Swali la kizushi kwa Kiranga.

Swali la kizushi kwa Kiranga.

unaweza nipa evidence ya kutokuwepo kwa Mungu??

Haiwezekaniki kutoa evidence ya kutokuwapo kitu. You can't prove a negative.

Swali hapa ni, unaweza kunipa evidence ya kuwapo mungu?

Anayesema kitu kipo ndiye anayeulizwa evidence. Anayesema hakipo hawezi kuulizwa evidence, kwa sababu hana evidence, hawezi kuwa na evidence ya kitu kisichokuwapo.

Wewe unaweza kunipa evidence kwamba ubongo wako hauna Higgs bosom particle ndogo sana zilizoandika jina "KILIMANJARO" katika medulla oblongata yako?

Evidence yoyote utakayonipa ntakwambia haitoshelezi kwa maana Higgs particle haziwezi kuwa detected.
 
Kiranga anamchukia Mungu hana kingine..unapoamua kuondoa kwa makusudi uwepo wa Mungu ili hali unajua yupo, uko ni kumchukia...yani kisaikolojia ni kwamba kwake uwepo wa Mungu unamsumbua unamgasi na unamnyima uhuru wa kufanya maouvu yake,au kuna kitu ambacho anahisi Mungu kamuonea haswa kwenye maumbile..sasa ili kujipa uhuru bandia wa kufanya maovu yake anajiaminisha Mungu hayupo..au kumkomesha kutokana na mapungufu aliyompa anakomaa kwamba hayupo..kwaio kama Mungu hayupo ata zile sheria zake hazina maana sana kwake..

Sijui umeiona hoja agnostic(wewe sio mkristo)???

Mimi nimekwambia simchukii mungu kwa sababu siamini kwamba yupo. Sijui utaanzaje kuchukia kitu ambacho hakipo.

Habari yako ya kwamba namchukia mungu ili nifanye maovu haina mshiko. Ukiangalia kuna waamini mungu wengi tu wanaua watu huko Nigeria kila siku.Waamini mungu ndo waliopiga nyuklia Hiroshima na Nagasaki. Waamini mungu ndo wamelipia magorofa na ndege 9/11, waamini mungu ndo wanaowafanya watoto wa Kikatoliki vibaya makanisani.

Tena ukisoma biblia na Quran unakuta mungu anachochea vita na upuuzi kibao. Kwa hiyo, contrary to your belief, mtu kama anataka kufanya mabaya anafanya, whether anaamini mungu au la. Tena anayeamini mungu ndo anatafuta justification kwenye vitabu vya dini kabisa na kuwa muuaji mkubwa kama Jim Jones au Osama.

So let's get that illusion cleared out. Mie siamini mungu na sijawahi na siko tayari kuua mtu kwa kutetea msimamo wangu huo, kuna waamini kibao ama washaua au wako tayari kuua kwa kutetea dini zao, sasa kati ya mie nisiyeamini mungu na hao wanaoamini mungu nani muovu zaidi kwa minajili hii?

Halafu habari ya kusema nataka kusema mungu hayupo ili niondoe umuhimu wa sheria zake hakuna maana. Kwa nini? Kwa sababu mtu anaweza asiamini katika uwepo wa mungu sio ili ajifungue kutoka sheria za mungu na kukosa cha kumfunga, bali kwa kutaka kupata muongozo uliojikita katika discipline zaidi kuliko sheria za mungu.

Sheria za mungu katika Judeo-Christian traditions (which include Islam and we might as well call it Judaic because that is where the cosmogony is derived from) ziko ambiguous, contradictory, subject to interpretation etc.

Ni kama methali za Kiswahili. Hapa unaambiwa "Haraka haraka haina baraka" hapa unaambiwa "Ngoja ngoja yaumiza matumbo". Ujanja wako tu. Unaweza kupinda maneno unavyotaka. Hizi si sheria za kuhusudiwa sana.

