Tabia ya waumini wengi wa KKKT kuondoka kabla ya ibada kuisha, Ni ishara kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa ibada


Mkuu mbona sijakuona nimesali ibada mbili ya kiswahili na Kiingereza. Kanisa Kuu Azania Front

Mdogo wangu alikuwa na Shukrani ya pekee.

Tulikuwa na mchungaji mzinga.
Mchungaji Mbowe.
Mchungaji Chaplain wa DAR TU. (Tudarco)
 
Mkuu mbona sijakuona nimesali ibada mbili ya kiswahili na Kiingereza. Kanisa Kuu Azania Front

Mdogo wangu alikuwa na Shukrani ya pekee.

Tulikuwa na mchungaji mzinga.
Mchungaji Mbowe.
Mchungaji Chaplain wa DAR TU. (Tudarco)
Hahaha mkuu kwani tunafahamiana?

Azania Front nimesali kipindi nikiwa naishi kwa ndg yangu mbezi beach....... Hata nikiwa huko nitasali hapo

Ingawa sasa nipo magheton nakuwa nasali mwenge au st Joseph cathedral katikati ya wiki!

Nitajitahidi kufika Tena Azania Front kusali nanyi mkuu...... Mviringo hall
 
Mkuu mbona sijakuona nimesali ibada mbili ya kiswahili na Kiingereza. Kanisa Kuu Azania Front

Mdogo wangu alikuwa na Shukrani ya pekee.

Tulikuwa na mchungaji mzinga.
Mchungaji Mbowe.
Mchungaji Chaplain wa DAR TU. (Tudarco)
Hongereni kwa Ibada na sadaka ya shukrani ni kitu kinachonipa amani sana sana........ Hongereni mkuu
 
Inategemea na siku hiyo ya ibada kuna kitu gani , ila makanisa ya kiroho mmezidi
 
Ukiacha dini ichezewe na kila mtu ndio matokeo yake hayo, but siku hizi umenisusa, niko outdated na muendelezo ila i hope unaendelea na masomo.
 
Kuna Jamaa Alinunua Wine Akawa Anaendesha Boda Barabara Kuu
Akajikuta Kadondoka Ghafla, Sababu Anasema Wine 🍷 Ilimpa Vibe
Jamaa kweli hakujipenda!
Wine ni moja ya kinywaji strong sana, Ndiyo maana hata emoji yake ipo nusu glass na sio pomoni.
 
Unaelewa maana ya kukaa na kupanga? Ushasema wanakaa na kupanga sasa unataka makao makuu yapange hadi muda wa kutoka.
Yn ww unaumia kuona hakuna mtu mmoja kuongoza makanisa yote duniani kama kwenu Katoliki 😂
Kwa facts anazoandika jamaa possible ni mwenzenu

Catholic muda wa ibada haupangwi Vatican hii kila Kanisa mahalia wanajipangia wenyewe,udhaifu ninaouna KKKT ni watu (kwa mujibu wa mleta mada) hawaijui mipaka yao mfano msoma matangazo ameshamaliza kusoma mchungaji anayarudia tena na kazi ya mchungaji siyo kusoma matangazo ni kuhubiri.

Chochote kikishafanyika nje ya utaratibu kinapoteza maana muhimu sana watu kujua wapi waanzie wapi wamalizie hata ikitokea kuhisiwa tangazo fulani linahitaji ufafanuzi wa kiongozi wa ibada basi iwe kwa kifupi sana au lipelekwe kwenye jumuiya waamini wakaeleweshane huko
 
Shakuambia ni Upumbavu na ujuha ,kumfuatilia Dini usiyo amini!
 
Mungu akusaidie utambue kuwa wale ni makuhani wamewekwa na Mungu kutimiza kazi yake. Suala la muda wa ibada kuwa mrefu ni jambo ambalo unaweza kufika ofisi ya mchungaji kiongozi ukatoa ushauri kuliko kuja hapa kulalamikia jambo ambalo wengi wa unaowalalamikia ni ama wa mlengo mwingine au si watu hata wanaoamini uwepo wa Mungu. Pia ufahamu suala la ibada ni nyeti na ni la kiroho kwa hiyo kuhani wa zamu anaweza kutumia muda wa ziada akifundisha au kuombea kwa kadri Roho wa Mungu atakavyomuongoza. Jambo la msingi la kujihoji wewe binafi ni kwa jinsi gani unapoingia ibadani unamwabudu Mungu katika Roho na kweli au unaenda kutimiza desturi tu. Mungu sio wa mazoea.
 
Tuwaonee huruma waliofariki wanahitaji bado maombi yetu kwa sababu hata kesho sisi tutahitaji kuombewa na tutakaowaacha,ibada bila nyimbo hapana hatujawa busy kiasi hicho Catholic kinachochukua muda sana ni matangazo.

Parokiani kwetu matangazo mengi yamehamishiwa kwenye ubao wa matangazo na kwenye whatsapp groups pia kwenye jumuiya so wakati wa ibada husomwa machache sana yale yanayohusu Kanisa as for me bado utaratibu wa ibada ni mzuri hauchukui muda mrefu japo kunahitajika mabadiliko fulani fulani baadhi ya sehemu.
 
Mbona usharika wa mbezi beach hauna hizi mambo

Mpangilio wa ibada uko vizuri sana na scripted.

Matangazo yanakuwa described kwa screen na ibada inakuwa imepangiliwa vizuri.

Kuanzia kwaya, praise na mambo mengine

Muda mfupi tu watu mnatoka kanisani.

Nadhani changamoto ya muda kuwa mrefu ni viongozi husika wa sharika

Kuna sharika zinajitambua sana pongezi kwa wachungaji wa mbezi beach wako well arranged ase.
 
Parokia karibia zote
Ni chache sana,mfano parokia niliyo mimi Bikira Maria Consolata Makabe Paroko wetu anajaribu kujenga umoja na hata wale waliokaa nje ya Kanisa kwa muda.

Nimeipenda sana hii program maana kwenye ngazi ya jumuiya muumini asiyeshiriki akihitaji huduma ya Kanisa viongozi wanamtisha hata kumnyima utambulisho wa form lakini Paroko anasisitiza apewe form isainiwe na viongozi wa ngazi zote ije kwake yeye ndiyo atajua anastahili huduma au hastahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…