Swali kwa Viongozi CHADEMA: Kumwombea Mbowe ni sehemu ya ibada kwa Mungu yupi?

Swali kwa Viongozi CHADEMA: Kumwombea Mbowe ni sehemu ya ibada kwa Mungu yupi?

Wewe sasa una mvi.
Umemtafuta Mungu tabgu utoto.
Hujawahi kumwona Mungu.
Bado unanishauri kumtafuta Mungu.
Crazy!

[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] Agnostic au Atheist, nakuambia kama huwa unaenda kanisani basi ni kama kutimiza wajibu tu na kushiriki na jamii, ila wewe u dont believe in God.
 
Now I have understood you Mama Amon.
You are an atheist.I can not argue with you.

I am a catholic.I pray when I face challenges in life.Prayers give me hope and resilience.

You as an atheist , What gives you strength when you have troubles??

Biiingo, huyu mama haamini katika Mungu, vitabu vya falsafa anayosoma vimemfanya ahoji uwepo wa Mungu, na kadiri anapokosa majibu ndipo anazidi kuwa mbali na Mungu.
 
Vipi kuhusu "mungu" bikira maria mnaemuomba awasamehe madhambi??
Tafiti kabla ya kuandika.
Wakatoliki wanaomna, wanaombewa na wanaomba kuombewa.
Wanaabudu wanaheshimu.
Bikira maria wanamheshimu na wanamwomba awaombee kwa Mungu kwa yeye ni Mama wa Mungu.
So, reframe your question... and I shall respond
 
Macho ya nyama ni matano: jicho, sikio, ulimi, pua, ngozi.
Rohoni ni wapi, na macho ya rohoni ni mangapi?
Kama jicho la kiroho maana yake ni jicho la kimantiki, kwa nini hutaki kutumia mantiki katika maongezi haya?
Return back to sanity.
Hahahahah...

And you came to correct your common question "Rohoni ni wapi?" Naona baada ya Roho kukutetemesha ukaja kuandika kwa upyaaaa..

Sikia wewe, wacha ubabaifu HUWEZI KUJENGA HOJA ZAKO ZA KIMANTIKIA JUU YA MUUMBA INGALI HIYO MANTIKI YATOKA KWA ALIYEKUUMBA

Je, Unaamini kuwa Mungu ndiye kakuumba?
 
Tafiti kabla ya kuandika.
Wakatoliki wanaomna, wanaombewa na wanaomba kuombewa.
Wanaabudu wanaheshimu.
Bikira maria wanamheshimu na wanamwomba awaombee kwa Mungu kwa yeye ni Mama wa Mungu.
So, reframe your question... and I shall respond

Naomba reference ya kwenye Biblia inayoonesha kuruhusu Bikira maria mnamuomba awaombee kwa Mungu..!! Nasubiri huo mstari.
 
Naomba reference ya kwenye Biblia inayoonesha kuruhusu Bikira maria mnamuomba awaombee kwa Mungu..!! Nasubiri huo mstari.

Unachoomba ni authority from scriptures pekee.
Kuna authority zaidi ya Biblia.
Umesahau kanuni ya REST.
Yaani: Reason, Experience, Scripture, Tradition (REST).
Wakatoliki wanatumia REST.

Soma zaidi hapa: Wesleyan Quadrilateral
 
Biiingo, huyu mama haamini katika Mungu, vitabu vya falsafa anayosoma vimemfanya ahoji uwepo wa Mungu, na kadiri anapokosa majibu ndipo anazidi kuwa mbali na Mungu.
Kuhoji uwepo wa Mungu ni tatizo kwako?

Labda umesahau.

BInadamu ni mnyama anayepambanuliwa na sifa kuu tano zifuatazo: (1) kuona, (2) kuhoji, (3) kuhukumu, (4) kutenda, na (5) kupima matokeo.

Kwa hiyo, kuhoji "uwepo wa Mungu mahali na wakati fulani" ni suala ambalo limo ndani ya mamlaka yake, na ni suala lenye afya.

