Taasisi yoyote makini haiwezi kujiendesha kidemokrasia

Taasisi yoyote makini haiwezi kujiendesha kidemokrasia

Demokrasia ililetwa ili kuwatishia nyau waliopo madarakani kwamba wasipofuata wakubwa wa Dunia wanavyotaka watawadondosha kutoka kwenye viti vya Enzi !!
Scratch my back I scratch yours otherwise tunakushughulikia !!
Ndiyo maana madikteta vibaraka kama wakina Bongo na Nguesso wanawaacha tu. Wale wazuri kama Gaddaf na Sankara wanadeal nao. Demokrasia ni hila.
 
Udikteka unaweza ukawa na maana ya capitalism ukichukua meaning ya marxist yan hata hy demokrasia yenu ilokuwa na viongoz wachache kwetu ni udikteta...muhm katk nch kuwe na busara ya kiongozi tu,ndy maana hata england malkia bd wanae mpk kesho.
 
Duniani Taasisi yoyote ile iliyo makini haiwezi kukubali kuendeshwa kidemokrasia. Taasisi inayotaka kuwa imara haiwezi kuendeshwa kidemokrasia. Ndiyo maana majeshi hayaendeshwi kidemokrasia. Yanaendeshwa kwa uwezo. Katika nchi nyingi majeshi ndiyo huwa taasisi zenye ufanisi zaidi.

Angalia kanisa Katoliki lilivyo stable na lenye ufanisi. Sababu kubwa ni kutoendeshwa kidemokrasia. Wanaangalia uwezo. Nenda huku KKT, demokrasia imewafanya kuwa taasisi dhaifu, yenye migogoro na ufisafi. Hata kwenye ngazi ya familia. Familia inayotaka kusonga mbele haiwezi endeshwa kidemokrasia.

Hata nchi. Nchi yoyote inayoenda kidemokrasia haiwezi kuwa stable. Haiwezi kuwa na ufanisi. Itakuwa tu kama KKT inakoelekea. Itakuwa tu kama jeshi linaloendehswa kidemokrasia. Nchi zinapoteza muda kuendeshwa kidemokrasia.
Wewe sijui leo umekula makande ya wapi, huu ndo ujinga mlimlisha mwendazake sasa kiko wapi, ukiona viongozi wa nchi flan hawataki demokrasia, lengo kuu ni kufisidi nchi kama ilivyokuwa kwa mwendazake,
 
Watu 341 wametoka mikoa tofaut pmj na appointees et wanawakilisha watu mil 60 sindo ujinga iti kitokachoamuliwa ndo maamuz ye2 wote!!sndo udiktiteta huo
 
England yenyewe Haina democracy...
USA yenyewe Haina democracy
Kwani Democracy ni nini?, yawezekana maana yenyewe ndiyo inatupiga chenga.
Kwangu mimi Democracy ni ile hali ya kutenda yale mliyokubaliana kuyafuata bila kuumiza au kupendelea upande wowote.
 
Kwani Democracy ni nini?, yawezekana maana yenyewe ndiyo inatupiga chenga.
Kwangu mimi Democracy ni ile hali ya kutenda yale mliyokubaliana kuyafuata bila kuumiza au kupendelea upande wowote.

Democracy ni government of the people for the people by the people
 
Democracy ni government of the people for the people by the people
Ndani yake utapata Majority rule minority rights...Sasa ukichanganua maneno hayo katika misingi ya maisha yetu ya kila siku ndipo utakutana na maneno kama HAKI, USAWA ndani ya Democracy hivyo itabidi sasa tuifafanue katika maisha yetu.

Haki ni hali ya kutomtendea mtu mwingine kile usichopenda wewe kutendewa, hapo ndipo utakuwa umetenda haki.

