Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

hawakuwa na hawana mlango bahari wa maji moto...ndo maana Crimea imekuwa sehemu ya Russia..binafsi naona kusambaratika kwa USSR ilikuwa mkakati mbinu...kwa nini Chechnya na south Ossetia Russia alishusha kipigo..wingi wa mabilionea Moscow nadhani ni shift of power hasa kuwa na hisa katika uchumi wa magharibi tofauti na hapo awali..ndo maana nashawishika kusema USSR haikusambaratika ila imejifunika ngozi ya kondoo na ku centralize power Moscow..Leo Moscow ni ya kushutumiwa kuchakachua chaguzi Washington?eti nguli wa NSA Edward snowden ni mkimbizi Moscow...mmiliki wa club ya Chelsea ni mrusi...laa nashindwa kuamini kusambaratika ...any way karibu idlib Syria kuna kazi inakamilika hivi karibuni.
Hivi kiongpzi hiyo IDLIB huko syria sio ndio marekani kaweka base ya wanajeshi kwa madai kuwa wanapambana na Magaidi
 
Mkuu GRU unaweza wafananisha na CIA!?.. Fine, kwenye Millitary/War Strategies marekani ubora wake upo wapi zaidi ya Russia!?..
Propaganda nakubaliana nawe!..
Mkuu pitia tena comment yangu kwa utulivu.
Katika millitary/war strategy Russia yupo vizuri sana lakini ili aweze ku last longer anahitaji financial power and stability. Hapo ndipo Marekani anapompiga tobo Russia
 
UNAJUA MAANA YA VITA BARIDI???
ndio maana yake

marekeni ilihitaji kujiunga na mataifa ya Ulaya yenye nguvu ili kushindana na USSR. Na kwa taarifa yako USA haijawahi kupigana vita peke yake ikashinda. inapenda kushirikisha washirika wake wa ulaya ili kuongeza nguvu na kupunguza gharama/madhara ya vita.
 
Kuwa na bajeti kubwa ya kijeshi haimaanishi na ubora wa jeshi utakuwa juu
Urusi kapitwa sana kibajeti kwenye jeshi na USA lakini naona hawajaachana pakubwa
Kwenye jeshi ni kuhakikisha mipango yenu inaenda sawa katika kujua mbinu za adui dhidi yenu na kujua namna ya kumdhibiti
 
Kuwa na bajeti kubwa ya kijeshi haimaanishi na ubora wa jeshi utakuwa juu
Urusi kapitwa sana kibajeti kwenye jeshi na USA lakini naona hawajaachana pakubwa
Kwenye jeshi ni kuhakikisha mipango yenu inaenda sawa katika kujua mbinu za adui dhidi yenu na kujua namna ya kumdhibiti
Lakini hiyo mipango nayo inahitaji bajeti
 
USSR kweli ilimeguka na kudondoka, lakini tusisahau kuwa USSR ilibebwa na mambo yote yaliratibiwa huko Russia, hivyo hata baada ya kuvunjika Russia ilibaki na mambo yote,si kwamba ilisambaratika kabisa kama tunavyoona ila bali bado vyombo vyake viliwndelea kufanya kazi,warusi ni watu ambao sisi tunaona kama wazungu lakini wao wako tofauti kabisa na wazungu.wakati ulaya na marekani walikuwa wanaamini russia imekufa lakini rusia yenyewe ilikuwa inahangaika kuhakikisha inanyanyuka, ndo hapo alipokuja kutokea mtu kama Putin, putin kainyanyua russia muda mfupi sana,si kwasababu ana miujiza ila ni kwasababu walikuwa na kila kitu kasoro kiongozi tu wa kusimamia kukua kwa uchumi wa russia.

