusi lakini kwanini iwasumbue ??
Mzeee huyo sio dhaifu bado wapo vizur sana kijeshi na technology japo ni kweli uchumi waliyumba lakin bado wanamiliki eneo kubwa zaid kwenye nchi yao ile ya awaliUmoja wa Kisovieti (USSR au CCCP) taifa lililozaliwa mwaka 1914-1991,
Lilikuwa ni moja ya taifa lenye nguvu sana duniani lakini lenye mwisho mbaya sana ambao ni aibu kwa watu wake mpaka leo. Kiuchumi walikuwa wana nguvu sana, kiteknolojia walikuwa mbele, nguvu kubwa ya viwanda, kijeshi walikuwa mbele na mifumo yao ya kitamaduni iliyotokana na ukomunisti ilishawishi dunia kuanzia barani Marekani, Asia hadi Afrika na kubwa ziadi walikuwa na idadi kubwa sana ya watu ambapo takwimu zinasema kwamba walikuwa ni milioni 293.
Lakini baada ya kusambaratika nchi hii ilipoteza kila kitu ambacho ilikuwa nacho kuanzia Idadi ya watu, jeshi, viwanda na teknolojia maana kila nchi iliondoka na watu wake, majeshi yake na sehemu kama Ukraine ikapata viwanda vya bure kabisa, Poland na Georgia nao hawakuwa nyuma kabisa. Ikawa nchi dhaifu na masikini kweli....
Sasa najiuliza kwanini taifa hili dhaifu ambalo lililoshindwa vita baridi linaendelea kumsumbua Marekani (The Only Super Power) pamoja na washirika wake kijeshi ambao ni zaidi ya 25 ???
CC: chige , FisadiKuu
Wewe umetumwa nn?KISIASA
1. Amesababisha sintofahamu kubwa ndani ya siasa za Marekani hasa kwa Donald Trump.
2. Anavuruga mipango ya Marekani kwa kutumia VETO kule Umoja wa Mataifa.
3. Amefanikiwa kuugawanya Umoja wa Ulaya (Schoeder wa Ujerumani anafanya kazi Rosneft)
4. Anaisaidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Alimsaidia Raisi wa Uturuki asipinduliwe na kuuwawa ambapo inasemekana CIA walihusika sana.
6. Amemtunza Edward Snowden ambaye kavujisha siri nyeti za Marekani.
KIJESHI
1. Kavamia Ukraine kijeshi na kumega Crimea kwa nguvu mno ya wanajeshi 70,000.
2. Kavuruga mpango wa Marekani na Israel wa kuvamia Syria na kumtoa Assad.
3. Anauza silaha nzito kwa mataifa hasimu wa Marekani kama Iran.
4. Anasidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Amevuruga majimbo ya Lugansk na Donestky hadi leo majeshi ya Ukraine hayana amani.
7. Yeye ndiyo mwenye jeshi la pili kwa ubora hapa duniani mbali na shida zote kiuchumi.
KITEKNOLOJIA
1. Marekani mpaka leo anategemea injini kutoka Urusi kwa ajili ya kurusha roketi zake.
2. Ametengeneza makombora mazito ambayo yanasafiri mara 10 zaidi ya sauti.
3. Walimwekea vikwazo vya injini za ndege kutoka Ukraine lakini katengeneza zake kwa haraka sana.
4. Ana wasomi wa sayansi ambao ni World Class kama 1,000,000 hivi.
5. Teknolojia ya kimtandao (Cyber Technology) yuko mbele sana na amethibitishia dunia mara nyingi.
KIUCHUMI
1. Amefanikiwa kutumia makampuni yake ya nishati kuwaumiza Ulaya hasa NORD Stream 2.
2. Amefanikiwa kutumia ushawishi wa nishati kuyavuta karibu mataifa kama Uchina, India na Uturuki.
3. Uturuki ameagiza silaha kutoka Urusi kitu ambacho kitampa faida za kiuchumi Mrusi.
4. Saudi Arabia ametengeneza viwanda vya Kalashnikov Ak-47 nchini kwake na Urusi karuhusu.
5. Amesaidia kutengeneza vyombo kama BRICS, The Shanghai Cooperation na Eurasia Economic Union
NB: Haya ni machache tu, sasa nchi iliyosambaratika inalisumbuaje taifa kubwa duniani ??
Naondoa hoja baada ya kuufatilia uziMALCOM LUMUMBA
NAONA NDUGU UNAYATUMIA VIBAYA MAJINA YA WANAZUONI WAKUBWA DUNIA HII
TAYARI HAPO AWALI UMESHATAJA NGUVU ALIZONAZO MRUSI,HALAFU BADO UNAJIULIZA KWA NN ANAMSUMBUA MMAREKANI
JE HUONI KUWA HIZO NGUVU MRUSI ALIZONAZO KUWA NDIZO ANAZOZITUMIA KUMCHACHAFYA MUAMERIKA?
Sent using Jamii Forums mobile app
Vita yoyote sio NGUVU, ni AKILI.NATO kwa pamoja wana idadi ya watu milioni 603.73.
URUSI peka yake ana idadi ya watu milioni 144.3.
NB: NATO ina watu mara sita zaidi ya Urusi lakini kwanini iwasumbue ??
jf ya namna hii bado ipo ". inategemea namuhusika wapenda kutembelea majukwaa yapi ""??Nilimiss Jf ya aina hii. Nimesoma comments zote na ni kama nimesoma Kitabu cha historia adimu.... Ahsante sana ndugu Lumumba na wengine
hatari sana huyu kiumbeMalcom Lumumba,you are the best when it comes to world history!
