Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Afu ukute haohao wanaoomba lift Wana majumba wamejenga uko chanika.....sijui huwa wanatumia matako kufikiria,unajenga nyumba ya ml 20 unaacha kununua gari ya mil 10 kuepuka aibu na kero ndogondogo.


Kuna mdau alileta nyuzi....kwa Karne hii kununua gari sio anasa,kama MTU WA nenda rudi gari au pikpki kwako ni lazima.
 
Mimi nashangaa sana watu wenye vitu vyao halafu vinawatesa....kwanini usijisikie huru na Mali yako!??? Mimi bhana upendo wa mshumaa Sina kwamba niwake huku nateketea hiyo big noo...kama ni Mimi ningewaambia TU nikitoka kazini siendi home Moja kwa Moja Niko na ratiba zangu nyingine....nani atakuuliza ratiba Gani...yaani mwanaume mzima umekuja kulalamika huku kwa ajili ya jambo dogo kama hili....Mimi hata ninapoishi rafiki yangu akiniomba aje kama sipo tayari namwambia usije kipindi hiki sitaki interaction na huwa wananielewa coz sipendi Ile umemkubalia mtu kitu halafu umnyanyase nacho....Mimi kama ni ndio inakuwa ndio kutoka moyoni na kama ni hapana ni hapana kweli sijali utanionaje au utanichukuliaje
 
Ukiachana na mafuta.
Mtu unanunua gari unahitaji Uhuru.
Nikitoka kazini nahitaji kuwa huru nipitie sehemu nnazozijua Mimi.
Nionane na watu nnaowajua Mimi huko njiani.

Mfanyakazi mwenzio sio ndugu yako ukifukuzwa kazi Leo kesho anakusahau.

Wakijaa kwenye gari makosa Uhuru wa kufanya mambo yangu na kuonana na watu wangu.
Na sihitaji wafanyakazi wenzangu wafahamu maisha yangu wala ratiba zangu za nje ya kazi
 
Mkuu kwan anakuwa amekuomba akausindikize unapoenda ww au umsogeze anapoenda yeye? C unamwambia tuu kuwa utamshusha njian mana ww unaenda njia tofauti, Yn mm umenipa lift naanzaje kwenda huko unapokwenda ww.
Kuna mwingine ukimwambia hivyo anaanza kuuliza kwani unaenda wapi huenda na mi naelekea hukohuko.
 
Hongera kwa kununua na kutujuza una gari, bloo. Ni kile kile kipasso au umenunua gari sasa?
PS
Unajua maana ya mpanda ngazi hushuka?
 
Mwamba ukiwa na muda wabebe wenzio Kama unakwenda mchepuko wapige kiswahili ukapate dhambi peke yako. Kama unauthubutu wajengee mazingira wachangi mafuta kiduchu wapate usafiri wa uhakika.
Mafuta sio shida sana, shida ni Uhuru wa Mimi kufanya mishe zangu.kabla sijaelekea home,
Kuna baadhi ya sehemu Huwa natamani kupitia ila sihitaji wajue
 
Una roho mbaya sana mpuuzi wewe,
ungejua hilo ni jeneza usingeandika mafi hayo hapa.
Kama hutaki si unakataa tu kwani lazima?
Ushamba na hilo unaita gari manual si itakua una skrepa wewe hujui tu nyau we.
Sio roho mbaya ila kupanga ni kuchagua mtu kama hana uwezo wa kununua gari labda ningesema namsaidia, ila hawa wenye uwezo ndio waninyime mi uhuru
 
Daah! Hii imenichekesha lakini ukiachana na mafuta Kuna baadhi ya michongo wengine hatupendi ifahamike kazini ila mtu unatamani ukitoka kazini upitie huko.hawa watu wakiwemo kwenye gari inakuwa ni ngumu tena
Chagua week yako moja Tu,unawaambia week hii nna ratiba ya kwenda mahali(tofauti na direction ya siku zote).Usipowapa lift week nzima watalisahaau gari.
 
Sitaki wajue Sasa kama mi Huwa Nina mizunguko yangu kabla ya kwenda nyumbani
 
Mafuta sio shida sana, shida ni Uhuru wa Mimi kufanya mishe zangu.kabla sijaelekea home,
Kuna baadhi ya sehemu Huwa natamani kupitia ila sihitaji wajue
Kwan hua unawabeba kila siku?
Nyie matajiri mna nongwa sana aisee 🙌 usikute huo uhuru unaoutaka n wa kwenda kwa malaya hvy hutak kujulikana
 
Hongera kwa kununua na kutujuza una gari, bloo. Ni kile kile kipasso au umenunua gari sasa?
PS
Unajua maana ya mpanda ngazi hushuka?
Najua, haihusiani na hii mada.
Hao ninaowapa lift baadhi Wana uwezo kunizidi
 
Chagua week yako moja Tu,unawaambia week hii nna ratiba ya kwenda mahali(tofauti na direction ya siku zote).Usipowapa lift week nzima watalisahaau gari.
Hii nayo mbinu nzuri
 
Mimi ninaona wewe una matatizo manne;

1. Una tatizo la roho mbaya na ubinafsi.

2. Bado ni maskini uliyejilazimisha kununua gari ndo maana unalialia kuhusu mafuta.

3. Huna misimamo yako binafsi. Lazima uwe na misimamo utakayoiheshimu ili na watu wengine waiheshimu. Hii itakusaidia kutoingilika hovyo kuombwa lift au kuazimwa gari. Kuwa kama Mzee Urassa ambaye kwenye pick up yake mtapanda wakati wa kwenda shamba kimashuku. Kinyume na hapo ni ngumu.

4. Pamoja na umaskini wako ila wenzako kazini ni mafukara zaidi.

Suluhisho ni wewe kuamua kuwa na misimamo mikali au kuwa na roho nzuri na kusema ndiyo kila ukiombwa lift au kuazimwa gari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…