Kila mtu ashinde mechi zake...
Ganja nilishaacha,
Kununua malaya nilishaacha,
Bolibo/Dubwi la mchina nilishaacha,
Makato/Nje ndani(Kamari ya karata) nilishaacha,
Kubeti sibeti
Kinachonisumbua kwa sasa:
Ulevi-Konyagi, bia, K-vant japo sio kila siku, kupiga kiberiti hata hela ya malengo hii imetokea mara nyingi sana.
Umalaya- Kutongoza mademu wengiwengi, wengine napiga(hela lazima kama muwajuavyo wanawake), wengine wananipuna vihela vya vocha tu na bila hata kuwagonga.
Fegi(Sigara)- Hapa nasumbuka pia, inaweza kuwa usiku nikishavuta fegi, naapa nasema kesho sivuti kabisa, ajabu yake ikifika asubuhi najikuta niko dukani nanunua Embassy nasema navuta hii tu, kutwa nzima ni fegi mpaka usiku tena
Mtoa mada shinda mechi zako, nishinde zangu