bongo dili
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 12,350
- 25,180
Walifanya usafi au walipiga picha wakifanya usafir.
Ingekua vyema sana kama ungeleta pia na proceedings za iyo kesi ya Mbarikiwa ili kuepukana na prejudiced perception, Sometimes equity is better than equalityView attachment 2766809
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
Mheshimiwa Jaji Mkuu,
Tarehe 29 Septemba 2023, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimhukumu kifungo cha miaka mitatu na siku 14 jela, Mchungaji anayeitwa Mbarikiwa Mwakipesile (39), baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuendesha huduma ya kikosi kazi cha Injili kabla ya kupata usajili kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kama sheria ya vyama vya kijamii inavyotaka.
Hukumu hiyo ilitolewa chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kijamii. Kifungu kinatoa fursa ya kulipa faini u kifungu, au vyote kwa pamoja. Mahakama imeamua kutoa adhabu ya kifungo.
Mchungaji Mwakipesile amekuwa anaituhumu serikali kwamba inawaona wanachi kama nyani au kenge. Yeye ni baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”,
View attachment 2766819
Lakini, kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake (tazama Kkiambatanisho hapa chini). Kesi yake iliendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mwishowe alitozwa faini, badala ya kifungo.
View attachment 2766818
Undumilakuwili huu unazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu.
Mahakama inayomheshimu jangili na kumtweza mchungaji ni mahakama yanhovyo sana. Mahakama inayomheshimu mwarabu mwenye asili ya Iran na kumtweza Mbantu wa Mbeya haina haki ya kuitwa mahakama. Mahakama inayowatukuza wenye mali na kuwakandamiza kabwela sio mahakama kamwe. Mahakama inayokumbatia kanuni ya umachiveli, isemavyo kwamba "good ends may justify any means, including evil means," haitakiwi nchini Tanzania.
Hivyo, tunatoa wito kwako Mheshimwa Jaji Mkuu: tunaomba ulinde heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kuchukua hatua stahiki za kufuta undumilakuwili huu.
============KIAMBATANSHO KUHUSU KESI YA MDOGO WAKE ROSTAM AZIZI==================
Mnamo 30 Oktoba 30 2018, saa 7 mchana maeneo ya Msasani, Jijini Dar, Akram Aziz, mdogo wake Rostam Aziz, alikamatwa na vyombo vya dola akiwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo Pembe za ndovu.
MUHTASARI WA KESI YA MDOGO WAKE BILIONEA ROSTAM AZIZ
Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.
Ilifahamika kuwa amekuwa ni “Mastermind” wa ujangili nchini kwa muda mrefu sana na ndiye kinara wa mauaji ya tembo na wanyama wengine kwenye mbuga zetu.
Taarifa za uhakika zilisema kuwa mtandao huo wa ujangili ulikuwa unasimamiwa na Kaka yake Rostam Aziz pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali katika awamu zilizopita. Hatimye Akram alitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faili badala ya kifungo. Picha zifuatazo ni baadhi ya silaha alizokamatwa nazo:
View attachment 2766815
View attachment 2766816
View attachment 2766817
Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P. P/Bag
Sumbawanga
30 Sep 2023
Ana kitalu Cha uimbaji na Sio uwindaji.Na huyo mchungaji alikuwa na yeye ana kitalu cha kuwindia kama Akram?
Kafungwa kwa kuwinda watu au wanyama huyo mchungaji?
Mbona huyasemi ya Tibaijuka, kapewa adhabu ya kuachoishwa kazi tu.
Jamaa mwingine naye mwenye makengeza hivi alikuwa ana kanisa huko Kigamboni linaunga mkono ushoga waziwazi naye alifungiwa baada ya kuonekana kuwa kumbe hakuwa na kibali.Hata Kanisa la WRM la Suguye halikuwa na usajili na hakufungwa bali huduma zilisitishwa tu.
Dar: Serikali yalifunga Kanisa la Nabii Suguye
Hellow Serikali imeingilia kati huduma za kiroho zitolewazo kanisa la WRM kivule maarufu kwa nabii Suguye mpaka sasa hawajatoa sababu maalumu ya kuzuia huduma hizo kusitishwa kwenye kanisa hilo. Kwa upande wangu kama walivyo chunguza hilo kanisa na kugundua mapungufu yaliyopo basi wafanye...www.jamiiforums.com
Issue ni ukosoaji.
Ingekua vyema sana kama ungeleta pia na proceedings za iyo kesi ya Mbarikiwa ili kuepukana na prejudiced perception, Sometimes equity is better than equality
Labda alikaodiHata Kanisa la WRM la Suguye halikuwa na usajili na hakufungwa bali huduma zilisitishwa tu.
Dar: Serikali yalifunga Kanisa la Nabii Suguye
Hellow Serikali imeingilia kati huduma za kiroho zitolewazo kanisa la WRM kivule maarufu kwa nabii Suguye mpaka sasa hawajatoa sababu maalumu ya kuzuia huduma hizo kusitishwa kwenye kanisa hilo. Kwa upande wangu kama walivyo chunguza hilo kanisa na kugundua mapungufu yaliyopo basi wafanye...www.jamiiforums.com
Issue ni ukosoaji.
