Tabia ya waumini wengi wa KKKT kuondoka kabla ya ibada kuisha, Ni ishara kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa ibada

Tabia ya waumini wengi wa KKKT kuondoka kabla ya ibada kuisha, Ni ishara kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa ibada

Nifute surual yangu kesho nikajumuike na waamini wa Azania Front DSM, secretarybird ushatoa tithing ni kesho Azania Front.......

Neno la Mungu

Takata....

Lililo tokaa mbingunii

Ambapo moto na kutu haviwezi kuliishinda

Twakushika siku zote maishani na kufani!

Mkuu mbona sijakuona nimesali ibada mbili ya kiswahili na Kiingereza. Kanisa Kuu Azania Front

Mdogo wangu alikuwa na Shukrani ya pekee.

Tulikuwa na mchungaji mzinga.
Mchungaji Mbowe.
Mchungaji Chaplain wa DAR TU. (Tudarco)
 
Mkuu mbona sijakuona nimesali ibada mbili ya kiswahili na Kiingereza. Kanisa Kuu Azania Front

Mdogo wangu alikuwa na Shukrani ya pekee.

Tulikuwa na mchungaji mzinga.
Mchungaji Mbowe.
Mchungaji Chaplain wa DAR TU. (Tudarco)
Hahaha mkuu kwani tunafahamiana?

Azania Front nimesali kipindi nikiwa naishi kwa ndg yangu mbezi beach....... Hata nikiwa huko nitasali hapo

Ingawa sasa nipo magheton nakuwa nasali mwenge au st Joseph cathedral katikati ya wiki!

Nitajitahidi kufika Tena Azania Front kusali nanyi mkuu...... Mviringo hall
 
Mkuu mbona sijakuona nimesali ibada mbili ya kiswahili na Kiingereza. Kanisa Kuu Azania Front

Mdogo wangu alikuwa na Shukrani ya pekee.

Tulikuwa na mchungaji mzinga.
Mchungaji Mbowe.
Mchungaji Chaplain wa DAR TU. (Tudarco)
Hongereni kwa Ibada na sadaka ya shukrani ni kitu kinachonipa amani sana sana........ Hongereni mkuu
 
Aah wapi mambo ni yale yale. Kuna kipindi mtu alinambia wako smart sana kwenye muda. Sasa nikaja kuishi naye siku ya J2 nampeleka na kumfata yaani kuna siku namsubiri nje 1hr, mara 30min mara 15min hakuna muda maalum haya makanisa yote viongozi kuna namna wanapaswa kujirekebisha uhuru wao umezidi.
Inategemea na siku hiyo ya ibada kuna kitu gani , ila makanisa ya kiroho mmezidi
 
Lilikua kanisa langu ni hatari, hapa ndo huwa naelewa mashekh wanaokataza bidaaa maaana mengi yanazushwa mpka ibada inakua imevurugika, imagine mpo Kati Kati ya ibada em simameni tumwish mchngaji a happy birthday basi hapo tunaanza kuimba somo la bidaa nalielewa vizuri sana
Ukiacha dini ichezewe na kila mtu ndio matokeo yake hayo, but siku hizi umenisusa, niko outdated na muendelezo ila i hope unaendelea na masomo.
 
Kuna Jamaa Alinunua Wine Akawa Anaendesha Boda Barabara Kuu
Akajikuta Kadondoka Ghafla, Sababu Anasema Wine 🍷 Ilimpa Vibe
Jamaa kweli hakujipenda!
Wine ni moja ya kinywaji strong sana, Ndiyo maana hata emoji yake ipo nusu glass na sio pomoni.
 
Unaelewa maana ya kukaa na kupanga? Ushasema wanakaa na kupanga sasa unataka makao makuu yapange hadi muda wa kutoka.
Yn ww unaumia kuona hakuna mtu mmoja kuongoza makanisa yote duniani kama kwenu Katoliki 😂
Kwa facts anazoandika jamaa possible ni mwenzenu

Catholic muda wa ibada haupangwi Vatican hii kila Kanisa mahalia wanajipangia wenyewe,udhaifu ninaouna KKKT ni watu (kwa mujibu wa mleta mada) hawaijui mipaka yao mfano msoma matangazo ameshamaliza kusoma mchungaji anayarudia tena na kazi ya mchungaji siyo kusoma matangazo ni kuhubiri.

Chochote kikishafanyika nje ya utaratibu kinapoteza maana muhimu sana watu kujua wapi waanzie wapi wamalizie hata ikitokea kuhisiwa tangazo fulani linahitaji ufafanuzi wa kiongozi wa ibada basi iwe kwa kifupi sana au lipelekwe kwenye jumuiya waamini wakaeleweshane huko
 
Ukristo wa kweli tunaujua jibu maswali kama ni uongo ...toa hoja ...ni Yesu au mtume au nabii gani aliye badilisha heshima ya nyumba ya mungu ya ibada hadi watu wakaingia na viatu na kukaa vitini .....mimi nimetoa elimu isiyo na shaka kuhusu nini kilicho tokea .....
Shakuambia ni Upumbavu na ujuha ,kumfuatilia Dini usiyo amini!
 
