Swali kwa waliooa tu: Mlipataje wanawake wa kuoa?

Swali kwa waliooa tu: Mlipataje wanawake wa kuoa?

capernaum ushauri mdogo ninaweza kukupa ni kuwa 'stop being a veeeeery good boy', wanawake wengi hawapendi 'simps', yaani usiwe na mwanamke ukamuonesha wewe ndiyo 'desperate' wa hayo mahusiano kumzidi hata yeye, utateswa mpaka uchanganyikiwe..!!

'show her that you do loves her yes, but still you can live your life fully without her in your life, be a man buddy', mwanamke ndiye awe mnyenyekevu kwako, siyo wewe uwe mnyenyekevu kwa mwanamke 'it doesn't work that way', umewahi jiuliza kwanini 'bad boys' ndiyo wanatesa wadada..??

Sababu WANAJIAMINI, na wanajua wao ni 'WANAUME'..!!
Anha sasa ume ni provia
Sasa sikilizieni shemeji yenu atajua hajui.
 
Sio Kwa ubaya njoo nikupe mdogo wangu ila sijajua ni din gan ila mdogo wangu na yeye anatafuta mume
 
Dada zetu hao wanapenda bad boys,ila baadae sana baada ya kuumizwa na kutendwa na kuzalishwa wanaanza kutafuta good/nice boys,yaani hutafuta kitu ambacho mwanzoni walikuwa nacho na kukidharau.

Mwanangu wewe kaza concentrate na mambo yako mke atakuja mwenyewe na husibadilike kitabia,eti uwe bad boys kuwa hivyo hivyo ndivyo Mungu alivyo kuumba,unaweza ukasema uchange kidogo eti uwe bad boys ukaja kupotea mazima.

Honestly wanawake ni wa kuonewa huruma hawajawahi kujua wanacho kitaka, kuna mabinti wawili yaani ni majirani ambao tumekuwa kama ndugu,wamekuja kuzalishwa na watu wa hovyo, wakati kulikuwa na wana walikuwa wapo tayari kwa kila kitu, mmoja kazalishwa na muimba singeli,mwengine bodaboda, maana walikuwa wanataka bad boys na kweli wamepewa mabad boys kiwango cha lami.

Bro usiumie kichwa concentrate na mambo yako mke wako atakuja mwenyewe.Huyo mwache na mara nyingi huwaga na tabia ya kurudi na kujuta, nimesha shuhudia sana marafiki zangu,achana nae fanya mambo yako.
Daah, kwahiyo wakirudi jamaa zako wanawapokea au?
 
Mimi nilishangaa tu gafla nmekutana na mtoto mzur mtoto rangi fulani hivi chokoleti amazing ndio mpk sasa amekuwa waifu sema nn kwa sasa kutafuta mke ni kazi kuliko kutafuta pesa
 
Tupate matangazo kidogo kwa hisani ya dronedrake

Tunakula ujana mabachela bachela
Waache waoane

Okay lets go
Mi ni chizi wa mapenzi
Na nina upendo
Ila kuhusu ndoa ndo sina mpango
Na ukipata niliyemuacha hauzibi pengo
Ndoa lini hizo kelele za chura kwa tembo
Guys listen to me napenda kuwa free
Wengi wapo kwenye ndoa na hawatulii
Nikisema ndoa ndoa hata mnitangaze BBC
Palipo furaha nipo kama moyo wangu una WiFi
Bachela vibe ni confidence maisha ni kuchagua tumechagua hapiness
Happiest no ndoa no stress vichwa vina mambo mengi tuna-refresh
Mi na shemeji yenu daily tuna-party
Mambo ya ndoa wote hatuyataki
Purukushani unarudi saa ngapi unachati na nani ndo vitu hatutaki

Bachelaz michango tutachanga changa
Kwenye harusi tutakuja kuja
Chakula tutakula kula
Na pombe tutalewa lewa
Wenyewe si bado tupo si bado tupo
Hivi wakina nani nyie

Sisi ndo mabachela bachela
Hatutaki ndoa mabachela bachela
Tunakula ujana mabachela bachela
Waache waoane

Sing again bachelors

Sisi ndo mabachela bachela
Hatutaki ndoa mabachela bachela
Tunakula ujana mabachela bachela

Waache waoane
NAKAZIA
 
Mshirikishe Mungu,
Amesema apataye mke amepata kitu chema,naye amejipatia kibali kutoka kwa Bwana

Lakini pia amesema katika kitabu cha Isaya

"Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana, hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake. Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza, na Roho wake atawakusanya pamoja..."

