Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Uzoefu unaonyesha kwamba wapewa lift wengi sio wachangiaji wa mafuta, hata ukipita kituo cha mafuta huwa hawajigusi. Ndio maana watoa lift wanapata makasiriko.
Kingine ni kumnyima mwenye gari uhuru
 
Kumwambia mtu kuwa sipiti uelekeo wako n kitu simple tuu ili kumkwepa usimpe lift kuliko kumpa lift na kuwa kwenye makasiriko.

Nilishawah kuomba lift, nikataja uelekeo wangu nikajibiwa anaenda uelekeo tofauti na mm, nikakutana nae kwenye foleni Mm nikiwa kwenye daladala.

Mbona simple tuu na roho yangu ikabaki na amani tele.
Gari mtu ananunua kwa matumizi binafsi,watu Wanahitaji privacy, 🔏.
Kwanini tunalazimisha ujamaa kwenye Mali za watu.
Kulazimisha msaada iwe haki huo ndio umaskini
 
Mtu akikukuta unakula chakula no ukamkaribisha. Huwa unamuuliza kwanza hayo maswali? Au huko kwenu hata chakula na majirani hamkaribishani?
Mtaani kwako mtu akipata shida ya ghafla usiku na hana gari wala pesa utaweza kumsaida kweli wewe?
Umeshasema shida ya ghafla tofautisha emergency na mipango.
Mtu unapoamka asubuhi kwenda kazini lazima ujue pia utarudi vipi sio kusumbua watu.
 
Hizo tabia za kijamaa za kuombaomba mnaendekeza sana.

Na ukiendekeza ipo siku utambeba mtu akafia kwenye gari na humjui hata jina lake

Ila na wewe una tatizo kubwa
Eti unampa gari mtu kwa kumuheshimu
Seriously?
Yeye kashindwa kuwa na Soni wala aibu kwa kukuomba gari lako, sasa wewe unamhurumiaje Ombaomba?

Sijawahi kuombwa gari wala kuomba gari kwa mtu
Hii ni tabia za kimasikini sana
Huna gari agiza Uber
Unampa gari mtu bahati mbaya kagonga na limeharibika itakuwa imekula kwako

Maana kama kashindwa ku request atakuwa na hela ya kukutengenezea?

Mtu hana hata Insurance unampaje gari lako na humjui

Mwanangu alipokuwa anajifunza gari alitaka aendeshe kidogo mtaani kwetu
Nikamwambia huwezi kuendesha bila Insurance
Nikamkatia hapo hapo ya masaa mawili nikalipia tukaondoka kwa raha bila wasiwasi
Una maana gani unaposema insurance.
 
Tukianzia hapo mdau kwenye "Sijui nidhibiti vipi hizi tabia" inatupa picha halisi ya mahusiano yako na colleagues wako hapo mishe mishe.

Gari si ulinunua kwa hela zako au ulipewa zawadi? Wewe ndio unajua uanze vipi inaonekana ni tabiq ambayo ipo hapo kazini kwenu ukute hata kabla hujawa na hio ndinga.

Naweza kusema tu kama utakua na private route zako siku hizo wadau wateme tu unawaambia mimi naelekea somewhere leo siendi direction hio au kuna familia naipitia mahali so sitaweza mpa mtu hitchhick.

Kama wadau wamekomaa fuvu lazima watakuelewa ila all in all tuwe fair na wana ila tusije kujinyima privacy zetu.
Kaka Mimi bora nisaidie mtu mbali au mtu wa mtaani kuliko wa pale kazini.
Kwa sababu sihitaji mfanyakazi mwenzangu ajue hata ratiba zangu baada ya kazi zikoje.
Muda wa kazi ukiisha Kila mtu achukue uelekeo wake.
Ukiniomba lift itapelekea baadhi ya mishe zangu nishindwe kufanya kwa kuogopa zitaleak
 