Kwanini NATO wanaihofia Russia?
Kwanza warusi ni watu wenye akili nyingi sana, hakuna kitu wanaweza panga wasishindwe kufanya, hivyo kwenye nyanja ya rasilimali watu ipo vizuri ina wasomi wa kutosha na wabunifu kwenye sekta zote kuanzia za ulinzi afya, na technolojia nyingine, kwahiyo NATO inawaogopa kwasababu wana uwezo wa kufanya chochote kwa akili na elimu zao walizonazo.
Wana technolojia, hapo nimekueleza kuwa wana akili na ni wasomi, sasa hivi vyote inawafanya wawe ni wavumbuzi wakubwa wa twchnolojia duniani,moja kati ya maeneno ambayo wamewekeza sana ni kwenye technolojia ya vita,huko hawa watu wana dhana za technolojia ya hali ya juu, wanaweza kupigana na yoyote aliyepopote pasipo hata wao kwenda, wanadhana za kinyuklia zenye uwezo mkubwa sana,wanamfumo mzuri wa mawasiliano pia ndio mabingwa wanaoendesha kituo cha anga cha kimataifa kwa sehemu kubwa, ikumbukwe kuwa maarifa ya anga za mbali urusi inashindana kwa karibu na marekani kuliko taifa lolote.

Urusi ina hadhina kubwa ya mariasili karibia zote duniani,nadhani ndiyo inaongoza kuwa na hiyo hadhina,kwa utajili walionao NATO wanajua kabisa wakimuacha atumie huo utajili kujiendeleza basi wameumia, nimekuambia awali hawa watu wana akili na ni wabunifu, hivyo wanachokosa wao ni uchumi tu wa kusaidia kufanya mambo yao, ana gesi ambayo ulaya nzima wanamtegemea yeye tu, ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta na mengine mengi....kwa hizi rasilimali tu anatoa hofu tosha kwa NATO

Wana jwshi imara, jesho lao ni kubwa sana, ni la pili duniani baada ya lile la marekani,jeshi hili kama nilivyoeleza hapo juu lina dhana za kila aina na lina technolojia kubwa,warusi wanajua kuwa wako hatarini kwahiyo wanawekeza sana kwenye jeshi lao, japo bajeti yao ni ndogo kushinda ya marekani lakini wanafanya ma,bo makubwa sana, uimara wa jeshi hili ni tishio kubwa sana kwa NATO

Uongozi mathubuti, hawa watu kumpata Putin walikula bingo sana, huyu Putin ni mpelelezi mstaafu aliyepikwa na akaiva enzi za KGB, huyu kafanya sana kazi ujerumani hivyo anawajua wamagharibi nje ndani, ni kiongozi wenye misimamo isiyoyumba,ni kiongozi ambaye anatamani urusi iwe kama zamani, hivyo anaimarisha sana nguvu za urusi ili iwe na ushawishi kimataifa kwa kila jambo, uwepo wa huyu mtu ni tishio tosha kwa NATO.

Historia inawalinda, warusi historia pia inawalinda maana walishawahi kuwa wakubwa wa dunia,vita vya pili ni wao ndo waliompigs mjerumani, wana historia ndefu ya ubabe toka enzi hivyo historia hiyo inawalinda na kuwabeba kitambo na kufanya mataifa mengine waiogope.

Yako mengi ila naomba niishie hapo kwa leo
safi sana mkuu.
 
Vyovyote vile, lakini kikawaida watu milioni 600 kutoka nchi tofauti zenye teknolojia na utajiri mwingi ni hatari kuliko watu milioni 144 kutoka taifa moja. Raisi wa zamani wa Singapore Lee Kuan Yew alishawahi kusema maneno haya " wakati Uchina inategemea kutumia vipaji wa vya watu wake Bilioni 1, Marekani inategemea kutumia vipaji vya watu Bilioni 7 kutoka duniani kote" hii imetokana na mifumo ambayo Marekani kajitengenezea kuruhusu watu toka sehemu mbalimbali za dunia kuijenga. Sasa hapa nchi vipaji vya watu Milioni 600 utalinganishaje na watu Milioni 144 ???
mkuu vipaji vya kuokota ni tofauti ya vipaji asilia,halafu siku ukisikia amerika kasambaratika ni ile hali ya kukusanya madodoki na makila kitu wakati utahukumu.
 
