Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Chief,
Kikubwa kiumeni mbadirike!!

Tusaidiane namna ya kuokoa jamii na sio kusimamia upande mmoja wa jamii huku ukijiaminisha kwamba mwingine ni dhaifu! Wengi wa kikeni wana fanya kama Pay back tu kiasi ambacho wanafikia kuumiza miili na nafsi(kile kile ambacho ndio ugonjwa wa kiumeni!)

Kikubwa tukubali tuu, hapa duniani hata sisi tumeumbwa kama nyinyi na kadiri tutakavyoendelea kupingana tutaendelea kushuhudia uovu husio mithirika!!

Siku yaja, tuandae majibu!!
Daaah Chief hakika Unatukandamiza Upper Cuts Za Maana Usoni Mwetu....

Pale Wanaume Tunapowashambulia wanawake kuwa ni SUBMISSIVE HUMANS...huwa ninafikiria...kwani KUUMBWA MWANAUME ni zawadi Bora kutoka kwa Allah?!!!

Je Allah Ameamua kutuumba WANAUME na kutupendelea?!!!
Je ningeumbwa mwanamke ndio nikubaliane na KUKANDAMIZWA kwa kuwa mm ni DHAIFU ninayestahili KUTAFUTIWA CHUMO la kutia tumboni mwangu Mara 3 kwa siku?!!!
Maswali yanakuwa mengi mno.....

Tatizo Hatupendi Kutafakari vyema.....

Chambilecho Coach,siku YAJA.....
 
Uislamu haumkandamizi mwanamke ila baadhi ya vikundi vya waislamu ndo vinatumia dini kumkandamiza mwanamke. Haya taliban imeweka sheria mwanamke akienda shule apigwe risasi haya hiyo sheria ipo kwenye aya gani au hadithi ipi. Tushukuru tu tupo kwenye utawala wa demokrasia maana kwa hoja zako na mtoa mada mngetupiga risasi wanawake tunaotafuta maendeleo ni vile tu mnaogopa dola.

Hiyo Taliban wala husishangae!! Imagine hao ni katika jamii ya kiumeni ambao mpaka leo wanapata wanawake (wake wa ndoa) kwa system ya “kamtwale tugende “ (kumteka njiani mpaka ndoani!)

Wanaume (naongelea wanaume haswaaa) wasimame imara! Watambue ukichwa wa familia sio ukichwa wa kichwa cha chini(mkia,Nyoka)!!
 
Dah ila aiseee wewe dada sijui mamdogo una akili ndogo sana. Samahani kama nitakuwa nimekufedhehesha ila umefeli kutumia akili yako vizuri kwenye hili.

Hivi hata ukisoma hapo alichoandika huyu jamaa kina shabihiana na argument yako uliyojibia hapa?!

Kweli kizazi hiki ni kinapotea kwa kukosa maarifa na kuwa nan fikra ndogo.

Mimi nitajaribu kukuelewesha tena usipoelewa basi ubakie ulivyo maana sidhani kama uzito wako wa kuelewa mambo ya hii dunia utakuja nigharimu anytime soon.

Huyu uliyemjibu hapo alichomaanisha ni kuwa nyuma ya ajenda ya kumnyanyua mwanamke kumejificha matukio ya kumtumia bila yeye kujijua na kimsingi ni kama wale wale wanaodai kumkomboa ndio hao hao wanaanza mshusha sasa indirectly bila kujijua.

Mfano amekupa hapo, ni kwann wanawake ndio wanatumia katika maeneo ya ushawishi wa kibiashara kama point si kumuuzia mteja mwenye interest ya kingono ndipo avutiwe na kitu chenye mvuto wa ngono, yaani mwanamke. Si hata kwenye. Mabasi ya mkoani tumeona hayo mambo wanawaka wadada kuvutia biashara, Bar, mahoteli na hata receptionists wengi hutegwa wanawake......