Tatizo unatumia vishazi ambavyo vimemeguka.

Maneno "uwepo wa Mungu" hayana maana yoyote mpaka hapo unapoyakamilisha kwa kusema "uwepo wa Mungu mahali na wakati fulani".

Mfano rahisi: maneno "uwepo wa nyoka" hayana maana yoyote mpaka yakamilishwe kwa kusema "uwepo wa nyoka mahali na wakati fulani".

Katika metafizikia tunasema kuwa, "as opposed to essensce, existence is predicated on spatial and temporal coordinates."

Jumapili njema!
 
Je, Unaamini kuwa Mungu ndiye kakuumba?
Niliumbwa na wazazi wangu, wazazi waliumbwa na mababu na mabibi, na mnyororo unaendelea kinyume nyume hadi huko mbali kwenye hatua ya kwanza ambako inaaminika kulikuwa na chanzo kisicho na mwanzo, kisababishi kisicho na kisababishi.

Chanzo cha kwanza ndiyo kitu ambacho baadhi ya watu hukiita Mungu. WEngine wanapinga, na mjadala unaendelea hadi leo na haujafungwa.

Usinijadili mimi mleta hoja, jielekeze kwenye hoja.
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] Agnostic au Atheist, nakuambia kama huwa unaenda kanisani basi ni kama kutimiza wajibu tu na kushiriki na jamii, ila wewe u dont believe in God.
Argumentum ad hominem!
 
That's exactly my point, mleta mada ana matatizo ya kiakili.
Wewe unayeshindwa kuelewa na kutumia the fundamental principle of individuation ndiye mwenye matatizo ya kiakili. Period!
 
You

You have all the characteristics of atheism.

1.You dont believe in religious teachings but you are quite knowledgably about religions.

2.You identify yourself as Mama Amon.This means your meaning of life is derived from having a family rather than worshiping God.

3.You sound very young.Most atheist are young male peoples.

The only thing that does not fit is that you are a female.
Argumentum ad hominem again!
 
Niliumbwa na wazazi wangu, wazazi waliumbwa na mababu na mabibi, na mnyororo unaendelea kinyume nyume hadi huko mbali kwenye hatua ya kwanza ambako inaaminika kulikuwa na chanzo kisicho na mwanzo, kisababishi kisicho na kisababishi.

Chanzo cha kwanza ndiyo kitu ambacho baadhi ya watu hukiita Mungu. WEngine wanapinga, na mjadala unaendelea hadi leo na haujafungwa.

Usinijadili mimi mleta hoja, jielekeze kwenye hoja.
Hahahaha..

We unajuvua nguo hadharani bwana.. nikukumbishe kitu? Jana ulisema MUNGU WAKO AMEKURUHUSU ULE KITIMOTO (naomba ushahidi thabiti katika hili..!)

Leo nipo free... You have my time.
 
Mungu aliyeniumba mimi ananiruhusu kula kitimoto.
Aliyemuumba Mufti anakataza kitimoto.
Hapo vipi?
Nipe ushahidi wa Mungu aliyekuumba kukuruhusu ule kitimoto...
Na...
JE MUNGU ALIYEKUUMBA WEWE NDO WAZAZI WAKO KAMA ULIVYOSEMA HAPO JUU?

Una balaa ya ki-ANTIBIOTIC..

Do you know Gentamicin?
 
JE MUNGU ALIYEKUUMBA WEWE NDO WAZAZI WAKO KAMA ULIVYOSEMA HAPO JUU?
Ukitaka twende pamoja, tuliza akili. Uliza maswali yenye usanifu.
Hili swali halina umakini wowote. Sijasema "Mungu aliyeniumba ni wazazi". Nimesema "walioniumba ni wazazi".

Kuumba ni kukipa kitu umbo. Baba alizalisha spematoza, mama akzalisha ovamu, kisha wazazi walitiana, spematoza ya baba ikasafiri kutoka kwenye mrija wa ngono hadi kwenye mrija wa falopia na kukutana na ovamu, urutubisho ukatokea, mimba ikashika kwenye tumbo la uzazi, mimba ikatunzwa humo kwa miezi 9, kisha nikazaliwa, wazazi wakanipa chakula, wakanilaza, wakanivalisha, wakanisomesha, hadi nikawa hivi nilivyo. Wameniumba. Simple.

