Sasa unadhani dharura ya mwanamke kutibiwa na mwanaume kwa zama hizi itaondoka bila kuruhusu wanawake wasome zaidi wakae katika fani hizo ?Hii ndiyo dharura sasa mzee.
Na ndiyo maana nikakwambia kutokea kwa migongano katika safu ya maswali ni Allah anataka kutuoyesha ni katika wakweli katika da'wa, na hili lipo sababu Allah lazima atupime. Na hapo nimewazungumzia masalafi sababu huwezi kuwaongelea Masalafi bila kuuongelea Usalafi.Hatuutuhumu usalafi tunawatuhumu masalafi.
Kama ambavyo hatuutuhumu uislamu bali tunawatuhumu waislamu.
Kuwa makini na wanayoyasema watu.
Acha manebo mengi mzee, sisi tunaishi nao kijaa, na utuambie wamesalimika vipi na dini zao, maana usione Dini ni stara na kusali pekee.Wewe uko serious mkuu ?
Wako wengi sana.
Nakupa mfano kuna hospitali moja siitaji jina kuna wamama kibao tu wanatibu wako salama na dini yao.
Wapo wengi tu wana dini na wamesoma udaktari wewe unasemaje na nawajua kwa majina ?
Alafu kwani mbona kuna wanaume ambao wanasoma udaktari na hawajasalimika na dini yao kwa hiyo hii tuwakataze na wanaume kusomea udaktari kwa kuwa kuna baadhi hawapo salama na dini yao ?
Migongano ya Kisalafi ni fitna, mathalani kuna fitna kipindi hiki ina vugu vugu, imeitwa fitna hiyo "Musa'afiqa" ukiifatitilia fitna hii imejengeka katika msingi wa husda,kutaka ukubwa na kuwazushia waislamu uongo. Kadhalika fitna nyingine zilizo pita.Pakiwa na migongano basi ina maana nyie kwa nyie kuna mmoja anamuona mwenzake yuko katika haki na mwingine yupo katika batili ndio maana mnagongana ati.
Ongeza umakini, nimekwambia Usalafi ndiyo Uislamu wenyewe mzee, katika jambo lolote la haki, mitihani lazima iwepo na huu ndiyo mwenendo wa Allah kwa waja wake, ili awaone waliothibiti katika hiyo haki na kuendelea kusafisha.Kama wote mnajiona mpo katika haki mbona sasa yatokee magomvi baina yetu kwa yenu nyie.
Hapa hatusemi usalafi tunawasema wanaofuata huo usalafi wana matatizo wengi katika wao kwa sababu kama alizotaja huyo shekhe rabee.
Nilikwambia huko mwanzo ya kuwa kuhoji hoji sana mpaka unahoji mambo ya kijinga, ambayo laiti ungesoma niliyo yaandika huko juu, usinge hoji.Katika hadithi ama aya gani inayosema kuwa kutafuta hela ni jambo letu sisi ?
Umesahau yule mkewe bwana mtume ambae alikuwa ni mfanya biashara mzuri tu katika maisha yake na Mtume pia akashiriki katika bishara hiyo ?
Wapi mtume alikemea utaratibu huo wa mwanamke kujitafutia katika vile vya halali ?
Qur'aan na Hadithi mara nyingi mara nyingi huwa vinaelezea mambo kwa ujumla wake. Yaani hutoa misingi, kisha matawi huja kutolewa na wannazuoni kwa kurejea misingi hiyo kama ushahidi. Mifano iko mingi sana. Mathalani aya ya 33 katika sura ya 33,huu ndiyo msingi, na aya nyingine katika sura ya pili aya ya 165 au 195,kwa kumbukumbu zangu, na aya ziko nyingi na hadithi ziko nyingi. Mfano mwepesi leo hii hakuna hadithi wala aya inayosema bangi ni haramu, lakini kwa mujibu wa sheria ya Uislamu bangi ni haramu, sababu katika bangi kuna "Ila" na katika usul al Fiqh, kuna kitu kinaitwa Qiyas, kina tumika kutoa hukumu ya jambo hilo.Hivyo vigezo kaviweka nani zaidi ya Allah na mtume wake ?
Na ni vipi hivyo ?
Nilikukanya huko juu, kuhoji sana mpaka unahoji mambo ya kijinga ambayo ni mepesi mno.Alafu kama unakubali kuwa hata wanaume yanawahusu yale ambayo wanawake yanawahusu katika mada hii mbona unamlenga mwanamke tu wakati huo mwanamke naye akienda nje atakutana na mwanaume ambaye wewe unaona haina shida kukutana na mwanamke..?