Tuko pamoja kabisa Comrade...
mkuu malcom mimi sio mzoefu lakini nahisi na kuamini kwamba urusi ni hatari sana hata sasa,sio nchi ya kuchezea chezea,kwa muktadha wa utajiri na kilichomo katika hiyo nchi basi ni watu hatari sana na au siku moja falme yao itawarejea,natamani kuwaita jeshi la kweli la mungu kwa wale wanaomwamini.Huangusha na kusumbua kila nguvu itawalayo na huogopwa sana.nahisi kuna la ziada.
 
Hoja nzuri sana hii,Mkuu ML
kwanza kabisa Urusi sio taifa dhaifu kabisa na wala halikuwahi kuwa dhaifu maishani,bali hizo ni propaganda za Mahasimu wake,bali Urusi iliwahi kupata ajali na kuugua,(ajali ni kuvunjika kwa umoja wa kisoviet,na kuugua ni madahra ya kupata ajali )yaani majeraha ya kuvunjiika Usovieti.
Ukuu wa Urusi ni uwezo wake wa kurudi haraka kutoka kwenye kuuguza majeraha(,kuvunjiaka usoviet).
Ni kweli haja ya Marekani ni kuitawala dunia bila upinzani wowote.
Sio tu furaha ya Marekani ilikua ni kuvunjika kwa Usoviet,bali kumaliza kabisa ushawishi, na allies wa Urusi,ndipo juhudi za kizigawa nchi zilizokua Warsaw pact ,na nchi za kisovieti zilipopamba moto.mfano mshirika mkubwa na ndugu wa damu wa Urusi nchi ya Yugoslavia ilipofanyiwa hujuma nzito na kubaki vipande vipande.
Urusi haikushindwa vita baridi kwa juhudi za west peke yake,bali kwa msaada wa taasisi nyingine kubwa duniani hasa kanisa KATOLIKI chini ya Baba Mt (PAPA) John Paul II,na hata Uislam.Hii haikua vita ndogo ya kuliangusha dubwana kuwa USSR.
UWEZO WA URUSI.
Elimu,maarifa,sayansi,teknolojia,mikakati na ulinzi na ufedhuri.
Marekani peke yake hamwezi Mrusi,hawezi kumdhibiti kwa sababu Urusi anavyo vitu vyote ambavyo marekani anavyo lakini wengine hawana navyo nimevitaja hapo juu,Urusi wana elimu,hapa ndio chimbuko la kila kitu duniani,ana maarifa kama vile marekani,ana sayansi na teknolojia kama vile marekani,ana mikakati thabiti ya kubaki kwenye game kama vile marekani ana uwezo wa ulinzi na usalama kama vile marekani,ili kumdhibiti labda uue wananchi wake wote ibaki ardhi tu.Ufedguri namaanisha ujasusi.
Ni kweli ML kuwa Urusi itawasumbua sana Marekani na washirika wake kwa sababu kiuchumi Urusi ana kila kitu ardhini hivyo hahitaji kununua kwa wengine, ambapo wangemfungia asinunue au asiuziwe.lakini kwa alivyonavyo watawazui wengine wasinunue kwake,hilo wanawewza.
kijeshi kumdhibiti Urusi ni kukusudia kuiangamiza dunia,kama sio kujaribu kujipiga risasi mwenyewe.vita ya Urusi na wao haitakua vita ya Kalashinikov na bunduki nyingine bali ita kua ni vita ya ICBM's
sasa fikiria marekani akirusha na urusi akirusha kuna kitu kitabaki?
dah mkuu nyote kwa umoja wenu mbarikiwe sana,tunawafuatili na kuwafurahia sana,asanteni sana kwa niaba ya wenye shukrani.
 
Ahsante sana mkuu. Lakini naomba nikuulize swali la msingi kutoka kwenye hoja yako: Mbona Urusi ya Kisovieti ilikuwa na Gesi, Mafuta, Chuma pamoja na Teknolojia kubwa sana lakini bado ikaanguka baada ya Uchumi wake kudorora?
kuna nadharia kuwa CCCP ilianguka kwasababu baadhi ya warusi waliona kuwa CCCP na sera za kikomunisti zimeua tamaduni za Russia (mf. Orthodox church) na pia ilitumia nguvu nyingi kueneza itikadi kwenye nchi nyingine badala ya kutumia rasilimali zao kuiendeleza Russia. Ukimsililiza Putin utaona mara moja moja anaongelea hayo. Kwa hiyo kuanguka kwa CCCP kunaweza kuwa ni mpango uliopangwa na kitengo ndani ya KGB.
 
