Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Wewe utakuwa na roho mbaya mkuu. Huku Afrika siyo ulaya huwa tunashirikiana.
Mfano unatoka posta unaenda mbweni ukimpa lift mtu ukamuacha mwenge unapungukiwa nini hapo?
Let's assume ana roho mbaya, ushirikiane na nani na mali hujachangia hata shilingi kutafuta

Kwanini upewe lift ? wakati unatoka kwako ulikua umepanga utafikaje huko unakotaka kwenda ?

Anyway kwani wewe ukitembea Kwa miguu au ukioanda daladala unapungukiwa Nini ?
 
Vaa uso wa mbuzi, mtu hana gari huo ujasiri wa kuazima gari anautoa wapi? Mimi gari yangu hakuna mtu mwingine anayeendesha zaidi yangu.
Yaani najilaumu kwanini hii tabia niliwazoesha mwanzoni mpaka wengine wanaambiana kaazime kwa mtu Fulani.
Kuna siku mtu kachukua gari kasema anaenda kula chakula muda wa kazi ulipoisha nilimsubiri zaidi ya dakika 40 hajatokea anarudi gari mafuta Haina Wala hajasema chochote
 
Gari sio kitu cha kuazimana bila dharura maalum, mgonjwa, msiba n.k.
Mtu anakuazima eti aende kula hotelini.
Wanachonikera watu wanaoazima ni vitu vitatu
1: Kujizoesha na kugeuza kuwa ni utaratibu
2: Uendeshaji mbaya
3:mtu anachukua gari mda wa kutoka kazini naanza kusubiri Tena
 
Habari,
Hivi Watanzania huu mtindo wa kuomba lift kwenye gari za watu muda wote mmeutoa wapi?
Walau mtu awe jirani yako umemkuta mbali huko kidogo ina make sense.

Sasa ndugu zangu mtu kazini wanakuvizia kwenye parking inakera sana aisee.

Tena zaidi mtu unamuuliza unaenda wapi badala akujibu na yeye anakuuliza kwani we unaelekea wapi utanishushia hukohuko!

Mtu unashindwa hata kupitia kwa kimchepuko chako kisa hawa watu.
Halafu huwezi jua mtu ana michongo yake gani anataka aifanye ila hapendi watu wa kazini wajue.

Pia tambueni gari mkipanda watu wengi hata ulaji wa mafuta unaongezeka tofauti na akiwa mtu mmoja au wawili.

Tabia ya nyingine ni kuazima gari yaani pale ofisini inafika mchana, mtu anakwambia niazime gari nikafuate chakula hotelini, daah! Yaani unampa mtu kupunguza lawama ila hii tabia inakera maana wengine Wana uendeshaji mbaya kama mi gari yangu ni manual Sasa wengine hawawezi hata kuziendesha vizuri ila wanaforce pia mafuta wakitumia hawa watu Huwa hawachangii hata tone.

Kwanini mtu kama hujataka kununua gari basi kwenye michongo yako bolt au kapande daladala usiwe kero kwenye Mali za watu wengine
Sijui nidhibiti vipi hizi tabia
Ubinadamu kazi
 
Gari mtu ananunua kwa matumizi binafsi,watu Wanahitaji privacy, 🔏.
Kwanini tunalazimisha ujamaa kwenye Mali za watu.
Kulazimisha msaada iwe haki huo ndio umaskini
Hilo sio tatizo la waomba lift, ni lako. Ulipaswa kuonesha hupendi mazoea kabla hawajakuzoea.
 
Inakatiwa kwa mtu au gari. Cjaelewa uliposema ulimkatia insurance
Unapokata insurance ni wewe unaeendesha
Insurance ya gari ila wewe ndio dereva
Yeye hana insurance ya kuendesha gari langu kwa hiyo namuwekea aendeshe gari langu kwa mda huo

Na likitokea la kutokea anakuwa ana kinga ya Insurance kwa hiyo mimi nitalipwa au kutengenezewa gari langu

Huko insurance inakuwaje swali kwako
Maana huwezi kuendesha gari lolote ili mradi eti lina insurance hapana, lazima na wewe uwe insured, unless uwe na fully comprehensive ndio unaweza kuendesha gari lolote.
Umenielewa hapo?
 
Habari,
Hivi Watanzania huu mtindo wa kuomba lift kwenye gari za watu muda wote mmeutoa wapi?
Walau mtu awe jirani yako umemkuta mbali huko kidogo ina make sense.

Sasa ndugu zangu mtu kazini wanakuvizia kwenye parking inakera sana aisee.

Tena zaidi mtu unamuuliza unaenda wapi badala akujibu na yeye anakuuliza kwani we unaelekea wapi utanishushia hukohuko!

Mtu unashindwa hata kupitia kwa kimchepuko chako kisa hawa watu.
Halafu huwezi jua mtu ana michongo yake gani anataka aifanye ila hapendi watu wa kazini wajue.

Pia tambueni gari mkipanda watu wengi hata ulaji wa mafuta unaongezeka tofauti na akiwa mtu mmoja au wawili.

Tabia ya nyingine ni kuazima gari yaani pale ofisini inafika mchana, mtu anakwambia niazime gari nikafuate chakula hotelini, daah! Yaani unampa mtu kupunguza lawama ila hii tabia inakera maana wengine Wana uendeshaji mbaya kama mi gari yangu ni manual Sasa wengine hawawezi hata kuziendesha vizuri ila wanaforce pia mafuta wakitumia hawa watu Huwa hawachangii hata tone.

Kwanini mtu kama hujataka kununua gari basi kwenye michongo yako bolt au kapande daladala usiwe kero kwenye Mali za watu wengine
Sijui nidhibiti vipi hizi tabia
Yaani ulichozungumza ni kweli kero sana ni kama kumfatilia mtu ratiba zake na kumjua zaidi. Hasa hilo la kuwauliza unakwenda wapi naye anakugeuzia wewe kwani unaenda wapi ntashuka huko huko. Hapo ukute pengine ulishapanga na staff wa kike ili uzungumze naye na kakubali ndiyo unakuta watu wanakusubiri.

Kingine unaamua kumpa mtu lifti kero nazochukia zaidi

1: Anazungumza na simu mwanzo wa safari hadi mwisho tena kwa sauti hata unashindwa sikiliza redio

2: Unapigiwa simu nyumbani ya maongezi privacy unaishia jibu tu ndiyo au ntakupigia baadaye.

3: Mara mwingine unasikia mimi AC huwa inaniumiza naumwa .

4: Mwingine unasikiliza pengine TBC Fm yeye anataka msikilize Wasafi.

Unaingia petro station ndiyo kwanza mwenzio anachart hata kujibalaguza basi na buku ten walau ongeza wese anakauka.
 
Habari,
Hivi Watanzania huu mtindo wa kuomba lift kwenye gari za watu muda wote mmeutoa wapi?
Walau mtu awe jirani yako umemkuta mbali huko kidogo ina make sense.

Sasa ndugu zangu mtu kazini wanakuvizia kwenye parking inakera sana aisee.

Tena zaidi mtu unamuuliza unaenda wapi badala akujibu na yeye anakuuliza kwani we unaelekea wapi utanishushia hukohuko!

Mtu unashindwa hata kupitia kwa kimchepuko chako kisa hawa watu.
Halafu huwezi jua mtu ana michongo yake gani anataka aifanye ila hapendi watu wa kazini wajue.

Pia tambueni gari mkipanda watu wengi hata ulaji wa mafuta unaongezeka tofauti na akiwa mtu mmoja au wawili.

Tabia ya nyingine ni kuazima gari yaani pale ofisini inafika mchana, mtu anakwambia niazime gari nikafuate chakula hotelini, daah! Yaani unampa mtu kupunguza lawama ila hii tabia inakera maana wengine Wana uendeshaji mbaya kama mi gari yangu ni manual Sasa wengine hawawezi hata kuziendesha vizuri ila wanaforce pia mafuta wakitumia hawa watu Huwa hawachangii hata tone.

Kwanini mtu kama hujataka kununua gari basi kwenye michongo yako bolt au kapande daladala usiwe kero kwenye Mali za watu wengine
Sijui nidhibiti vipi hizi tabia
Ukweli mchungu....ngoja waomba lift waje kwanza.
 
Back
Top Bottom