Lakin pia Amesema tena katika kitabu cha isaya 60:22

When the time is right,
I,THE LORD, will come quickly...I will make these things happen

Na Mungu akupe hitaji la moyo wako
Maneno matamu sasa njoo kwenye practical aloooh! Shida kweli kweli
 
Hii thread ni Tamu Sana...Imenifundisha vingi sana
Ata mie imenifundisha kikubwa wanaume tupate wake wakati mambo hayajatiki. Yule atakaye vumilia wakati unasubiri mchongo utiki huyo ndio wife.
Mlaze kwenye godoro, no nauli no presents na importantly hakuna kugegeda
 
Aise mimi nilisema nitatafuta mke wakati sina kazi ya kueleweka! Na kila mwanamke niliyempata kipindi kile nilikuwa namleta ghetoni kwangu kwa lengo la kuona mazingira tu! Wasichana wengi waliokuwa wanakuja gheto baada ya hapo hata simu zangu walikuwa hawapokei baada ya kuondoka! Baadaye alitokea mwanamke mmoja aliyekuja ghetoni na yeye aliyakubali yale mazingira na tukaanza mahusiano mpaka leo ndiye mke wangu miaka 6 sasa! Naweza kusema miongoni mwa wanawake kumi bora sio kwa sura kwa tabia nzuri za wife material yeye basi ni namba moja! Mpaka leo nina kazi nzuri hajawahi kubadilika! Wewe uwe na hela usiwe na hela utamfurahia tu! Kipindi chote cha uchumba sikuwahi kumpa zawadi yoyote na kipindi chote cha uchumba na mahusiano hatukuwahi kufanya mapenzi!! Ndivyo nilivyompata mke wangu
Brother uyo mwanamke apewe maua
 
Pumzika kama mwaka hivi kisha anzisha mahusiano na binti mbichi miaka 18 - 24 kisha leta mrejesho, mabinti wengi 25 na kuendelea hisia za mapenzi zinakuwa haziko stable
Unataka ummalize mwenzio, mabinti wa huo umri tajwa wengi wao bado hawajafaidi hii dunia, watakua wanapishana sana na mdau ,jamaa anataka kufanya jambo la msingi yeye anataka kupariiii
 
Moja ya swali ambalo najiuliza daily ,mlipataje wanawake wa kuoa .nasoma uzi wote nipate uzoefu.
 
Hbr wana JF,

Mwaka jana nilipata binti mmoja ambae tulifahamiana kwa muda kidogo tukaanza mahusiano. Nilimpenda sana, nikajitahidi kumtimizia kila analohitaji. Nilijifunza kwenye mahusiano yangu ya awali, nikasema huyu nifanye tofauti sasa na mimi niwe na familia. Mwanzo mapenzi yalikua motomoto, tukaanza kupanga mipango ya ndoa kabisa huu mwaka tuwe mume na mke.

Baada ya miezi kadhaa, akaanza kubadilika. Nakumbuka alianza kununa tukiwa vacation Zanzibar. Akawa kama ana moods hivi, ukimuuliza kuna changamoto gani hasemi. Nikaona mambo ya kike labda nitulie. Basi kuanzia hapo akawa kama anani dharau na hanijali tena kama mwanzo. Nilikua naumia ila nikawa navumilia. Lakini kwa tabia zile alizoanzisha ikanilazimisha baadhi ya mambo tulipanga kufanya - kama kwenda kujitambulisha kwao tusitishe kwanza maana sikua namuelewa, anasahau mpaka tarehe muhimu kwenye mahusiano yetu kitu ambacho sio cha kawaida. Baada ya muda nikaenda nje ya nchi kikazi, katika nchi ambayo tulikua tunapishana masaa na hapo ndio mapicha picha yakazidi akawa hapokei simu kabisa akidai yuko busy etc. Kwa muda wote niliokua nje ya nchi kama miezi miwili hatukuwahi kuongea kwenye simu, kila nikijaribu kumtafuta anasema yuko busy atanicheki lakini hafanyi hivyo. Basi nikaanza kufanya maamuzi magumu, nikaacha kumpa monthly allowance na kumnunulia zawadi kama nilivyokua nafanya mwanzo. Nilivyorudi nchini, bado nikamtafuta kujua tatizo ni nini na nakumbuka pamoja na tofauti tulizokua nazo bado nilitoka ulaya na zawadi kadhaa nimemchukulia nikampa. Kikao hakikuenda sawa, binti akaniambia hana feelings na mimi na nikitaka kuwasiliana nae lazima nifanye appointment au nitafute mwanamke mwingine wa kua nae. Aisee, kikao kiliishia hapo. To cut the story short, mahusiano yaliisha pia.

Hii ni case moja tu kati ya nyingi ambazo nimeshakumbana nazo. Katika miaka 10 iliyopita nishakua kwenye mahusiano mengi sana na yamekwama kwa sababu tofauti tofauti, ingawa hii ya juzi iliniuma maana nilijitahidi kufanya kila kitu inavyotakiwa na mhusika mwenyewe pia nilijua anajitambua maana at 31 ni mtu mzima sio mtoto mdogo ni mwanamke aliepitia mengi. Mwaka umeanza nimekata tamaa kama naweza kweli na mimi siku moja kupata mke, nikaanzisha familia na kua na watoto. Kila kitu ninacho - kazi nzuri, kipato kizuri yani ni mke tu ndio imekua changamoto. Kuna wakati najilaumu labda ningekua nakunywa pombe & mtu wa starehe huenda ingekua rahisi kwangu maana haya maisha ya kua busy na kazi muda wote nayo ni changamoto sikutani na watu ila ndio nafanyaje sasa na pesa naitaka pia.

Naomba ushauri wadau, nifanyeje?!


NB:
Niliwahi kuandika uzi humu wa kutafuta : A wife is needed
Mapenzi hayalazmishi mtu unafanya ujinga unakaa na kusema unampenda...hapo hakuna mke ni matatizo unajitafutia tu
 
Back
Top Bottom