Haja hakuna sababu waliopo katika hao Wanawake wanatosheleza wengine.1.kunawake zetu na mama zetu ambao kisheria wanatakiwa watibiwe na wanawake wenzao huko mahospitalini,kusoma wanawake udaktari kunasaidia kuwepesisha jambo hilo.ila kwa dharula ya uhaba wa wanawake ndo wanatibu wanaume.
Hujakatazwa kuhoji ila hoji vitu vya maana.Naendelea kuhoji kuwa kwa mujibu wa sheria ya dini ni mwanamke peke yake ndo anayekatazwa kuwa katika mchanganyiko na wanaume ama hata mwanaume anakatazwa kuchanganyika na wanawake ?
Hii ndiyo dharura sasa mzee.Munkari huo ni ule wa mke wako,mke wangu,mama yako,mama yangu kufunuliwa nguo na kuonwa tupu zake na daktari wa kiume ambaye ndo alisomea udaktari kwa sababu wale wanawake mliwakataza.
Mwanamume haruhusiwi kuchanganyika na Wanawake na yeye anaingia katika hili. Sababu tunaangalia suala la Mwanamke na kutafuta, ndiyo maana kutafuta kwa mwanamke ni dharura ila kutafuta kwetu sisi Wanaume ni wajibu na hili ni jambo letu.Kwa hiyo wanaume wanaruhusiwa kuchanganyika na wanawake ila wanawake tu ndo hawaruhusiwi kuchanganyika na wanaume ?
Madhara yanayo patikana katika uchukuaji wa Elimu hiyo ndiyo hufanya jambo hilo kuwa haramu, sababu ni haramu kuzidhuru nafsi zetu.Kwani hapo tatizo ni uharamu wa elimu au tatizo ni uharamu wa mchanganyiko ?
Fitna ya mchanganyiko iko wazi sana katika Uislamu, hii inaingia kwetu sote, ila kutafuta kwa mwanamke ni jambo la dharura, na dharura hukadiriwa kwa makadirio yake.Sheria yenu hiyo ya kuwakataza wanawake tupu imetokea wapi ?
Swadaktaa, huu ndiyo Uislamu.Kwa hiyo unakubali kuwa kama haifai mwanamke kusoma kwa zama hizi kutokana na mazingira basi na mwanaume pia haifai kusoma kwa sababu kama ni baya basi baya kwa wote ?
Nimecheka sana, sababu mimi situmii akili zangu zaidi ya kurejea kwa wakubwa zangu, hili ni jambo rahis sana kwangu.Unajitutumua sana aisee ila ndo hivyo tu,mambo mazito haya.
Inataka ufahamu kuacha ushabiki na ufulani kasema.
Suala la mchanganyiko hili ni la haramu kwa wote. Ila tunalo kuja kuangalia, kutafuta hela kwa mwanamke, hili si jambo lake ni jambo letu sisi,ndiyo maana mpaka mwanamke atoke na akatafute vigezo vyake kuvikidhi ni muhali hasa kwa nchi zetu hizi ambazo hazifati sheria za dini. Ila Wanaingia wanawake wote katika madhara haya, ukimuharibu mwanamke ujue umeharibu jamii kubwa sana.Hizo athari si zinafanywa na wanawake na wanaume.sasa mbona akatazwe mwanamke tu wakati hizo athari zinatokea kwa kutekeleza wote wawili mwanamke na mwanaume.
Suala la migongano baina ya Masalafi hili si jambo la ajabu na hii migongano haionyeshi ya kuwa Masalafi hawako katika haki ila hii ni mitihani tu ili Allah awaone ni kina nani Wakweli katika hili, na kuonyesha watu hilo, na kila mgongano unao usikia katika safu ya Masalafi una julikana chanzo chake.Allah akubaarik ndugu.
Umeongea maneno mazima sana.
Umegusia mambo makubwa sana.
Na nilimuambia bwana zurri kuwa huo msimamo wake ndio ambao unawaponza masalafy wengi kukatana kila kukicha,magomvi hayaishi,kejeli wao kwa wao mpaka unashangaa hawa jamaa vipi hawa.
Leo hakuna salafy ambaye amesalimika na mwenzake,huyu atamsema tule,yule atamsema yule mwingine na mwingine atamsema mwingine basi tafrani tupu kwa hawa ndgu.
Wanaziendea hadithi pasi na ufahamu,kuharibu kwaao ni kukubwa sana kuliko kutengeneza.
Usalafi ndiyo Uislamu wenyewe, hili hakuna anae pinga isipokuwa mtu wa matamanio na mzushi.Masalafi wengi sana wanaamini kuwa chao ndo sahihi na kufuata kisichokuwa chao basi ni dhwalaala.
