Tangu Freeman Mbowe alipokamatawa na kufunguliwa mashtaka yanayohusiana na ugaidi, viongozi wa Chadema Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam wamekuwa wanahamasisha maombi katika makanisa mbalimbali, bila kujali Mbowe anamwamini Mungu yupi.
Kuna wanaopeleka matoleo kwenye makanisa ya parokia Katoliki. Wengine wanapepeleka makanisa ya KKKT. Na baadhi wanasali novena barabarani.
Nina swali kwa Viongozi wa Chadema: Kumwombea Mbowe ni sehemu ya ibada kwa Mungu yupi?
Kanuni za kuzingatiwa:
Kusudi, viongozi wa Chadema waweze kuelewa msingi wa swali langu na kulitendea haki, naweka hapa kanuni zinazopaswa kuongoza mjadala huu:
Mosi, ni kanuni ya kutambua kitu kimoja chenye majina tofauti, yaani
the principle of the Identity of indescernibles.
Kwa mujibu wa kanuni hii, kunapokuwa na majina mawili yanayorejea kitu kimoja kile kile, hiyo maana yake ni kwamba, kila sifa iliyofungamana na kitu chenye jina la kwanza pia imefungamana na kitu chenye jina la pili, na kinyume chake ni kweli.
Yaani, kwa kila jozi ya vitu, vyenye majina X na Y, jina X litakuwa linamaanisha kitu kile kile kinachomaanishwa na jina Y, endapo na endapo tu:
Kwa pamoja, sentensi kwamba:
(1) kila sifa iliyofungamana na kitu X pia imefungamana na kitu Y;
na sentensi kwamba:
(2) kila sifa iliyofungamana na kitu Y pia imefungamana na kitu X.
ni za kweli.
Kwa mfano,
- Julius ni jina linalorejea mtu yule yule anayeitwa Nyerere. Yaani, Julius na Nyerere ni majina ya kitu kimoja.
- Na, DOG ni jina linalorejea kitu kile kile kinachoitwa MBWA. Yaani, DOG na MBWA ni majina ya kitu kimoja.
Pili, ni kuhusu
kanuni ya kutofautisha vitu vinavyohesabika, yaani
the principle of dissimilairty of the diverse.
Kwa mujibu wa kanuni hii, kunapokuwa na vitu viwili vinavyoonekama kuwa tofauti, kiasi kwamba tunaweza kusema kuwa hiki ni kitu cha kwanza, na kile ni kitu cha pili, basi, hiyo maana yake ni kwamba, vitu hivyo vina tofauti inayotokana na ukweli kwamba, kuna angalau sifa moja iliyofungamana na kitu cha kwanza lakini sifa hiyo haikufungamana na kitu cha pili, na kinyume chake ni kweli.
Yaani, tukikutana na vitu viwili, X na Y, tunaweza kuvitofautisha endapo tu:
Ama:
(1) katika seti ya sifa za kitu X angalau kuna sifa moja S, ambayo haipatikani kwenye seti ya sifa za kitu Y,
Au:
(2) katika seti ya sifa za kitu Y angalau kuna sifa moja S, ambayo haipatikani kwenye seti ya sifa za kitu X.
Kwa mfano:
- Mipira miwili ya tufe, iliyowekwa mezani, na ambayo inafanana kwa kila kitu, bado tunaitambua kuwa ni mipira miwili tofauti kwa kuwa, kila mpira unayo anwani yake ya kijiografia. Hata watoto mapacha sisisi tunawatofautisha kwa njia hiyo.
- Vivyo hivyo, Miungu inayependa kuabudiwa Ijumaa (Miungu ya Waislamu) na Miungu inayependa kuabudiwa Jumapili (Miungu ya Wakristo) ni Miungu tofauti, kwa sababu hiyo pekee.
- Kadhalika, Miungu inayependa kuabudiwa Jumamosi (Miungu ya Wasabato) na Miungu inayependa kuabudiwa Jumapili (Miungu ya Wakristo bado) ni Miungu tofauti, kwa sababu hiyo pekee.
- Aidha, Miungu inayoruhusu waamini kutumia kondomu (Miungu ya Waanglikana) na Miungu inayokataza kondomu (Miungu ya Wakatoliki) ni Miungu tofauti, kwa sababu hiyo pekee.
- Vile vile, Miungu inayokataza makuhani kuoa (Miungu ya Wakatoliki) na Miungu inayoruhusu makuhani kuoa (Miungu ya Waanglikana na Walutheri) ni Miungu tofauti, kwa sababu hiyo pekee.
- Mungu anayewaunga mkono watu wanaotaka Mbowe atiwe hatiani na Mungu anayewaunga mkono watu wanaotaka Mbowe asitiwe hatiani ni Miungu wawili tofauti!
- Na mifano inaendelea kama inavyothibitishwa na utitiri wa usajili wa taasisis za kidini katika ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Hivyo basi:
Mungu wa KKKT anayemwabudiwa na Mbowe ni tofauti na Mungu wa Wakatoliki wanayejaribu kumwomba wafuasi wa Mbowe.
Mbowe hamtambui Mungu wa Wakatoliki tangu siku alipobatizwa chini ya madhehebu ya KKKT, na hadi leo hajatwambia kama amemkana Mungu wa KKKT na kumkubali Mungu wa Wakatoliki.
Kwa hiyo, Mungu wa Wakatoliki hawezi kusikiliza wala kupokea matoleo yanayopelekwa ndani ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya kumwomba Mungu wa Wakatoliki amtetee Mbowe, mpaka hapo Mbowe atakapomkiri kwamba yeye pekee ndiye Mungu wa kweli.
Hivyo, viongozi wa Chadema acheni maigizo kama ya "mitano kwanza" na "mitano tena" tuliyoshuhudia mwaka jana.
Msitufikishe mahali kanisa lile lile moja linapokea matoleo ya kuomba mbowe
atiwe hatiani na kuyabariki leo; halafu kesho, kanisa hilo hilo linapokea matoleo ya kuomba mbowe
asitiwe hatiani na kuyabariki. Dini zitadhalilika sana kwa njia hii.
Ukweli ni kwamba: Mungu anayewaunga mkono watu wanaotaka Mbowe
atiwe hatiani na Mungu anayewaunga mkono watu wanaotaka Mbowe
asitiwe hatiani ni Miungu wawili tofauti!
Lakini, tunafundishwa kuwa Mungu wa kweli habadiliki wala kubadilisha mawazo yake.
Kwa hiyo, mmojawapo kati ya miungu hawa wawili atakuwa ni Mungu feki, yaani Mungu wa kuchonga (
constructed God), wakati mwingine ni Mungu wa kweli (
essential God).
Ukweli ndio huo!