Taasisi ya Kidini ya Spirit Word Ministry yafutiwa usajili

Taasisi ya Kidini ya Spirit Word Ministry yafutiwa usajili

Jamaa yuko deep vizuri sana kufundisha neno ila ana vitu kadhaa simuungi mkono...
Aliomba msamaha kwa serikali na wananchi kwa maneno kuhusu ushoga etc....kwanini serikali isingempa onyo kuliko kumfungia. Aliomba msamaha.

Jamaaa ana vitu fulani adimu, nilifuatilia mafundisho yao fulani kuhusu fungu la 10 nilimuelewa sana
 
Sijui waumini wake walikuwa wanavumilia vipi kusikiliza maubili yake.
Jamaa ana mafundisho fulani mazuru sana ingawa kwelu kuna baadhi ya mahubiri yake sikubaliani nayo, ukiyoa hilo la Ushoga jamaa yuko vizuri sana
 
View attachment 2639633
Wizara ya Mambo ya Ndani imesitisha usajili wa Jumuiya ya kidini iitwayo Spirit Word Ministry iliyopo eneo la Stakishari Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2023/24.

Masauni amesema katika kudhibiti na kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili Ofisi ya Msajili wa Jumuiya imesitisha shughuli za Jumuiya ya kidini iitwayo Spirit Word Ministry iliyopo eneo la Stakishari Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

“Jumuiya hiyo imefutiwa usajili kwa sababu ya kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na kutoa ujumbe wenye kuhafifisha jitihada za kupambana na vitendo vya ushoga nchini,”amesema.

Aidha, Masauni amesema taarifa zimekusanywa zinazohusu idadi ya vituo vya kulea watoto na shule zinazotoa mafundisho ya dini kwa watoto wadogo.

Amesema lengo ni kutambua idadi ya vituo au shule za bweni zinazotoa mafunzo yenye mwelekeo unaokinzana na maadili ya nchi yetu ikiwemo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, ambapo katika mwaka 2023/24 wizara imepanga kuandaa mwongozo wa taratibu za kuabudu na ithibati ya taasisi zinazotoa elimu ya dini, kuimarisha ufuatiliaji na utendaji wa Jumuiya za Kidini na zisizokuwa za Kidini.

Pia katika mwaka huo watafanya ukaguzi na tathmini ya vihatarishi vya kiusalama kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na kutoa mafunzo kwa Viongozi wa Jumuiya yatakayochangia kudumisha amani na utulivu nchini.
Yule mchungaji alibugi Sana, eti Kama Mimi shoga inakuhusu Nini?. Yani unaongea mambo ya ushoga kanisani. Bora serikali imewafungia maana walikuwa Wana kiburi Sana.
 
Jamaa yuko deep vizuri sana kufundisha neno ila ana vitu kadhaa simuungi mkono...
Aliomba msamaha kwa serikali na wananchi kwa maneno kuhusu ushoga etc....kwanini serikali isingempa onyo kuliko kumfungia. Aliomba msamaha.


Bora wamfungie tu. Sikuyakubali mafundisho yake. Anapinga kila kitu hadi Biblia anaipinga. Bora asalie nyumbani kwake.
 
Yaani kwa ukubwa wa tatizo jinsi ulivyo nchini waziri anasimama kutangaza kusitisha usajiri wa kataasisi hako kamoja tu?
NIlitaraji tangazo lake la kwanza lingeondoka na taasisi na ministry kama 1,000 hivi.
Hapo ndiyo mtaamini hizo taasisi zina mkono wa serikali au zimeanzishwa na serikali yenyewe ili kuzififisha dini kwa kuingiza viongozi na ministry za kitapeli ambapo itafika mahali wananchi wattaona dini ni utapeli tu na kuacha kuzifuata.

Mpango huu ni mbinu ambayo CCP iliwapatia CCM waitumie ili kuua ushawishi wa dini nchini. Mbinu hii haikuishia hapo, wameipeleka mpaka mdani ya Lanisa Katoliki amnapo ili ku discourage waumini wame introduce michango mingi sana isiyo na kichwa wala miguu.
Hata hiyo taasisi iliyofungiwa unaweza kukuta ilikua ni project ya serikali ni vile wameona approach hii imekua too much ndiyo maana wameishia kuifuta tu bila kuwachukulia hatua yoyote na hata ufutaji wake umekuja kwa kuchelewa sana.
Mchawi mkubwa wa nchi hii ni CCM na Serikali yake.

Huyo alifungiwa kwa mengi Sana. Halafu hilo Kanisa lilihamasisha ushoga hadharani sio kwa kificho. Wengine watadakwa tu ndani ya muda.
 