Vijana mnachekesha sana aliyejibu swali la mkewe mtume alikuwa anafanya vipi biashara zake baada ya kuolewa. Asili ni mwanamke kukaa nyumbani. Hili nalirudia zaidi ya mara mbili sasa, sasa usiulize tena swali kama hiki.Asili gani unayoisema wewe na umeshabainishiwa huko juu kuwa hata mkewe mtume alikuwa mfanya biashara na wanawake wa zama hizo walikuwa wengi wakitengeza mapambo na kuuza,walikuwa wanafanyia biashara majumbani ?
Asili gani inayokeukwa ?
Dalili nilikupa, aya nikakupa kaida ya kiusuli ya kuonyesha hali kadhaa juu ya ufanyaji mambo na kuwa haramu kwake, kwa kuanzia katika ile kaida uliyoitoa ya kuwa kila jambo kiasili ni lenye kufaa, kutokea hapa Wanazuoni wakazama na kutoa uchambuzi wa hali tatu,kwa kurejea katika hadithi na aya zenye mafhumu ya katazo la watu kuzidhuru nafsi zao.Jambo ambalo ni mubaaha wewe unayekataza ndo utoe dalili.
Tokea hapo nimekuambia kusomea fani mbali mbali zaelimu isiyokuwa ya Allah na Mtume ni jambo la mubaaha.
Na mubaaha inajuzu mpaka dalili ya kukataza ije.
Unayo dalili ya kukataza mwanamke kusoma fani hizo ?
Unaposema mwanamke atoke kwa dharura ambayo hukadiriwa kwa makadirio na kwa haja.
Kwani mwa amke kwenda kazini kutafuta hela sio haja ambayo anahitajia kutimizamajukumu yake ya ndani ?
Au haja ya mwanamke kutoka ambayo hawezi kuifanya mwingine ni ipi ili tuone kuwa haja hizo kumbe mwanamke lazima atoke bila yeye hafanyi mwingine ?
Tatizo sio kutoa aya,tatizo kutoa aya ambazo haziendani na mambo unayoharamisha.Dalili nilikupa, aya nikakupa kaida ya kiusuli ya kuonyesha hali kadhaa juu ya ufanyaji mambo na kuwa haramu kwake,
Kaida hii ya kuwa kila jambo kiasili ni lenye kufaa tulikubaliana kuwa kweli ipo.Unachoshindwa kuelewa ni kuwa hii kaida inajengeka katika mambo mawili.kwa kuanzia katika ile kaida uliyoitoa ya kuwa kila jambo kiasili ni lenye kufaa, kutokea hapa Wanazuoni wakazama na kutoa uchambuzi wa hali tatu,kwa kurejea katika hadithi na aya zenye mafhumu ya katazo la watu kuzidhuru nafsi zao.
Hizi aya unazotoa zinawahusu wanawake na wanaume pia.قال الله تعالى : ( وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ) البقرة /195.
وقال الله تعالى : ( وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ إِنَّ اللَّهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ) النساء /2
Hii hadithi inawahusu wanawake tu mzee ?لا ضَرَرَ ولا ضِرارَ
Hakuna anayekataa asili hiyo,lakini haifidishi kuwa haruhusiwi kutoka kwa haja zake binafsi.Vijana mnachekesha sana aliyejibu swali la mkewe mtume alikuwa anafanya vipi biashara zake baada ya kuolewa. Asili ni mwanamke kukaa nyumbani. Hili nalirudia zaidi ya mara mbili sasa, sasa usiulize tena swali kama hiki.
Siyo kwali, sababu hoja yako inaonyesha kuwaingiza na Wanaume. Sasa nilikukanya huko nyuma ya kuwa, hakuna baya ambalo ni baya tu kwa mwanaume na mwanamke asiingie, mpaka libainishwe.Tatizo sio kutoa aya,tatizo kutoa aya ambazo haziendani na mambo unayoharamisha.
Hakuna aya umetoa ikajibu swala langu kwa sababu unaulizwa kingine unaenda kwingine.
Nawaingiza na wanaume kwa sababu ndio asili ya mambo yalivyo,huwezi kuwatoa wanaume kwenye mambo ambayo unamharamishia mwanamke bila dalili yeyote.Siyo kwali, sababu hoja yako inaonyesha kuwaingiza na Wanaume
Sasa kama unafahamu hivi kwanini unashindwa kuweka dalili ambayo imebainisha kuwa mwanaume anaruhusiwa kuchanganyika kusoma fani kuchanganyika ambako mwanamke haruhusiwi?Sasa nilikukanya huko nyuma ya kuwa, hakuna baya ambalo ni baya tu kwa mwanaume na mwanamke asiingie, mpaka libainishwe.
