Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Nilipokuwa nafanya kazi kuna kamadam kana ki ist chake yani wale walimu bila haya midume mizima inafuatilia ratiba ya madam anatoka saa ngapi au anamaliza vipindi saa ngapi ili wapate lift na ni kila siku

Utakuta mtu kama ana kipindi muda ambao madam anaondoka atamuomba mwalimu mwenzie amfundishie atakuja kufundisha kipindi mbadala cha kesho aisee kwangu nilikuwa naona ajabu
Kweli binadamu tuko tofauti yaani Kuna watu kwao aibu hakuna kabisa
 
Vijana wengi walionunua magari lengo lao kuu ni kubeba mademu tu hamma la maana .
Sio kweli mkuu, lengo la kununua gari ni kuondoa adha ya usafiri.
Pia kukupa uhuru wa mambo yako
 
Punguza wema mkuu,binadamu wenyewe hawana hata kumbukumbu hawa.

Aliyekuazima gari siku akila mzinga huko utajiona mjinga sana!

Gari aazimishwe/apewe mwenye gari tu,hawa wasiokuwa hata na uzoefu barabarani ni kutafuta lawama.
Na ukimlipisha atakuona una roho mbaya
 
Wapunguze kisaikolojia liache gari nenda kwenye issue zako ukirudi hutokuta mtu. Mtu akikuomba gari kwenda chukua chakula mwambie gari ina shida kwenye eng unaendesha kwa machale aka mashariti ya teach wako... Baadae siku unaliacha au unatoa upepo yaani...
Hii nayo mbinu nzuri naichukua
 
Hizo ndio sifa za umasikini huna gari unaenda omba gari ya jirani unaitumia huweki mafuta wala safisha nawakati mwingine unaibonda only in Africa kuna mshikaji aliuwa gari na akauza kwa ujinga huu
Kuna Mmoja nilimpa karudi nayo imechubuka rangi mbele akaniambia dereva guta aliikwangua.
Nkaenda kupiga rangi kwa gharama zangu.
Kuna huyu mwingine anaondoka na gari gia kaweka namba Moja halafu anakanyaga mafuta mpaka mwisho Hadi gari inalalamika. Yaani uendeshaji wake hata simuelewielewi, watakuja kuniulia gari hawa
 
Hii tabia alikuwa nayo Babu yangu mmoja mkienda msikitini mkimaliza kuswali anakuja na nyie kwa Miguu anaiacha Gari na akiacha Gari mkiwa njiani anasema amesahau Gari anarudi kuichukua Ila lengo alikuwa hataki mtu apande hilo Gari.

Ni mwaka juzi lile Gari watoto wake wameshalipima .na Babu is no longer alive

So keep spread positive Energy nothing last.
 
Huo ndio ukweli wenyewe.. kuna watu wanajisahau sana kwa kuona ubest wa kazini ni wa maisha... nilikua nikisikia wakubwa wakisema kazini hakuna rafiki bali wanafiki... fanya kazi kwa bidii get paid and go home.

Kuna yale mazoea ya after kazi ndio hufanya wengi washindwe kutoboa mishe zao baada ya kazi.
Yaani urafiki wa kazini uishie kazini.
Watu tunahitaji kuwa na maisha mengine huku nje.
Hii wafanyakazi wengi Huwa inatupa ugumu.
Unakuta marafiki ni walewale wa kazini mnashindwa hata kujadili vitu vipya, mnashindwa mnaongelea mambo yaleyale
 
Let's assume ana roho mbaya, ushirikiane na nani na mali hujachangia hata shilingi kutafuta

Kwanini upewe lift ? wakati unatoka kwako ulikua umepanga utafikaje huko unakotaka kwenda ?

Anyway kwani wewe ukitembea Kwa miguu au ukioanda daladala unapungukiwa Nini ?
Mfumo wa ujamaa umewaharibi sana watu, wanageuza msaada kuwa haki,
Inabidi utambue Mali ya mtu mwingine huna haki nayo.
Lazima mtu ujifunze kujitegemea sio kusubiri hisani
 
Habari,
Hivi Watanzania huu mtindo wa kuomba lift kwenye gari za watu muda wote mmeutoa wapi?
Walau mtu awe jirani yako umemkuta mbali huko kidogo ina make sense.

