Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Wewe mkuu ndo una tatizo.
Wanawake karne na karne wanashiriki shughuli za uchumi mpaka wakoloni walipoleta mambo yao.
Na huo utaratibu wa kuwafungia wanawake umeshindwa maana wanaume peke yao hawawezi kutosheleza mahitaji ya familia.

Kwa hiyo kinachoendelea sasa hata baba zetu wanatuunga mkono ndo maana wanatupeleka shule.
 
Uislamu haumkandamizi mwanamke ila baadhi ya vikundi vya waislamu ndo vinatumia dini kumkandamiza mwanamke. taliban imeweka sheria mwanamke akienda shule apigwe risasi hiyo sheria ipo kwenye aya gani au hadithi ipi. Tushukuru tu tupo kwenye utawala wa demokrasia maana kwa hoja zako na mtoa mada mngetupiga risasi wanawake tunaotafuta maendeleo ni vile tu mnaogopa dola.
😁😁😁 Na wangewamaliza...Yaani sisi ndio wanaume tunaojuana vema mentality zetu kuanzia huku kwenye vijiwe vya kahawa,Al Kasus mpaka Maskani za Bao na Keram...

Unajua umeongea Kitu kizito ndugu yangu aiseee acha tu.....mngetandikwa Kama wale wa Kandahar.....

Tatizo sisi wanaume wenzao tukiwaambia KWA upole tu,wanatubandika majina kibwena,mara ooo DUYUTH anatawaliwa na mkewe "mzungu wa tabia mjaa laana" daah😁😁 Mara Ooo Munafiq anayekaribia kuwa Murtad,Sasa unakaa unajitafakari na kuishia kucheka tu na ARGUMENTUM AD HOMINEM zao.....
Hatareee😁😁
 
Naomba niandike maoni yangu kwa juzi (experiences) zangu!

Dunia ilipo leo sipo ilipokua miaka kenda ilopita!
Zamani iliwawia rahisi sana kumtenga na kumnyanyasa mwanamke (eti ni dhaifu!)lakini kwa sasa imekua ngumu kwenu kwa maana hata husipompeleka shule bado jamii ya kisasa (social media’s) itamfunza tu, tena itamfunza bila kujali yeye ni nani, amezaliwa na nani wala ametokea wapi!(dunia imekua kijiji!)

Zama hizo tumevumilia utumwa juu yenu ili mradi maisha yetu yaende (ninyi mlisema “mnatusitiri “), mkatupanga kwa foleni ya mke wa kwanza mpaka bi mdogo + nyumba ndogo bado tukajaza maji mdomoni na kukaa kimya tukiamini kweli tuna’sitiriwa’ hatuna ujanja wala uwezo wa kwenda sambamba nanyi!! Kuja kushtuka tayari tumetua ndani ya enzi za sayansi na technology na kushuhudia uwezo wetu kupitia wenzetu!! (Hamtudanganyi tena eti sisi ni “dhaifu”!!)

Zama hizo hizo mlituaminisha ya kwamba “upendo” wa dhati na “heshima “ (kama kijakazi kwa bwanake) ndio msingi mkuu wa ndoa !!! Wala hatukubisha tukaitika ‘ndio bwana’ na maisha yakaenda kwa raha na starehe, kustaajabu tukajikuta tumepangwa kama team ya soccer tukisubiri magoli ya dakika 3 kila mmoja (mke wa kwanza, wa pili, wa 3, wa 4, nyumba ndogo, vimada, wajasiliamwili, na one night stands za kutosha!!) Matokeo yote haya yakazaa viumbe (watoto) wasiokua hata na idea kwanini wameletwa hapa duniani huku sisi wafuasi waaminifu (wamama wa nyumbani) tukibaki na ombwe zito juu ya namna ya kuwawezesha hawa viumbe (watoto) kutambua umuhimu wao hapa duniani (hata kama hawakupanga kuzaliwa ila “ngono” kasababisha) na matokeo yake sasa ndio hawa “millennials “ (kizazi kipya) tunaowaona sasa!!

Ndugu zangu wa kiume, mwanamke hakuumbwa kuwa mjakazi (mtumwa) wako!! Kumbuka hata Muumba wa vyote (God Almighty, Allah Subhanah) aliona wewe “Adam” bila mimi “Hawa” bado hujakamilika!! Akakuzima kwa muda then akanitengeza mimi!!