Mtu anaweza kukataa sheria za dini aka adopt a more reasonable secular humanism. Bertrand Russell katika criticism yake nzuri ya Ukristo "Why I am not a Christian" iliyopo hapa Why I Am Not A Christian, by Bertrand Russell (nakusisitiza uisome kwa makini kama unaweza) kaongelea juu ya kwamba hajafurahishwa na jinsi Yesu alivyowatendea wanyama na mimea. Kawatupa wale nguruwe kwenye mto wakafa bila ya ulazima, kaulani mti mtini kwa kutozaa matunda wakati mti mtini presumably kwa cosmogony ya kikristo umeumbwa hivyo, the height of blaming the victim. Huyu mtu ndo unataka mie niishi kwa sheria zake? Mtu anayesema "Mama Mgumba asiyezaa achomwe moto maana hatuzalii matunda" basically?

Yesu angekuwa anaishi leo watu wa PETA wangemkwida kwa kukosa maadili.

Kwa hiyo, nikisema kwamba kwa kutoamini uwepo wa mungu, sitafuti njia rahisi isiyofungwa na sheria, bali natafuta muongozo ambao ni wa logic zaidi na una viwango vikubwa zaidi sitakosea.

By the way, sina kilema chochote significantly cha mwili kama unavyodai (which is a weird assumption anyway - but what do I expect from you?- na kama kila atheist angekuwa kilema tungejua)

This brings an interesting topic, kwa nini mungu aliye na uwezo wote na upendo wote kwa watu wote aumbe wengine vilema na wengine wako fit?
 
ahahahhaaaaaaaaaa_umenichekesha sana mkuu,..sina hasira zozote mkuu hasa kuhusu kale ka..thread ketu ka kilugha kako poa tu mbona,..

Btw..mwanzo wa maarifa yoyote ni kuhoji mkuu_hivyo sidhani kama kuhoji kwa kiranga kama ni chuki dhidi ya Mungu...mimi sio mpagani...ni mkristo kwa kuzaliwa na wazazi wakristo(si unajua mambo ya mbeya tena_full makanisa)..ila Kiranga have a point kwenye argument zake nyingi..so to speak.

Nb:..wewe sidhani kama unafanya haki kwa kumhukumu Kiranga kuwa anamchukia Mungu(ambaye hata haamini kama yupo)....hebu sisi waamini tujenge hoja za uwepo wa Mungu ili kina Kiranga watuelewe....tusikimbilie hoja dhaifu za kusema eti wanamchukia mungu(God hater)

Kuna quote moja ya Oliver Cromwell ( I just can't find the exact quote), mtu wa imani sana, inayosema something to the effect of waumini wa kweli wanapaswa kuwashukuru wasioamini kuwapo mungu wanavyouliza maswali magumu kwa sababu kama wanaweza kuwajibu maswali yao vilivyo na kubakia na imani yao, hao wasioamini kuwapo kwa mungu wanawasaidia waumini kuimarisha imani zao.

Hakusema nini kitokee kama maswali magumu hayajibiwi.

Labda badala ya kunisema kama hasidi mchukia mungu, waumini waniangalie kwa jicho chanya kama mtu ninayeweza kuimarisha imani zao (kama wataweza kunijibu vilivyo) au kuwafungua macho vinginevyo.

Muumini wa kweli haogopi challenge.
 
Mimi nimekwambia simchukii mungu kwa sababu siamini kwamba yupo. Sijui utaanzaje kuchukia kitu ambacho hakipo.

Habari yako ya kwamba namchukia mungu ili nifanye maovu haina mshiko. Ukiangalia kuna waamini mungu wengi tu wanaua watu huko Nigeria kila siku.Waamini mungu ndo waliopiga nyuklia Hiroshima na Nagasaki. Waamini mungu ndo wamelipia magorofa na ndege 9/11, waamini mungu ndo wanaowafanya watoto wa Kikatoliki vibaya makanisani.

Tena ukisoma biblia na Quran unakuta mungu anachochea vita na upuuzi kibao. Kwa hiyo, contrary to your belief, mtu kama anataka kufanya mabaya anafanya, whether anaamini mungu au la. Tena anayeamini mungu ndo anatafuta justification kwenye vitabu vya dini kabisa na kuwa muuaji mkubwa kama Jim Jones au Osama.

