Tabia za Ajabu za Watoto

Tabia za Ajabu za Watoto

Hapa kitaani dogo mmoja anatabia ya kuchungulia watu chooni. Actually bora hiyo ya kuchungulia, tabia nisiyoipenda zaidi ni ile ya kupiga ngoma dirishani kwangu..! Yaani anasubiria siku za weekend nimekesha kudownload muvi usiku mzima mipango yangu ni kulala mpaka saa tano asubuhi then yeye anakuja kupiga ngoma dirishani kwangu..! Aisee ipo siku nitapiga kwenzi moja huyu dogo mpaka tumbo la uzazi cha mama yake litetemeke..!
WATOTO WA WATU SIKU HIZI HAWAGUSWI UNAWEZA SINGIZIWA KESI UMEBAKA...NA MTOTO NAE AKAFUNDISHWA UONGO...HUO NI MTEGO...

SIO KAMA ZAMANI MWANA WA WA MWENZIO NI WAKO...SIKU HIZI MWANA WA MWENZIO HAKUHUSU YATAKUPATA YANAYOKUHUSU YAKUSHINDE...
 
Hasa wazazi wanawake, halaf wepesi wa kugombana na watu sababu ya kitu kidogo vha mtoto maybe kapigwa wamepigana nje mama ake atakavyouvagaa huo ugomvi utadhani wa mtu mzima, kuna vitu kama mzazi lazima uwe mkali mazoea hujenga tabia, mwisho wa siku mtoto anakua hashikiki, samaki mkunje angali mbichi

Huku kwetu kuna wale wa weee zaa wako umpige koma kunipigia mwanangu,
yan hiyo tabia ya wazazi kutokutaka watoto wao waadhibiwe ,kuna wazazi walikua na watoto wadogo aisee walikua wadokozi mno,ukiweka kitu vibaya hakipo basi majirani wakiwapiga au kuwasemelea kwa wazazi wao wanawaambia waacheni hizo ni stages tu wakikua wataacha,baadaye wazazi walifariki wakabaki wao pekee ile tabia ya wizi waliendelea nayo hadi wamekua wakubwa and now mmoja ni marehemu alipigwa mpk kufa sababu ya wizi, mwingine yupo jela kitambo sasa. haya mambo ya watoto haya bora kumkanya tangu akiwa mtoto tu.
 
Asilimia kubwa ya malezi ya watoto sis wanawake tunachangia kuwaharibu tukijiona tunawapenda sana

Kuna rafiki yangu akitoka kwenda mjini au kokote lazima ampe mtoto wake hela hata kuanzia mia mbili namwambia kuna siku utakosa utamfundisha udokoz na kweli anasachi pochi ya mama ake anachukua hela anatoka ana miaka miwili tu

Muda mwengine tunaogopa kusema sana au kuact na hivo vitendo sababu ya wenzetu hatujui wanavotuchukulia
Wewe dada nimekupenda bure...wewe wajua kulea sanaa....wewe ndo mwanamke wa kuzaa nae sasa...mtoto wako atakuwa kwenye misingi inayotakiwa...

Wengi wa wazazi wa zama hizi wanajikuta wanawapenda sana watoto wao kuliko hata wao walivyokuwa wanapendwa na mama zao...sasa kinachofuata ni kuharibu watoto wao...mitoto inakuwa haina adabu...
 
Tabia za watoto bwana.... Binti yangu wa miaka miwili alimwabia mgeni *toka hapa*........ Oka apa kwa sauti yake ya kitoto...! Nilimgombeza hadi akaomba msamaha.
Kumgombeza haitoshi aisee...ningemnyong'onyea mapaja mpaka angejua kweli baba amechukia...
 
