Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 1,710
- 8,690
Wasaalam wapendwa viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo makundi yote.
Narejea vikao vyetu na viongozi wenu kuhusu ajenda zinazohusu maendeleo ya biashara zenu kuwa: leo Tarehe 22 Julai, 2025 saa 8 mchana kutakuwa na mkutano wa kidigitali (zoom) nchi nzima mikoa yote yaani kati ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, OR TAMISEMI na mikoa yote pamoja na Viongozi wa Wafanyabiashara ndogondogo makundi yote ngazi ya Taifa, Mikoa na Halmashauri.
Lengo la kikao: kupokea taarifa za maendeleo ya uratibu wa usajili wa wafanyabiashara ndogondogo kwenye mfumo wa kidigitali sambamba na usambazaji wa vitambulisho husika vya kidigitali baada ya usajili pamoja na utoaji mikopo ya masharti nafuu ya riba ya 7% kwa mtu mmoja mmoja mwanaume au mwanamke mwenye biashara na kitambulisho cha kidigitali.
Vilevile, kupokea taarifa ya hatua za kuelekea ziara ya ufuatiliaji miradi ya maendeleo ya wafanyabiashara ndogondogo itakayohitimishwa na Kongamano la elimu na tamasha kwa kila mkoa.
Anuani ya kikao kwa Viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo itapatikana kwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga (SHIUMA).
Mwenyekiti wa Kikao nitakuwa mimi Dkt. Gwajima Dorothy, (Mb), Waziri wa Maendeleo ya Jamii.
Ndugu Mfanyabiashara ndogondogo, usikose taarifa za yatokanayo na ushirikiano huu kutoka kwa kiongozi wako pia, endelea kufuatilia taarifa kwenye kurasa za wizara ya maendeleo ya jamii. Usipitwe na fursa na kusikia shuhuda za waliozofikia fursa za mikopo nafuu ya riba ya 7% NMB bila kikundi yaani wewe mwenyewe na biashara yako na kitambulisho chako cha kidigitali, mwanamke au mwanaume.
Kazi na Utu, Tunasonga mbele✍️🇹🇿
Ahsanteni kwa ushirikiano wenu 🙌