Niko serious sana, ndiyo maana nikaandika huu uzi.
Naendelea kushangaa, kama mumeo amekosea na wewe ukosee ?
Wenzako hawataki raha, sababu kushindana na mwanaume ndiyo mmefundishwa, mmefubdishwa ya kuwa hutakiwi kubweteka wala hutajiwi kumtegemea mwanaume, huku mkimaliza kwa kusema "kuna leo na kuna kesho". Sasa unapo andika uongo ambao kwa hali yoyote ile hamuutendei kazi, huku ni kuikosea adabu akili.
Unapo ona mumeo hatimizi majukumu, unatakiwa uangalie njia bora yenye maslahi kwako na kwa watoto wako, siyo unachagua njis ambayo itakugharimu wewe na watoto wako huku si kuatua tatizo na akili iliyo salama ina kataa hili.
Kwahiyo msitake kutulazimisha ya kuwa historia ndiyo sababu wakati jambo hili, tunajua limekuja toka umagharibini.
Sasa bibie mbona bado mmelala, na huku mnadai mmeamka au hujui maana ya kuamka ? Maana haya mnayo yafanya yalifanyika zama na zama zilizopita na sisi tunaziita zama za Jaahiliya (Zama za ujinga) na ni ujinga gani mkubwa kuliko ujinga wenu huu ambao mnakuwa kama Mshumaa, unaumia wewe kwa ajili ya kuwafurahisha wengine ?
Hii ni hoja ya kitoto sana bibie, unapo tumia leo mkono wa kulia, kwa ajiki ya kula au kupokea kitu au kuta kitu, hakumaanishi ya kuwa mkono wa kushoto hauwezi kufanya hayo bali, kutumia mkono wa kulia ni adabu na vizuri zaidi. Kwahiyo unapoambiwa ukae nyumbani haimaanishi kuwezi kutafuta na ukapata, unaweza ila kufanya kwako huko siyo jukumu lako, kwani kimaumbile utaharibu lile la msingi zaidi, la kusimamia nyumba ambalo ndiyo jambo lako hasa.