Taasisi yoyote makini haiwezi kujiendesha kidemokrasia

Ndiyo maana madikteta vibaraka kama wakina Bongo na Nguesso wanawaacha tu. Wale wazuri kama Gaddaf na Sankara wanadeal nao. Demokrasia ni hila.

Ha ha ha. Ila nchi za western mungu anawaona aisee. Yaani ukiwa dikteta unayekula na western utaonekana ni mwanademokrasia mzuri, lakini ukiwa dikteta ambaye uko against na sera za western unaundiwa zengwe.
 
Ila concept ya wengi wape kwenye mfumo wa demokrasia huwa ina mushkeli sana. Yaani wengi tuwape tu hata kama mawazo yao ni ya kijinga.
 
Wewe sijui leo umekula makande ya wapi, huu ndo ujinga mlimlisha mwendazake sasa kiko wapi, ukiona viongozi wa nchi flan hawataki demokrasia, lengo kuu ni kufisidi nchi kama ilivyokuwa kwa mwendazake,
Labda haufahamu, ila kwenye demokrasia ufisadi huwa mkubwa kuliko hata kwenye udikteta.
 
Kwani Democracy ni nini?, yawezekana maana yenyewe ndiyo inatupiga chenga.
Kwangu mimi Democracy ni ile hali ya kutenda yale mliyokubaliana kuyafuata bila kuumiza au kupendelea upande wowote.
Hiyo siyo demokrasia. Ulichoelezea kinaitwa uaminifušŸ™‚
 
Demokrasia haiguarantee minority rights. Ndiyo maana Marekani ilijiita nchi ya kidemokrasia lakini minority bado walikuwa hawana haki kama raia wngine. Demokrasia ni kama udikteta wa walio wengi. Yaani badala ya kuwa na dikteta mmoja mnakuwa nao wengi.
 
Wagiriki wa kale waliiponda demokrasia kwa namna hii hii. Walisema kuwa mkiwa melini mtachagua nahodha kidemokrasia au kwa kuangalia uwezo wake?
 
🤣demokrasia ipo, ila ipo sirini,

kwa mfano walipokua wanamchagua Papa wao baada ya John Paul wa pili kuaga Dunia, alichaguliwa mtu alafu walipochoma kura zake ukafuka Moshi mweusi ishara kua hafai na mpaka leo huyo askofu hajulikani ni nani na wawapi, wakarudia kura ndipo akapatikana papa Francisco baada ya Moshi mweupe kufuka baada ya kura zake kuchomwa.

Pia mtu anapoteuliwa Askofu au paroko, mwingine hawezi fahamu kwanini huyu na si yeye.

Matokeo yake hayupo wa kulaumiwa kwa aidha upendeleo, udanganyofu au wizi wa kura.
na hapo ndipo panatofautisha hilo dhehebu na madhehebu au taasisi nyingine.

so uwezo ni moja lakini usiri ni muhimu Zaidi.
 
Una hoja. Ila umeandika kwa hasira
 
Uchaguzi ni sehemu tu ndogo ya demokrasia. Jinsi taasisi inavyojiendesha has ndipo demokrasia ilipo. Je, kiongozi na watu, na vikundi vingine wana nguvu kiasi gani kwenye maamuzi. Pia kwenye demokrasia kila mkatoliki angekuwa na sifa za kugombea upapa.
 
Hakuna demokrasia RC, RC ni moja ya taasisi inayo ongozwa kidikteta kupita maelezo hata waamini wake wanafahamu hilo.

Yule sijui mchungaji kimaro wa KKKT angekuwa shemasi,frateri au father wa RC angefukuzwa mara moja au kuhamishwa mbali kabisa na hakuna muumini hata moja angeinua mdomo wake kama walivyo fanya waumini wa KKKT
 
yaani muumini awe na power juu ya mpakwa mafuta?
 
Demokrasia ya RC, waamini wanachaguana wao kwa wao kwenye uongozi wao huko Jumuiya na makasisi wanapangwa na Maaskofu wa majimbo na Papa anachaguliwa na makadinali na hakuna kampeni.

Kampeni huzalisha makundi na ndipo vita hutokea kwenye makanisa kwasabb ya faulo, upendeleo na wizi wa kura.

Hiarakia inaheshimiwa na kuzingatiwa mno na wakatoliki.
Umewahi soma RC seminary ?
hapana
 
Demokrasia ya vitabuni inahimiza Transparency hakuna demokrasia kwenye usiri wa kimaamuzi.

Hakuna demokrasia ambapo hakuna uwanja sawa.

Udikteta wa kiuchaguzi, kiuongozi na kimaamuzi umetawala RC.

Uongozi wa juu wa kanisa ukiamuru utekelezaji wa adhimio fulani inabaki waamini kutekeleza pasipo pingamizi.

Maamuzi ya RC yana amriwa na kikundi kidogo kwenda kwa wengi pasipo kujali mitazamo hasa ya kundi zima.

Nakupa hii : Sio waamini wote wa RC wana kubaliana na utaratibu wa jumuhiya na michango kutumika kama fimbo kwa mfu lakini hawana nguvu ya kidemokrasia kuzuia maamuzi ya kanisa.
 
nakubaliana na wew pakubwa.

Hawa jamaa ni vichwa mno walijua tangu mapema kuwa wakiwa na chaguzi kama zilivyo kwenye makanisa mengine, na taasisi za kiraia kama serikali kungekuapo na manung'uniko mengi na pengine mgawanyiko mkubwa mno nyakati za uchaguzi lakini pia pangekua na gharama kubwa na Rushwa, wizi na upendeleo kama ilivyo KKKT ambao wanafanya uchaguzi kama wa serikali tu.

Kuwa na alieshinda na alieshindwa tayari ni kitu ambacho RC wamekiepuka mapema sana.

Asant sana kwa Elimu tupo pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…