Kuna watu wanataka sifa, wanataka glory, wanataka u star. Wanataka kuonekana wao zaidi ya kufanya mabadiliko hata bila kuonekana.
Watu hao wakiwa mbali na Tanzania hawajulikani na hizo jamii huko, wanaonekana huyu muafrika tu, especially na watu wa nje. Ukiwa umekaa nje ya Tanzania halafu unarudi Tanzania unaona watu wanavyo ku treat differently ndiyo utajua hili.
Kama hujakaa nje ya Tanzania, hususan Ulaya, Asiana America kwa muda mrefu wa kuanzia mwaka mmoja na kuendelea ni vigumu kuelewa hili.
Watu hawa hawawezi kukaa nje muda mrefu.Inabidi waje Tanzania kupata kuabudiwa na Watanzania.
Tunawaona malimbukeni wa aina hii wapo wengi huku Marekani na Ulaya, utakuta mtu anarudi Tanzania mara mbili tatu kila mwaka, hata hana shughuli ya maana.
Anapenda kuwakoga watu tu kwamba yeye katoka Marekani au Ulaya.
Polepole naye alikuwa na ushamba huu.
Ndiyo maana utamsikia anajimwayamwaya na Kihispania chake cha kuombea maji "Tulipokuwa Kuba..." "Adios companeros..."
Sasa Watanzania unawakoga na Kihispania wanaelewa nini?
Polepole ilikuwa lazima akamatwe kwa sababu ya ubishoo wake. Yani yule ni mtu bishoo mpaka jambo la kufa na kupona kwake analifanyia ubishoo.
Unafanya ubishoo ukiwa Dar kuichana serikali vile wakati unaenda live kwa masaa? Hujui ile kuwa online tu ni risk? Hujui kila mtu anayejua ulipo ni risk? Including family.
Alikuwa na uwezo wa kwenda Sweden, kwenda Belgium, kwenda nchi kibao za Ulaya na Marekani. Kupata ukimbizi akasema alilotaka relatively safely kutoka huko.
Lakini yeye kataka kwenda Dar afanye ubishoo akiwa kajificha.
Hili jambo linaonesha mtu asiye na strategy, anayeendeshwa na kuuza sura zaidi ya kutaka mabadiliko ya kweli.
Mtu anayetaka mabadiliko ya kweli angeweza kufanya mengi kwa kubakia ndani ya mfumo akawa analeak mambo tu wengine wanasema.
Unafikiri Polepole angemtumia Mange Kimambi, au Jasusi Chahali, au mtu mwingine yeyote ambaye angemchagua yeye, akatuma habari na documents wabongo wasingejua anachotaka kusema?
Angeweza kuwa muandika script anayebaki nyuma.
Polepole angeandika yote anayoyajua katika kitabu halafu akakiachia ingekuwaje?
Au kama alitaka kusema mwenyewe si angeweza kwenda Scandinavia huko au Belgium. Watu wanamjua huyu mtu kashakuwa balozi na msemaji wa CCM. Angeomba ukimbizi anaupata ndani ya siku cahache tu.
Lakini yeye aliona hoja si muhimu, muhimu aonekane kaisema yeye, tena akiwa karibu na wapambe wake kajificha Dar.
This was the move of a reckless tactless emotional man with no strategy.
This was not the work of a mastermind revolutionary.