Huyu nabii mwenyewe anaonekana ni shoga
Hasa yule msaidizi wake. Yeye alihubiri live madhabahuni kwamba Kama yeye ni shoga inakuwashia Nini?. Nadhani baada ya happy ndipo kanisa likafungwa.
 
Jamaaa ana vitu fulani adimu, nilifuatilia mafundisho yao fulani kuhusu fungu la 10 nilimuelewa sana
Mwalimu wa uongo, ndio maana serikali imempiga Chini. Wewe unapingaje zaka?. Wakati zaka Ni agizo kwa kila aaminiaye?. Mimi tangu aanze kupinga Biblia nilimuona nabii wa uongo. Uzuri serikali ikamla kichwa.
 
Jamaa ana mafundisho fulani mazuru sana ingawa kwelu kuna baadhi ya mahubiri yake sikubaliani nayo, ukiyoa hilo la Ushoga jamaa yuko vizuri sana
Uzuri kwenye Nini? Kupotosha Biblia. Naishukuru serikali kwa kudeal na wahuni walianza Zumaridi, akaja mzee wa kucha na wakamalizana na mzee wa ushoga. Wasilichafue kanisa.
 
Manabii wanashindwa kujisimamia mpaka serikali imeamua kuingilia Kati. Mara wajiite Mungu, Mara waagize kucha, Mara kuhubiriwa ushoga. Kwa hili naipongeza serikali ishughulike na wahuni wachache wanao lichafua kanisa.
 
Upumbavu, mbona Yesu aliwakumbatia makahaba?

Kanisa ndio mahali pa kurekebisha watu wakiwemo mashoga!

Mnataka kanisa liwafukuze mashoga? Halafu??
Nadhani sio hivyo. Ni baada ya mchungaji kuhubiri kwamba yeye akiwa shoga inakuhusu Nini?. Sasa hilo ni dosari huwezi kutetea dhambi madhabahuni. Ndio maana kwa kugundua hilo kosa waliomba msamaha kwa watanzania.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

we mwehu kweli, jamii yenyewe hii ya machokoraa na mafisadi unataka iharibike mara ngapi?
Usihalalishe ubaya kisa wengine wanafanya ubaya. Itafika sehemu tutashindwa kufanya chochote. Maana muuaji atasema naua kwasababu ufisadi upo nk.
 
Mashoga wanahitaji neno la Mungu ili wabadilike mbona wazinzi wapo wengi na still wanacheka nao tunataka haki sawa kwa wote
Shida kuhamasisha ushoga. Ulimsikia yule mchungaji chumvi alivyosema. Kwamba Yeye akiwa shoga inawahusu nini. Kwa hivyo tuwe na mchungaji analiwa na wanaume kisa machangudoa wapo?. Sio sahihi kabisa, Tena madhabahuni.
 
Tofa
Kabisa, wanataka makanisa yawafukuze mashoga badala ya kuwakaribisha na kuwasaidia?

Mbona hata mafisadi na mafiraji yanaenda kanisani? Kwanini mashoga wasiende kanisani?

Tutumie falsafa ya Yesu ya kuwakumbatia makahaba, hakuwahukumu.

Asiye na dhambi na awe wa kwanza kutupa jiwe. HAKUNA, wote majizi, wauaji na mafisadi, tena wengine ndo wachafu kuliko. MAKAHABA, WAZINZI, wachafu wa kila aina.

Tofautisha toba na kuhamasisha ushoga. Yesu alihamsisha toba kwa wazizinzi sio kuhamasisha uzinzi. Wale Spirit world wanadai Hakuna dhambi, maana yake hawaamini kwenye toba ya dhambi.
 
Tofa
Kabisa, wanataka makanisa yawafukuze mashoga badala ya kuwakaribisha na kuwasaidia?

Mbona hata mafisadi na mafiraji yanaenda kanisani? Kwanini mashoga wasiende kanisani?

Tutumie falsafa ya Yesu ya kuwakumbatia makahaba, hakuwahukumu.

Asiye na dhambi na awe wa kwanza kutupa jiwe. HAKUNA, wote majizi, wauaji na mafisadi, tena wengine ndo wachafu kuliko. MAKAHABA, WAZINZI, wachafu wa kila aina.

Tofautisha toba na kuhamasisha ushoga. Yesu alihamsisha toba kwa wazizinzi sio kuhamasisha uzinzi. Wale Spirit world wanadai Hakuna dhambi, maana yake hawaamini kwenye toba ya dhambi.
 
Biblia ipo mfiraji na mfirwaji wote ni kwenye ziwa la Moto. Anakuja mchungaji anasema ushoga hauna shida. Anapingana na Biblia hiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom