Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Ulitumia mbinu gani mpaka watu wakaacha kukuazima gari?
Sikutumia mbinu yoyote... mmoja alichukua gari akalipiga mzinga mtakatifu. Ela ya kulipa hana nikaliuza kama skrepa. Nikanunua gari lingine. Mimi huwa siazimi gari la mtu hivyo na mimi simpi mtu gari. Yani usitoke huko eti niazime gari unless nione una shida nikupe mwenyewe napo ni nadra sana.
Anza kuwa kauzu baadaye wakishakuelewa haitakusumbua. Watu ambao huwa wako straight watu huwa hawawachukii wanakuwa washajua msimamo wao.
 
Inawezekana pia hili jambo linategemea watu waliokuzunguuka. Wengine ni utamaduni wao kutoa lifti bila kuombwa. Miaka ya nyuma nilihamia kinyerezi kwenye nyumba ya ndugu yangu aliyekuwa haishi hapo. Huo mtaa nilizungukwa na majirani wenye magari na maisha mashallah, hapo ndio nimeanza kazi. Yaani asubuhi nilikuwa napewa lifti hadi nikawa najishtukia. Ikafika mahali najichelewesha kutoka nyumbani ili wenye magani wawe wameondoka, kumbe kuna mwingine naye siku hiyo amechelewa kutoka. Niliteseka hadi nikanunu la kwangu.
 
Halafu ukiwanyima wanaogeleshana wenyewe eti mungu atakulipa 😀
 
Haya ndio matatizo ya kushindwa kusema hapana/sitaki. Jifunze hiyo misamiati migumu na usiogope lawama. Fanya kile unachofurahia kukifanya hata kama kinakwaza wengine ila mradi ni halali na ni haki yako.
 
Ukiwa huna gari na una shida ya usafiri mtu akikunyima lifti unamuona ana roho mbaya sana.Ila cku ukimiliki gari utamsamehe maana utaelewa kwann alikuwa anakutosa watu wana mishe nyingi hapa mjini we unawaza kwenda hm tu.
 
next time toboa matairi mawili yapaye pancha then waambie wayafungue wakazibe pancha
 
Sawa kaka
 
Walau ulijishtukia au kuwa na aibu na sio Kila anayekupa lift amependa wengine ni huruma,wengine wanaogopa lawama,wengine wachawi.
Mimi naweza kumpa mtu lift anayeishi mtaani kwangu ila sio mtu wa kazini kwangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…