unaweza nipa evidence ya kutokuwepo kwa Mungu??
Kiranga anamchukia Mungu hana kingine..unapoamua kuondoa kwa makusudi uwepo wa Mungu ili hali unajua yupo, uko ni kumchukia...yani kisaikolojia ni kwamba kwake uwepo wa Mungu unamsumbua unamgasi na unamnyima uhuru wa kufanya maouvu yake,au kuna kitu ambacho anahisi Mungu kamuonea haswa kwenye maumbile..sasa ili kujipa uhuru bandia wa kufanya maovu yake anajiaminisha Mungu hayupo..au kumkomesha kutokana na mapungufu aliyompa anakomaa kwamba hayupo..kwaio kama Mungu hayupo ata zile sheria zake hazina maana sana kwake..
Sijui umeiona hoja agnostic(wewe sio mkristo)???
ahahahhaaaaaaaaaa_umenichekesha sana mkuu,..sina hasira zozote mkuu hasa kuhusu kale ka..thread ketu ka kilugha kako poa tu mbona,..
Btw..mwanzo wa maarifa yoyote ni kuhoji mkuu_hivyo sidhani kama kuhoji kwa kiranga kama ni chuki dhidi ya Mungu...mimi sio mpagani...ni mkristo kwa kuzaliwa na wazazi wakristo(si unajua mambo ya mbeya tena_full makanisa)..ila Kiranga have a point kwenye argument zake nyingi..so to speak.
Nb:..wewe sidhani kama unafanya haki kwa kumhukumu Kiranga kuwa anamchukia Mungu(ambaye hata haamini kama yupo)....hebu sisi waamini tujenge hoja za uwepo wa Mungu ili kina Kiranga watuelewe....tusikimbilie hoja dhaifu za kusema eti wanamchukia mungu(God hater)
Mimi nimekwambia simchukii mungu kwa sababu siamini kwamba yupo. Sijui utaanzaje kuchukia kitu ambacho hakipo.
Habari yako ya kwamba namchukia mungu ili nifanye maovu haina mshiko. Ukiangalia kuna waamini mungu wengi tu wanaua watu huko Nigeria kila siku.Waamini mungu ndo waliopiga nyuklia Hiroshima na Nagasaki. Waamini mungu ndo wamelipia magorofa na ndege 9/11, waamini mungu ndo wanaowafanya watoto wa Kikatoliki vibaya makanisani.
Tena ukisoma biblia na Quran unakuta mungu anachochea vita na upuuzi kibao. Kwa hiyo, contrary to your belief, mtu kama anataka kufanya mabaya anafanya, whether anaamini mungu au la. Tena anayeamini mungu ndo anatafuta justification kwenye vitabu vya dini kabisa na kuwa muuaji mkubwa kama Jim Jones au Osama.
So let's get that illusion cleared out. Mie siamini mungu na sijawahi na siko tayari kuua mtu kwa kutetea msimamo wangu huo, kuna waamini kibao ama washaua au wako tayari kuua kwa kutetea dini zao, sasa kati ya mie nisiyeamini mungu na hao wanaoamini mungu nani muovu zaidi kwa minajili hii?
Halafu habari ya kusema nataka kusema mungu hayupo ili niondoe umuhimu wa sheria zake hakuna maana. Kwa nini? Kwa sababu mtu anaweza asiamini katika uwepo wa mungu sio ili ajifungue kutoka sheria za mungu na kukosa cha kumfunga, bali kwa kutaka kupata muongozo uliojikita katika discipline zaidi kuliko sheria za mungu.
Sheria za mungu katika Judeo-Christian traditions (which include Islam and we might as well call it Judaic because that is where the cosmogony is derived from) ziko ambiguous, contradictory, subject to interpretation etc.
Ni kama methali za Kiswahili. Hapa unaambiwa "Haraka haraka haina baraka" hapa unaambiwa "Ngoja ngoja yaumiza matumbo". Ujanja wako tu. Unaweza kupinda maneno unavyotaka. Hizi si sheria za kuhusudiwa sana.