Walipigwa picha wakifanya usafi ili tuone na kuamini kuwa walifanya usafi. Hiyo picha ilikuwa endelevu, lakini zoezi lenyewe la kufanya usafi liliishia hapohapo.Walifanya usafi au walipiga picha wakifanya usafir.
Kuna vitu havihitaji kuwa professor,just common sense, kwa hili hata mtu ambaye hajaenda shule kabisaa anakupa jibu,sio jibu tu Bali jibu sahihi.Wewe umesomea sheria?
Tofauti ya kesi hizo mbili ni kuwa Akramu hakushindana/kutunishia serikali misuli kama Mbarikiwa alivyo kuwa anafanya hivi karibuni kwenye mitandao. Yeye Mbarikiwa ni Mchungaji ila kaweka maandiko ya kuheshimu mamlaka kando. Kwa utaratibu huo ataanza kujifunza. Ajifunze kwa Kakobe na Muhingira!View attachment 2766809
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
Mheshimiwa Jaji Mkuu,
Tarehe 29 Septemba 2023, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimhukumu kifungo cha miaka mitatu na siku 14 jela, Mchungaji anayeitwa Mbarikiwa Mwakipesile (39), baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuendesha huduma ya kikosi kazi cha Injili kabla ya kupata usajili kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kama sheria ya vyama vya kijamii inavyotaka.
Hukumu hiyo ilitolewa chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kijamii. Kifungu kinatoa fursa ya kulipa faini u kifungu, au vyote kwa pamoja. Mahakama imeamua kutoa adhabu ya kifungo.
Mchungaji Mwakipesile amekuwa anaituhumu serikali kwamba inawaona wanachi kama nyani au kenge. Yeye ni baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”,
View: https://youtu.be/JSVmJqUmbHg
Lakini, kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake (tazama Kkiambatanisho hapa chini). Kesi yake iliendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mwishowe alitozwa faini, badala ya kifungo.
View: https://youtu.be/-FWpqOItZrI
Undumilakuwili huu unazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu. Na tatizo liko hivi:
- Mahakama inayomheshimu jangili na kumtweza mchungaji au shehe ni mahakama ya hovyo sana.
- Mahakama inayomheshimu mwarabu na kumtweza Mbantu wa Mbeya haina haki ya kuitwa mahakama. Mahakama inayowatukuza wenye mali na kuwakandamiza kabwela sio mahakama kamwe.
- Mahakama inayotukuza watu wenye mamlaka ya kisasa na kutwatweza wanyonge inakuwa na watendaji ambao wana mashudu kichwani badala ya ubingo.
- Kwa ujumla, mahakama inayokumbatia kanuni ya umachiveli, isemavyo kwamba "good ends may justify any means, including evil means," haitakiwi nchini Tanzania.
Hivyo, tunatoa wito kwako Mheshimwa Jaji Mkuu: tunaomba ulinde heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kuchukua hatua stahiki za kufuta undumilakuwili huu, wenye kutokana na hiari ya kimaamuzi kuhusu adhabu waliyo nayo mahakimu na majaji.
============KIAMBATANSHO KUHUSU KESI YA MDOGO WAKE ROSTAM AZIZI==================
MUHTASARI WA KESI YA MDOGO WAKE BILIONEA ROSTAM AZIZ
View attachment 2766818
Mnamo 30 Oktoba 30 2018, saa 7 mchana maeneo ya Msasani, Jijini Dar, Akram Aziz, mdogo wake Rostam Aziz, alikamatwa na vyombo vya dola akiwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo Pembe za ndovu.
Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.
Ilifahamika kuwa amekuwa ni “Mastermind” wa ujangili nchini kwa muda mrefu sana na ndiye kinara wa mauaji ya tembo na wanyama wengine kwenye mbuga zetu.
Taarifa za uhakika zilisema kuwa mtandao huo wa ujangili ulikuwa unasimamiwa na Kaka yake Rostam Aziz pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali katika awamu zilizopita. Hatimye Akram alitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faili badala ya kifungo. Picha zifuatazo ni baadhi ya silaha alizokamatwa nazo:
View attachment 2766815
View attachment 2766816
View attachment 2766817
Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P. P/Bag
Sumbawanga
30 Sep 2023
Nasindikiza Kwa ZABURI 35Serikali ya Bibi yenu imetafuta namna yake ili kukabiliana Ukristo Tanzania. Something will happen, Mungu ni Mkuu daima
Tofauti ya kesi hizo mbili ni kuwa Akramu hakushindana/kutunishia serikali misuli kama Mbarikiwa alivyo kuwa anafanya hivi karibuni kwenye mitandao. Yeye Mbarikiwa ni Mchungaji ila kaweka maandiko ya kuheshimu mamlaka kando. Kwa utaratibu huo ataanza kujifunza. Ajifunze kwa Kakobe na Muhingira!
Unajua kwanini sheria ni noble profession? AnywayKuna vitu havihitaji kuwa professor,just common sense, kwa hili hata mtu ambaye hajaenda shule kabisaa anakupa jibu,sio jibu tu Bali jibu sahihi.
Alilipishwa faini kama fedha ya chai tuuFafanua kidogo
FaizaFoxy tetea tuu na huku