Uchaguzi 2020 Swali kwa Rais Magufuli: Hofu ya nini juu ya Vyombo vya Habari?

Wa kulaumiwa hapo ni vyombo vya usalama na ulinzi kwa kutoona mwelekeo wa taifa,kwa nini mtu mmoja anafanya maamuzi kinyume na katiba?
Hao viongozi wa hivyo vyombo wanateuliwa na nani?
 
TBC kuna balance ya habari?? Ni lini wamewahi kurusha taarifa za upinzani isipokua zile mbaya! O tolerance inakuja hivi punde!
 
Hii inanisikitisha sana. Wale wajuzi zaidi tusaidieni alternative ways kuendelea kupata habar toka BBC, DW, VOA etc pale watawala watakapozuia local media kujiunga na vyombo hivi vya nje.
 

Tutapopata serikali yenye mgombea:



Maisha yatakuwa murua sana.

Eeh mola wetu na ukazisikie sala zetu.
 
Moja wa wahanga wakubwa katika utawala wowote wa kiimla ni vyombo vya habari sambamba na vyama vya upinzani na wanaharakati.

Hilo halina ubishi, tulikuwa tunayasikia huko kwingineko lkn sasa yametufika. Ukiona mwenzako anateseka ama kweli usishangilie hujui ya kesho.
 
Kiingereza hajui halafu analazimisha kufungia radio zinazotangaza kwa lugha kiswahili???
kuna siku watanzania wote watalazimishwa kuongea kisukuma ili mabeberu wasituelewe wakaingilia mipango yetu.....useless and primitive leadership!
 

Mnataka vyombo vya habari viwe vinatoa taarifa za uongo ndo uwe uhuru wa habali?
Je huo uongo ukishapewa unapata faida gani?
Au mnanufaika nao vipi?
Juzi mnyika kamdanganya Tundu lisu kuwa magufuli kakopa tirioni 41 je huo ndo uhuru wa habali mnaoutaka?
Je huo sio uongo?
Mkipenda inchi iwe ya waongo sidhani kama kutakuwa na maendeleo na ndio maana tanzania kwa uongouongo mnaongoza.
Hata kwa ngazi ya jamii uongo ni mkubwa badala ya watu kufanya kazi wao wanabaki kuongea watu.
Vyombo vya habali vinatakiwa kutumia taaruma yao na si mazoea ili walete mabadiliko.
Sijawahi kuona waandishi wa habali tanzania hata wakijaribu kuchambuwa hotuba za viongozi kwa maslahi ya nchi.

Mathalani mgombea katoa ahadi, je hiyo ahadi inaweza kutekerezwa kwa asilimia nagapi? Je ina faida kiasi gani je ina hasara kiasi gani ikitekerezwa ili wananchi tuamue kukingana na data zenye faida.
 
Hivi mtu anayependwa na wanyonge wote wa Tz huku akiwa ameleta maendeleo ambayo hayajawahi kuonekana Nchini kwanini anahangaika kiasi hiki cha kufungia medias?
 
Hivi kama mtu unajiamini kwamba una strong track record kwenye utendaji wako hofu zinakuwa ni za nini ?
 
Hao TCRA wamewapa wapinzani wa JPM hoja nyingine kwenye kampeni za urais mwaka huu. Kwa miaka hii 5 tumeona uminyaji mkubwa wa kusambaza na kupata habari, sijui huu uoga unatokea wapi.

Vv
Kweli kabisa. Tena hoja hii ni msumari kweli kweli. We ngoja tu utaona
 
Zikitolewa habari za uongo kuna vyombo vya sheria vyenye mamlaka ya kusema huu ni uongo au sio. Hatuwezi kuambiwa na CCM upi ni uongo na upi ni ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…