Babu Rama seems kifo chake kina utata. Unaidaije serikali mabilioni kisha unapata stress na kujiua?
Wataalam wa saikolojia mtueleze hii inakuwaje hii
Kwa wafanyabiashara wanaweza kuelewa msongo wa mawazo ambao Babu Rama alikuwa akipitia kwa huo muda mrefu kutokana na mwenendo wa biashara.
Kikubwa hapo si deni analowadai TRA, kwani hao mabwana hata wakikubali kukulipa hiyo fidia, itakuwa ya mtindo wa msamaha wa kodi wa thamani ya kiasi hicho cha pesa.
Biashara hadi kuwa kubwa kama hiyo ya Babu Rama huwa ina mambo mengi, hasa hizi za kuagiza nje bidhaa au malighafi.
Fikiria bidhaa iliyokuwa ununue jana kwa milioni 900, halafu leo ukakuta dola imepanda kwa shilingi 50, maana yake ni lazima uongeze leo leo ili upate bidhaa.
Hivyo, kupanda kwa thamani ya dola kunaweza kukuzalishia madeni ya dhamana ya mali zako. Kwani hakuna muda mrefu wa kusubiri upate hela ya kuongezea.
Lakini, kinachoweza kukupa ujasiri wa kuyaingia hayo madeni ni uwezo wa biashara yako na uzoefu wako katika biashara husika. Kama ikienda kama kawaida madeni yanalipika na faida unapata.
Sasa inapotokea biashara yako hiyo ikaharibiwa kwa kiwango kama cha Babu Rama (900M), ni lazima uingie kwenye migogoro ya madeni makubwa
Na siku zote mgogoro wa madeni hufanya ufikie kupoteza mali zako za thamani kubwa kwa hela kidogo sana uliyokopa na ikapotea. So, unauelekea umasikini.
Kuna ugumu mkubwa wa kuikabili hali hiyo, ni wachache sana walifaulu. Wengi walipata maradhi ya kupooza kama marehemu RG wengine kufa kwa sonona.
Ova