So let's get that illusion cleared out. Mie siamini mungu na sijawahi na siko tayari kuua mtu kwa kutetea msimamo wangu huo, kuna waamini kibao ama washaua au wako tayari kuua kwa kutetea dini zao, sasa kati ya mie nisiyeamini mungu na hao wanaoamini mungu nani muovu zaidi kwa minajili hii?

Halafu habari ya kusema nataka kusema mungu hayupo ili niondoe umuhimu wa sheria zake hakuna maana. Kwa nini? Kwa sababu mtu anaweza asiamini katika uwepo wa mungu sio ili ajifungue kutoka sheria za mungu na kukosa cha kumfunga, bali kwa kutaka kupata muongozo uliojikita katika discipline zaidi kuliko sheria za mungu.

Sheria za mungu katika Judeo-Christian traditions (which include Islam and we might as well call it Judaic because that is where the cosmogony is derived from) ziko ambiguous, contradictory, subject to interpretation etc.

Ni kama methali za Kiswahili. Hapa unaambiwa "Haraka haraka haina baraka" hapa unaambiwa "Ngoja ngoja yaumiza matumbo". Ujanja wako tu. Unaweza kupinda maneno unavyotaka. Hizi si sheria za kuhusudiwa sana.

Mtu anaweza kukataa sheria za dini aka adopt a more reasonable secular humanism. Bertrand Russell katika criticism yake nzuri ya Ukristo "Why I am not a Christian" iliyopo hapa Why I Am Not A Christian, by Bertrand Russell (nakusisitiza uisome kwa makini kama unaweza) kaongelea juu ya kwamba hajafurahishwa na jinsi Yesu alivyowatendea wanyama na mimea. Kawatupa wale nguruwe kwenye mto wakafa bila ya ulazima, kaulani mti mtini kwa kutozaa matunda wakati mti mtini presumably kwa cosmogony ya kikristo umeumbwa hivyo, the height of blaming the victim. Huyu mtu ndo unataka mie niishi kwa sheria zake? Mtu anayesema "Mama Mgumba asiyezaa achomwe moto maana hatuzalii matunda" basically?

Yesu angekuwa anaishi leo watu wa PETA wangemkwida kwa kukosa maadili.

Kwa hiyo, nikisema kwamba kwa kutoamini uwepo wa mungu, sitafuti njia rahisi isiyofungwa na sheria, bali natafuta muongozo ambao ni wa logic zaidi na una viwango vikubwa zaidi sitakosea.

By the way, sina kilema chochote significantly cha mwili kama unavyodai (which is a weird assumption anyway - but what do I expect from you?- na kama kila atheist angekuwa kilema tungejua)

This brings an interesting topic, kwa nini mungu aliye na uwezo wote na upendo wote kwa watu wote aumbe wengine vilema na wengine wako fit?

ahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.....hii inafikirisha sana
 
Hivi Kiranga umewahi shuhudia mazingaombwe? (watu kuchinjwa na kurudishwa hai, vijiti kuwa penseli) huwa unayatafsiri namna gani? ni sayansi imefika kikomo imeshindwa kuyaelezea au ni kuna nguvu ndani yake inayozidi uwezo wa kibinadamu?. sijajua kama atheism yako inabase kwenye facts kwamba hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kwamba mungu yupo!? ila kama ndiyo sayansi huwa inatwambia ikishindwa kuthibitisha kitu haimaanishi hakipo ila inawezekana haina uwezo wa kupima.
 
Last edited by a moderator:

Nimesoma historia ya mazingaombwe, the common hand sleights, tricks za Harry Houdini etc.

This "mazingaombwe", if you go down to etimology (one of my favorite passtimes), is really "mazingira ombwe". The creation of an illusion that devoids the whole environment of reality, pushing the envelope of believability by the use of tricks, angles, colors and manipulation of time and space. Hakuna tofauti kati ya mtu kuchinjwa na karata tatu if you take the time to investigate.

Tatizo wengi hatutaki ku investigate.

Your question, and the whole mazingaombwe meme, brings about a larger point.

One can argue that far and above mazingaombwe, everything that does seem supernatural, seems so only due to the poverty of our minds. As times goes on and we perfect our knowledge base, all types of seemingly supernatural phenomena will be deciphered as purely natural.