Halafu mtu anakuja na kusema "aliyekuumba ni Mungu" Kivipi? Wengine eti alishirikiana na wazazi. Kivipi? Nakataa yote mawili mpaka hapo ushahidi utakapowekwa mezani. Mjadala uendelee
 
Do you know Gentamicin?
Hili swali nimelipuuza mara zote ulipoliuliza. It is intended to be used analogically by you. Proceed as you wish. I don't have to invest my time doing your work... Hata kama sijui, nitatafiti na kujua, then nitakujibu.
 
View attachment 1897959
Rodrick Lutembeka, mmoja wa viongozi wa Baraza la Wazee Chadema

Tangu Freeman Mbowe alipokamatawa na kufunguliwa mashtaka yanayohusiana na ugaidi, viongozi wa Chadema Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam wamekuwa wanahamasisha maombi katika makanisa mbalimbali, bila kujali Mbowe anamwamini Mungu yupi.

Kuna wanaopeleka matoleo kwenye parokia za Kanisa Katoliki. Wengine wanapepeleka makanisa ya KKKT. Na baadhi wanasali novena barabarani.

Kama mambo haya yangefanyika kabla ya Matengenezo ya Kiprotestanti (Reformation) yaliyoendeshwa na Martin Luther wa Ujerumani, yangeweza kuingia akilini. Wakati huo Kanisa la Kikristo lilikuwa moja. Lakini hali sio hivyo leo. Ukweli wa leo ukom hivi:

  1. Kwa mujibu wa kanuni ya kutofautisha vitu vinavyohesabika kwa kutumia vigezo vya lazima na vyenye kutosheleza utambulisho wa kitu katika upekee wake, kila mahali penye utofauti katika idadi ya sifa za utambulisho wa vitu vilivyo mbele ya mtazamaji kutakuwa na vitu vingi, na kila mahali pasipo na tofauti katika idadi ya sifa za utambulisho wa vitu vilivyo mbele ya mtazamaji kutakuwa na kitu kimoja.
  2. Kuna utofauti katika idadi ya sifa za utambulisho wa Mungu wa Wakatoliki, Mungu wa Walutheri, Mungu wa Waislamu, MUngu wa Wasabato, na kila muungu baki.
  3. Kwa hiyo, Mungu wa Wakatoliki, Mungu wa Walutheri, Mungu wa Waislamu, MUngu wa Wasabato, na kila muungu baki, ni Mungu tofauti, na uwepo wa kila Mungu aliyetajwa unakubaliwa kwa vitendo na wafuasi wa Mungu huyo na kukanwa kwa vitendo na watu wasio wafuasi wa Mungu huyo.
That is:
  1. According to the principle of necessary and sufficient conditions for the individuality of an entity, wherever there is property difference between two entities there is numeric diversity and that wherever there is absolute property similarity between two entities there is numerical identity.
  2. There are property differences between Catholic God, Lutheran God, Islamic God, SDA God , etc
  3. Thus, Catholic God, Lutheran God, Islamic God, SDA God, and so on, are distinct Gods, where the existence of each God is practically asserted by its followers and practically denied by its non-followers.
Accordingly:
  • For a catholic X, a Lutheran God is not.
  • A believer in the non-existence of a given God is called an atheist.
  • Thus, with respect to a Lutheran God, X is an atheist.
Again:
  • For a Lutheran Y, a Catholic God is not.
  • A believer in the non-existence of a given God is called an atheist.
  • Thus, with respect to a catholic God, Y is an atheist.
In effect:
  • We may pray for atheists so that they may be converted from unbelief status to belief status and not otherwise.
  • For these reasons, all Lutherans including Mbowe are atheists with respect to Catholic God.
  • And all Catholics, including Pope Francis, are atheists with respect to Lutheran God.
Finally:
  • The god of the Old Testament whose third person is disincarnated is not identical with the god of the New Testament whose third person is incarnated ;
  • A contraceptophobic god of the Catholic Church is not identical with a contraceptophilic god of the Lutheran Church;
  • A god whose third person comes from the father and the son, as taught by the Western Christian Churches, is not identical with a god whose third person comes from the father alone as taught by the Eastern Christian Churches.
  • A god who prefers to be worshipped on Sunday is not identical with a god who prefers to be worshipped on Saturday;
  • A god who prefers to be worshipped in Friday is not identical with a god who prefers to be worshipped in another day;
  • A god who prohibits his followers to eat pork is not identical with a god who allows his followers to eat pork;
This is what the elementary metaphysical principle of individuation, properly understood, teaches us.

