Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Hivi kiongpzi hiyo IDLIB huko syria sio ndio marekani kaweka base ya wanajeshi kwa madai kuwa wanapambana na Magaidi
 
Mkuu GRU unaweza wafananisha na CIA!?.. Fine, kwenye Millitary/War Strategies marekani ubora wake upo wapi zaidi ya Russia!?..
Propaganda nakubaliana nawe!..
Mkuu pitia tena comment yangu kwa utulivu.
Katika millitary/war strategy Russia yupo vizuri sana lakini ili aweze ku last longer anahitaji financial power and stability. Hapo ndipo Marekani anapompiga tobo Russia
 
UNAJUA MAANA YA VITA BARIDI???
ndio maana yake

marekeni ilihitaji kujiunga na mataifa ya Ulaya yenye nguvu ili kushindana na USSR. Na kwa taarifa yako USA haijawahi kupigana vita peke yake ikashinda. inapenda kushirikisha washirika wake wa ulaya ili kuongeza nguvu na kupunguza gharama/madhara ya vita.
 
Kuwa na bajeti kubwa ya kijeshi haimaanishi na ubora wa jeshi utakuwa juu
Urusi kapitwa sana kibajeti kwenye jeshi na USA lakini naona hawajaachana pakubwa
Kwenye jeshi ni kuhakikisha mipango yenu inaenda sawa katika kujua mbinu za adui dhidi yenu na kujua namna ya kumdhibiti
 
Lakini hiyo mipango nayo inahitaji bajeti
 
safi sana mkuu.
 
mkuu vipaji vya kuokota ni tofauti ya vipaji asilia,halafu siku ukisikia amerika kasambaratika ni ile hali ya kukusanya madodoki na makila kitu wakati utahukumu.
 
Tuko pamoja kabisa Comrade...
mkuu malcom mimi sio mzoefu lakini nahisi na kuamini kwamba urusi ni hatari sana hata sasa,sio nchi ya kuchezea chezea,kwa muktadha wa utajiri na kilichomo katika hiyo nchi basi ni watu hatari sana na au siku moja falme yao itawarejea,natamani kuwaita jeshi la kweli la mungu kwa wale wanaomwamini.Huangusha na kusumbua kila nguvu itawalayo na huogopwa sana.nahisi kuna la ziada.
 
dah mkuu nyote kwa umoja wenu mbarikiwe sana,tunawafuatili na kuwafurahia sana,asanteni sana kwa niaba ya wenye shukrani.
 
Ahsante sana mkuu. Lakini naomba nikuulize swali la msingi kutoka kwenye hoja yako: Mbona Urusi ya Kisovieti ilikuwa na Gesi, Mafuta, Chuma pamoja na Teknolojia kubwa sana lakini bado ikaanguka baada ya Uchumi wake kudorora?
kuna nadharia kuwa CCCP ilianguka kwasababu baadhi ya warusi waliona kuwa CCCP na sera za kikomunisti zimeua tamaduni za Russia (mf. Orthodox church) na pia ilitumia nguvu nyingi kueneza itikadi kwenye nchi nyingine badala ya kutumia rasilimali zao kuiendeleza Russia. Ukimsililiza Putin utaona mara moja moja anaongelea hayo. Kwa hiyo kuanguka kwa CCCP kunaweza kuwa ni mpango uliopangwa na kitengo ndani ya KGB.
 

1. Lakini sasa mbona leo hii Kremlin inahangaika sana kujaribu kuziweka jirani nchi zile zilizojitoa kwenye muungano wakati KGB na Politburo ya CPSU ndiyo iliamua kuua muungano wao ???

2. Hao KGB walivyokuwa wanavunja muungano hawakutabiri kwamba kutakuwa na madhara makubwa sana kiulinzi huko mbeleni ???

NB: Basi kama KGB walifanya hivyo nadhani kuna hatihati siku watafanya tena wakichoka.....
 
Kuna uwezekano kuwa vita ya Afghanistan na vita baridi vilidhoofisha sana uchumi kiasi kwamba nchi yao ingeweza hata kuvamiwa ilibidi "wazee" wafanye "bluff" kabla mambo hayajaharibika zaidi.

Katika kufanya hivyo wakaona wavunje muungano na kumuweka mlevi (Yeltsin) ili kuudanganya ulimwengu kuwa wao sio watu wakuchukuliwa 'serious' huku teyari wakiwa na mtu wao (Putin) au wewe unasemaje kuhusu maneno haya ya Sun Tzu "All warfare is based on deception."
 
Haya maneno aliyasema Anotoliy Golitstyn kwenye vitabu vyake vya The Perostroika Deception na New Lies for the old. Kuna kipindi nilimsoma sana nikaja kugundua kuna mambo mengi sana ya uongo wanayasema.

Russia bila hata kwenda Afghanistan ilikuwa ni lazima ianguke tu. Mtafute mtu anaitwa Prof Emmanuel Todd ni mfaransa, wakati ana miaka 26 alitabiri anguko la USSR tena kipindi hicho ndiyo wanaongoza kwenye teknolojia kubwa kama Satellite, Makombora na Silaha lakini alichekwa hadi na Wamarekani.

Alisema kwamba kwa mfumo wa Uchumi wa Kikomunisti lazima Urusi itaanguka tu. Miaka kama 30 baadae asilimia 75% ya aliyoyasema yalitokea na siyo tu Urusi. Lakini nchi karibia zote za kijamaa ziliangukia pua ikiwemo Tanzania yetu. Uchina aligundua mapema mchezo, akaruhusu mfumo wa masoko na uwekezaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…