D Metakelfin
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 3,728
- 4,181
- Thread starter
-
- #101
Mwanzoni ilikuwa mara mojamoja lakini sasahivi Kila siku nakuta wananisubiri parking.Kwan hua unawabeba kila siku?
Nyie matajiri mna nongwa sana aisee 🙌 usikute huo uhuru unaoutaka n wa kwenda kwa malaya hvy hutak kujulikana
Mbona huwa easy tu, ukiwaambia gari yangu haibebi abiria kwani watakupinga mawe. Niliwahi kuona ofisi moja mfanyakazi akiwatoza nauli wafanyakazi wenzake na waliridhika na maisha. Ni uamuzi wako tu, lakini kuja mtadaoni kulallamika haisaidii na wala ujumbe hautawafikia walengwa.Ukiachana na mafuta.
Mtu unanunua gari unahitaji Uhuru.
Nikitoka kazini nahitaji kuwa huru nipitie sehemu nnazozijua Mimi.
Nionane na watu nnaowajua Mimi huko njiani.
Mfanyakazi mwenzio sio ndugu yako ukifukuzwa kazi Leo kesho anakusahau.
Wakijaa kwenye gari makosa Uhuru wa kufanya mambo yangu na kuonana na watu wangu.
Na sihitaji wafanyakazi wenzangu wafahamu maisha yangu wala ratiba zangu za nje ya kazi
Kama unashindwa kukataa kwenye mali zako mwenyewe basi pole sanaHabari,
Hivi Watanzania huu mtindo wa kuomba lift kwenye gari za watu muda wote mmeutoa wapi?
Walau mtu awe jirani yako umemkuta mbali huko kidogo ina make sense.
Sasa ndugu zangu mtu kazini wanakuvizia kwenye parking inakera sana aisee.
Tena zaidi mtu unamuuliza unaenda wapi badala akujibu na yeye anakuuliza kwani we unaelekea wapi utanishushia hukohuko!
Mtu unashindwa hata kupitia kwa kimchepuko chako kisa hawa watu.
Halafu huwezi jua mtu ana michongo yake gani anataka aifanye ila hapendi watu wa kazini wajue.
Pia tambueni gari mkipanda watu wengi hata ulaji wa mafuta unaongezeka tofauti na akiwa mtu mmoja au wawili.
Tabia ya nyingine ni kuazima gari yaani pale ofisini inafika mchana, mtu anakwambia niazime gari nikafuate chakula hotelini, daah! Yaani unampa mtu kupunguza lawama ila hii tabia inakera maana wengine Wana uendeshaji mbaya kama mi gari yangu ni manual Sasa wengine hawawezi hata kuziendesha vizuri ila wanaforce pia mafuta wakitumia hawa watu Huwa hawachangii hata tone.
Kwanini mtu kama hujataka kununua gari basi kwenye michongo yako bolt au kapande daladala usiwe kero kwenye Mali za watu wengine
Sijui nidhibiti vipi hizi tabia
1, Sina roho mbaya ndio mwanzoni ilikua mara mojamoja nasaidia najua huenda mtu bajeti zake hazikaa vizuri ila Sasa ni kero maana imekua utaratibu halafu kwenye gari maswali mengi sana.Mimi ninaona wewe una matatizo manne;
1. Una tatizo la roho mbaya na ubinafsi.
2. Bado ni maskini uliyejilazimisha kununua gari ndo maana unalialia kuhusu mafuta.
3. Huna misimamo yako binafsi. Lazima uwe na misimamo utakayoiheshimu ili na watu wengine waiheshimu. Hii itakusaidia kutoingilika hovyo kuombwa lift au kuazimwa gari. Kuwa kama Mzee Urassa ambaye kwenye pick up yake mtapanda wakati wa kwenda shamba kimashuku. Kinyume na hapo ni ngumu.
4. Pamoja na umaskini wako ila wenzako kazini ni mafukara zaidi.
Suluhisho ni wewe kuamua kuwa na misimamo mikali au kuwa na roho nzuri na kusema ndiyo kila ukiombwa lift au kuazimwa gari.
Sio umaskini ni kujiendekeza tuUmasikini mbaya sana, tutafuteni pesa jamani naona dharau zimezidi sasa.
Fanyia kazi namba 3.1, Sina roho mbaya ndio mwanzoni ilikua mara mojamoja nasaidia najua huenda mtu bajeti zake hazikaa vizuri ila Sasa ni kero maana imekua utaratibu halafu kwenye gari maswali mengi sana.
2,Bado ni maskini,Hapo ni kweli gari nilinunua kupunguza adha ya usafiri tu,japo hela za mafuta naimudu.
3.sina misimamo, hapo uko sahihi pia. Tatizo mi nahofia majungu watakayoanza.
4.hawa wanaoomba lift wote kipato Chao wanamudu kununua magari labda Kama pesa zao wameamua kutumia kwa matumizi mengine.na Kuna baadhi wamenizidi kipato
Halafu kwenye shughuli zangu naendajeUza hilo gari kuepuka lawama ndogondogo kama hizo!👿
Kwani nyie msio na magari hamuanguki huko maofisini?Kuna watu wana roho ngumu sn, yani unaona heri uondoke na gari ukiwa peke yako na kuwaacha wafanyakazi wenzio wanatembea kwa mguu. Hujui ukianguka ghafla hapo kazini hilo gari halitakupeleka hospitali lenyewe, na hata ndugu zako watafika too late. Labda km hao wafanyakazi wenzako mnabifu or else tenda wema uende zako.
Na hisia zangu zinanituma, wewe utakuwa "MWALIMU." maana hawa ndo wakipata kidogo wanajiona madoni, na majivuno kibao (ASHAKUMU SIYO MATUSI). "Niwie radhi km nitakuwa nimekukwaza kwa niliyoongea". Mfungo mwema.
Sio umaskini ni kujiendekeza tu
Sasa utateseka Hadi lini...!?? Ndio upendo wa mshumaa sasa huo...unataka uwaridhishe wengine huku wewe unaumia....endelea kujinafikia nafsi Yako....unatafuta pesa Yako then pesa Yako ikutese huo unafiki kwangu hauna nafasiSitaki wajue Sasa kama mi Huwa Nina mizunguko yangu kabla ya kwenda nyumbani
Au nisingekuwa na gari ingekuaje wangeniacha?Kwani nyie msio na magari hamuanguki huko maofisini?
Mkianguka mnasaidiwaje hadi huyo mwenye gari umwambie akianguka atasaidiwaje?
Acha ushamba kung'ang'ania gari kwa vitisho eti akianguka hamtamsaidia.
Sasa kama mtu uwezo anao Tena amekuzidi kipato.Kuna wakati Mungu anakubariki ili na wengine wabarikiwe kupitia wewe, hakuna asiyependa kumiliki gari lake
Unawaazima wenye nayo👿Halafu kwenye shughuli zangu naendaje
Naogopa sana kutumia kitu Cha mtu mwingine.Unawaazima wenye nayo👿