Mimi nimekwambia simchukii mungu kwa sababu siamini kwamba yupo. Sijui utaanzaje kuchukia kitu ambacho hakipo.
Habari yako ya kwamba namchukia mungu ili nifanye maovu haina mshiko. Ukiangalia kuna waamini mungu wengi tu wanaua watu huko Nigeria kila siku.Waamini mungu ndo waliopiga nyuklia Hiroshima na Nagasaki. Waamini mungu ndo wamelipia magorofa na ndege 9/11, waamini mungu ndo wanaowafanya watoto wa Kikatoliki vibaya makanisani.
Tena ukisoma biblia na Quran unakuta mungu anachochea vita na upuuzi kibao. Kwa hiyo, contrary to your belief, mtu kama anataka kufanya mabaya anafanya, whether anaamini mungu au la. Tena anayeamini mungu ndo anatafuta justification kwenye vitabu vya dini kabisa na kuwa muuaji mkubwa kama Jim Jones au Osama.
So let's get that illusion cleared out. Mie siamini mungu na sijawahi na siko tayari kuua mtu kwa kutetea msimamo wangu huo, kuna waamini kibao ama washaua au wako tayari kuua kwa kutetea dini zao, sasa kati ya mie nisiyeamini mungu na hao wanaoamini mungu nani muovu zaidi kwa minajili hii?
Halafu habari ya kusema nataka kusema mungu hayupo ili niondoe umuhimu wa sheria zake hakuna maana. Kwa nini? Kwa sababu mtu anaweza asiamini katika uwepo wa mungu sio ili ajifungue kutoka sheria za mungu na kukosa cha kumfunga, bali kwa kutaka kupata muongozo uliojikita katika discipline zaidi kuliko sheria za mungu.
Sheria za mungu katika Judeo-Christian traditions (which include Islam and we might as well call it Judaic because that is where the cosmogony is derived from) ziko ambiguous, contradictory, subject to interpretation etc.
Ni kama methali za Kiswahili. Hapa unaambiwa "
Haraka haraka haina baraka" hapa unaambiwa "Ngoja ngoja yaumiza matumbo". Ujanja wako tu. Unaweza kupinda maneno unavyotaka. Hizi si sheria za kuhusudiwa sana.
Mtu anaweza kukataa sheria za dini aka adopt a more reasonable secular humanism. Bertrand Russell katika criticism yake nzuri ya Ukristo "Why I am not a Christian" iliyopo hapa
Why I Am Not A Christian, by Bertrand Russell (nakusisitiza uisome kwa makini kama unaweza) kaongelea juu ya kwamba hajafurahishwa na jinsi Yesu alivyowatendea wanyama na mimea. Kawatupa wale nguruwe kwenye mto wakafa bila ya ulazima, kaulani mti mtini kwa kutozaa matunda wakati mti mtini presumably kwa cosmogony ya kikristo umeumbwa hivyo, the height of blaming the victim. Huyu mtu ndo unataka mie niishi kwa sheria zake? Mtu anayesema "Mama Mgumba asiyezaa achomwe moto maana hatuzalii matunda" basically?
Yesu angekuwa anaishi leo watu wa PETA wangemkwida kwa kukosa maadili.
Kwa hiyo, nikisema kwamba kwa kutoamini uwepo wa mungu, sitafuti njia rahisi isiyofungwa na sheria, bali natafuta muongozo ambao ni wa logic zaidi na una viwango vikubwa zaidi sitakosea.
By the way, sina kilema chochote significantly cha mwili kama unavyodai (which is a weird assumption anyway - but what do I expect from you?- na kama kila atheist angekuwa kilema tungejua)
This brings an interesting topic, kwa nini mungu aliye na uwezo wote na upendo wote kwa watu wote aumbe wengine vilema na wengine wako fit?