Tabia hizi za Wachagga za kujenga nyumbani zinapaswa kuigwa na Makabila yote

Tabia hizi za Wachagga za kujenga nyumbani zinapaswa kuigwa na Makabila yote

Ungeandika tabia hii na siyo tabia hizi... Usifanye Kiswahili kuwa kigumu.
Wakuu, Kati ya kitu ambacho makabila mengine yanapaswa kuiga kwa wachagga ni hii tabia ya kujenga nyumbani (kwenye asili yako).

Hii picha nimeipiga Huko Moshi Vijijini, ndanindani sana huko kijiji cha Kirua.

Hii tabia ndio inayowahamasisha kurudi makwao mwisho wa Mwaka, kwasababu wanajua wanamaeneo mazuri yakufikia.
Tabia nzuri na ya kuigwa.

View attachment 1838693
 
Sawa wachagga kwetu tunajenga ila tuna sifa za kihaya mwisho wa mwaka au utokee msiba.
 
Sababu inayofanya mikoa mingine watu wasijenge nyumba vijijini ni Uchawi na Ushirikina.

Kwa jamii za wachaga vijijini ni fahari kuona mtoto wa mwenzie amejenga, amenunua gari amefaulu mtihani n.k

Lakini kwenye vijiji vya mikoa mingine thubutuuuu.

Ndiyo maana maendeleo maeneo yoyote yenye uchawi hakuna sababu akijitokeza mtu au watu kufanya jambo la maendeleo wanamuua au kumrudisha nyuma .!
 
Iwapo tutaamua kuacha uchawi na ushirikina na uvivu na kufurahia mafanikio ya mtoto wa mwenzio badi ndipo tutaanza kwenda mbele kimaendeleo.
 
Wachaga wanapiga kazi jamani hata Mama wa nyumbani ni kazi hakuna kulala.

Yani wao kuamka wa kwanza kuchelewa kulala ni jambo la kawaida sana kwao.

Siyo unaenda mikoa mingine unaenda kwenye mgahawa umefungwa watu wamelala!

Utazalisha saa ngapi uchumi ukue wa mtu binafsi na jamii hatimae Taifa??
 
Sababu inayofanya mikoa mingine watu wasijenge nyumba vijijini ni Uchawi na Ushirikina.

Kwa jamii za wachaga vijijini ni fahari kuona mtoto wa mwenzie amejenga, amenunua gari amefaulu mtihani n.k

Lakini kwenye vijiji vya mikoa mingine thubutuuuu.

Ndiyo maana maendeleo maeneo yoyote yenye uchawi hakuna sababu akijitokeza mtu au watu kufanya jambo la maendeleo wanamuua au kumrudisha nyuma .!
Makafala ya damu ya mbuzi na matambiko yametamalaki uchagani
 
Kuna mitazamo tofauti.
Kujenga kijijini inaweza kuwa misallocation of resources.
Unawekeza investment kubwa ambayo ungeweka mjini ungeweza kupata fedha nyingi. Mtu ameweka ghorofa kijijini, ni kujionyesha au ndio nyumbani.
 
Ndiyo maana huwa nawaambia watu msiwachukie na kuwa husuda hao watu badala yake tuwapende tujiweke karibu yao tujifunze kutoka kwao kisha tufanye yenye kufaa tuendelee.

Tubadilishe mindsets zetu tuache kujihurumia na uvivu .

Tuache kuzani umaskini ni mapenzi ya Mungu wakati vitabu vitakatifu vyote vinahimiza watu kufanya kazi na asiye Fanya kazi asile.

Yani Mungu amekuwa mkali na serious kuwa asiye Fanya kazi na asile ili kama ni kufa na afe potelelea mbali.
 
Makafala ya damu ya mbuzi na matambiko yametamalaki uchagani

Labda.

Lakini tujiulize Je kama wanafanya hivyo ni for their sake au ni kwaajili ya kumdhuru mtoto wa jirani asifanikiwe au afe?

Hayo hata jamii nyingine matharani Wahindi , Chinese wanaweza kuwa nayo lakini ni kwa wao wenyewe kuamini yanawapa nguvu lakini siyo kuwaharibia wengine.

Kama kwa kufanya hivyo hawamdhuru mtoto wa jirani wala kuzuia maendeleo yake kunakuwa na shida gani?

Hiyo itakuwa ni swala lake na Mungu wake kama ni dhambi.

Tatizo ni pale kwenye jamii ambapo wakisikia mtoto wa jirani amefaulu Shule wanamroga asiende mbele au hata kumuua kwa msukule au kumtia kichaa.

Wakisikia mtu anajenga au amenunua gari wanamtafuta kumdhuru!
 
Back
Top Bottom