Wewe dada nimekupenda bure...wewe wajua kulea sanaa....wewe ndo mwanamke wa kuzaa nae sasa...mtoto wako atakuwa kwenye misingi inayotakiwa...
asante sana, aaamin inshallah

Wengi wa wazazi wa zama hizi wanajikuta wanawapenda sana watoto wao kuliko hata wao walivyokuwa wanapendwa na mama zao...sasa kinachofuata ni kuharibu watoto wao...mitoto inakuwa haina adabu...
na mtu anavyolea anaona ndoo analea, mwanae akicheza nje asiguswe akiguswa n shida, mtu anampenda mtoto mpaka mtoto anajua me napendwa
 
ni kweli mana muda mwingi mtoto anashinda na sisi kuliko nyie, tunahadaika na malezi ya kizungu bila kujua tunawaharib

Kuna mtoto wa jirani yangu aliwah kunitukana matusi makubwa ambayo hata kuyatamka ni mtihani nilimchapa mbele ya mama ake mwisho nikamwambia mama ake ukiwa unatukana hakikisha watoto wako hawapo karibu wanawasikia leo amentukana mm nimemchapa kesho atatukana kwengine sjui watamfanyaje na kama mzazi unajitia aibu

Yan malezi ya siku hizi ni mabovu sana mtoto anakua anajua mama ananipenda hawezi kunichapa hawezi kunifokea hawezi kunifanya kitu, matokeo akishakia mkubwa mzaz anamshindwa mapemaa
AISEE HUYO MAMA WA HUYO MTOTO MPAKA LEO MWAONGEA NAE VEMA KWELI?

HAJAKUWEKEA KISASI...?

MY FRIEND SIKU HIZI GUSA MTOTO WA MWENZIO UONE...ATAKWAMBIA ZAA WAKO UMCHAPE...
 
Raha ya mtoto umsemee akusikie, mtoto awe kasikivu, ukikiambia acha kanaacha kweli,

Kuna mtoto alikua anapenda kuja sana home akikuta nimetandika vizur sitting room anatoa vitambaa anatupa chini, me naokota natandika tena anakuja ana toa kama mchezo mwisho nilimkata jicho mtoto wa watu aliteremka akaenda kwao akawa ananiogopa mpaka nakaonea huruma

Mtoto aliezoea kuomba omba sjui najisikiaje yan asione mtu kapita na kitu anamfata anaomba hii tabia binafsi inanikera sana
Wewe dada umeolewa kweli...yan wewe ndo wa kuzaa nae kbs...hayo ndio malezi ya mama...sio majongoo ya siku hizi...

Kuna wakati mtoto anaingia ht ndan kwa watu anachukua kitu bila kuomba anakula...aisee...kwanza kuanzia ndani mwanangu usichukue kitu mpaka uruhusiwe na mama...na hutakiwi kumuomba mtu mwingine zaidi ya baba na mama tu...
 
Hasa wazazi wanawake, halaf wepesi wa kugombana na watu sababu ya kitu kidogo vha mtoto maybe kapigwa wamepigana nje mama ake atakavyouvagaa huo ugomvi utadhani wa mtu mzima, kuna vitu kama mzazi lazima uwe mkali mazoea hujenga tabia, mwisho wa siku mtoto anakua hashikiki, samaki mkunje angali mbichi

Huku kwetu kuna wale wa weee zaa wako umpige koma kunipigia mwanangu,
ohoo sasa mtu akikwambia zaa wako ndyo umpige duh basi inabidi uwe mpole tu, wazazi wengine bana , kuna dogo alikuja home sasa kuna kuku alikua ameatamia sasa ile ametoka eti huyo dogo kavunja mayai karibia yote eti anataka kuangalia kama kuna vitoto ndani jamani dah, nilimwambia tu aondoke kwao sitaki kumwona
 
Tunaongea vyema sana tu tena tunaheshimiana hatujawah kuvunjiana heshima, hajaniwekea kisasi hata hivo sipendi kuishi kwa visasi hatujafika huko
AISEE HUYO MAMA WA HUYO MTOTO MPAKA LEO MWAONGEA NAE VEMA KWELI?

HAJAKUWEKEA KISASI...?

MY FRIEND SIKU HIZI GUSA MTOTO WA MWENZIO UONE...ATAKWAMBIA ZAA WAKO UMCHAPE...
 