Usawa ni hali ya wote kupata haki bila kuegemea upande wowote katika mazingira mnamoishi.
Kwangu mimi natafsiri Democracy kama hali ya kutenda yale mliokubaliana kuyatekeleza katika msingi wa kujiletea maendeleo bila kuegemea upande wowote. Iwapo kuna kitu kinawakwaza basi itabidi mkubaliane kuijadili na kupata muafaka wa kuifuta au kutoifuta ...hapo ndipo maneno ya majority rule minority rights.

Swali ni je, majority rule minority rights tunaizingatia?
Kama democracy haiwezi kutuletea maendeleo ni namna gani uamuzi wa Kiimla ya mtu mmoja itapimwa kuwa ilikuwa ndiyo njia sahihi? Wakati mapendekezo ya watu wengine hayapewi nafasi ya kusikilizwa.
 
Wewe jamaa Una umri gani?
Mada inajadili democracy
Ghafla ishageuka Tanzania na machafuko na discipline...
Kwani mleta mada amesema democracy ifutwe Tz?
Au ushakimbilia conclusion yako na hofu zako na assumptions zako?
Unaongea kuhusu discipline wakati hata discipline ya Ku stick na main point huna?
Unaogopa nini ndugu unazungumzia umri wangu, unataka kunipa mke?

Unafaham kitu kinaitwa context au unaruka ruka tu hapa.
 
Ndani yake utapata Majority rule minority rights...Sasa ukichanganua maneno hayo katika misingi ya maisha yetu ya kila siku ndipo utakutana na maneno kama HAKI, USAWA ndani ya Democracy hivyo itabidi sasa tuifafanue katika maisha yetu.

Haki ni hali ya kutomtendea mtu mwingine kile usichopenda wewe kutendewa, hapo ndipo utakuwa umetenda haki.

Usawa ni hali ya wote kupata haki bila kuegemea upande wowote katika mazingira mnamoishi.
Kwangu mimi natafsiri Democracy kama hali ya kutenda yale mliokubaliana kuyatekeleza katika msingi wa kujiletea maendeleo bila kuegemea upande wowote. Iwapo kuna kitu kinawakwaza basi itabidi mkubaliane kuijadili na kupata muafaka wa kuifuta au kutoifuta ...hapo ndipo maneno ya majority rule minority rights.

Swali ni je, majority rule minority rights tunaizingatia?
Kama democracy haiwezi kutuletea maendeleo ni namna gani uamuzi wa Kiimla ya mtu mmoja itapimwa kuwa ilikuwa ndiyo njia sahihi? Wakati mapendekezo ya watu wengine hayapewi nafasi ya kusikilizwa.
Geuza kinyume chake ndiyo usahihi wake.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Demokrasia ya vitabuni na ukomunisti wa vitabuni havina tofauti ni vitu vya kufikirika tu inshort haviwezekani kutekelezwa kutokana na uasilia wa watu.
 
Mfano kidogo, watu 20 wanachagua kiongozi wao kidemokrasia. 5 ni wasomi wazuri ila 15 wanajua tu kuandika na kusoma. Katika uchaguzi watamchagua mtu anaejua tu kusoma na kuandika. Hiyo jamii ya watu 20 itakuwa na maendeleo? Hapo ni mwendo wa akili kubwa kuongozwa na akili ndogo. Democratic ipigwe chini. Hilo kundi la watu 20 udikteta ungetumika "huyu ndiye kiongozi wenu"

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Utawala unapaswa kuzingatia geographic location, cultural, nature na mambo wa kadha wa kadha mtu wa magharibi hawezi kuwa sawa na mtu wa mashariki, mtu wa kaskazini hawezi kuwa sawa na mtu wa kusini.

Mchina hawezi kuwa sawa na mzungu, mzungu hawezi kuwa sawa na mwafrika, mwarabu hawezi kuwa sawa na mlatino.

Waarabu mfumo wa kifalme una nafasi kubwa sana ya kuenda vyema tofauti na mfumo mwengine kuna vitu waarabu vinawakataa na kuna vitu waafrika vinawakataa, kuna vitu wachina, wakorea, wajapan vinawakataa na kuna vitu wazungu vinawakataa
 
Back
Top Bottom