Unaposema dini kusalimika kwa mwanamke unataka iwe vipi ?Acha manebo mengi mzee, sisi tunaishi nao kijaa, na utuambie wamesalimika vipi na dini zao, maana usione Dini ni stara na kusali pekee.
Asili ya hilo jambo linafaa ndio maana hakuna dalili ya kukataza.unapodai dalili ya kukataza wakati hilo ni jambo la kujuzu kiasili unakuwa unatushangaza.Wala hakuna hadithi wala aya inayo waruhusu wanawake watoke wakatafute ugali na kulea familia au kwa mambo yake biafsi
Jawabu langu ni moja tu.Bora ni mwanamke awe tabibu na,akatibu na akahifadhi dini yake.Sasa kipi bora, mwanamke akatibiwa na akabaki na dini yake, na mwanamke akawa tabibi, akatibu na akatabiwa na akapoteza dini yake ?
Lazima udharau kwa sababu ya ile taassub ya mashekhe ambayo wengi mko nayo..Nilikudharau na kukuona wa ajabu pale uliposema hata Sheikh angekuwa hai ungemuhoji,
Bwana mkubwa sote tumesoma secular,tumesoma sekondari origin ya mtu ni wapi ama katokana na nini.Usiwe unapinga mambo ambayo huyajui. Udaktari wa kisekula unakwambia nini kuhusu viumbe hai na visivyo hai ? Udaktari wa Kisekula unakwambia nini kuhusu sababu za ugonjwa ?
Sasa ulitakiwa kuweka wazi kusudio lako.Hizo ni huduma sasa na sio malezi.nilichokusudia ni malezi ya kukaa nyumbani na kulea familia,kuwaangalia watoto na kadhalika.
Hii kazi ya kuwaangalia watoto na kuwavisha na kuwapa malezi mbalimbali kuwabeba n.k kiasili ni ya wanawake.
Ama unakataa pia kuwa hii sio asili yao wanawake ?
Kama umeshaelewa bado hali iko pale pale kuwa ikiwa asili ya mwanamke ni kusimamia mambo ya nyumbani hiyo haina maana ya kuwa kusimamia mambo ya nyumbani mwanaume ni haramu.Sasa ulitakiwa kuweka wazi kusudio lako.
Asili yetu ni kusimamia na wanawake asili yao ni kukaa nyumbani na kusimamia mambo ya nyumbani.
Hapa nimecheka sana. Wapi aya imesema kutoka hovyo hovyo ? Mtoko wa wanawake wa Jahiliya unaujua mzee ?Aya iliyonukuu haikatazi mwanamke kutoka kwenda kwenye mahitaji yake mbalimbali bali inamkataza kutoka ovyo ovyo.
Nanukuu :dalili ya kuwa mwanamke hawezi kutoka pasi na maharim,mwanamke hawezi kutoka ila kwa dharura...
Kwa hiyo anaruhusiwa kutoka ovyo ?Hapa nimecheka sana. Wapi aya imesema kutoka hovyo hovyo ? Mtoko wa wanawake wa Jahiliya unaujua mzee ?
Ndugu hatuzungumzii kusafiri.Mwanamke haijuzu kusafiri bila ya kuwa na Mahram.” [Al-Bukhaariy 3006 na Muslim 1341]
Kwanza nilikuweka sawa juu ya mahitaji,mahtaji si kufanya kazi wala si kutafuta hela, mahitaji ni matumizi na hitajio.dalili ya kuwa mwanamke hawezi kutoka pasi na maharim,mwanamke hawezi kutoka ila kwa dharura...
Hujatoa dalili ambazo zimeashiria kuwa mwanamke atoke kwa dharura hujatoa aya wala hadithi ikitaja hilo.
Unachoweka wewe ni maneno yasiyokuwa Qurani kusapoti msimamo wako bwana mkubwa.
Kumbuka kuwa hujaweza hoja yeyote ambayo inamkataza mwanamke kutoka kwenda kwenye mahitaji yake,hujatoa dalili.
Aya iliyonukuu haikatazi mwanamke kutoka kwenda kwenye mahitaji yake mbalimbali bali inamkataza kutoka ovyo ovyo.