Point yake ni kuwa mwanamke anapoolewa si kwamba asifanye kazi au kujazia kipato cha familia. Ila anajaribu kuiweka bayana kuwa kwa sasa mwanamke anakuwa busy sana na purukushani za maisha kiasi kwamba anakuwa na less efforts na time kwaajiri ya familia yake jambo ambalo ni chukizo na kinyume na maagizo ya MUNGU.

Sasa wewe umekazania katika kumpinga badala ya kuzungumzia hoja yake.....

Hoja ya mwenzako ni kwamba, kadili mwanamke anapojiweka mbali na maisha ya familia ndivyo anavyozidi kuwa katika mazingira ya ushawishi wa kufanya maasi kama kuwa na mwenzi nje ya ndoa, kuzaa nje ya ndoa, kutokujali ndoa, kuingia katika ulevi na ukahaba wa kisasa, na kadhalika.

Hivi wewe huwa hauwezi kujibu hoja bila kumdhihaki mtu. Sio mara ya kwanza wala mwisho kuona hii tabia yako jifunze kujibu hoja kistaarabu mbona utaeleweka tu.
 
Wewe kama unajiona una akili sana sawa.

Tena acha mambo ya kuniquote kama huwezi kujibu kistaarabu.
 
Hivi wewe huwa hauwezi kujibu hoja bila kumdhihaki mtu. Sio mara ya kwanza wala mwisho kuona hii tabia yako jifunze kujibu hoja kistaarabu mbona utaeleweka tu.

Nikwambie kitu Chief?!, kiumeni silaha kuu kwenda kikeni ni kashfa na maneno ya hovyo yanayoamsha hisia......ila....achana nao! Husikubali wakutoe kwenye njia, puuza ujinga simamia hoja!! Kamwe husijibizane nje ya hoja!

Hoja kwa hoja, sauti zetu ni silaha ila busara zetu humtoa nyoka pangoni!
 
Wewe kama unajiona una akili sana sawa.

Tena acha mambo ya kuniquote kama huwezi kujibu kistaarabu.
Nimekujibu kistaarabu. Kuna maneno hapa nikiyatumia utahisi au utasema nimekutusi wacha niishie hapa....
 
Hiyo Taliban wala husishangae!! Imagine hao ni katika jamii ya kiumeni ambao mpaka leo wanapata wanawake (wake wa ndoa) kwa system ya “kamtwale tugende “ (kumteka njiani mpaka ndoani!)

Wanaume (naongelea wanaume haswaaa) wasimame imara! Watambue ukichwa wa familia sio ukichwa wa kichwa cha chini(mkia,Nyoka)!!
😂😂😂😂😂😂😂Loooh

Sasa Kweli Mwanaume "Kichwa Wa Familia" atataka kufanya rejea kwa Taliban na Jamaa Zetu Wa Najd Anaowapenda Jurjani?!!

Nami niliambiwa kuwa hao FEMINISTS Ni wabayaa....sisemi kuwa kila wasemalo Ni Bora...laa hasha ila nilipozidi kukua nikajifunza kuwa MSIKILIZAJI NA MTAFAKARI wa hoja nisizozipenda😁😁....yeah kuna Mengi ya Maana TUNAYAKOSA simply kwa UJAHILI na MORI wa kiume tulioukuta juu ya JAMII ZETU....
 
Sasa okey tufanye kusoma ni ibada,yaani kusoma udaktari ni ibada,kusoma unesi ni ibada,kusoma urubani ni ibada twende kwa ufahamu wako huo.

Sasa ibada hizi za udaktari,urubani,unesi wanaruhusiwa wanaume tu kuzifanya na sio wanawake ?

Sasa sawa ni ibada je Ushahidi kuwa wanawake hawatakiwi kuzifanya ibada hizi uko wapi ?

Nadhani unatambua fika kuwa ibada yeyote akiruhusiwa mwanaume basi na mwanamke inamuhusu mpaka ije dalili ya kumvua mwanamke kuwa hii na hii haimuhusu.