Haya ndiyo madhara ya kutumia ufahamu wako pasi na marejeo kwa Wakubwa, matokeo yake ni kukosea juu ya kukosea, unatakiwa ujue tunazungumzia nini mpaka muda huu, suala mazingira linamdhuru msomaji na linamfunga na kumuweka mbali na majukumu yake ya asili. Kwahiyo hili linamuhusu kila atakaye ingia katika mazingira hayo. Sasa hapa huna hoja ya kuyaepuka mazingira kijana.2.Asili ya kitu chenye kudhuru kulingana na mtu mwenyewe na hakimdhuru kila mtu.
Mfano kuna watu wakila nyama ya bata wanadhurika,hapa nyama ya bata itakuwa haramu kwa huyu anayedhurika tu na wala haifai kwake kuwadhuru wengine ambao hawadhuriki na nyama hiyo ya bata.
Sasa hapa ile "hakuna kudhuru wala kujidhuru" inakuwa kwako wewe inayokudhuru na wala haifai kuharamisha kitu hicho kwa wengine wote ati kwa kuwa kuna baadhi kina wadhuru.
Hakuna mchanganyiko usiyo dhuru kijana, acha kujidanganya,wala hakuna baya lisilo dhuru, ndiyo maana dharura hukadiriwa kwa makadirio yake.Sasa hapa ile "hakuna kudhuru wala kujidhuru" inakuwa kwako wewe inayokudhuru na wala haifai kuharamisha kitu hicho kwa wengine wote ati kwa kuwa kuna baadhi kina wadhuru.
Usiwe unapinga mambo ambayo huyajui. Udaktari wa kisekula unakwambia nini kuhusu viumbe hai na visivyo hai ? Udaktari wa Kisekula unakwambia nini kuhusu sababu za ugonjwa ?Sasa kusomea udaktari mwanamke kwa kuangalia ile fani yenyewe ya udaktari inamdhuru nini mwanamke
Kijana mbona unarudia kuuliza maswali ambayo majibu yake nimeshayatoa ? Au umeishiwa hoja ?Hizi aya unazotoa zinawahusu wanawake na wanaume pia.
Unani potezea muda. Narudia tena kwa mara nyingine na natarajia hutarudia tena kuuliza hili ambalo nilishakujibu.je mwanaume anaruhusiwa kuiuwa nafsi yake katika kusomea hizo fani ila mwanamke haruhusiwi ?
Mwanaume anaruhusiwa kujiingiza katika maangamivu ila mwanamke haruhusiwi ?
Sasa huko kutoka kwake kwenda kujitafutia ndiyo dharura yenyewe na moaka akidhi vigezo. Kinyume na hapo akae nyumbani wale wenye wajibu wakumletea watamletea na atakidhi haja zake.Hakuna anayekataa asili hiyo,lakini haifidishi kuwa haruhusiwi kutoka kwa haja zake binafsi.
Nitakuuliza je anawajibika kutoka ? Je akitoka anakidhi masharti ? Je hayupo wa kumtimizia haja zake ?Asili kukaa nyumbani ila je akienda kazini kwa ajili ya kupata kipato halali akimaliza akalazimiana na nyumba yake asili iko palepale,tofauti na mwanaume akitoka kazini aenda vijiweni na sehemu zingine.
Nacheka sana, kijana sijui aya ile hujaielewa aisee, unaoata shida sana, kuweka matamanio yako mbele ya nususi ma hili huliwezi.Ukisikia asili kukaa nyumbani unadhani ni kuwa haruhusiwi kutoka kwa namna yeyote ile ?
Sasa aliwafukuza vipi katika miji wakati walikuwa wanakaa majumbani isipokuwa kwa dharura ?Mtume alikataza mwanamke kutoka nyumbani kwake hali kajipulizia manukato.
Kwa maana ATOKE akiwa hajajipulizia manukato yeyote.
Sasa ikiwa mtume anatambua kuwa mwanamke anaweza akatoka lakini kwa sharti ya kuwa asijipulizie manukato wewe ndugu una darja ipi kumzidi Mtume wa Allah ?
Hakuna hadithi yeyote ambayo Mtume alikataza wanawake kutoka majumbani mwao kuziendea haja zao za kimaisha,na wala haikuthibitipo kuwa Mtume aliwafukuza wanawake katika miji warudi majumbani mwao.
Mbona unauliza mambo ambayo sijayasema kijana, wapi niliandika Mwanaume ameruhusiwa kuchanganyika ? Usipoteze muda kujadili mambo ambayo hayapo, huku ni kupoteza muda na kuishiwa hoja.Kama kuchanganyika ni haramu kwa nini iwe haramu kwa mwanaume wakati madhara ya kuchanganyika yanawakuta wote kama tulivyokubaliana ?