View attachment 2766809
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
Mheshimiwa Jaji Mkuu,
Tarehe 29 Septemba 2023, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimhukumu kifungo cha miaka mitatu na siku 14 jela, Mchungaji anayeitwa Mbarikiwa Mwakipesile (39), baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuendesha huduma ya kikosi kazi cha Injili kabla ya kupata usajili kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kama sheria ya vyama vya kijamii inavyotaka.
Hukumu hiyo ilitolewa chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kijamii. Kifungu kinatoa fursa ya kulipa faini u kifungu, au vyote kwa pamoja. Mahakama imeamua kutoa adhabu ya kifungo.
Mchungaji Mwakipesile amekuwa anaituhumu serikali kwamba inawaona wanachi kama nyani au kenge. Yeye ni baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”,
View attachment 2766819
Lakini, kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na
kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake (tazama Kkiambatanisho hapa chini). Kesi yake iliendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mwishowe alitozwa faini, badala ya kifungo.
View attachment 2766818
Undumilakuwili huu unazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu.
Mahakama inayomheshimu jangili na kumtweza mchungaji ni mahakama yanhovyo sana. Mahakama inayomheshimu mwarabu mwenye asili ya Iran na kumtweza Mbantu wa Mbeya haina haki ya kuitwa mahakama. Mahakama inayowatukuza wenye mali na kuwakandamiza kabwela sio mahakama kamwe. Mahakama inayokumbatia kanuni ya umachiveli, isemavyo kwamba "
good ends may justify any means, including evil means," haitakiwi nchini Tanzania.
Hivyo, tunatoa wito kwako Mheshimwa Jaji Mkuu: tunaomba ulinde heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kuchukua hatua stahiki za kufuta undumilakuwili huu.
============
KIAMBATANSHO KUHUSU KESI YA MDOGO WAKE ROSTAM AZIZI==================
View: https://youtu.be/-FWpqOItZrI
MUHTASARI WA KESI YA MDOGO WAKE BILIONEA ROSTAM AZIZ
Mnamo 30 Oktoba 30 2018, saa 7 mchana maeneo ya Msasani, Jijini Dar, Akram Aziz, mdogo wake Rostam Aziz, alikamatwa na vyombo vya dola akiwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo Pembe za ndovu.
Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.
Ilifahamika kuwa amekuwa ni “Mastermind” wa ujangili nchini kwa muda mrefu sana na ndiye kinara wa mauaji ya tembo na wanyama wengine kwenye mbuga zetu.
Taarifa za uhakika zilisema kuwa mtandao huo wa ujangili ulikuwa unasimamiwa na Kaka yake Rostam Aziz pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali katika awamu zilizopita. Hatimye Akram alitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faili badala ya kifungo. Picha zifuatazo ni baadhi ya silaha alizokamatwa nazo:
Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P. P/Bag
Sumbawanga
30 Sep 2023