Sasa huu udaktari,uhandisi,unesi kama hizi ni ibada wapi mwanamke kakatazwa asizifanye ?
Unapiulizwa swali, unatakiwa ujibu swali, siyo unaleta makadirio, mara "tuchukulie kadha" hili ni jambo la dini, na limeshahukumiwa.

Pili, ongeza umakini ili usiwe unapoteza muda kuandika kitu ambacho hujaulizwa.
Huo uchambuzi uweke wewe ili uwaongoe watu kinyume na ninavyofanya mimi sio kuwa na madai matupu ndugu jurjani

Mwanachuoni wa usuli na Mufasiri, aitwae Muhammad al Amiinash Shanqiitwiy al Jakaniy (Allah amrahamu) ana maelezo mazuri sana katika kuelezea hiyo Kaida uliyo iweka hapa, na hapa nakunukulia alichokiandika katika kitabu chake cha Tafsiri ya Qur'aan, kiitwacho "Adh'wau al Bayaan fiy Idhwah Qur'aan bil al Qur'aan"

Anasema yafuatayo :

وقد حقّق الشيخ المفسّر محمد الأمين الشنقيطي رحمه الله تعالى هذه المسألة ؛ فقال :
" إن كان فيها ضرر لا يشوبه نفع ، فهي على التحريم ؛ لقوله - صلى الله عليه وسلم: ( لا ضرر ولا ضرار ) .
وإن كان فيها نفع من جهة ، وضرر من جهة أخرى ، فلها ثلاث حالات :
الأولى : أن يكون النفع أرجح من الضرر .
والثانية : عكس هذا .
والثالثة : أن يتساوى الأمران .
فإن كان الضرر أرجح من النفع أو مساويا له ، فالمنع ؛ لحديث: ( لا ضرر ولا
ضرار ) ، ولأن درء المفاسد مقدم على جلب المصالح .
وإن كان النفع أرجح ، فالأظهر الجواز ؛ لأن المقرر في الأصول : أن المصلحة الراجحة تقدم على المفسدة المرجوحة " انتهى من " أضواء البيان " (7 / 793 - 794) .
(Mwisho wa kunukuu)

Madhara yanaanzia katika namna ya mazingira ya upatikanaji wa hizo Elimu.
 
Naomba niandike maoni yangu kwa juzi (experiences) zangu!

Dunia ilipo leo sipo ilipokua miaka kenda ilopita!
Zamani iliwawia rahisi sana kumtenga na kumnyanyasa mwanamke (eti ni dhaifu!)lakini kwa sasa imekua ngumu kwenu kwa maana hata husipompeleka shule bado jamii ya kisasa (social media’s) itamfunza tu, tena itamfunza bila kujali yeye ni nani, amezaliwa na nani wala ametokea wapi!(dunia imekua kijiji!)

Zama hizo tumevumilia utumwa juu yenu ili mradi maisha yetu yaende (ninyi mlisema “mnatusitiri “), mkatupanga kwa foleni ya mke wa kwanza mpaka bi mdogo + nyumba ndogo bado tukajaza maji mdomoni na kukaa kimya tukiamini kweli tuna’sitiriwa’ hatuna ujanja wala uwezo wa kwenda sambamba nanyi!! Kuja kushtuka tayari tumetua ndani ya enzi za sayansi na technology na kushuhudia uwezo wetu kupitia wenzetu!! (Hamtudanganyi tena eti sisi ni “dhaifu”!!)

