Overdue ni siku siyo saa.
Kama unatakiwa kulipa Ijumaa.
Alhamis utakumbushwa.
Ijumaa utadaiwa. So hata kama ni Ijumaa saa 1 asubuhi tayari ni Ijumaa
Mkuu,
Kweli si kwamba watu wote watakua waaminifu. Lakini,nchi zilizoendelea,kwa nini zimeweza? Mfano,marekani,ukilimbikiza madeni,utajuta kuhudumiwa. Si uzuri wanajua unapata?
Sasa,maisha yetu ya kibongo bongo, wenyewe si mnayajua? Wekeni mambo safi. Kama mtu kaajiliwa,mjue kweli atalipa?
Kwani nyie,kuwapigia wadhamini kabla hamjatoa mkopo mnashindwa? Hii italeta nidhamu. Pigia mtu kistaarabu,mueleze sababu ya kumpigia, muulize kama mkopaji anamtambua na kweli anastahili kiasi alichokopa? Kama hajaambiwa, rudi kwa mhusika,mwambie hadhaminiki. Mueleze,atafute mdhamini. Na ikiwezekana, wekeni sehemu ya picha na vitambuliaho vya mdhamini.
Kwenye kurejesha,akishindwa, siyo mshuke na matusi. Ongeeni kistaarabu. Mbona hiyo hela kama mtu hana,anakopa na anarejesha?!
Nyie mlikuja wa msaada sana kwa watu,sema tu mnafanya biashara na watu wasiojielewa. Dakika 3 unikopeshe hela,hunijui sikujui,nishindwe kukopa tena? Haiwezekani. Sina ya kurejesha, naenda kwa mtu nakaa nae, namuomba pesa, nalipa, nakopa hapo hapo,hela yake namrudishia; wiki sijapata pesa ya kurejesha?!
Ajirini wanaodai wastaarabu tuuu. Kauli ziwe nzuri tu. Muone kama mtakosa wakopaji.