Carleen
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 7,982
- 27,272
Guys,
Naomba tuweke utani wa siku zote pembeni, mnishauri kitu na tuwe serious kidogo tafadhali.
Mimi nina tabia moja hivi, napenda kumchokoza hasa mtu ninayempenda sana, yaani naanzisha kama kaugomvi mpaka nahakikisha mtu kapanic ile aanze kutype meseji ndefu kama mvua.
Kisha nakaa pembeni, naanza kucheka yaani nacheka mpaka nalia lakini unakuta mtu kakasirika kweli na anakuwa anaamini tunagombana lakini deep down Mimi nipo zangu sawa, na nikimjibu namchokoza zaidi naye anaendelea kufunguka akiwa very serious, ila Mimi ndiyo raha yangu nimuone tu hivyo nafuraaahi.
Hii kitu siyo mara moja wala mara mbili, wala mara tatu, mpaka sasa naona hii siyo hali ya kawaida..!! Nikikaa zangu huko naanza zangu tu kuchokoza mtu, na nina enjoy ajabu.
Nimejaribu kuacha nashindwa maana nitajikuta tu tayari nishaanza kutafuta ugomvi ambao hata haupo.!! Yaani tukae muda kidogo hakuna purukushani.? Sijiskii kabisa nitatafuta tu chanzo na lazima nitakipata, nakaa pembeni na popcorn zangu naanza kuenjoy sasa.
Hivi hili litakuwa tatizo gani?