Zama hizo hizo mlituaminisha ya kwamba “upendo” wa dhati na “heshima “ (kama kijakazi kwa bwanake) ndio msingi mkuu wa ndoa !!! Wala hatukubisha tukaitika ‘ndio bwana’ na maisha yakaenda kwa raha na starehe, kustaajabu tukajikuta tumepangwa kama team ya soccer tukisubiri magoli ya dakika 3 kila mmoja (mke wa kwanza, wa pili, wa 3, wa 4, nyumba ndogo, vimada, wajasiliamwili, na one night stands za kutosha!!) Matokeo yote haya yakazaa viumbe (watoto) wasiokua hata na idea kwanini wameletwa hapa duniani huku sisi wafuasi waaminifu (wamama wa nyumbani) tukibaki na ombwe zito juu ya namna ya kuwawezesha hawa viumbe (watoto) kutambua umuhimu wao hapa duniani (hata kama hawakupanga kuzaliwa ila “ngono” kasababisha) na matokeo yake sasa ndio hawa “millennials “ (kizazi kipya) tunaowaona sasa!!

Ndugu zangu wa kiume, mwanamke hakuumbwa kuwa mjakazi (mtumwa) wako!! Kumbuka hata Muumba wa vyote (God Almighty, Allah Subhanah) aliona wewe “Adam” bila mimi “Hawa” bado hujakamilika!! Akakuzima kwa muda then akanitengeza mimi!!

Wala hakuna ubaya katika mimi Mama wa watoto wako, mwalimu mkuu wa kizazi chako kutafuta Mali (kufanya kazi,biashara,sanaa n.k) Mimi pia ni kama wewe!! Niko na ndoto (life dreams) nahitaji kuzitimiliza! Niko na malengo nahitaji kuyafikia! Niko na dada, Kaka, mama, Baba,ndugu, jamaa na marafiki nahitaji kusaidia! Niko na mipango nahitaji kuikamilisha! Niko na WATOTO nahitaji kuwaandalia baadae yao!!

Suala la kudhalilika sio la mwanamke tu hata mwanamume naye anadhalilika sana tu!! Wangapi?! Situnashuhudia kila kukicha??

Halafu nani anamdhalilisha na kumuangamiza Mwanamke kama sio Mwanamume???? Hebu hii mada igeukie upande wa pili(kiumeni)mjichunguze kwanini yawafaa kuona “udhalili “ wa mwanamke ndio furaha yenu?!?!?

Maoni yangu jamani!! Sitaki kupondwa mawe na wala Msinifokee!!!! [emoji6]
Thread closed
 
Nimekujibu kistaarabu. Kuna maneno hapa nikiyatumia utahisi au utasema nimekutusi wacha niishie hapa....

Kwahiyo unajisifu kuwa na maneno yenye ukakasi🙄

Kujibizana kwa hoja bila kutumia lugha ya ukakasi hata kama unaemjibu amepotoka kunaonesha ukomavu wa hali ya juu.

Jifunze kujibu kwa hoja mkuu sio hivyo unavyofanya.
 
Kwa hiyo kama chenye kuleta madhara ni haramu.
Bila shaka kabisa.
Maana yake udaktari ambao una maanisha ni ibada ni haramu kwa mwanamke udaktari huo ambao kwako kusomea ni ibada ?

Kwa hiyo urubani ambao pengine una maanisha ni ibada,hii ibada ya urubani ina madhara kwa m2anamke kusomea ?
Haya sasa unasema wewe, nilikuuliza swali ambalo hukulijibu, nilikuuliza kusoma ni ibada au si ibada ? Nikaona ukaanza kuleta malezo mengi yasiyo na misingi ga kielimu.
Au unaposema jambo lenye kuleta madhara ni haramu huu msingi unahusiana nini na mada yetu hii inayohusiana na mwanamke kusomea fani hizo ?
Hili ni tatizo lingine la kukosa umakini juu ya mada na kukurupuka, huwezi kuuliza swali hili, isipokuwa wewe hauko makini, hapa tunaangalia madhara ya kile ambacho wanaishi nacho wanawake wa kileo, na huu msingi upo humu.

Madhara yako mengi, kimwili na kiroho (Kidini).

Sasa uharamu wa chakula itakuwa kwako na sio kwa wote.yaani kama bata anakudhuru ukila bata anakuwa haramu kwako wewe na sio kwa watu wote hata
Usiwe unarudia mambo ambayo yako wazi tayari, nani amesema uharamu utakuwa kwa mwingine kwa muda huo ? Huo msingi,ambao kutokana na msingi huo tunarejea.
 
