ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 55,787
- 131,638
Inaweza kuwa vyote viwili au kimoja, ila hata ingekuwa wewe...mbebe workmate siku 22 za kazi bila yeye kukwambia shika 10 hilo uongezee mafuta.Shida kuchangia au kupanda gari?
Inaweza kuwa vyote viwili au kimoja, ila hata ingekuwa wewe...mbebe workmate siku 22 za kazi bila yeye kukwambia shika 10 hilo uongezee mafuta.Shida kuchangia au kupanda gari?
Sawa bosi.Hapo umesema ni shida.
Wewe unajua unapaswa kwenda kazini na kurudi iweje utegemee lift kila siku? Wakati unaajiriwa uliambiwa kwamba work mate wako atakuwa anakupa lifti?
Kuna mambo sio lazima kumfanyia mtu, tunasaidiana kwenye shida ni sawa, ingawa pia kumsaidi mtu sio lazima.
Anayependa kutoa lift atoe na asiyependa usimlazimishe maana sio lazima, kuna watu hawapendi msongamano.
Nunueni magari na kama bado hujafanikiwa chapa mwendo na miguu, shida zako zisiwe kero kwa mwingine.
Mimi ni muwazi naongea as joking lakin namaanisha ningewaambiaInaweza kuwa vyote viwili au kimoja, ila hata ingekuwa wewe...mbebe workmate siku 22 za kazi bila yeye kukwambia shika 10 hilo uongezee mafuta.
Tatizo letu ni ujamaa, tunatamani kuishi kijamaa lakini dunia inatuendesha kibepari.Mimi ni muwazi naongea as joking lakin namaanisha ningewaambia
Kila mtu ni mnafique tu, watoa lift wanafiki...wanachekacheka ila moyoni hawana furaha, wapewa lift nao wanafique...anachekacheka ili mwenye gari yake awe huru.Kumwambia mtu kuwa sipiti uelekeo wako n kitu simple tuu ili kumkwepa usimpe lift kuliko kumpa lift na kuwa kwenye makasiriko.
Nilishawah kuomba lift, nikataja uelekeo wangu nikajibiwa anaenda uelekeo tofauti na mm, nikakutana nae kwenye foleni Mm nikiwa kwenye daladala.
Mbona simple tuu na roho yangu ikabaki na amani tele.
We jamaa bana.Sawa bosi.
Akili yako inakutuma kwamba kila anayeomba LIFTI au msaada basi ANA SHIDA???
Kwako wewe ukiwa na gari huhitaji ushirikiano na watu wengine?
Msongamano upo kwenye gari tu? Nyumba za iibada je? Kila mtu awe na yake ili kuonesha hawana shida?
Leo una gari lakini kesho unaweza usiwe nayo. Lakini hao unaotaka kuwanyima lift leo wanaweza wakawa na magari yao kesho. Unataka nao wakunyanyapae kama unavyotaka kuwafanyia?Najua, haihusiani na hii mada.
Hao ninaowapa lift baadhi Wana uwezo kunizidi
Unajua tukiwa wazima huwa tunakuwa wajuaji na wenye kujivuna sn, ila Mungu akikupa mtihani ndo utaona mali zote ulizonazo ni takataka tu, hata hilo gari wakikuambia uuze 1,000 km hauna namna utauza ili kuokoa uhai. Muhimu omba uwe mzima majigambo, fitina, starehe nk ni vitu vya muda tu.Kwani nyie msio na magari hamuanguki huko maofisini?
Mkianguka mnasaidiwaje hadi huyo mwenye gari umwambie akianguka atasaidiwaje?
Acha ushamba kung'ang'ania gari kwa vitisho eti akianguka hamtamsaidia.
Mshamba na Limbukeni huyo.Wewe utakuwa na roho mbaya mkuu. Huku Afrika siyo ulaya huwa tunashirikiana.
Mfano unatoka posta unaenda mbweni ukimpa lift mtu ukamuacha mwenge unapungukiwa nini hapo?
Pole ukiwa na dharura au ishu nyingine mjibu huelekeo wako ni mwingine.Habari,
Hivi Watanzania huu mtindo wa kuomba lift kwenye gari za watu muda wote mmeutoa wapi?
Walau mtu awe jirani yako umemkuta mbali huko kidogo ina make sense.
