Yote uliyosema ni kweli ila unayatafsiri vibaya hasa unapotaka kutenganisha function ya security na ya intelligence ambazo naturally ziko intertwinned.
Nikurudisha nyuma tena kuwa CIA hawana jurisdiction ndani ya nchi, hawaruhusiwi kabisa kufanya ujasusi ndani ya nchi. Mambo yote ambayo CIA wangependa kuyajua yanapotokea ndani ya mipaka, yanakuwa ni crimes inayoshughulikiwa na FBI ambao wana kitengo kinaitwa Intelligence Branch (IB). Iwapo uhalifu huo unafanyika ndani ya mipaka ukiwa unahusisha na watu walioko nje ya nchi, basi NSA ndiyo inayoshulikia. Electronic surveilance ni sehemu moja tu ya kazi za NSA lakini zipo nyingine. It happens tu kuwa mtu anayefanya mambo yanayodhaniwa kuwa ya ughaidi akiwa anashirikian na watu wa nje atatumia mawasiliano electronic, kwa hiyo ndiyo maana electronic surveillance inaonekana kuwa ni kubwa sana, lakini elewa pia kuwa CIA nao wana electronic surveilance yao. Kwa hiyo ni kweli kuwa NSA ina juridiscation ndani na nje ya nchi hivyo ni kubwa zaidi ya CIA, lakini kuna majukumu ambayo yamepewa CIA tu nje ya mipaka ambayo NSA hawawezi kuyafanya . Hiyo ni pamoja na kuwa CIA inaweza kufanya sabotages mbalimbali pamoja na assasination ya magaidi ambao ni hatari kwa usalama wa Marekani, vitu ambavyo NSA haiwezi kuvifanya.
Siyo kweli kuwa security agencies zote ni za ujasusi kama wa CIA wala hazina malengo yanayofanana. Agencies hizo nyingi ni za ujasusi wa kijeshi kulingana na branches za jeshi la marekani. Agency za kiraia, zaidi ya CIA, FBI, na NSI (hii iko pande zote za kiraia na kijeshi) nyingine ni pamoja na ONSI (ujasusi wa kutafuta taarifa za vyanzo vya madawa ya kulevya), OICI (Ujasusi wa kutafuta habari zinazohatarisha nishati ndani ya nchi pamoja na ujasusi wa kutafuta habari kuhusu matumuizi mabaya ya nishati ya nyuklia) na INR ( kwa ajili ya ujasui kutafuta habari zinazohusu usalama wa mabalozi). Agencies nyingine huwa hazifanyi ujasusi bali zinafanya analysis ya habari za kijasusi zinazopatikana kutoka kwenye agencies nyingine kwa malengo maalumu. Hizi ni pamoja na OIA (kuchambua taarifa mbalimbali za kijsausi kuangalia kama zinahusisha utakatishaji wa pesa) na I&A ( hii inakusanya taarifa mbalimbali za kijasusi na kuchambua namna ya kuzifikisha kwenye idara zinazaozhitaji habari hizo zaidi). Agency nyingine zote za kijasusi zilizobaki ni kwa sababu ya branches mbalilmbali za kijeshi tu, sasa hivi imeongezwa moja ya Space Delta 7 kwa ajili ya ujasusi unaohusiana na usalama wa satellites tu