Mkuu labda hujaelewa hawa watu wanajua kabisa mi ninakoishi, hivyo wanapanda wakijua naelekea Goba Sasa nikisema nielekee njia ya tofauti italeta maneno na majungu.na wao wameshageuza ni utaratibu Sasa kupanda gari yangu ila kiukweli mi Kuna muda Huwa nahitaji kwenda kwenye mishe zangu nyingine ila sipendi wao wajue,je nafanyeje na wameshapanda kwenye gari huku wanajua kabisa ni muda wa kwenda majumbani
Huna dharura?? Inawaambia leo kuna sehemu naenda nitachelewa kurudi.. hivyo watafute njia mbadala
 
Kaka Mimi bora nisaidie mtu mbali au mtu wa mtaani kuliko wa pale kazini.
Kwa sababu sihitaji mfanyakazi mwenzangu ajue hata ratiba zangu baada ya kazi zikoje.
Muda wa kazi ukiisha Kila mtu achukue uelekeo wake.
Ukiniomba lift itapelekea baadhi ya mishe zangu nishindwe kufanya kwa kuogopa zitaleak
Huo ndio ukweli wenyewe.. kuna watu wanajisahau sana kwa kuona ubest wa kazini ni wa maisha... nilikua nikisikia wakubwa wakisema kazini hakuna rafiki bali wanafiki... fanya kazi kwa bidii get paid and go home.

Kuna yale mazoea ya after kazi ndio hufanya wengi washindwe kutoboa mishe zao baada ya kazi.
 
Hyo ofisi ina watu wa ajabu sana..hawana mshipa wa aibu...
Watu wanajiendekeza tabia za ovyo sana.
Maana uwezo wa kununua gari wanao,uwezo wa kubolt wanao,uwezo wa kuita Uber wanao.
Daladala zinapita mbele ya ofisi.
 
Hapo umesema ni shida.
Wewe unajua unapaswa kwenda kazini na kurudi iweje utegemee lift kila siku? Wakati unaajiriwa uliambiwa kwamba work mate wako atakuwa anakupa lifti?
Kuna mambo sio lazima kumfanyia mtu, tunasaidiana kwenye shida ni sawa, ingawa pia kumsaidi mtu sio lazima.

Anayependa kutoa lift atoe na asiyependa usimlazimishe maana sio lazima, kuna watu hawapendi msongamano.
Nunueni magari na kama bado hujafanikiwa chapa mwendo na miguu, shida zako zisiwe kero kwa mwingine.
Yaani bora ofisi ingekuwa porini ofisi Iko posta hapo.
Kuna Kila means ya usafiri ila still watu wamegeuza utaratibu kusubiri kwenye parking uwape lift.
Yaani hawajui kiasi gani watu tunahitaju privacy kwenye mambo yetu.
Na hao wote uwezo wa kununua magari wanao ila wameamua kuweka mbele vipaumbele vyao vingine mwishowe tunasumbuana
 
Tatizo letu ni ujamaa, tunatamani kuishi kijamaa lakini dunia inatuendesha kibepari.

Kila mtu anataka ku-save pesa yake, ndio maana anakuja kuomba lift na kupata urahisi wa kufika anakoenda. Ila kiuhalisia kabisa ukipewa lift jiongeze, hata mgeni akija home utaishi nae kwa muda fulani, baada ya kipindi kirefu kupita utauliza vipi upo hapa kwa muda gani.
Ujamaa unafanya watu msaada waone haki
 
Vaa uso wa mbuzi, mtu hana gari huo ujasiri wa kuazima gari anautoa wapi? Mimi gari yangu hakuna mtu mwingine anayeendesha zaidi yangu.
 
Na kazini huwa anaomba msaada wa kueleweshwa jinsi ya kufanya kazi na Hao ambao hataki kusongamana kwenye kigari chake
Lazima ujifunze kuwa kitu Cha mwingine siyo chako na msaada sio haki
 
Individualist culture ipo kwa wazungu Sana, hawapendi kabisa Mambo ya kujuana juana, sie ngozi, nyeusi bado kidogo, tuna kaujamaa ndani, yetu, bado tunafikri cha mwingine ni cha kwangu, au nina haki ya kusaidiwa,
Wakatalie tu watajifunza na, kuzoea,
Na ndio utakuwa mwanzo wa majungu pale kazini, nina Imani hawatoniacha hivihivi lazima watanichafua
 
Back
Top Bottom