KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Castr pita hapa
 
Twin_Kids

Mahakamani unaweza kupelekwa na kesi ikawa against your favor.

Ukienda BRAC au NMB kukopa unaweka dhamana kitu. Online hauweki kitu, in theory tunatarajia hitaji lako la next loan ndilo litakupush ulipe (in practice ni mchanganyiko na sitaandika)

a) Ili nijue riba ya kampuni natakiwa kujua principal amount aliyopokea mleta uzi na alichotakiwa kurudisha. Riba imo ndani ya maelekezo ya BOT.

b) Mkopo ni wa online. Kuonana, kunaua logic ya msingi ya mkopo wa online.

c) Unatumiwa SMS/ Unapigiwa na namba tofauti kwakua mteja una stages. Kuna stage 0 (Kabla haujaoverdue), stage 1 (baada ya kuoverdue kwa siku 1 mpaka 3 au 7), stage 2 (umeoverdue kuanzia siku 4 n.k) so ni lazima utapigiwa na namba tofauti kwakua hizo stages zote zina staff tofauti.

2) Upo sahihi. Kuna namna za kuongea na mteja na emergency contacts. Hizi contacts ambazo wamepata access sijui sheria inasemaje. Hizi siwezi kuzisemea, kama unahisi unaweza kushinda mahakamani jaribu kumshirikisha mwanasheria.

3) Taasisi zinajulikana. Nilielezea ni kwanini mnafeel hazijulikani but zinajulikana. So kutojulikana usiutumie kama msingi, as I said earlier ni ngumu online platform na mteja kukutana kudiscuss malipo, ikiwa mteja anaona kuna umuhimu huo ni bora akapokea simu na kujielezea.

Of course kampuni nyingi hua zinaweza kumfanyia exemption mteja mfano badala ya 35K akalipa 25K. Kwa ulichoandika hapa naona haujui Fintech inafanyaje kazi kwa % kubwa.

Hela za kugawa kama njugu? Hili swali ni la kitoto mno sioni kama ni level yangu ya uelewa kulijibu. Kama mitandao ya simu itakua inakata pesa kutakua hakuna haja ya uwepo wa debt collectors.
 
Overdue gani mimi watu wametumiwa sms asubuhi saa nne wakati nilitakiwa nilipe saa kumi
 
Wanafanya kusudi hao wakopeshaji...lengo tu ili endelee kuwa mateka wao wa kuwakopa maana washakuchafua kwa jamaa zako lazima kurudi kwao kukopa.

Kudhibitisha hilo, mwenzetu hapo katueleza kuwa PS wao alilipa deni lakini bado wakamtangaza kwa jamaa zake hajalipa.
 
Pole kwa yaliyokukuta ndugu Putin;

Kwa sasa wewe walipe pesa yao kwanza; halafu rudi kwenye Vigezo na Masharti ya mkopo, inawezekana hukusoma vizuri ama ulisoma vizuri na hakuna popote ambapo kulikuwa na suala la Contacts kwenye simu yako kujulishwa juu ya kushindwa kwako kulipa mkopo.
Kutokulipa mkopo kwa wakati sio utapeli.

Kama una muda wa kutosha kushughulikia hili basi endelea na kesi; ila nikushauri tu kwa sasa jipe muda kwanza walau siku tatu ukae na utafakari.

Nikupe ushauri tu; kwa kweli usiwaze sana kuhusu kudhalilika kwa sababu hao watu unawaona na kudhani kuwa hawana mikopo wapo ambao wanayo mikopo. Na hata wale ambao hawana mikopo bado hawawezi kushangaa kudaiwa 50,000/- ni maisha tu na matukio yake.
 
Overdue gani mimi watu wametumiwa sms asubuhi saa nne wakati nilitakiwa nilipe saa kumi
Overdue ni siku siyo saa.

Kama unatakiwa kulipa Ijumaa.

Alhamis utakumbushwa.

Ijumaa utadaiwa. So hata kama ni Ijumaa saa 1 asubuhi tayari ni Ijumaa
 
Watu wengi hawajui vitu ila wanaandika kama wanajua.

Hii ndiyo shida ya online.

Katika watu wote kuna jamaa anaandika lakini naona ni anaandika kwa hisia huku hana taarifa sahihi.

Vladmir Putini elewa kila nilichoandika. Nimekuandikia vingi nimegusa hadi hiyo option ya mahakama ambayo kuna member anasema wakipata kauzu atapiga hela.
 