Wala hakuna ubaya katika mimi Mama wa watoto wako, mwalimu mkuu wa kizazi chako kutafuta Mali (kufanya kazi,biashara,sanaa n.k) Mimi pia ni kama wewe!! Niko na ndoto (life dreams) nahitaji kuzitimiliza! Niko na malengo nahitaji kuyafikia! Niko na dada, Kaka, mama, Baba,ndugu, jamaa na marafiki nahitaji kusaidia! Niko na mipango nahitaji kuikamilisha! Niko na WATOTO nahitaji kuwaandalia baadae yao!!

Suala la kudhalilika sio la mwanamke tu hata mwanamume naye anadhalilika sana tu!! Wangapi?! Situnashuhudia kila kukicha??

Halafu nani anamdhalilisha na kumuangamiza Mwanamke kama sio Mwanamume???? Hebu hii mada igeukie upande wa pili(kiumeni)mjichunguze kwanini yawafaa kuona “udhalili “ wa mwanamke ndio furaha yenu?!?!?


Maoni yangu jamani!! Sitaki kupondwa mawe na wala Msinifokee!!!! [emoji6]
Nice speech. But unfortunately, it comes from place of fear, pain, vengeance and revenge. Kimsingi comment yako imebase katika kulipizia rather than kutazama society in general, social responsibility, and gender roles.

Focus yako kwa sasa ni kutaka kuprove kitu ambacho ni hypothetical, yaani kusema wanaume wanaume eti wanawageuza wanawake watumwa kwa kutaka wakae ndani.

My dear maybe u are sourcing your information from the wrong sources. Mwanaume hakuwahi kutaka mwanamke awe slave wake au mfungwa, rather alitaka mtu wa kushirikiana nae katika kujenga jamii. Mwanaume ndie amekuwa slave kwa mwanamke kwa miaka yote akitumia nguvu na jitihada zake kusupport familia yake yaani watoto na mama yao. Sidhani kama kuna mwanamke anaweza kufanya the same thing.

Kwa maneno yako ni wazi kuwa wewe si mshika imani na dini yako whatever type ya dini unayoabudu. Wewe ndie kile kizazi kilichopotea, umeongea ukweli ila kwa namna potofu.

Mwisho wa siku tukubaliane kuwa wewe unapelekeshwa na maisha ya hii dunia ya sasa, sisi ambao tumakupinga tunasimamia misingi.

Binadamu leo hata akijustify kula nyama ya mtu hatakosa hoja ya kutetea huo uamuzi na atakushawishi. Ila unachotakiwa kusimamia ni je, MUNGU anaruhusu wewe kumuua mwanadamu mwenzako kwaajiri ya chakula?!

Ni nani aliesema kuwa nyakati za upotofu zikifika kila atauweza uona uovu na kutetea utukufu wa MUNGU katika dunia iliyojaa maasi. Mojawapo ya maasi ni hivi kuikana taasisi ndoa hadharani na kusapoti maisha ya kifuska ya hii dunia. Hata miaka ya nyuma kwenye hadithi za kiimani, utaona kuna wale mitume na watu waliomheshimu MUNGU kipindi walipofanya jumu lao la kusimamia ukweli wa MUNGU na maagizo yake walidhihakiwa na kutamkiwa maneno ya kejeli na ujuaji. Wale wanatofauti gani na wewe nyakati hizi za kizazi cha technology ya social media?!

Unajitapa kabisa hapa na kukiri kuwa hauna namna ila kuhasi maagizo ya muumba wako ya kutii na kuheshimu taasisi ndoa na majukumu yako ndani ya hiyo ndoa.....

Hizi fujo na usichana huwa vinaisha... Kumbuka kuna maisha baada ya hapa duniani. Huko tuendako utaulizwa jambo moja tu, ulitii mafunzo ya muumba wako, sasa sijui utamjibu na hoja zako hizi hizi mufllisi ya kibinadamu.

Jitafakari upya katika hii vita umechagua kusimama na nani, maana ni aidha shetani, au MUNGU.

Mwanamke huwezi kuongea maneno ya fedheha hivi na ukaona ni sawa.
 