The common convergence surely points to this point, even if it will be shrouded by the Planck scale asymptote and some Heisenberg like uncertainties catapulted by the inherent probabilistic heartbeat of the universe.
 
Haiwezekaniki kutoa evidence ya kutokuwapo kitu. You can't prove a negative.

Swali hapa ni, unaweza kunipa evidence ya kuwapo mungu?

Anayesema kitu kipo ndiye anayeulizwa evidence. Anayesema hakipo hawezi kuulizwa evidence, kwa sababu hana evidence, hawezi kuwa na evidence ya kitu kisichokuwapo.

Wewe unaweza kunipa evidence kwamba ubongo wako hauna Higgs bosom particle ndogo sana zilizoandika jina "KILIMANJARO" katika medulla oblongata yako?

Evidence yoyote utakayonipa ntakwambia haitoshelezi kwa maana Higgs particle haziwezi kuwa detected.
naona ingefaa zaidi ungesema hufahamu/huna uhakika kama mungu/super natural power haipo lakini kusema moja kwa moja kwamba hayupo unatakiwa ulete ushahidi. kama hao wanasayansi wa ulaya hawawezi sema higgs particles/god's particles hazipo mpaka wawe na njia za kuaminika za kupimia ndio wata kuja na hitimisho.
 
Hahahaha Kiranga hata wakina rwaakatare,kakobe,mwingira n tb joshua cant prove the existence of god never the thing is so confusing ukiisoma biblia its so complicating book for even the followe of so called bible ukija kuran never will tell all of them are against written lol.aisee welcome karibu sana .mimi niko pembeni nawatch hizi dini and see the end .naamini once u die there its your end ,no life after death,siwezi amini mtu sijawahi mwona,nikufikirika tututu hakuna aliyekufa akarudi kutuhabarisha,
 
Last edited by a moderator:
naona ingefaa zaidi ungesema hufahamu/huna uhakika kama mungu/super natural power haipo lakini kusema moja kwa moja kwamba hayupo unatakiwa ulete ushahidi. kama hao wanasayansi wa ulaya hawawezi sema higgs particles/god's particles hazipo mpaka wawe na njia za kuaminika za kupimia ndio wata kuja na hitimisho.

Ama hunisomi vizuri ama mgumu wa kuelewa.

Nishasema kwamba you cannot prove a negative. Huwezi ku prove kwamba mungu hayupo kwa sababu ukisema haonekani kwa macho utaambiwa mungu ni roho, ukisema haonekani kwa hesabu utaambiwa mungu hahesabiki, ukisema haonekani kwa logic utaambiwa mungu haonekani kwa logic ya kibinadamu.

Mungu by definition, ili kuusitiri uongo wa idea nzima ya kuwapo kwa mungu, hawezi kuwa proven. Kwa sababu ukifanya proof ya kuwapo au kutokuwapo mungu tayari usha m contain katika a certain system (logic, math etc) na mungu hakusanyiki katika systems hizi, na ukiweza kumkusanya huyu si mungu. Unaona complications hapo?

Yaani ku prove existence/ non existence of god ni kama ku count up to infinity. Ukiweza ku count to infinity, hiyo unayofikiri infinity si infinity, kwa sababu imeshakuwa finite.

Yaani sio tu kwamba huwezi ku prove kwamba mungu hayupo, hata ukiweza ku prove kwamba mungu yupo utakuwa ume prove kwamba mungu hayupo. Kwa sababu mungu characteristic yake ni ku defy proofs na categorizations kwa mujibu wa Judeo Christian tradition at least. No wonder he is - his character that is, he does not exist I maintain so far- is so schizophrenic.

Kwa kusema hivyo, nimeshakubali kwamba hakuna anayeweza kusema kwa uhakika kwamba mungu hayupo.

Kama vile ambavyo hakuna anayeweza kusema kwa uhakika kwamba binadamu hawezi kupita katikati ya ukuta wa tofali bila kutumia mlango, dirisha, uchawi wala kupindisha sheria za physics.

