USSR kweli ilimeguka na kudondoka, lakini tusisahau kuwa USSR ilibebwa na mambo yote yaliratibiwa huko Russia, hivyo hata baada ya kuvunjika Russia ilibaki na mambo yote,si kwamba ilisambaratika kabisa kama tunavyoona ila bali bado vyombo vyake viliwndelea kufanya kazi,warusi ni watu ambao sisi tunaona kama wazungu lakini wao wako tofauti kabisa na wazungu.wakati ulaya na marekani walikuwa wanaamini russia imekufa lakini rusia yenyewe ilikuwa inahangaika kuhakikisha inanyanyuka, ndo hapo alipokuja kutokea mtu kama Putin, putin kainyanyua russia muda mfupi sana,si kwasababu ana miujiza ila ni kwasababu walikuwa na kila kitu kasoro kiongozi tu wa kusimamia kukua kwa uchumi wa russia.
Kwanini NATO wanaihofia Russia?
Kwanza warusi ni watu wenye akili nyingi sana, hakuna kitu wanaweza panga wasishindwe kufanya, hivyo kwenye nyanja ya rasilimali watu ipo vizuri ina wasomi wa kutosha na wabunifu kwenye sekta zote kuanzia za ulinzi afya, na technolojia nyingine, kwahiyo NATO inawaogopa kwasababu wana uwezo wa kufanya chochote kwa akili na elimu zao walizonazo.
Wana technolojia, hapo nimekueleza kuwa wana akili na ni wasomi, sasa hivi vyote inawafanya wawe ni wavumbuzi wakubwa wa twchnolojia duniani,moja kati ya maeneno ambayo wamewekeza sana ni kwenye technolojia ya vita,huko hawa watu wana dhana za technolojia ya hali ya juu, wanaweza kupigana na yoyote aliyepopote pasipo hata wao kwenda, wanadhana za kinyuklia zenye uwezo mkubwa sana,wanamfumo mzuri wa mawasiliano pia ndio mabingwa wanaoendesha kituo cha anga cha kimataifa kwa sehemu kubwa, ikumbukwe kuwa maarifa ya anga za mbali urusi inashindana kwa karibu na marekani kuliko taifa lolote.
Urusi ina hadhina kubwa ya mariasili karibia zote duniani,nadhani ndiyo inaongoza kuwa na hiyo hadhina,kwa utajili walionao NATO wanajua kabisa wakimuacha atumie huo utajili kujiendeleza basi wameumia, nimekuambia awali hawa watu wana akili na ni wabunifu, hivyo wanachokosa wao ni uchumi tu wa kusaidia kufanya mambo yao, ana gesi ambayo ulaya nzima wanamtegemea yeye tu, ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta na mengine mengi....kwa hizi rasilimali tu anatoa hofu tosha kwa NATO
Wana jwshi imara, jesho lao ni kubwa sana, ni la pili duniani baada ya lile la marekani,jeshi hili kama nilivyoeleza hapo juu lina dhana za kila aina na lina technolojia kubwa,warusi wanajua kuwa wako hatarini kwahiyo wanawekeza sana kwenye jeshi lao, japo bajeti yao ni ndogo kushinda ya marekani lakini wanafanya ma,bo makubwa sana, uimara wa jeshi hili ni tishio kubwa sana kwa NATO
Uongozi mathubuti, hawa watu kumpata Putin walikula bingo sana, huyu Putin ni mpelelezi mstaafu aliyepikwa na akaiva enzi za KGB, huyu kafanya sana kazi ujerumani hivyo anawajua wamagharibi nje ndani, ni kiongozi wenye misimamo isiyoyumba,ni kiongozi ambaye anatamani urusi iwe kama zamani, hivyo anaimarisha sana nguvu za urusi ili iwe na ushawishi kimataifa kwa kila jambo, uwepo wa huyu mtu ni tishio tosha kwa NATO.
Historia inawalinda, warusi historia pia inawalinda maana walishawahi kuwa wakubwa wa dunia,vita vya pili ni wao ndo waliompigs mjerumani, wana historia ndefu ya ubabe toka enzi hivyo historia hiyo inawalinda na kuwabeba kitambo na kufanya mataifa mengine waiogope.
Yako mengi ila naomba niishie hapo kwa leo