Unatumia maandiko vibaya..
Mfano wa aya hizo zipo nyingi tu mfano..
Allah kasema "wala msipelelezane..."
Aya hii huwezi kuitumia kuwa ni katazo la kumchunguza ama kumpeleleza mchumba ambaye unataka kumuoa ati kwa kuwa aya imesema hivyo.
Pakitokea haja ya kuchunguza basi inafaa kuchunguza.
Kama ambavyo ikitokea haja ya mwanamke kutoka nje ya njumba itafaa kutoka.
Kutumia himizo la kukaa ndani kuwa ndo dalili ya kuwa haifai kutoka katika mahitaji yake ya kila siku huo ni ufahamu wa mbali sana.
Kwa hiyo mpaka hapo huwezi kutumia aya hii kumkataza mwanamke kutoka kwani mfano wa haya hizo zipo nyingi sana ambazo hazikatazi kinyume chake penye haja.
Umeona ulivyokuwa msahaulifu, ulipo niuliza swali la mwanamke harusiwi kutoka ila kwa dharura, au bila mahrim wake ulikuwa una dalili ya kupinga hili ?Kwa hiyo anaruhusiwa kutoka ovyo ?
Nimecheka sana, hukumu ya safari inapimwaje mzee ? Hukumu ya safari hukadiriwa kwa kuzingatia ada na desturi, hataka kutoka kimara mpaka kibaha, hii ni safari kijana,kwahiyo bado huna hoja ya kusema hadithi haipo.Ndugu hatuzungumzii kusafiri.
Hili la kusafiri liko wazi kabisa.
Kutoka ambako si safari ni kama kwenda sokoni au duka la karibu, na hili pia huangaliwa usalama wa mtokaji. Hatoki toki tu.Tunazungumzia kutoka ambako sio safari,hatujagusia suala la safari.
Hukumu ya safari mtume aliikadiriaje ? Embu nipe faida hapa. Maana naona unaleta maneno ambayo huna hata marejeo kwayo.Hili la mahrim ni khaaaswa akiwa anakusudia kusafiri na wala sio katika utokaji wa maeneo ya mji wake pekee.
Hili nimeshalibainisha tayari.Ama haruhusiwi kutoka kabisa kwa hali yeyote ?
Hii si asili, bali haya ni katika mila na desturi zao, zilikuwa ni kuchukia watoto wa kike, na hii ilikuwa ni katika imani potofu.Mfano asili ya waarabu ilikuwa ni kuchukia watoto wa kike,hii asili ni haramu katika uislamu kwa sababu imebainishwa.
Ukiwa unaandika uwe unarudia kusoma kwa makini, ili usiwe unarudia kile nilichokiandika.Kama umeshaelewa bado hali iko pale pale kuwa ikiwa asili ya mwanamke ni kusimamia mambo ya nyumbani hiyo haina maana ya kuwa kusimamia mambo ya nyumbani mwanaume ni haramu.
Tofautisha kati ya asili na kawaida mzee.Mfano wa asili ungine ni kuwa asili ya kimaumbile ni kuwa anaezaa ndio anyonyeshe.
Kusoma siyo hoja, hoja ni kusoma na ukaelewa. Kwahiyo usilete hoja za kitoto kwamba umesoma. Wangapi wamesoma Secular lakini wanaamini ya kuwa Jua halitembei ? Sasa usijifarague kwamba umesoma, hali ya kuwa hukijui ulichokisoma.Bwana mkubwa sote tumesoma secular,tumesoma sekondari origin ya mtu ni wapi ama katokana na
Kaka mbona unaandika yasiyo kuwa na msingi ? Hakuna aliyesema secular ni haramu bali nimesema katika secular kuna vitu vya hovyo vitu vya kufru.Zipo nadharia zinazosema kuwa binadamu wa kwanza ni nyani n.k
Huwezi kuharamisha secular ama kuharamisha kusoma somo la history kwa sababu ya nadharia hii ambayo inaenda kinyume na Mungu.itabaki kuwa nadharia yao na history itabaki kuwa history.
Kuharamisha kusoma kwa sababu ya mapungufu ya masomo hayo sio jambo jema kwa sababu pale husomi dini,unasoma utabibu ambao mengi ni mawazo ya watu.
Kwa ambae anaijua dini yake atakuwa anajua kuwa hizo mambo sio za kweli na hazina ukweli wowote atafanya yenye manufaa tu.
Ndio maana hata katika Qurani na hadithi zimenukuu baadhi ya hoja potofu za baadhi ya wapotofu na zikaonesha kuwa hoja hizo sio sahihi.
Na mtu akiwa kasoma dini huwezi kumuambia kuwa mtu wa kwanza alikuwa nyani.hili haliwezekani kabisa.
Sasa huwezi ukakataa fani nzima kwa sababu ya baadhi ya nadharia ambazo haziendani na dini.
Kusema nimesoma secular tena waona najifaragua mkuu?Kusoma siyo hoja, hoja ni kusoma na ukaelewa. Kwahiyo usilete hoja za kitoto kwamba umesoma. Wangapi wamesoma Secular lakini wanaamini ya kuwa Jua halitembei ? Sasa usijifarague kwamba umesoma, hali ya kuwa hukijui ulichokisoma.
Sasa kama kusoma secular sio haramu basi jua pia na huo udaktari sio haramu ati kwa sababu kuna baadhi ya mambo yanapingana na itikadi ya uislamu.Kaka mbona unaandika yasiyo kuwa na msingi ? Hakuna aliyesema secular ni haramu bali nimesema katika secular kuna vitu vya hovyo vitu vya kufru.
Mimi nazungumzia asili na nimekupa mifano lukuki kuthibitisha hilo.Tofautisha kati ya asili na kawaida mzee.
Pinga basi kuwa ni haramu mwanaume kuangalia nyuma kazi ambayo kiasili ni ya mwanamke ?Ukiwa unaandika uwe unarudia kusoma kwa makini, ili usiwe unarudia kile nilichokiandika.
Asili na mila havipishani mzee.Hii si asili, bali haya ni katika mila na desturi zao, zilikuwa ni kuchukia watoto wa kike, na hii ilikuwa ni katika imani potofu.
Hakuna sehemu ama ushahidi umetoa unaosema kuwa kwa dharura hakuna ushahidi ulioweka hapa.Umeona ulivyokuwa msahaulifu, ulipo niuliza swali la mwanamke harusiwi kutoka ila kwa dharura, au bila mahrim wake ulikuwa una dalili ya kupinga hili ?
Safari ni kwa mujibu wa ada za watu.Nimecheka sana, hukumu ya safari inapimwaje mzee ?
Hii ni kwa mtazamo wako bwana,watu wengi hawaoni kuwa hiyo ni safari,wapo kama wewe mtaona kuwa ni safari lakini wapo ambao wanaona kuwa sio safari.Hukumu ya safari hukadiriwa kwa kuzingatia ada na desturi, hataka kutoka kimara mpaka kibaha, hii ni safari kijana
Mbona nilikuambia kuwa hadithi hiyo ya mahrim iko wazi kabisa haina utata,alafh wewe unaniambia sina hoja ya kusema kuwa hadithi haipo ?kijana,kwahiyo bado huna hoja ya kusema hadithi haipo.
Unaposema karibu kwa mujibu wa sheria ni wapi ?Kutoka ambako si safari ni kama kwenda sokoni au duka la karibu, na hili pia huangaliwa usalama wa mtokaji. Hatoki toki tu.
Mtume hakuainisha kuwa safari ni kilomota ngapi wala ngapi.Hukumu ya safari mtume aliikadiriaje ? Embu nipe faida hapa. Maana naona unaleta maneno ambayo huna hata marejeo kwayo
Nahitaji kufanya kazi nipate pesa.Kwanza nilikuweka sawa juu ya mahitaji,mahtaji si kufanya kazi wala si kutafuta hela, mahitaji ni matumizi na hitajio
Naam haswaa aombe ruhusa.aombe ruhusa,
Hii ya mahrim ni katika safari tu ndugu mbona iko wazi kabisa kuwa mwanamke asisafiri pasi na mahrim.awe na mahrim wake na mfano wa hayo.