Hivi siyo mimi ambaye nilikuwa nashusha magazeti humu kukemea maovu hadi nikaitwa feminist sijui activist? Tena bora mimi nilikuwa nakemea maovu ya jinsia zote wanaume na wanawake ninyi mnachofanya hapa ni kukemea maovu ya wanawake tu kana kwamba wanaume hawana maovu yoyote tena kama wewe ndiyo kila siku kuwatukana wanawake tu sijawahi hata siku moja kuona umeyaongelea maovu ya wanaume sijui lengo lako huwa ni lipi hasa!

Nashukuru Mungu wapo watu wachache sana waliokuwa wananielewa kuwa mimi siyo feminist wala activist ila ninachofanya ni kuhighlight maovu ya jinsia zote kwenye jamii na kuona ni namna kila jinsia inaweza kubadilika kwa nafasi yake bila kutupa lawama kwa jinsia nyingine! But it seems wanaume mnajiona very innocent na mnataka wanawake tu ndiyo waonekane waovu mnawatupia lawama kwa kuleta hoja za bustani ya eden sijui ujinga gani!

Yaani wanaume ni either mmeamua kwa makusudi kabisa kuyafumbia macho maovu yenu! Au labda maovu yenu mnayaona ni madogo na kwamba hata yakiendelea mnaona hayana madhara yoyote kwenye jamii ndiyo maana mnashupalia ya wanawake tu!

Siku nikiona mwanaume kaanzisha mada ya kukemea maovu ya jinsia zote mbili bila kutupa lawama kwa jinsia moja pekee hakika hiyo mada ndiyo itakuwa mada bora ya karne! Vinginevyo wote humu mtabaki kuwa wanafiki na Mungu mnamtaja bure tu!
Mmmmmmhmn maovu gani hayo ambayo utakemea usiungwe mkono?!
 
Uislamu haumkandamizi mwanamke ila baadhi ya vikundi vya waislamu ndo vinatumia dini kumkandamiza mwanamke. taliban imeweka sheria mwanamke akienda shule apigwe risasi hiyo sheria ipo kwenye aya gani au hadithi ipi. Tushukuru tu tupo kwenye utawala wa demokrasia maana kwa hoja zako na mtoa mada mngetupiga risasi wanawake tunaotafuta maendeleo ni vile tu mnaogopa dola.
Bibie salama kwako ni bora ungekaa kimya. Hakuna mtu mwenye akili timamu anaufadhilisha mfumo wa Kidemokrasia, soma vitabu, angalia hali halisi kisha tafakari kwa umakini. Sababu Demokrasia ni Ushetani na ni Kufru.

Watalibani wanajulikana, na maovu yako wazi, hakuna sheria ya Kiislamu inayo hukumu hilo, na sisi si katika wao, bali sisi tunarejea ule Uislamu sahihi, soma surat al Ahzab aya ya 33,kisha upate kujifunza.

Hivi kuna Uislamu ambao unaruhusu haya unayo yapigia upatu ? Bila kuangalia maslahi na ufisadi ?

Bibie, inaonekana Dini huijui, basi salama yako usiiongelee, sababu kufanya hivyo ni makosa. Bora kwao uulize.
Uislamu, umekuja kuweka sawa mambo matano, hapa nakutajia mambo matatu, uislamu umekuja kwa ajili ya kulinda akili za watu na vizazi vya watu, kadhalika mali za watu.
 
Dunia ilipo leo sipo ilipokua miaka kenda ilopita!
Zamani iliwawia rahisi sana kumtenga na kumnyanyasa mwanamke (eti ni dhaifu!)lakini kwa sasa imekua ngumu kwenu kwa maana hata husipompeleka shule bado jamii ya kisasa (social media’s) itamfunza tu, tena itamfunza bila kujali yeye ni nani, amezaliwa na nani wala ametokea wapi!(dunia imekua kijiji!)
Zamani unayo izungumzia wewe ni ipi ? Kabla ya mitume au karne ya 17 mpaka 18 ? Sasa usilazimeishe Historia ambayo inatumika tu kama kichaka, ila maazimio ndiyo ya kutaka kufanana ndiyo mnayaweka mbele.

Akili salama imeumbwa kuangalia faida na hasara, vipi unapo kutana na jambo ambalo lina faida chache na hasara kubwa, vipi utaendelea kulifanya kwa kauki mbiu ya kujikomboa au utarudi nyuma na kuacha sababu lina madhara mengi ?