Kuna mwalimu wetu mmoja yeye hakubaliani na mambo ya maulidi na dua za msikitini,lakini anavyoyazungumzia kwa utaratibu na ustaarabu mpaka wengine wanamsema kuwa anatetea watu wa bidaa,lakini maalim yeye harudi nyuma anasema kuwa wale ni watu wana maoni yao ijapokuwa kwa upande wangu naona sio sahihi.
Hawa ndio watu wa kusoma kwao ni watu wenye busara na hekima na uvumilivu.
Usalafi ndiyo Uislamu wenyewe, hili hakuna anae pinga isipokuwa mtu wa matamanio na mzushi.
Mimi nawapa kazi nyinyi, mlete ushahidi wenu ya kuwa ni binti gani aliyesomea udaktari na akafanya kazi ya fani, amesalimika katika dini yake.
Uovu unakimbiwa uovu haufatwi.
Ahsante.
Hatuutuhumu usalafi tunawatuhumu masalafi.Usalafi ndiyo Uislamu wenyewe, hili hakuna anae pinga isipokuwa mtu wa matamanio na mzushi.
Wewe uko serious mkuu ?Mimi nawapa kazi nyinyi, mlete ushahidi wenu ya kuwa ni binti gani aliyesomea udaktari na akafanya kazi ya fani, amesalimika katika dini yake.
Ndo hayo tunayazungumza.Suala la migongano baina ya Masalafi hili si jambo la ajabu na hii migongano haionyeshi ya kuwa Masalafi hawako katika haki ila hii ni mitihani tu ili Allah awaone ni kina nani Wakweli katika hili, na kuonyesha watu hilo, na kila mgongano unao usikia katika safu ya Masalafi una julikana chanzo chake.
Shaykh Rabee Allah amuhifadhi hili amelibainisha wazi na miongoni mwa sababu alizo taja ni vijana kupenda ukubwa, kupenda kuwa na wafuasi, kupenda umaarufu na husda.
Enheee..Suala la mchanganyiko hili ni la haramu kwa wote
Katika hadithi ama aya gani inayosema kuwa kutafuta hela ni jambo letu sisi ?Ila tunalo kuja kuangalia, kutafuta hela kwa mwanamke, hili si jambo lake ni jambo letu sisi
Hivyo vigezo kaviweka nani zaidi ya Allah na mtume wake ?ndiyo maana mpaka mwanamke atoke na akatafute vigezo vyake kuvikidhi ni muhali hasa kwa nchi zetu hizi ambazo hazifati sheria za dini. Ila Wanaingia wanawake wote katika madhara haya, ukimuharibu mwanamke ujue umeharibu jamii kubwa sana.
Kwa hiyo ni sahihi kwa upande wako mwanaume apitie kuyafanya ya haramu haina shida kwa kuwa anatafuta riziki sio ?Swadaktaa, huu ndiyo Uislamu.
Unasema hakuna tija wala baraka binafsi nina mtu wangu wa karibu wa kike ametibiwa mara nyingi na madaktari wa kike tena kutibiwa ambako kunahitaji kufunua maungo yake.Ama hiyi ya Wanawake kwenda kusoma hakuna barakka wala natija ya jambo hilo kwani uovu ndiyo unakuwa maradufu. Hakuna mwanamke anaesoma fani ya Udaktari kisha akajipangia yeye kazi ya kufanya, lazima afate mfumo ulio pangwa na kuratibiwa. Ndiyo maana Wanawake wanasoma na wanapoteza dini zao sababu hakunw mazingira yanayo waunga mkono katika jambo hilo.
Fitna ya mchanganyiko iko wazi sana katika Uislamu, hii inaingia kwetu sote, ila kutafuta kwa mwanamke ni jambo la dharura, na dharura hukadiriwa kwa makadirio yake.
Asili gani unayoisema wewe na umeshabainishiwa huko juu kuwa hata mkewe mtume alikuwa mfanya biashara na wanawake wa zama hizo walikuwa wengi wakitengeza mapambo na kuuza,walikuwa wanafanyia biashara majumbani ?Sasa niambie ulazima wa jambo ambalo linakiuka asili ya mwanamke ni upi ?
Naam.Aya inasema wanawake walazimiane na majumba yao.
Jambo ambalo ni mubaaha wewe unayekataza ndo utoe dalili.Aya inasema wanawake walazimiane na majumba yao. Ikitokea wakatoka basi watoke kwa haja, hii haja inakuwa katika mlango wa dharura, na dharura hukadiriwa kwa makadiriyo yake. Kwahiyo unapo uliza swali la hovyo kama hili ulitakiwa utoe ushahidi wa kuruhusu jambo hili, toka katika hadithi au Qur'aan. Sasa Uislamu wetu umeruhusu watu kuhoji ila umekataza kuhoji ujinga, na tukapigiwa mfano kwa Wana wa Israeli walivyo potea kwa kuhoji hoji kwao ujinga.