Ki ufupi mahakamani siendi, na deni silipi, nimeshakopa makampuni 8 sasahivi na sina mpango wa kuwalipa, mahakamani waanze wao kwenda
 
Overdue ni siku siyo saa.

Kama unatakiwa kulipa Ijumaa.

Alhamis utakumbushwa.

Ijumaa utadaiwa. So hata kama ni Ijumaa saa 1 asubuhi tayari ni Ijumaa
Hivi unajua maana ya overdue unayoizungumzia wewe.

Mimi nnachojua overdue ni kupitiliza siku/mda ulitakiwa kulipa.

Leo ni jumatatu natakiwa kulipa leo jumatatu pesa, alafu iweje asubuhi tu uamke uanze kuwatumia sms watu mimi ni tapeli.

Ungesubiri jumanne ifike ndiyo useme nime overdue
 
Ushauri wako mzuri, ila kuwalia siwalipi, wanadharau sana hao jamaa.

Nimepoteza vingi sana kwa sababu ya sms yao
 
Ushauri wako mzuri, ila kuwalia siwalipi, wanadharau sana hao jamaa.

Nimepoteza vingi sana kwa sababu ya sms yao
Well, unaweza kuamua usiwalipe naamini ipo ndani ya uwezo wako.

Labda nikuulize, ulichelewa kuwalipa wakaamua kukudhalilisha kwa ndugu jamaa, marafiki, business partners, wafanyakazi wenzako, majirani, bodaboda, mashemeji na wakwe zako.
Wao wataendelea kutuma hizo meseji kwa hao watu mfululizo kwa siku hata kwa wiki kadhaa. Ipi bora kwako, kulipa na kuendelea na maisha yako au hao contacts zaklo waendelee kupokea meseji za kwamba wewe ni Tapeli?
Mambo ya kuzingatia yapo kwenye haya maswali
1. Je ni kweli ulikopa? - Wakati uliopita
2. Je ni kweli ulikuwa na nia ya kulipa? - Jukumu la sasa

Hakuna atakayeshangaa wewe kukopa na kudaiwa ila kila mtu atashangaa kwamba ulikopa na sasa hutaki kulipa.

Sijui una umri gani ila maisha yamenifundisha kuwa ni rahisi kuishi kama utaruhusu mambo yaishe. Katika hili kuruhusu kuisha ni kukubali kulipa.

Zingatia kuwa siungi mkono suala la hii kampuni kutuma hizo meseji kwa contacts zako.
 
K
Ni kweli nilikopa.

Ni kweli nilikuwa na nia ya kuwalipa.

Na kitu kingine ni kwamba sikupitiliza mda wa kuwalipa.

Mfano : natakiwa kulipa deni leo jumatatu, then wao wakaamka asubuhi hiyo jumatatu wakasambaza sms kwa contact zangu kuwa mimi nina nia ya kuwatapeli.

Sms hizo zilifanya niingie doa sana kwa baadhi ya watu nna heshimiana nao wakiamini kwamba mimi niliwaweka kama wadhamini.

Ni kibaya zaidi wakawa wanawapigia baadhi simu wakiwaambia wananidai laki 5 instead of 56,000/=

Hali hiyo ilinivuruga na kunipa msongo wa mawazo na ndiyo hapo nia ya kutowalipa ilipoondoka kabisa.

Maana nikaona kama kudhalilika nishadhalilika alafu hao hao walionidhalilisha eti niwalipe tena, kwangu mimi hapana.

Nikuulize wewe swali, kwenye muktadha wako wa kukubali yaishe, unadhani nikiwalipa ndiyo udhalilishaji walionifanyia utafutika na kurudisha heshima yangu kwa watu hao kama mwanzo ?

Kama jibu itakuwa ni hapana, unadhani kwanini sasa niwalipe ?
 
Upo sahihi; hawakuzingatia muda wa mkopo
 
Usiwalipe kama ambavyo umeamua.
 
Walisha haribikiwa kisaikolojia kwamba ukichelewa Tu kuwalipa hata kama ni siku tatu kabla ya siku za rejesho wanaanza vitimbi vya kizalilishaji.

Mimi nilivyoona wameanza huo ujinga niliachana na mamikopo Yao. Yaani walisha athirika na kutapeliwa tatizo Lao ni Liba kubwa muda mfupi MTU mwenye njaa anaona Acha akope hivyo hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…