Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Nilichoona kwa mtoa mada na baadhi ya wanaosapoti kilichoandikwa na mtoa mada ni wana roho mbaya tuu, huwez kulalamika ety Ukitoa lift kwa mtu mmoja mafuta yattaisha, bc n sawa mafuta yataisha c unawaambia tuu wachangie mafuta au unaenda uelekeo tofauti na wao kwa nia ya kuwakwepa tuu kuliko kuwa kwenye makasiriko yasiyo na msingi
 
Ukikataa kutoa lift au kumpa mtu gari utapatwa na nini!!??
 
Uzoefu unaonyesha kwamba wapewa lift wengi sio wachangiaji wa mafuta, hata ukipita kituo cha mafuta huwa hawajigusi. Ndio maana watoa lift wanapata makasiriko.
 
Nikiwa mgodo morng kuna jirani yetu alikuwa anafanya kazi NSSF so morng alikuwa anasubir lift kutoka home akaona akiwa kwenye gar hayupo huru akaona kama anajidharirisha ndani ya miezi minne akanunua gari ain ya PORT nikaanza mm kuomba lift niwai shule nikiona wa home wanachelewa kutoka napanda lake
 
Watu wana roho mbaya sana humu, ety lift ya mtu mmoja inaongeza ulaji wa mafuta 🙌
 
Uzoefu unaonyesha kwamba wapewa lift wengi sio wachangiaji wa mafuta, hata ukipita kituo cha mafuta huwa hawajigusi. Ndio maana watoa lift wanapata makasiriko.
Shida kuchangia au kupanda gari?
 
Hii ni ishara ya udhaifu kitu chako nacho una kililia humu , Bila shaka nyie ndo wale ambao ata mkiombwa pesa na mwanamke hata kama huna uwezi sema sina na upo tayari uka kope uumpe
Unafiki broo
 
Uzoefu unaonyesha kwamba wapewa lift wengi sio wachangiaji wa mafuta, hata ukipita kituo cha mafuta huwa hawajigusi. Ndio maana watoa lift wanapata makasiriko.
Kumwambia mtu kuwa sipiti uelekeo wako n kitu simple tuu ili kumkwepa usimpe lift kuliko kumpa lift na kuwa kwenye makasiriko.

Nilishawah kuomba lift, nikataja uelekeo wangu nikajibiwa anaenda uelekeo tofauti na mm, nikakutana nae kwenye foleni Mm nikiwa kwenye daladala.

Mbona simple tuu na roho yangu ikabaki na amani tele.
 
Wewe utakuwa na roho mbaya mkuu. Huku Afrika siyo ulaya huwa tunashirikiana.
Mfano unatoka posta unaenda mbweni ukimpa lift mtu ukamuacha mwenge unapungukiwa nini hapo?
Kwani usipopewa lift utapungukiwa nini mkuu? Shida za mtu zisiwe kero kwa mwingine
 
Wewe hujiamini, waambie wenyewe, huku unaposema labda unaturingishia tu kuwa una gari, la sivyo mwanaume simamia misimamo Yako sio kulialia hapa, sisi hao watu hatuwajui kabisaaaaa
 
Mtu akikukuta unakula chakula no ukamkaribisha. Huwa unamuuliza kwanza hayo maswali? Au huko kwenu hata chakula na majirani hamkaribishani?
Mtaani kwako mtu akipata shida ya ghafla usiku na hana gari wala pesa utaweza kumsaida kweli wewe?
Kwani usipopewa lift utapungukiwa nini mkuu? Shida za mtu zisiwe kero kwa mwingine
 
Tukianzia hapo mdau kwenye "Sijui nidhibiti vipi hizi tabia" inatupa picha halisi ya mahusiano yako na colleagues wako hapo mishe mishe.

Gari si ulinunua kwa hela zako au ulipewa zawadi? Wewe ndio unajua uanze vipi inaonekana ni tabiq ambayo ipo hapo kazini kwenu ukute hata kabla hujawa na hio ndinga.

Naweza kusema tu kama utakua na private route zako siku hizo wadau wateme tu unawaambia mimi naelekea somewhere leo siendi direction hio au kuna familia naipitia mahali so sitaweza mpa mtu hitchhick.

Kama wadau wamekomaa fuvu lazima watakuelewa ila all in all tuwe fair na wana ila tusije kujinyima privacy zetu.
 
Mtu akikukuta unakula chakula no ukamkaribisha. Huwa unamuuliza kwanza hayo maswali? Au huko kwenu hata chakula na majirani hamkaribishani?
Mtaani kwako mtu akipata shida ya ghafla usiku na hana gari wala pesa utaweza kumsaida kweli wewe?
Hapo umesema ni shida.
Wewe unajua unapaswa kwenda kazini na kurudi iweje utegemee lift kila siku? Wakati unaajiriwa uliambiwa kwamba work mate wako atakuwa anakupa lifti?
Kuna mambo sio lazima kumfanyia mtu, tunasaidiana kwenye shida ni sawa, ingawa pia kumsaidi mtu sio lazima.

Anayependa kutoa lift atoe na asiyependa usimlazimishe maana sio lazima, kuna watu hawapendi msongamano.
Nunueni magari na kama bado hujafanikiwa chapa mwendo na miguu, shida zako zisiwe kero kwa mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…