TAARIFA: Uzinduzi wa JamiiAfrica pamoja na Mpango Mkakati wake

TAARIFA: Uzinduzi wa JamiiAfrica pamoja na Mpango Mkakati wake

Hongera sana Mkuu Max na kampani yako.

Hii ndo Digital Leadership ambayo itaifanya JamiiForums kuwa na nguvu barani Afrika.

Kwa wanachama wakongwe Kama sie twaona ni mabadiliko ya lazima na yenye tija.
 

Kwa siku za hivi karibuni huenda, kupitia mitandao yetu ya kijamii umeona mwonekano wetu mpya kuanzia kwenye logo mpaka grafiki na ukapata maswali mengi kuhusu nini hasa kinaendelea kwenye taasisi yetu.

Habari njema ni kwamba sasa taasisi yetu imekua zaidi, na ili kuendana na kasi yetu na ya kufikia maeneo mengi zaidi barani jina letu linabadilika kutoka Jamiiforms hadi JamiiAfrica.


Mabadiliko haya yana lengo la kuakisi dhamira yetu ya
kujenga jumuiya jumuishi kidigitali huku tukieneza na kuendeleza Upatikanaji wa Taarifa Bora na za Kuaminika katika maeneo mengi Barani Africa

Uzinduzi huo umefanyika Aprili 24, 2025 ambapo umeenda sambamba na Mpango Mkakati wa Taasisi wa Mwaka 2025-2030 unaoelekeza dira mpya ya taasisi katika kukuza ushirikiano, uwazi na maendeleo endelevu ndani na nje ya Tanzania.


Mabadiliko hayo ya JamiiAfrica yanalenga kupanua wigo wa kusimamia kile ambacho kimekuwa kikisimamiwa na Taasisi ikiwemo kukuza Demokrasia shirikishi ya Kidijitali, ushiriki mpana wa raia katika ajenda za maendeleo pamoja na kushirikiana na Wadau mbalimbali.

Uzinduzi huo umefanyika Aprili 24, 2025 ambapo umeenda sambamba na Mpango Mkakati wa Taasisi wa Mwaka 2025-2030 unaoelekeza dira mpya ya taasisi katika kukuza ushirikiano, uwazi na maendeleo endelevu ndani na nje ya Tanzania.💗💗💗
 
Wakati umefika sasa Kwa wale wanaohusika na kufanya verification za account wawe active.Mfano me nimeomba kuwa verified yapata mwaka sasa cha ajabu hakuna kilichofanyika na Basi kama mtu hujakidhi vigezo ama kuna mapungu ni Bora iwe Rejected ili mtu ujue kuliko kukaa kimya kusububiri inakuwa kama twasibiria pepo bwana.
 
Back
Top Bottom