Sasa ndugu zangu mtu kazini wanakuvizia kwenye parking inakera sana aisee.
Tena zaidi mtu unamuuliza unaenda wapi badala akujibu na yeye anakuuliza kwani we unaelekea wapi utanishushia hukohuko!
Mtu unashindwa hata kupitia kwa kimchepuko chako kisa hawa watu.
Halafu huwezi jua mtu ana michongo yake gani anataka aifanye ila hapendi watu wa kazini wajue.
Pia tambueni gari mkipanda watu wengi hata ulaji wa mafuta unaongezeka tofauti na akiwa mtu mmoja au wawili.
Tabia ya nyingine ni kuazima gari yaani pale ofisini inafika mchana, mtu anakwambia niazime gari nikafuate chakula hotelini, daah! Yaani unampa mtu kupunguza lawama ila hii tabia inakera maana wengine Wana uendeshaji mbaya kama mi gari yangu ni manual Sasa wengine hawawezi hata kuziendesha vizuri ila wanaforce pia mafuta wakitumia hawa watu Huwa hawachangii hata tone.
Kwanini mtu kama hujataka kununua gari basi kwenye michongo yako bolt au kapande daladala usiwe kero kwenye Mali za watu wengine
Sijui nidhibiti vipi hizi tabia
Of course kuchukua mkopo na kununua gari ni uboya, ujinga, ulimbukeni,Halafu wakiwa pembeni utasikia, mimi siwezi kuchukua mkopo nikanunua gari hahahaha
Na ukiwa na kazi zako ofisini usiombe usaidiwe hata kama umesafiri utazifanya mwenyewe acha ubinafsi gari lenyewe la mkopo, nani kakwambia ununue gari kwa mkopo? matokeo yake unakuja na makasiriko dhidi ya wafanyakazi wenzioTena ingekuwa ni mara Moja,Sasa hivi wamegeuza utaratibu, utasikia "kaka twende ukaniache palepale pa Jana"
Yeah ni kuchangamsha maongezi tu hawa malimbukeni wanaomiliki magari ya mikopo wanasumbua sanaSio kuchunguza, n vile tuu kuchangamsha maongezi. N mara chache sana mfanyakazi mwenzako au mtu wako wa karibu umpe lift afu aanze kuuliza kuhusu gari lako, hapo lazima mtapiga story khs kazini ila kwa mtu ambaye hamna ukaribu sana ndo ataanza kuuliza khs gari kwa nia ya kuchangamsha maongezi tuu na sio kuchunguza.
Tatizo lenu mnachukulia mambo negative sana
Hii aione D Metakelfin
Introduction of ujamaa village (ARUSHA DECLARATION) hapa ndipo shida ilipo anzia..Hayo ndo madhara ya siasa za ujamaa kuomba omba kama masikini kwanini unataka mimi ni share "your poverty" kwa kunishirikisha umasikini wako.
Wewe hauna gari ndio maana hauoni tatizo alilo wasilisha mtoa mada.....hizo tabia zinakera vibaya , kuna watu wamenunua private car sababu ya kulinda privacy zao nmk......kwahy naww kama unatabia kama hiyo nakusihi sana uache bora iwe inayokea mala moja moja mtu kakukuta njian na sio kumsubiri utadhan wewe haupokei mshaharaWewe utakuwa na roho mbaya mkuu. Huku Afrika siyo ulaya huwa tunashirikiana.
Mfano unatoka posta unaenda mbweni ukimpa lift mtu ukamuacha mwenge unapungukiwa nini hapo?
Yaani ulivyo boya unaona sawa tu, wafanyakazi wenzio kukujua kwamba ni mchoyo wa lifti,Msaada au lift hailazimishwi..ni kweli tunasaidiana lakini tusijiendekeze! Ikitokea mara moja moja sawa... kusaidiana kupo ila busara itawale..
Sema mletaa mada kama huna amani usibebe mtu ueleweke kua huzimiki hayo mambo hutaona mtu akijileta.... usijistukie ..mbona mimi siombwi lifti ila tu watu wanajuaga sipendi haya mambo ya ujima..navimba mwenyewe kwenye chuma la watu 7.
Siku nikiwa sina gari hua nakwea mwendokasi
.bolt au bajaji sisumbui mtu.