Sasa swali kuu na majibu yangu

Kwa hiyo basi, ninawaalika Viongozi wa Chadema kujiuliza na kujibu swali lifuatalo: Kumwombea Mbowe ni sehemu ya ibada kwa Mungu yupi?

Kwa kuzingatia matakwa yakanuni ya kutofautisha vitu vinavyohesabika kwa kutumia vigezo vya lazima na vyenye kutosheleza utambulisho wa kitu katika upekee wake, kama ilivyofafanuliwa hapo juu, binafsi napendekeza yafuatayo:
  • Kwamba, Mungu wa KKKT anayeabudiwa na Mbowe ni tofauti na Mungu wa Wakatoliki anayeabudiwa na wafuasi wa Mbowe ambao ni Wakatoliki;
  • Kwamba, Mbowe amekuwa anamkana kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo Mungu wa Wakatoliki.
  • Na kwamba, kwa sababu hiyo, Mbowe hana haki ya kuombewa na wafuasi wake kupitia kwa Mungu asiyemwamini.
Mbowe hamtambui Mungu wa Wakatoliki tangu siku alipobatizwa chini ya madhehebu ya KKKT, na hadi leo hajatwambia kama amemkana Mungu wa KKKT na kumkubali Mungu wa Wakatoliki.

Kwa hiyo, Mungu wa Wakatoliki hawezi kusikiliza wala kupokea matoleo yanayopelekwa ndani ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya kumwomba Mungu wa Wakatoliki amtetee Mbowe, mpaka hapo Mbowe atakapomkiri kwamba yeye pekee ndiye Mungu wa kweli.

Hivyo, viongozi wa Chadema wanapaswa kuacha maigizo kama yale ya "mitano kwanza" na "mitano tena" tuliyoshuhudia mwaka jana.

Vinginevyo watayafikisha makanisa mahali ambapo kanisa lile lile moja linapokea matoleo ya kuomba mbowe atiwe hatiani na kuyabariki leo; halafu kesho yake, kanisa hilo hilo linapokea matoleo ya kuomba mbowe asitiwe hatiani na kuyabariki.

Dini zitadhalilika sana kwa njia hii.

Nijuavyo mimi, ukweli ni kwamba: Mungu anayewaunga mkono watu wanaotaka Mbowe atiwe hatiani na Mungu anayewaunga mkono watu wanaotaka Mbowe asitiwe hatiani ni Miungu wawili tofauti!

Lakini, tunafundishwa kuwa Mungu wa kweli habadiliki wala kubadilisha mawazo yake.

Kwa hiyo, mmojawapo kati ya miungu hawa wawili atakuwa ni Mungu feki, yaani Mungu wa kuchonga (constructed God), wakati mwingine ni Mungu wa kweli (essential God).