Habari wakuu,

Mimi dhehebu langu ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),

Kanisa letu lina utaratibu wa kufuata kalenda ya mwaka, ni jambo zuri, Lakini kuna haja ya kufanya mabadiliko kwenye baadhi ya vitu ili kuendana na dunia ya leo

Usomaji wa matangazo ya week,

Kwa dunia ya sasa kuna namna nyingi matangazo kuwafikia waumini, Unakuta mzee wa kanisa kamaliza kusoma matangazo, mchungaji naye anakuja kutolea ufafanuzi wa matangazo yale yale

Ibada binafsi kuunganishwa na ibada za jumapili,

Mfano issue za ubatizo watoto zingefaa zipangiwe muda wa kipekee, Kama ilivyo ibada ya kufunga Ndoa,n.k

Muingiliano wa ratiba nyingi katikati ya ibada unapekea waumini wengi kushindwa kuvumilia kukaa mpaka mwisho, matokeo yake mchungaji akimaliza neno utaona idadi kubwa ya waumini wanaondoka kabla ya Ibada kuisha, hii sio ishara nzuri sana, kama kanisa inabidi kutafakari hili kwa kina

Wote tunajua lengo kuu la ibada ni Kusifu, kuabudu na kupata chakula cha kiroho (Neno la Mungu)
Ibada kuwa ndefu sio tatizo ,ila inategemea ime base upande gani, haya ni mawazo yangu binafsi,

Asanteni
Mungu akusaidie utambue kuwa wale ni makuhani wamewekwa na Mungu kutimiza kazi yake. Suala la muda wa ibada kuwa mrefu ni jambo ambalo unaweza kufika ofisi ya mchungaji kiongozi ukatoa ushauri kuliko kuja hapa kulalamikia jambo ambalo wengi wa unaowalalamikia ni ama wa mlengo mwingine au si watu hata wanaoamini uwepo wa Mungu. Pia ufahamu suala la ibada ni nyeti na ni la kiroho kwa hiyo kuhani wa zamu anaweza kutumia muda wa ziada akifundisha au kuombea kwa kadri Roho wa Mungu atakavyomuongoza. Jambo la msingi la kujihoji wewe binafi ni kwa jinsi gani unapoingia ibadani unamwabudu Mungu katika Roho na kweli au unaenda kutimiza desturi tu. Mungu sio wa mazoea.
 
Mimi ni RC, nilidhani hili ni tatizo huku kwetu tu. Ukweli ibada ndefu ni chukizo kwa wakati huu. Jumapili ni mapumziko kwa alie jitosheleza (yupo? Hata yesu alifanya kazi siku ya sabato). Nyimbo, maombi kwa marehemu na matangazo zinachukua muda mrefu sana. Mabadiliko ni muhimu.
Tuwaonee huruma waliofariki wanahitaji bado maombi yetu kwa sababu hata kesho sisi tutahitaji kuombewa na tutakaowaacha,ibada bila nyimbo hapana hatujawa busy kiasi hicho Catholic kinachochukua muda sana ni matangazo.

Parokiani kwetu matangazo mengi yamehamishiwa kwenye ubao wa matangazo na kwenye whatsapp groups pia kwenye jumuiya so wakati wa ibada husomwa machache sana yale yanayohusu Kanisa as for me bado utaratibu wa ibada ni mzuri hauchukui muda mrefu japo kunahitajika mabadiliko fulani fulani baadhi ya sehemu.
 
Mbona usharika wa mbezi beach hauna hizi mambo

Mpangilio wa ibada uko vizuri sana na scripted.

Matangazo yanakuwa described kwa screen na ibada inakuwa imepangiliwa vizuri.

Kuanzia kwaya, praise na mambo mengine

Muda mfupi tu watu mnatoka kanisani.

Nadhani changamoto ya muda kuwa mrefu ni viongozi husika wa sharika

Kuna sharika zinajitambua sana pongezi kwa wachungaji wa mbezi beach wako well arranged ase.
 
Parokia karibia zote
Ni chache sana,mfano parokia niliyo mimi Bikira Maria Consolata Makabe Paroko wetu anajaribu kujenga umoja na hata wale waliokaa nje ya Kanisa kwa muda.

Nimeipenda sana hii program maana kwenye ngazi ya jumuiya muumini asiyeshiriki akihitaji huduma ya Kanisa viongozi wanamtisha hata kumnyima utambulisho wa form lakini Paroko anasisitiza apewe form isainiwe na viongozi wa ngazi zote ije kwake yeye ndiyo atajua anastahili huduma au hastahili.
 
Back
Top Bottom