kuna nadharia kuwa CCCP ilianguka kwasababu baadhi ya warusi waliona kuwa CCCP na sera za kikomunisti zimeua tamaduni za Russia (mf. Orthodox church) na pia ilitumia nguvu nyingi kueneza itikadi kwenye nchi nyingine badala ya kutumia rasilimali zao kuiendeleza Russia. Ukimsililiza Putin utaona mara moja moja anaongelea hayo. Kwa hiyo kuanguka kwa CCCP kunaweza kuwa ni mpango uliopangwa na kitengo ndani ya KGB.

1. Lakini sasa mbona leo hii Kremlin inahangaika sana kujaribu kuziweka jirani nchi zile zilizojitoa kwenye muungano wakati KGB na Politburo ya CPSU ndiyo iliamua kuua muungano wao ???

2. Hao KGB walivyokuwa wanavunja muungano hawakutabiri kwamba kutakuwa na madhara makubwa sana kiulinzi huko mbeleni ???

NB: Basi kama KGB walifanya hivyo nadhani kuna hatihati siku watafanya tena wakichoka.....
 
1. Lakini sasa mbona leo hii Kremlin inahangaika sana kujaribu kuziweka jirani nchi zile zilizojitoa kwenye muungano wakati KGB na Politburo ya CPSU ndiyo iliamua kuua muungano wao ???
2. Hao KGB walivyokuwa wanavunja muungano hawakutabiri kwamba kutakuwa na madhara makubwa sana kiulinzi huko mbeleni ???
Kuna uwezekano kuwa vita ya Afghanistan na vita baridi vilidhoofisha sana uchumi kiasi kwamba nchi yao ingeweza hata kuvamiwa ilibidi "wazee" wafanye "bluff" kabla mambo hayajaharibika zaidi.

Katika kufanya hivyo wakaona wavunje muungano na kumuweka mlevi (Yeltsin) ili kuudanganya ulimwengu kuwa wao sio watu wakuchukuliwa 'serious' huku teyari wakiwa na mtu wao (Putin) au wewe unasemaje kuhusu maneno haya ya Sun Tzu "All warfare is based on deception."
 
Kuna uwezekano kuwa vita ya Afghanistan na vita baridi vilidhoofisha sana uchumi kiasi kwamba nchi yao ingeweza hata kuvamiwa ilibidi "wazee" wafanye "bluff" kabla mambo hayajaharibika zaidi.

Katika kufanya hivyo wakaona wavunje muungano na kumuweka mlevi (Yeltsin) ili kuudanganya ulimwengu kuwa wao sio watu wakuchukuliwa 'serious' huku teyari wakiwa na mtu wao (Putin) au wewe unasemaje kuhusu maneno haya ya Sun Tzu "All warfare is based on deception."
Haya maneno aliyasema Anotoliy Golitstyn kwenye vitabu vyake vya The Perostroika Deception na New Lies for the old. Kuna kipindi nilimsoma sana nikaja kugundua kuna mambo mengi sana ya uongo wanayasema.

Russia bila hata kwenda Afghanistan ilikuwa ni lazima ianguke tu. Mtafute mtu anaitwa Prof Emmanuel Todd ni mfaransa, wakati ana miaka 26 alitabiri anguko la USSR tena kipindi hicho ndiyo wanaongoza kwenye teknolojia kubwa kama Satellite, Makombora na Silaha lakini alichekwa hadi na Wamarekani.

Alisema kwamba kwa mfumo wa Uchumi wa Kikomunisti lazima Urusi itaanguka tu. Miaka kama 30 baadae asilimia 75% ya aliyoyasema yalitokea na siyo tu Urusi. Lakini nchi karibia zote za kijamaa ziliangukia pua ikiwemo Tanzania yetu. Uchina aligundua mapema mchezo, akaruhusu mfumo wa masoko na uwekezaji.
 
Back
Top Bottom