Sasa ndugu zangu mtu kazini wanakuvizia kwenye parking inakera sana aisee.

Tena zaidi mtu unamuuliza unaenda wapi badala akujibu na yeye anakuuliza kwani we unaelekea wapi utanishushia hukohuko!

Mtu unashindwa hata kupitia kwa kimchepuko chako kisa hawa watu.
Halafu huwezi jua mtu ana michongo yake gani anataka aifanye ila hapendi watu wa kazini wajue.

Pia tambueni gari mkipanda watu wengi hata ulaji wa mafuta unaongezeka tofauti na akiwa mtu mmoja au wawili.

Tabia ya nyingine ni kuazima gari yaani pale ofisini inafika mchana, mtu anakwambia niazime gari nikafuate chakula hotelini, daah! Yaani unampa mtu kupunguza lawama ila hii tabia inakera maana wengine Wana uendeshaji mbaya kama mi gari yangu ni manual Sasa wengine hawawezi hata kuziendesha vizuri ila wanaforce pia mafuta wakitumia hawa watu Huwa hawachangii hata tone.

Kwanini mtu kama hujataka kununua gari basi kwenye michongo yako bolt au kapande daladala usiwe kero kwenye Mali za watu wengine
Sijui nidhibiti vipi hizi tabia
Gari la kwanza ni sadaka ukija kununua la pili usiwakubalie.
 
Wapakie na waeleze kuhusu ratiba zako, hata kama kuna mahali unakwenda, nenda huko na park gari yako, washuke wakusubiri.
Kuhusu kuazima gari, wanyime.
Usiwe muoga kwenye kitu chako, unless nawe uwe uliishi maisha hayo kabla haujapata gari.
Mimi sikuwahi kuazima gari la mtu Wala kuomba lift.
Kwanza Huwa Sina mazoea sana na watu hapa kazini,zaidi ya wachache ambao utendaji wetu wa kazi unaingiliana.
Hawa wanaoniomba lift sikuwahi kuzoeana nao,wameanza mazoea baada ya kununua hii gari.
Kuna mwingine wiki iliyopita kaniazima gari limerudi mafuta yote kanitumia akaanza kujiongelesha kuwa posho za vikao zikitoka atanipoza.
Posho za vikao zimetoka kakaa kimya tu nami sijamkumbusha.
Ijumaa kanifata eti nimpe gari aende supermarket nikamwambia kuwa Nina ratiba ya kutoka muda sio mrefu
 
Yaani ulichozungumza ni kweli kero sana ni kama kumfatilia mtu ratiba zake na kumjua zaidi. Hasa hilo la kuwauliza unakwenda wapi naye anakugeuzia wewe kwani unaenda wapi ntashuka huko huko. Hapo ukute pengine ulishapanga na staff wa kike ili uzungumze naye na kakubali ndiyo unakuta watu wanakusubiri.

Kingine unaamua kumpa mtu lifti kero nazochukia zaidi

1: Anazungumza na simu mwanzo wa safari hadi mwisho tena kwa sauti hata unashindwa sikiliza redio

2: Unapigiwa simu nyumbani ya maongezi privacy unaishia jibu tu ndiyo au ntakupigia baadaye.

3: Mara mwingine unasikia mimi AC huwa inaniumiza naumwa .

4: Mwingine unasikiliza pengine TBC Fm yeye anataka msikilize Wasafi.

Unaingia petro station ndiyo kwanza mwenzio anachart hata kujibalaguza basi na buku ten walau ongeza wese anakauka.
Hiyo ya pili inanikuta sana hiyo.
 
Mtu akikukuta unakula chakula no ukamkaribisha. Huwa unamuuliza kwanza hayo maswali? Au huko kwenu hata chakula na majirani hamkaribishani?
Mtaani kwako mtu akipata shida ya ghafla usiku na hana gari wala pesa utaweza kumsaida kweli wewe?
hyo ni shida muhimu dharura lazma kusaidia.
Ila lift kuomba ni aibu yan kila siku umekaza mshipa lift
 
Back
Top Bottom