Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Waomba lift wanakera sana.wakishapanda wanaanza kuchunguza mara waseme hii gari nzuri mara ni CC ngapi gari Yako?
Sio kuchunguza, n vile tuu kuchangamsha maongezi. N mara chache sana mfanyakazi mwenzako au mtu wako wa karibu umpe lift afu aanze kuuliza kuhusu gari lako, hapo lazima mtapiga story khs kazini ila kwa mtu ambaye hamna ukaribu sana ndo ataanza kuuliza khs gari kwa nia ya kuchangamsha maongezi tuu na sio kuchunguza.

Tatizo lenu mnachukulia mambo negative sana

Hii aione D Metakelfin
 
Daah! Hii imenichekesha lakini ukiachana na mafuta Kuna baadhi ya michongo wengine hatupendi ifahamike kazini ila mtu unatamani ukitoka kazini upitie huko.hawa watu wakiwemo kwenye gari inakuwa ni ngumu tena
fanya hivyo kama unaona wanapenda kitonga
 
Daah! Hii imenichekesha lakini ukiachana na mafuta Kuna baadhi ya michongo wengine hatupendi ifahamike kazini ila mtu unatamani ukitoka kazini upitie huko.hawa watu wakiwemo kwenye gari inakuwa ni ngumu tena
Mkuu kwan anakuwa amekuomba akausindikize unapoenda ww au umsogeze anapoenda yeye? C unamwambia tuu kuwa utamshusha njian mana ww unaenda njia tofauti, Yn mm umenipa lift naanzaje kwenda huko unapokwenda ww.
 
hata nje huko wote hawana magari
Sijui ccm wanawachukuliaje ndio maana mna aminishwa gari ni anasa wakati ni kitu cha kawaida kwa maisha ya sasa.Ungekuwa unaishi nje ndani ya mwaka ushamiliki.
 
Acha roho mbaya,aliyekypa wewe ndio aliyewanyima wao,kama unaenda njia tofautina wao we elejea unakoenda wenyewe watashuka tu njiani,acha ubinafusi
Mkuu labda hujaelewa hawa watu wanajua kabisa mi ninakoishi, hivyo wanapanda wakijua naelekea Goba Sasa nikisema nielekee njia ya tofauti italeta maneno na majungu.na wao wameshageuza ni utaratibu Sasa kupanda gari yangu ila kiukweli mi Kuna muda Huwa nahitaji kwenda kwenye mishe zangu nyingine ila sipendi wao wajue,je nafanyeje na wameshapanda kwenye gari huku wanajua kabisa ni muda wa kwenda majumbani
 
Habari,
Hivi Watanzania huu mtindo wa kuomba lift kwenye gari za watu muda wote mmeutoa wapi?
Walau mtu awe jirani yako umemkuta mbali huko kidogo ina make sense.

Sasa ndugu zangu mtu kazini wanakuvizia kwenye parking inakera sana aisee.

Tena zaidi mtu unamuuliza unaenda wapi badala akujibu na yeye anakuuliza kwani we unaelekea wapi utanishushia hukohuko!

Mtu unashindwa hata kupitia kwa kimchepuko chako kisa hawa watu.
Halafu huwezi jua mtu ana michongo yake gani anataka aifanye ila hapendi watu wa kazini wajue.

Pia tambueni gari mkipanda watu wengi hata ulaji wa mafuta unaongezeka tofauti na akiwa mtu mmoja au wawili.

Tabia ya nyingine ni kuazima gari yaani pale ofisini inafika mchana, mtu anakwambia niazime gari nikafuate chakula hotelini, daah! Yaani unampa mtu kupunguza lawama ila hii tabia inakera maana wengine Wana uendeshaji mbaya kama mi gari yangu ni manual Sasa wengine hawawezi hata kuziendesha vizuri ila wanaforce pia mafuta wakitumia hawa watu Huwa hawachangii hata tone.

Kwanini mtu kama hujataka kununua gari basi kwenye michongo yako bolt au kapande daladala usiwe kero kwenye Mali za watu wengine
Sijui nidhibiti vipi hizi tabia
Hii tabia walikuwa nayo walimu wangu wa O-level kuna mwalimu mwenzao mwenye gari akitoka tu wanaenda kujazana kwenye gari lake awape lifti wasivyo na haya wanakaa hadi kwenye buti, ishu ni kwamba watanzania wengi tunapenda vitonga.
 
Mwamba ukiwa na muda wabebe wenzio Kama unakwenda mchepuko wapige kiswahili ukapate dhambi peke yako. Kama unauthubutu wajengee mazingira wachangi mafuta kiduchu wapate usafiri wa uhakika.
 
Una roho mbaya sana mpuuzi wewe,
ungejua hilo ni jeneza usingeandika mafi hayo hapa.
Kama hutaki si unakataa tu kwani lazima?
Ushamba na hilo unaita gari manual si itakua una skrepa wewe hujui tu nyau we.
 
Back
Top Bottom