Kanuni nne za kuongoza mjadala:

Kusudi, viongozi wa Chadema waweze kuelewa msingi wa swali langu hapo juu na kulitendea haki, hapa chini nafafanua kanuni NNE zinazopaswa kuongoza mjadala huu. Kanuni hizo ni:
  • kanuni ya kutambua kitu kimoja chenye majina tofauti (principle of identity),
  • kanuni ya kutofautisha vitu vinavyohesabika (principle of difference), na
  • kanuni ya kutengeneza fasili zinazotaja sifa za lazima na zenye kutosheleza utambulisho wa kitu.
  • kanuni ya sifa za lazima katika utambulisho wa kitu (principle of necessity)
  • Kanuni ya sifa zenye kutosheleza utambulisho wa kitu (principle of sufficiency).
Kanuni ya kutambua kitu kimoja chenye majina tofauti

Mosi, ni kanuni ya kutambua kitu kimoja chenye majina tofauti, yaani the principle of the Identity of indescernibles.

Kwa mujibu wa kanuni hii, kunapokuwa na majina mawili yanayorejea kitu kimoja kile kile, hiyo maana yake ni kwamba, kila sifa iliyofungamana na kitu chenye jina la kwanza pia imefungamana na kitu chenye jina la pili, na kinyume chake ni kweli.

Yaani, kwa kila jozi ya vitu, kimoja kikiwa na jina X na na kingine kikiwa jina Y, jina X litakuwa linamaanisha kitu kile kile kitu kinachorejewa na jina Y, endapo na endapo tu:

Kwa pamoja, sentensi kwamba:

(1) kila sifa iliyofungamana na kitu X pia imefungamana na kitu Y;

na sentensi kwamba:

(2) kila sifa iliyofungamana na kitu Y pia imefungamana na kitu X.

ni za kweli.

Kwa mfano,
  • Julius ni jina linalorejea mtu yule yule anayeitwa Nyerere. Yaani, Julius na Nyerere ni majina ya kitu kimoja.
  • Na, DOG ni jina linalorejea kitu kile kile kinachoitwa MBWA. Yaani, DOG na MBWA ni majina ya kitu kimoja.
Kanuni ya kutofautisha vitu vinavyohesabika

Pili, ni kanuni ya kutofautisha vitu vinavyohesabika, yaani the principle of dissimilarity of the diverse.

Kwa mujibu wa kanuni hii, kunapokuwa na majina mawili yanayorejea vitu tofauti kwa mujibu wa utaratibu wa kuhesabu, basi, hiyo maana yake ni kwamba, sio kila sifa iliyofungamana na kitu chenye jina la kwanza pia imefungamana na kitu chenye jina la pili, na kinyume chake ni kweli.

Yaani, kwa kila jozi ya vitu, kimoja kikiwa na jina X na na kingine kikiwa jina Y, jina X litakuwa linamaanisha kitu tofauti na kile kitu kinachorejewa na jina Y, endapo na endapo tu:

Ama:

(1) katika seti ya sifa za kitu X angalau kuna sifa moja P, ambayo haipatikani kwenye seti ya sifa za kitu Y,

Au:

(2) katika seti ya sifa za kitu Y angalau kuna sifa moja Q, ambayo haipatikani kwenye seti ya sifa za kitu X.

Kwa mfano:
  • Mipira miwili ya tufe, iliyowekwa mezani, na ambayo inafanana kwa kila kitu, bado tunaitambua kuwa ni mipira miwili tofauti kwa kuwa, kila mpira unayo anwani yake ya kijiografia. Hata watoto mapacha sisisi tunawatofautisha kwa njia hiyo.
  • Vivyo hivyo, Miungu inayependa kuabudiwa Ijumaa (Miungu ya Waislamu) na Miungu inayependa kuabudiwa Jumapili (Miungu ya Wakristo) ni Miungu tofauti, kwa sababu hiyo pekee.
  • Kadhalika, Miungu inayependa kuabudiwa Jumamosi (Miungu ya Wasabato) na Miungu inayependa kuabudiwa Jumapili (Miungu ya Wakristo bado) ni Miungu tofauti, kwa sababu hiyo pekee.
  • Aidha, Miungu inayoruhusu waamini kutumia kondomu (Miungu ya Waanglikana) na Miungu inayokataza kondomu (Miungu ya Wakatoliki) ni Miungu tofauti, kwa sababu hiyo pekee.
  • Vile vile, Miungu inayokataza makuhani kuoa (Miungu ya Wakatoliki) na Miungu inayoruhusu makuhani kuoa (Miungu ya Waanglikana na Walutheri) ni Miungu tofauti, kwa sababu hiyo pekee.
  • Mungu anayewaunga mkono watu wanaotaka Mbowe atiwe hatiani na Mungu anayewaunga mkono watu wanaotaka Mbowe asitiwe hatiani ni Miungu wawili tofauti!
  • Na mifano inaendelea kama inavyothibitishwa na utitiri wa usajili wa taasisis za kidini katika ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Kanuni ya kutengeneza fasili zinazotaja sifa za lazima na zenye kutosheleza utambulisho wa kitu