Kaka! Why unanifokea!? Uwongo wangu uko wapi??

Siku nyingine husirudie kuni “generalize” hovyo hovyo!!

*msaidizi wa ndani ‘mdogo mdogo’ ili kichwa cha familia hasimguse! (Wakubwa wakubwa kupindua nyumba sekunde haiishi!)

*mimba/watoto hovyo hovyo mtoa mbegu mwanaume!!

*kwingine kote jisome kama unajiambia mwenyewe!!

Mama zetu wahenga walituasa “”Mwanamume hasiyejua hiyana hana maana!”

[emoji6]
😁😁
 
Kwahiyo unajisifu kuwa na maneno yenye ukakasi[emoji849]

Kujibizana kwa hoja bila kutumia lugha ya ukakasi hata kama unaemjibu amepotoka kunaonesha ukomavu wa hali ya juu.

Jifunze kujibu kwa hoja mkuu sio hivyo unavyofanya.
Okay, my bad... Forgive my rudeness, i had no intention to offend you at all.
 
Sina haja ya kuandika risala ndefu kuonyesha uislamu unavotumika na baadhi ya wanaume kama wewe na kikundi cha taliban kuwarudisha nyuma, kuwadidimiza na kuwatawala wanawake. Uzi wako, mawazo yako na reply zako zinaprove yote hayo kwa ufasaha zaidi.
Bibie nakukumbusha tu ya kuwa Uislamu ndiyo muongozo, na haiwezekani mtu akautumia Uislamu halafu akawa ana mkandamiza mwanamke.

Bibie nasema tena, hapa tunaandika elimu na siyo maoni kwa kujaza kuponi, ndiyo maana hili nililo kuuliza huwezi kulifanya siyo kwamba kisa umeamua, la hasha bali huwezi sababu huna elimu ya kuliandika hili.
 
Kosa ni la kwenu nyie wanaume mmeshindwa kusimamia nafasi zenu. Mnawaza sunna ya kuoa wake wanne yani kila wiki upo busy kuwaza kutimiza wajibu kwa wake wote kwa usawa. Ukipiga viwili huku na kule upige viwili pesa utatafuta saa ngapi? Tupishe na itikadi zako za radio iman kukataza wanawake wasipige simu ety sauti ya kike ni shubha. Yani mnawaza ngono mda wote. Likija kwenye swala la kuwa nyuma kielimu na kimaendeleo haswa kwenye mikoa ya pwani kama tanga, lindi etc mnasema ety wakristo wapo kwenye system hvyo wanawapiga vita waislamu wasiendelee. Acheni kulalamika mda wote mpo kwenye vibanda vya kahawa mnapiga porojo na kucheza bao maendeleo mtapata wapi .wanawake wa kiislamu tumeamua kusoma na kujiendeleza kibiashara n.k mnaleta mawazo ya kusema tunashindana na wanaume. Hao wanaume wanaoshinda vijiweni kupiga soga? Acha basi unaudhalilisha uislamu akhy
Bibie unafurahisha sana, kuna kaida ya kiusuli ina sema hivi "Nia njema haihalallishi njia".

Pili, mwenzako anapo kosea na wewe ndiyo ukosee au unatakiwa ufanye jambo kwa uzuri zaidi ? Hao walio kosea na wewe ndiyo umeauma kukosea ? Sasa mbona huipi akili nafasi yake bibie ?

Tatu, Uislamu hauko hivyo unavyo uchukulia wewe, kwamba usione madhara na kutolea ufafanuzi. Wewe ndiyo unautia dosari kwa kuandika mambo ya uongo, kwa kuanzia pale ulipo mzulia mama Khadija.

Nne, bibi Uislamu ni shule na Uislamu haupelekwi kwa hisia na maoni, bali kwa elimu na burhani na kurejea katika nususi za kisheria.
 
Back
Top Bottom