Sasa huoni ya kuwa jamii ya kisasa inamfunza mtu kuwa mjinga zaidi, sababu haimfunzi huyo mwanamke kukabiliana na madhara anayaokutana nayo zaidi ya kuyafumbia macho na kujifanya hayaoni, mwisho wa siku wao wenyewe wanaugulia moyoni

Asili haibadiliki, ila mitazamo na fikra za watu ndiyo zinabadilika. Mwanadamu wa leo ndiyo mwanadamu wa kale, mahitaji ya leo ndiyo mahitani ya kale, heshima haikuwai kupitwa na wakati.
 
Ndugu zangu wa kiume, mwanamke hakuumbwa kuwa mjakazi (mtumwa) wako!! Kumbuka hata Muumba wa vyote (God Almighty, Allah Subhanah) aliona wewe “Adam” bila mimi “Hawa” bado hujakamilika!! Akakuzima kwa muda then akanitengeza mimi!!
Kwani kukaa nyumbani na kulea watoto ni utumwa ? Bibie jikite kwenye mada.

Mtume wetu alimuomba Allah aliye juu kwa kusema hivi "Ewe Allah mpe madhambi yule ambaye atawafanyia uovu madhaifu wawili,ambao ni Mayatima na Wanawake". Mwanamke utabakia kuwa dhaifu kwa maana ya kimaumbile na silika, kiasili shuruba na mikiki tumeachiwa sisi, na nyinyi mkapewa majumba kuyasimamia. Sasa unaposema wewe siyo dhaifu wakati ni dhaifu, haya bi matumizi mabaya ya akili bibi, na huwezi kushindana na asili, na ndiyo maana zama hizi mmekuwa bidhaa.

Narudi...
 
Umemaliza kila kitu! Ninafurahi kuona wanawake wakiislamu wanakua ma mawazo yao huru na kuweza ku question baadhi ya sheria na kanuni. Kila siku naamini uislamu hauna shida, shida ipo kwa wanaume walio katika "leadership positions" hivyo wana twist n turn rules to accommodate their primitive needs.
Sasa mbona huufati huo Uislamu ambao unakubali ya kuwa hauna shida ?

Anasema Allah aliye juu :

33. Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. (al Ahzab : 33)

Sasa bibir kuna Uislamu mwingine ambao upo kinyume na hiyo aya ? Basi ujue huo siyo Uislamu.

Halafu tabia ya kutoka toka majumbani ni tabia ya kijahiliya (Ya zama za ujinga). Kwa ufupi ni kuwa pamoja na kujisema kwamba mmegutuka au kukombolewa, lakini ukweli ni kuwa mmerudi katika zama za Ujinga ? Swali, unajua maana ya UJINGA bibie ?
 
Shout out kwa wanawake wote wanaojituma katika shughuli mbalimbali kwa ajili yao na familia zao. Muumba azidi kuwatia nguvu na nia mfikie malengo yenu.

Ombi langu msione mmefanikiwa mkaanza kutupangia ratiba ngumu za papuchi, mtatufanya tusione umuhimu wa mnachokifanya maana haka ndo kaugonjwa kakurithi tuliko nako
 
Bado nipo na Alexis Carrel...

Nanukuu
...

"Katika kitabu chake ameweka sura moja yenye jina “Kazi za Kijinsia na Jenetiksi” katika sura hiyo anasema; korodani na ovari zina kazi nyingi sana. Viungo hivi havizalishi mayai na mbegu za uzazi na hivyo muungano wake kusababisha kuzaliwa kwa binadamu mpya peke yake, lakini pia huzalisha uowevu (fluid) ambao humwagwa katika damu na hivyo husababisha tabia za kike na kiume katika hisia zetu na katika tishu na viungo vyetu vya mwili. Ni uoevu unaozalishwa na korodani ambao husababisha ukakamavu, ushujaa, moyo (thabiti) na kutoogopa. Ni sifa hizi zinazomtofautisha ng’ombe maksai na fahali. Ovari pia humuathiri mwanamke hivyo hivyo. Tofauti zilizopo kati ya mwanaume na mwanamke hazihusiani pekee na sura ya viungo vyao vya uzazi au mwanamke kuwa na tumbo la uzazi na kujifungua watoto na mfumo wao maalum wa elimu, bali ni matokeo ya sababu kubwa zaidi. Inatokana na kemikali zinazozalishwa na tezi za uzazi na kumwagwa katika damu.