Pia hujafuatilia maandishi yangu ya sio tu kutokujua kitu, bali pia kutokujua kutokujua kwangu.

Nikisema sikubali kwamba mungu yupo nakusudia kuwapa challenge wanaoamini kwamba mungu yupo zaidi ya kusema kwamba mungu hayupo kwa uhakika.

Uhakika ni nyumba ya mjinga, mwerevu mara zote anahakiki. Na mhakiki hana hakika.

Nishasema siwezi kutoa evidence au ku prove kwamba mungu hayupo, kwa nini unafikiri nasema nina hakika mungu hayupo?

Mie ningependa sana mungu awepo.

Kwa sababu mungu akiwepo, mzigo woote wa ulimwengu uko juu yake. Mazingira yanaharibika? Utasema watu wanaharibu mazingira? Lakini hao watu wameumbwa na nani? Aliyewapa au kuwanyima akili nani?

Unasema shetani mbaya? Ndiye chanzo cha mabaya yote? Aliyemuumba na kumpa uwezo wa kuwa mbaya nani?

Kila kitu kingekuwa kinamrudia mungu.

Lakini nasikitika kusema kwamba kwa kadiri mambo yanavyoonekana hili ni jibu rahisi sana kwa ukweli ulio na matatizo mengi.

Watu wanapenda uongo mtamu (mungu yupo, ukipata matatizo muombe kama mtoto anavyomuomba baba, usi complicate mambo) kuliko ukweli mchungu (we are on our own and we have to figure things out, prayer has no value apart from being therapy on the cheap)
 
Mi naomba kufahamu hili:
je, ni sahihi kusema "mungu mwenyezi" huwa anakasirika, anaona wivu, na anasikitikia maamuzi yake mwenyewe kama alivyosikitikia mafuriko ya nuhu na kuahidi hatofanya vile tena?
 
Kiranga hapa ndipo christians walipofichiwa ukweli kwamba 'MUNGU NI ROHO NAO WAMWABUDUO WANAPASWA KUMWABYDU KATIKA ROHO NA KWELI:hapa ndipo uongo ulipo.hata hawa wahubiri wakubwa ukiwauliza the same question hawana jibu sahihi watakuambia tunaamini yupo sababu ya matendo yake makuu anayoyafanya,swali mbona yata shetani hufanya miujiza? Just try to ask hakuna hata mmja atakuambia existence of called God never,zaidi utaishia kutishiwa tishiwa tu.naamini kweli if God is there watu wanaobuni vitendo vibaya ,ushoga ,wizi,wauaji asingeewaacha waishi,nendeni mahospitalini muone jinsi watoto wadogo wanazaliwa na magonjwa hatari kansa ,yaani ukifika ocean road utasikitika .hii imewafanya wengi kuwa wajinga na maskini na ndio sababu wazungu wengi hawana dini,they live and wait to die only ;god existence ni dhana iliyotumiwa na waliotuzidi akili pia ni dhana ya woga tuliopandikizwa ili iwe rahisi kutuibia.god never exist.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu IGWE,
naomba uje kuweka wazi, tena bila upendeleo,
unazionaje hoja za pande zote mbili?
 
Kiranga,
christmas inakaribia na imenikumbusha swali jingine.
Baada ya kusoma hapa na pale, unamsimamo/fikra gani juu ya existance ya Jesus, yule wa kwenye gospel, aliishi kweli?
 
Mkuu hapa haitaji hata IGWE aje maana ukisoma post Zote Kiranga hawajamuweza hata kwa point moja. shida yetu hapa watu tunaongea kwa imani na Kiranga keshawaambia haamini akatika kuamini
 
Last edited by a moderator:
Kiranga,
christmas inakaribia na imenikumbusha swali jingine.
Baada ya kusoma hapa na pale, unamsimamo/fikra gani juu ya existance ya Jesus, yule wa kwenye gospel, aliishi kweli?
Mkuu tiger hapa naona unataka kuharibu imani za watu, maana humu humu kuna wakristo hawaamini katika hili la christmass sasa sijui unatka Kiranga aseme nini hapa
 
Last edited by a moderator:
Kila nikimsoma Kiranga najikuta najifunza kitu, maana sio lazima ukubaliane na anayosema ila anatujenga kujibu maswali kwa logic na uelewa sio kwa kukurupuka. Anajua sana kujenga hija . Kudos Kiranga ila kwenye imani mi ni muumini wa imani usiniulizea maswali lakini lol
 
Last edited by a moderator:
Ama hunisomi vizuri ama mgumu wa kuelewa.