Mtu anaweza kukataa sheria za dini aka adopt a more reasonable secular humanism. Bertrand Russell katika criticism yake nzuri ya Ukristo "Why I am not a Christian" iliyopo hapa Why I Am Not A Christian, by Bertrand Russell (nakusisitiza uisome kwa makini kama unaweza) kaongelea juu ya kwamba hajafurahishwa na jinsi Yesu alivyowatendea wanyama na mimea. Kawatupa wale nguruwe kwenye mto wakafa bila ya ulazima, kaulani mti mtini kwa kutozaa matunda wakati mti mtini presumably kwa cosmogony ya kikristo umeumbwa hivyo, the height of blaming the victim. Huyu mtu ndo unataka mie niishi kwa sheria zake? Mtu anayesema "Mama Mgumba asiyezaa achomwe moto maana hatuzalii matunda" basically?
Yesu angekuwa anaishi leo watu wa PETA wangemkwida kwa kukosa maadili.
Kwa hiyo, nikisema kwamba kwa kutoamini uwepo wa mungu, sitafuti njia rahisi isiyofungwa na sheria, bali natafuta muongozo ambao ni wa logic zaidi na una viwango vikubwa zaidi sitakosea.
By the way, sina kilema chochote significantly cha mwili kama unavyodai (which is a weird assumption anyway - but what do I expect from you?- na kama kila atheist angekuwa kilema tungejua)
This brings an interesting topic, kwa nini mungu aliye na uwezo wote na upendo wote kwa watu wote aumbe wengine vilema na wengine wako fit?
Hivi Kiranga umewahi shuhudia mazingaombwe? (watu kuchinjwa na kurudishwa hai, vijiti kuwa penseli) huwa unayatafsiri namna gani? ni sayansi imefika kikomo imeshindwa kuyaelezea au ni kuna nguvu ndani yake inayozidi uwezo wa kibinadamu?. sijajua kama atheism yako inabase kwenye facts kwamba hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kwamba mungu yupo!? ila kama ndiyo sayansi huwa inatwambia ikishindwa kuthibitisha kitu haimaanishi hakipo ila inawezekana haina uwezo wa kupima.
naona ingefaa zaidi ungesema hufahamu/huna uhakika kama mungu/super natural power haipo lakini kusema moja kwa moja kwamba hayupo unatakiwa ulete ushahidi. kama hao wanasayansi wa ulaya hawawezi sema higgs particles/god's particles hazipo mpaka wawe na njia za kuaminika za kupimia ndio wata kuja na hitimisho.Haiwezekaniki kutoa evidence ya kutokuwapo kitu. You can't prove a negative.
Swali hapa ni, unaweza kunipa evidence ya kuwapo mungu?
Anayesema kitu kipo ndiye anayeulizwa evidence. Anayesema hakipo hawezi kuulizwa evidence, kwa sababu hana evidence, hawezi kuwa na evidence ya kitu kisichokuwapo.
Wewe unaweza kunipa evidence kwamba ubongo wako hauna Higgs bosom particle ndogo sana zilizoandika jina "KILIMANJARO" katika medulla oblongata yako?
Evidence yoyote utakayonipa ntakwambia haitoshelezi kwa maana Higgs particle haziwezi kuwa detected.
naona ingefaa zaidi ungesema hufahamu/huna uhakika kama mungu/super natural power haipo lakini kusema moja kwa moja kwamba hayupo unatakiwa ulete ushahidi. kama hao wanasayansi wa ulaya hawawezi sema higgs particles/god's particles hazipo mpaka wawe na njia za kuaminika za kupimia ndio wata kuja na hitimisho.
Mkuu hapa haitaji hata IGWE aje maana ukisoma post Zote Kiranga hawajamuweza hata kwa point moja. shida yetu hapa watu tunaongea kwa imani na Kiranga keshawaambia haamini akatika kuaminiMkuu IGWE,
naomba uje kuweka wazi, tena bila upendeleo,
unazionaje hoja za pande zote mbili?
Mkuu tiger hapa naona unataka kuharibu imani za watu, maana humu humu kuna wakristo hawaamini katika hili la christmass sasa sijui unatka Kiranga aseme nini hapaKiranga,
christmas inakaribia na imenikumbusha swali jingine.
Baada ya kusoma hapa na pale, unamsimamo/fikra gani juu ya existance ya Jesus, yule wa kwenye gospel, aliishi kweli?
Kiongozi vp hapo umemkubali si ndio ?ahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.....hii inafikirisha sana
Kweli inataka moyoAma hunisomi vizuri ama mgumu wa kuelewa.
Nishasema kwamba you cannot prove a negative. Huwezi ku prove kwamba mungu hayupo kwa sababu ukisema haonekani kwa macho utaambiwa mungu ni roho, ukisema haonekani kwa hesabu utaambiwa mungu hahesabiki, ukisema haonekani kwa logic utaambiwa mungu haonekani kwa logic ya kibinadamu.
Mungu by definition, ili kuusitiri uongo wa idea nzima ya kuwapo kwa mungu, hawezi kuwa proven. Kwa sababu ukifanya proof ya kuwapo au kutokuwapo mungu tayari usha m contain katika a certain system (logic, math etc) na mungu hakusanyiki katika systems hizi, na ukiweza kumkusanya huyu si mungu. Unaona complications hapo?
Yaani ku prove existence/ non existence of god ni kama ku count up to infinity. Ukiweza ku count to infinity, hiyo unayofikiri infinity si infinity, kwa sababu imeshakuwa finite.
Yaani sio tu kwamba huwezi ku prove kwamba mungu hayupo, hata ukiweza ku prove kwamba mungu yupo utakuwa ume prove kwamba mungu hayupo. Kwa sababu mungu characteristic yake ni ku defy proofs na categorizations kwa mujibu wa Judeo Christian tradition at least. No wonder he is - his character that is, he does not exist I maintain so far- is so schizophrenic.
Kwa kusema hivyo, nimeshakubali kwamba hakuna anayeweza kusema kwa uhakika kwamba mungu hayupo.
Kama vile ambavyo hakuna anayeweza kusema kwa uhakika kwamba binadamu hawezi kupita katikati ya ukuta wa tofali bila kutumia mlango, dirisha, uchawi wala kupindisha sheria za physics.
Pia hujafuatilia maandishi yangu ya sio tu kutokujua kitu, bali pia kutokujua kutokujua kwangu.
Nikisema sikubali kwamba mungu yupo nakusudia kuwapa challenge wanaoamini kwamba mungu yupo zaidi ya kusema kwamba mungu hayupo kwa uhakika.
Uhakika ni nyumba ya mjinga, mwerevu mara zote anahakiki. Na mhakiki hana hakika.
Nishasema siwezi kutoa evidence au ku prove kwamba mungu hayupo, kwa nini unafikiri nasema nina hakika mungu hayupo?
Mie ningependa sana mungu awepo.
Kwa sababu mungu akiwepo, mzigo woote wa ulimwengu uko juu yake. Mazingira yanaharibika? Utasema watu wanaharibu mazingira? Lakini hao watu wameumbwa na nani? Aliyewapa au kuwanyima akili nani?
Unasema shetani mbaya? Ndiye chanzo cha mabaya yote? Aliyemuumba na kumpa uwezo wa kuwa mbaya nani?
Kila kitu kingekuwa kinamrudia mungu.
Lakini nasikitika kusema kwamba kwa kadiri mambo yanavyoonekana hili ni jibu rahisi sana kwa ukweli ulio na matatizo mengi.
Watu wanapenda uongo mtamu (mungu yupo, ukipata matatizo muombe kama mtoto anavyomuomba baba, usi complicate mambo) kuliko ukweli mchungu (we are on our own and we have to figure things out, prayer has no value apart from being therapy on the cheap)
Mkuu hapa haitaji hata IGWE aje maana ukisoma post Zote Kiranga hawajamuweza hata kwa point moja. shida yetu hapa watu tunaongea kwa imani na Kiranga keshawaambia haamini akatika kuamini
What it do hommie TigerKiranga mwenye anakiri kuwa imani haiepukiki.
Kwahiyo hata "upagani" waweza kuwa "imani" kwa namna nyingine.