Na tatu, ni kanuni ya kutengeneza fasili zinazotaja sifa za lazima na zenye kutosheleza utambulisho wa kitu. Yaani necessary and sufficient definitions.

Ukitaka kukitambulisha kitu kama vile kitu chenye umbo mraba, kwa namna ambayo inatofautisha umbo mraba na vitu baki, lazima kutaja vigezo vinavyomwezesha msikilizaji kufanya mambo mawili.

Mosi, ni kutambua mraba ni kitu gani. Na pili ni kutambua mraba sio kitu gani.

Kazi hizi mbili zinafanyika kwa njia ya kutaja vigezo ambavyo ni vya lazima na vyenye kutosheleza utambulisho wa kitu kinachoongelewa.

Kuhusu vigezo vya lazima, tuchukue mfano wa fasili ya kitu chenye umbe la mraba. Ni lazima kila mraba uwe na pande nne.

Lakini, sifa hii haitoshi kuutofautisha mraba na maumbo baki kama vile mstatili ambayo pia yanazo pande nne.

Na kwa upande mwingine, kuna vigezo ambavyo vinatosheleza kukitambulisha kitu, lakini sio vya lazima kwa ajili ya utambulisho huo.

Mfano, katika mazingira ya shule mwanafunzi anayepata alama ya A anapasi kozi.

Lakini, alama ya A sio alama ya lazima ili kumfanya wanafunzi huyo apasi kozi. Anaweza kupasi kwa kupata alama ya B, C au hata alama D.

Hivyo, kupata alama ya A ni kigezo cha lazima katika kupasi kozi, lakini sio kigezo kinachotosheleza matakawa ya kumpa mwanafunzi sifa ya kuhesabiwa amepasi mtihani, kwani hata wale wanaopata B, C na D hupasi pia.

Kwa sababu hii, kwa ajili ya kueleza mraba ni kitu gani na sio kitu gani kwa mpigo, tunahitaji mambo mawili:

(1) kutaja kigezo kimoja kimoja ambacho ni lazima kihusike katika kutambulisha mraba.

Na (2) kutaja seti ya vigezo vyote ambavyo kwa pamoja vitatosheleza kutofautisha mraba na maumbo baki yenye pande nne.

Kwa hakika, kila mraba lazima uwe na sifa zifuatazo kwa mpigo: pande nne, pande zilizo nyooka, pande zinazolingana, pande zilizoungana katika ncha zake, pale zilizo katika ubapa mmoja, na lazima uwe na kona nne zenye nyuzo 90 kila moja.

Kanuni hizi tatu zilizotajwa hapo juu, zinapaswa kutumika katika kutambua na kutambulisha kitu chochote kama vile mbuzi, kondoo, mti, mtu, miungu, na kadhalika.

Hivyo basi:

Ukweli ndio huo, na hayo ndiyo madhara yasiyotarajiwa yaliyoletwa na Matengenezo ya Kiprotestanti (Reformation) yaliyoaasisiwa na Matrin Luther wa Ujerumani.

Kwa uelewa zaidi soma kitabu: The Unintended Reformation: How a Religious Revolution Secularized Society by Brad S. Gregory (Attached).
Ukiwekeza nafsi yako kwenye 'Dini' badala ya kuwekeza kwa 'Yesu Kristo' nachelea kusema utapata 'kizunguzungu'.
 
Back
Top Bottom