KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Usiwalipe kama ambavyo umeamua.
Sawa.

Nimependa kauli yako moja kwamba "ni rahisi kuishi kama utaruhusu mambo yaishe".

Nimeipenda hii na nimeichukua ila siwezi kuitumia kwa wapuuzi kama hawa.

Ingekuwa kwamba nikilipa udhalishashaji ungefutika kwa hao watu na heshima yangu kurudi kama mwanzo basi ningeitumia kanuni yako, kuwalipa yaishe.

Ila kwa sababu udhalilishaji walionifanyia hauwezi kufutika kwa watu wangu wa karibu, basi acha tu nisiwalipe
 
Hivi unajua maana ya overdue unayoizungumzia wewe.

Mimi nnachojua overdue ni kupitiliza siku/mda ulitakiwa kulipa.

Leo ni jumatatu natakiwa kulipa leo jumatatu pesa, alafu iweje asubuhi tu uamke uanze kuwatumia sms watu mimi ni tapeli.

Ungesubiri jumanne ifike ndiyo useme nime overdue
Ukisoma hicho ulichoquote mbona nimeaddress kila kitu.

Shida unanijibu kwa presha
 
Ila sisi watz sio wakukopesha bila dhamana, Mimi nadaiwa na karibu makampuni yote ya online yaliyojaribu kunikopesha.
Mbaya zaidi Hela ninabetia na ninapigwa.
Kama sio kubeti nisingefanya huu ujinga wa kuwakopa
Ningekua na ID ningekopa kwingine nihamishe madeni asee,sasa hapa nina license tu ambayo ipo limited kwa makampuni mengine
 
Jiunge na Hypersonic muwashtaki. Nae alipiga porojo tu huku kuwa atawashtaki. Hadi leo chali na kudhalilishwa kadhalilishwa.
 
Duh we jamaa 😂😂😂

Unakijua unachoandika kweli?
Kama kipi mkuu!! Kwani umetembea na mke wa mtu? Hicho kitakushushia hadhi.
Kwani,umemdhulumu yatima au mjane? Hicho, nafsi itakusuta.

Kutowalipa si kwamba hutaki kulipa. Kwani shida zimeisha? Zipo. Ila sasa. Umekopa kwa sababu umekwama. Na huenda kwenye kulipa,umekwama.
1. Kwa nini wasiweke utaratibu hata wa kulipa kidogo kidogo?
2. Kwa nini watukane mteja kama kweli wapo kibiashara?

3. Kwa nini wakudhalilishe? Wakikupigia simu,wakajitambulisha, utashindwa kuongea nao?

4. Kwa nini ukute namba zaidi ya 50, zinakupigia, zinakutumia sms, zote zinakudai. Kampuni ni ipi kati ya hizo?! Wengine wanaenda mbali, wanakwambia utume hiyo pesa kwenye number furani. Kwa nini wasisisitize utumie njia ulotumia kukopa!

Wakiacha matusi yao na sms za kihuni, mbona watapata! Utaratibu mbovu, ndo chanzo cha yote hayo
 
Overdue ni siku siyo saa.

Kama unatakiwa kulipa Ijumaa.

Alhamis utakumbushwa.

Ijumaa utadaiwa. So hata kama ni Ijumaa saa 1 asubuhi tayari ni Ijumaa
Mkuu,

Kweli si kwamba watu wote watakua waaminifu. Lakini,nchi zilizoendelea,kwa nini zimeweza? Mfano,marekani,ukilimbikiza madeni,utajuta kuhudumiwa. Si uzuri wanajua unapata?
Sasa,maisha yetu ya kibongo bongo, wenyewe si mnayajua? Wekeni mambo safi. Kama mtu kaajiliwa,mjue kweli atalipa?
Kwani nyie,kuwapigia wadhamini kabla hamjatoa mkopo mnashindwa? Hii italeta nidhamu. Pigia mtu kistaarabu,mueleze sababu ya kumpigia, muulize kama mkopaji anamtambua na kweli anastahili kiasi alichokopa? Kama hajaambiwa, rudi kwa mhusika,mwambie hadhaminiki. Mueleze,atafute mdhamini. Na ikiwezekana, wekeni sehemu ya picha na vitambuliaho vya mdhamini.

Kwenye kurejesha,akishindwa, siyo mshuke na matusi. Ongeeni kistaarabu. Mbona hiyo hela kama mtu hana,anakopa na anarejesha?!

Nyie mlikuja wa msaada sana kwa watu,sema tu mnafanya biashara na watu wasiojielewa. Dakika 3 unikopeshe hela,hunijui sikujui,nishindwe kukopa tena? Haiwezekani. Sina ya kurejesha, naenda kwa mtu nakaa nae, namuomba pesa, nalipa, nakopa hapo hapo,hela yake namrudishia; wiki sijapata pesa ya kurejesha?!

Ajirini wanaodai wastaarabu tuuu. Kauli ziwe nzuri tu. Muone kama mtakosa wakopaji.
 
Ila sisi watz sio wakukopesha bila dhamana, Mimi nadaiwa na karibu makampuni yote ya online yaliyojaribu kunikopesha.
Mbaya zaidi Hela ninabetia na ninapigwa.
Kama sio kubeti nisingefanya huu ujinga wa kuwakopa
🤣🤣🤣

Wewe hawaja kudhalilisha ?

Nikiona comment kama hizi napata ujasiri sana japo ni comment ya kipuuzi ila kitu flan ndani yake
 
🤣🤣🤣

Wewe hawaja kudhalilisha ?

Nikiona comment kama hizi napata ujasiri sana japo ni comment ya kipuuzi ila kitu flan ndani yake
Huenda wanatuma msg ila sipatak mrejesho.
Sijalipa app nying tu.
Hapa nasubir kesho Kuna kama app 3 waanze kunisumbua wale block then nivute mda nianze kopa Tena.
 
Back
Top Bottom