Sahihi kabisa, mm nasali KKKT Manzese, ibada inaanza saa moja afu kutoka n saa 5:30 huko.
Mambo yanayofanyika n upuuzi tuu.
Kwanza, saa 1:00 - 1:30 ni muda wa kusubiri wachelewaji, yn mchungaji kabisa anasema huo n muda wa kusubiri wale ambao bado hawajafika kanisani.
Pili, kwenye matangazo lazima mchungaji awe na matangazo yake binafsi na mengine tayari yalishasomwa ila atayarudia tena yn kama vile waumini n watoto wadogo kwamba wanasahau hapo hapo. Kila siku matangazo yale yale ad muda wa kuingia kanisani bado mtaambiwa kuwa n saa moja.
Tatu, tukio hadi la mwaka jana bado litasemwa mwaka huu mwezi wa tatu, mfano mwisho wa mwaka huo kuna siku maalum ya sadaka ya mavuno, ila hy sadaka itasemwa kila siku hata miezi sita ipite.
Nne, mzunguko wa kutoa sadaka ni wa kupoteza muda kinoma, kuna sadaka ya jengo na uwakili hizi sadaka zinatolewa kwenye bahasha hvy n mzunguko mmoja ila wanalazimisha iwe mizunguko miwili.
Yn mm vitu vya maana naona havizidi hata saa 3.