Ni kutokana na kuipuuza nukta hii muhimu ndio baadhi ya watetezi wa harakati za wanawake wanafikiri kuwa jinsia zote mbili zinaweza kupata aina moja ya elimu na mafunzo na wanaweza kuchukua elimu na mafunzo ya aina moja na wanaweza kusomea aina moja ya fani/kazi na majukumu yanayofanana. Kwa kusema kweli mwanamke anatofautiana na mwanaume katika mambo mengi.(Mwisho wa kunukuu)

Bado tunaendelea kuwazindua wanawake wa leo ambao wanadai zama zimebadilika, huku wakiyafanyia kazi maazimia ya haki za binadamu na si sheria za kimaembile ambazo zimewarudisha katika zama kijinga za kale.

Tunaendelea kuwaonyesha ya kuwa maumbile ndiyo yana chagua.
 
😁😁😁 Na wangewamaliza...Yaani sisi ndio wanaume tunaojuana vema mentality zetu kuanzia huku kwenye vijiwe vya kahawa,Al Kasus mpaka Maskani za Bao na Keram...

Unajua umeongea Kitu kizito ndugu yangu aiseee acha tu.....mngetandikwa Kama wale wa Kandahar.....

Tatizo sisi wanaume wenzao tukiwaambia KWA upole tu,wanatubandika majina kibwena,mara ooo DUYUTH anatawaliwa na mkewe "mzungu wa tabia mjaa laana" daah😁😁 Mara Ooo Munafiq anayekaribia kuwa Murtad,Sasa unakaa unajitafakari na kuishia kucheka tu na ARGUMENTUM AD HOMINEM zao.....
Hatareee😁😁
Samahani kama nimeingilia yasiyonihusu. Bila shaka kwa uliyiyaandika unamgusia mleta Uzi. Binafsi sikubaliane kwa hoja yake na ni Muislam pia. Nafikiri ni bora zaidi ukajadiliwa mtizamo wake kuliko yeye mwenyewe binafsi. Licha ya kwamba mtizamo wake ni wa kutatiza ni heri zaidi kumvuta karibu na kumfahamisha. Pengine katika hilo heri inaweza ikapatikana vilevile. Itumike mbinu ya kumfahamisha, isitumike mbinu ya kumzodoa.

Samahani kama nitakuwa nimekukwaza.
 
Mmmmmmhmn hapo sasa umeamua tu kunifokea. Ila mada imemlenga mwanamke na sio kulaumu mwanamke.

Hapa mleta mada anakemea mfumo ambao ninyi wanawake bila kujua mnautetea na kudhani unamsaada kwenu na kwa jamii ila ukitazama ni kuwa huu mfumo kwanza ni mgeni kwetu na si sehemu ya desturi zetu.

Mleta mada alikuwa anawahoji ninyi kama wanawake namna mnatetea jambo ambalo bila ninyi kujua kuwa linawaexploit, je hamjaona au mnajaribu tu kuwa changamoto.....

Siyo mada hii tu! Wewe nakuonaga kwenye mada nyingi sana huwa unakandia wanawake tu na je hata kama mada imemlenga mwanamke kwanini msiongezee na ninyi matatizo yenu au hamjui nini maana ya kuchangia mada?
 
Kabisa!!

Hivi unajiitaje kichwa cha familia muda huo huo unaharibu mtoto wa familia nyingine??

Duniani wote tunahitajiana wala sio kwa ngono tu (manake ndio msukumo mkubwa wa wenzetu) ila pia ili hayo mnayoita “mmomonyoko wa maadili “ ni wajibu wetu wote kwa pamoja kusimamia!!

Huwezi kusema mwanamke anadhalilishwa wakati mdhalilishaji mkuu ni wewe!! Utapigana na ukuta tu!!

Si ndio hapo sasa! Siku wakijua kuyaona na kuyaongelea na maovu yao na kuamua kuyaacha na kubadilika hakika hizi kelele zitapungua sana!
 
Mmmmmmhmn maovu gani hayo ambayo utakemea usiungwe mkono?!

Wewe tumeshakutana sana kwenye nyuzi nyingi kama hii na kila nilichokuwa nasema kuhusu maovu ya wanaume ulikuwa lazima upinge na ulikuwa mmoja wa waliokuwa wananiita feminist mara activist! Unafikiri sikumbuki?
 
Back
Top Bottom