Waswahili wana msemo wao mtoto umleavyo ndivyo akuavyo ni sahihi kabisa

Nakumbuka had nakua najifaham ile mtu kuniambia mjinga wewe niliona tusi kubwa sana achilia hayo mengine mekuja yajua ukubwani na sikuwah wasikia wazazi wangu wakiyatamka

Unakuta toto kubwa haliamkii watu halaf mama ake anaona sawa kabisa unakutana naye mnaangaliana macho kwa macho kuna mmoja niliwah kumtania kwa kukuamkia na akanijibu marahaba hujambo nikajua anajua kuamkia kafanya kusud tu
YAANI WEWE MWANAMKE NI MIONGONI MWA WANAWAKE BORA WALIO HATARINI KUTOWEKA...

KUNA MTOTO HUYO HASALIMIAGI KABISA...NAMWAMBIA URAFIKI NA MIMI SINA...NA ZAWADI SIKUPI NA KWANGU USIJE...NA USICHEZE NA MWANANGU...SIPENDI WATOTO WATUKUTU...
 
yaani nilimkata jicho yule mtoto aakawa ananiogopa sana kuna vitabia tabia sjui hua najionaje

Unakuta mtoto wa kiume kadogo anaingiza mkono kwenye suruali anajivuta vuta maumbile yake bas nakua nakabetua mkono wake hahaaha yan had hua mama angu ananambia Mungu ampe umri aje ashuhudie wanangu ntakavyowalea
Nataka nikuoe tuzae...
 
Wanaanzaga kama mchezo kukujaribu...akiona unamchekea...ety oooh yan wewe e mtoto mtunduuu...

Anaona kumbe mwapenda eeh..sasa ndo anaendelea...
 
me kuna mmoja alinambia

Hujui mtu uchungu wake ulikuja vip shida gan alipitia had akajifungua huyo mtoto anemuona kama lulu, nikamwwmbia unapokua na mtoto waza kesho itakuaje ukiwa haupo kwenye uso wa dunia, mlee vile kila mtu ampende kuishi naye mlee aishi na yoyote yule usiwape watu kazi ya kuanza kulea upya akabaki anatabasam tu na ndio mwenye mtoto anepewa hela za mama ake akikosa anapekua mikoba anachukua hela
YAANI WANAJIKUTA WENGINE KAMA KUZAA NDIO WAMEANZA KUANZA WAO...NA UCHUNGU NDIO WAMEUPATA WAO TU...KWAHIYO MTOTO ANALELEWA KAMA YAI...MBONA MAMA ZETU HAWAKUTULEA HIVYO...
 
Me mtu akishanambia hivo hua sitak hata kumkaribia mtoto wake wala kumtuma chochote sipendi bugdha na watu kabisa, hahaha huyo at least alikua ana make sense japo kavunja mayai yote huyo unamwambia tu siku nyingine usivunje s umeona hakuna mtoto alietoka? Watoto ni shida sana nina mama angu mdogo ana watoto wa kike wa tatu, wa kwanza ndio form two now yan chumba chao ukiingia utasema tuko karume au manzese hua nikienda wakijua naenda watafanya usafi mama yao hasemi nao tena hata kuwamabia labda mtoto wa kike anapaswa kua msafi hamna, wa mwisho anakojoaga kitandani sasa hafui nguo zake yuko la tatu u can imagine hiyo harufu huko chumbani kwao mama yao yupo nao 24/7 haongei kabisa napataga tabu sana
ohoo sasa mtu akikwambia zaa wako ndyo umpige duh basi inabidi uwe mpole tu, wazazi wengine bana , kuna dogo alikuja home sasa kuna kuku alikua ameatamia sasa ile ametoka eti huyo dogo kavunja mayai karibia yote eti anataka kuangalia kama kuna vitoto ndani jamani dah, nilimwambia tu aondoke kwao sitaki kumwona
 
Kuna kengine kalikuja home na mama yake
Na mimi nikawa home likizo kipindi hiko nipo chuo
Sasa mi kwa kawaida sipendi mazoea na vitoto
Sikuiyo nipo sebuleni na pc kakaja nako kuangalia
Sijui ikaweje nimesahau. Kakaniambia "wewe hufanyagi kazi unakaa tu hapa kula" nilitamani nikapige sana ila kwa kuwa najua hasira zangu ningekaumiza ilibidi nikafukuze sebuleni
Hako kalitumwa na wazazi wake...hasa mama yake...my friend ondoka hapo hawakutaki...
 
Back
Top Bottom