Asante sana.
Hoja nzuri sana hii,Mkuu MLUmoja wa Kisovieti (USSR au CCCP) taifa lililozaliwa mwaka 1914-1991,
Lilikuwa ni moja ya taifa lenye nguvu sana duniani lakini lenye mwisho mbaya sana ambao ni aibu kwa watu wake mpaka leo. Kiuchumi walikuwa wana nguvu sana, kiteknolojia walikuwa mbele, nguvu kubwa ya viwanda, kijeshi walikuwa mbele na mifumo yao ya kitamaduni iliyotokana na ukomunisti ilishawishi dunia kuanzia barani Marekani, Asia hadi Afrika na kubwa ziadi walikuwa na idadi kubwa sana ya watu ambapo takwimu zinasema kwamba walikuwa ni milioni 293.
Lakini baada ya kusambaratika nchi hii ilipoteza kila kitu ambacho ilikuwa nacho kuanzia Idadi ya watu, jeshi, viwanda na teknolojia maana kila nchi iliondoka na watu wake, majeshi yake na sehemu kama Ukraine ikapata viwanda vya bure kabisa, Poland na Georgia nao hawakuwa nyuma kabisa. Ikawa nchi dhaifu na masikini kweli....
Sasa najiuliza kwanini taifa hili dhaifu ambalo lililoshindwa vita baridi linaendelea kumsumbua Marekani (The Only Super Power) pamoja na washirika wake kijeshi ambao ni zaidi ya 25 ???
CC: chige , FisadiKuu
USA,ndio nchi inayopokea misaada ya kijeshi kiulinzi na kijasusi Duniani kuliko nchi yeyote ili kuikabili Russiah Federation (RF)NATO kwa pamoja wana idadi ya watu milioni 603.73.
URUSI peka yake ana idadi ya watu milioni 144.3.
NB: NATO ina watu mara sita zaidi ya Urusi lakini kwanini iwasumbue ??
UNAJUA MAANA YA VITA BARIDI???Ahsante sana mkuu,
Sasa kama Urusi alikuwa na nguvu nyingi zaidi ya hizi za leo kwanini alishindwa Vita Baridi ??
Katika mantiki hii unataka kuniambia kwamba Urusi ya zamani ilikuwa na nguvu kuliko Marekani ??
Kumbe majibu unayo alafu unauliza maswali jamaniKISIASA
1. Amesababisha sintofahamu kubwa ndani ya siasa za Marekani hasa kwa Donald Trump.
2. Anavuruga mipango ya Marekani kwa kutumia VETO kule Umoja wa Mataifa.
3. Amefanikiwa kuugawanya Umoja wa Ulaya (Schoeder wa Ujerumani anafanya kazi Rosneft)
4. Anaisaidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Alimsaidia Raisi wa Uturuki asipinduliwe na kuuwawa ambapo inasemekana CIA walihusika sana.
6. Amemtunza Edward Snowden ambaye kavujisha siri nyeti za Marekani.
KIJESHI
1. Kavamia Ukraine kijeshi na kumega Crimea kwa nguvu mno ya wanajeshi 70,000.
2. Kavuruga mpango wa Marekani na Israel wa kuvamia Syria na kumtoa Assad.
3. Anauza silaha nzito kwa mataifa hasimu wa Marekani kama Iran.
4. Anasidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
5. Amevuruga majimbo ya Lugansk na Donestky hadi leo majeshi ya Ukraine hayana amani.
7. Yeye ndiyo mwenye jeshi la pili kwa ubora hapa duniani mbali na shida zote kiuchumi.
KITEKNOLOJIA
1. Marekani mpaka leo anategemea injini kutoka Urusi kwa ajili ya kurusha roketi zake.
2. Ametengeneza makombora mazito ambayo yanasafiri mara 10 zaidi ya sauti.
3. Walimwekea vikwazo vya injini za ndege kutoka Ukraine lakini katengeneza zake kwa haraka sana.
4. Ana wasomi wa sayansi ambao ni World Class kama 1,000,000 hivi.
5. Teknolojia ya kimtandao (Cyber Technology) yuko mbele sana na amethibitishia dunia mara nyingi.
KIUCHUMI
1. Amefanikiwa kutumia makampuni yake ya nishati kuwaumiza Ulaya hasa NORD Stream 2.
2. Amefanikiwa kutumia ushawishi wa nishati kuyavuta karibu mataifa kama Uchina, India na Uturuki.
3. Uturuki ameagiza silaha kutoka Urusi kitu ambacho kitampa faida za kiuchumi Mrusi.
4. Saudi Arabia ametengeneza viwanda vya Kalashnikov Ak-47 nchini kwake na Urusi karuhusu.
5. Amesaidia kutengeneza vyombo kama BRICS, The Shanghai Cooperation na Eurasia Economic Union
NB: Haya ni machache tu, sasa nchi iliyosambaratika inalisumbuaje taifa kubwa duniani ??
Ushawahi kushiriki mijadala kabla, lazima kuwe na mtu wa kuchokoza mjadala.
Eneo ambalo urusi litamsumbua sana kuweza kumfikia Marekani ni Propaganda, Intelligency na Millitari/War strategies.Ahsante sana mkuu,
Sasa kama Urusi alikuwa na nguvu nyingi zaidi ya hizi za leo kwanini alishindwa Vita Baridi ??
Katika mantiki hii unataka kuniambia kwamba Urusi ya zamani ilikuwa na nguvu kuliko Marekani ??