Nishasema kwamba you cannot prove a negative. Huwezi ku prove kwamba mungu hayupo kwa sababu ukisema haonekani kwa macho utaambiwa mungu ni roho, ukisema haonekani kwa hesabu utaambiwa mungu hahesabiki, ukisema haonekani kwa logic utaambiwa mungu haonekani kwa logic ya kibinadamu.

Mungu by definition, ili kuusitiri uongo wa idea nzima ya kuwapo kwa mungu, hawezi kuwa proven. Kwa sababu ukifanya proof ya kuwapo au kutokuwapo mungu tayari usha m contain katika a certain system (logic, math etc) na mungu hakusanyiki katika systems hizi, na ukiweza kumkusanya huyu si mungu. Unaona complications hapo?

Yaani ku prove existence/ non existence of god ni kama ku count up to infinity. Ukiweza ku count to infinity, hiyo unayofikiri infinity si infinity, kwa sababu imeshakuwa finite.

Yaani sio tu kwamba huwezi ku prove kwamba mungu hayupo, hata ukiweza ku prove kwamba mungu yupo utakuwa ume prove kwamba mungu hayupo. Kwa sababu mungu characteristic yake ni ku defy proofs na categorizations kwa mujibu wa Judeo Christian tradition at least. No wonder he is - his character that is, he does not exist I maintain so far- is so schizophrenic.

Kwa kusema hivyo, nimeshakubali kwamba hakuna anayeweza kusema kwa uhakika kwamba mungu hayupo.

Kama vile ambavyo hakuna anayeweza kusema kwa uhakika kwamba binadamu hawezi kupita katikati ya ukuta wa tofali bila kutumia mlango, dirisha, uchawi wala kupindisha sheria za physics.

Pia hujafuatilia maandishi yangu ya sio tu kutokujua kitu, bali pia kutokujua kutokujua kwangu.

Nikisema sikubali kwamba mungu yupo nakusudia kuwapa challenge wanaoamini kwamba mungu yupo zaidi ya kusema kwamba mungu hayupo kwa uhakika.

Uhakika ni nyumba ya mjinga, mwerevu mara zote anahakiki. Na mhakiki hana hakika.

Nishasema siwezi kutoa evidence au ku prove kwamba mungu hayupo, kwa nini unafikiri nasema nina hakika mungu hayupo?

Mie ningependa sana mungu awepo.

Kwa sababu mungu akiwepo, mzigo woote wa ulimwengu uko juu yake. Mazingira yanaharibika? Utasema watu wanaharibu mazingira? Lakini hao watu wameumbwa na nani? Aliyewapa au kuwanyima akili nani?

Unasema shetani mbaya? Ndiye chanzo cha mabaya yote? Aliyemuumba na kumpa uwezo wa kuwa mbaya nani?

Kila kitu kingekuwa kinamrudia mungu.

Lakini nasikitika kusema kwamba kwa kadiri mambo yanavyoonekana hili ni jibu rahisi sana kwa ukweli ulio na matatizo mengi.

Watu wanapenda uongo mtamu (mungu yupo, ukipata matatizo muombe kama mtoto anavyomuomba baba, usi complicate mambo) kuliko ukweli mchungu (we are on our own and we have to figure things out, prayer has no value apart from being therapy on the cheap)
Kweli inataka moyo
 
Mkuu hapa haitaji hata IGWE aje maana ukisoma post Zote Kiranga hawajamuweza hata kwa point moja. shida yetu hapa watu tunaongea kwa imani na Kiranga keshawaambia haamini akatika kuamini

Kiranga mwenyewe anakiri kuwa imani haiepukiki.
Kwahiyo hata "upagani" waweza kuwa "imani" kwa namna nyingine.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom